Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel leo imeipongeza Timu ya wanawake Tanzania
ya Kilimanjaro Queens kufatia ushindi wa walioupata katika michuano ya
Challenge Afrika Mashariki na Kati 2016 maarufu kama CECAFA
Timu
ya kili Queen iliyosheheni vijana kutoka Airtel Rising Stars imeibuka
washindi wa michuano hiyo baada ya kuichapa harambee Queens ya Kenya bao
2-1
akiongea wakati wa timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel leo ,
Mwenyekiti wa soka la wanawake Tanzania , Bi Amina Karuma alisema"
Tumekuja hapa Airtel leo na kuleta kombe hili kwani tunathamini sana
mchango mkubwa unaofanywa na Airtel kupitia program ya Airtel Rising
Stars ambayo imetuwezesha kupata wachezaji mahiri na waliotuwezesha
kuleta ubingwa huu nchini.
"Tunajisikia
faraja kuona Airtel iko bega kwa bega na sisi katika kuhakikisha soka
la wanawake linaendelezwa na kukua kwa kasi, juhudi hizi zilizofanywa
kwa miaka sita sasa zimezaa matunda kwa timu ya wanaume ya Serengeti
boys na sasa kwa timu yetu ya Kilimanjaro Queens.
"Napenda
kuchukua fursa hii kuwapongeza na kuwaomba waendelee kushirikiana nasi
katika kukuza, kulea na kubaini vipaji chini ya mpango wa Airtel Rising
Stars ambao umekuwa tija skwa maendeleo ya soka nchini", alisema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso aliwapongeza
wachezaji wa Kili Queens kwa ushinid wa kishindo kikubwa na kuahidi
kuendelea kudhamini michuano ya Airtel Rising Stars ili kubaini vipaji
vipya zaidi na kuwawezesha vijana kuzifikia ndoto zao ili kutimiza
dhamira ya kampuni yake chini ya Mpango wake kabambe wa Airtel FURSA.
Kufatia
ushindi huo Airtel imewazawadia wachezaji hao kila mmoja kiatu cha
mpira ikiwa ni motisha kwa wachezaji kuchezea na kuendelea kufanya
vizuri na kupata vifaa bora vya michezo
wachezaji wa
Kili
Queens wanane walitoka katika michuano ya Airtel Rising Stars ambao ni
pamoja na Stumai Abdallah, Sherida Boniface, Anna Ezron , Anastazia
Antony, Amina Ally, Donisia Daniel, Najiat Abbasi na Maimuna Khamis
Afisa uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akiwapokea wachezaji wa Kili Queens wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel makao makuu leo