JAJA ‘ABWAGA MANYANGA’ YANGA SC, MAXIMO AMLETA EMERSON KUZIBA NAFASI YAKE

November 22, 2014

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI Genilson Santana Santos ‘Jaja’ amejiondoa Yanga SC akiwa likizo nchini mwao, Brazil na sasa nafasi yake itazibwa na kiungo mkabaji, Emerson Oliveira Neves Roque, BIN ZUBEIRY imeipata hiyo. Jaja amesema ana matatizo ya kifamilia yanayomzuia kurejea Tanzania kufanya kazi- lakini BIN ZUBEIRY inafahamu mshambuliaji huyo ameshindwa kumudu presha ya mashabiki wa klabu ya Jangwani. Wapenzi wa Yanga SC hawajaridhishwa na uwezo wa Jaja, aliyeichezea klabu hiyo mechi 11 na kuifungia mabao sita.
Genilson Santana Santos 'Jaja' anaondoka Yanga SC baada ya kuichezea mechi 11 na kuifungia mabao sita
Kocha Maximo ambaye yuko likizo Brazil pamoja na Msaidizi wake, Leonardo Leiva na kiungo Andrey Coutinho, amewatumia taarifa Yanga SC kwamba Jaja hatakuja, badala yake anakuja kiungo mkabaji Emerson. Emerson mwenye umri wa miaka 24 mzaliwa wa Rio de Janeiro, anakuja Yanga SC akitokea klabu ya  Bonsucesso ya mjini humo, ambayo imewahi kucheza Ligi ya Serie B mara mbili, ingawa kwa sasa inacheza ligi ya jimbo la Rio.
Jaja atakumbukwa kwa mabao yake mawili aliyofunga katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Azam FC, mechi ya Ngao ya Jamii
Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Jumanne kwa ajili ya kufanyiwa majaribio na akifuzu atafanyiwa vipimo vya afya, kabla ya kusajiliwa. Wazi mchezaji huyo ana nafasi ya kusajiliwa Yanga SC kwa kuwa analetwa na kocha Maximo. Jaja alijiunga na Yanga SC msimu huu, lakini hakuwahi kuwavutia wapenzi wa klabu hiyo, ingawa atakumbukwa kwa mabao yake mawili aliyofunga wakati Yanga SC ikiifunga Azam FC 3-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii Septemba 14, mwaka huu.

IFM YAANZA VEMA MASHINDANO YA SHIMUTA ,YAIBAMIZA TANGA CEMENT MABAO 2-1.

November 22, 2014

MKUU WA WILAYA YA MUHEZA,SUBIRA MGALU AKIKAGUA TIMU YA IFM LEO

 TIMU ya Kiwanda Cha Cement Mkoani Tanga(Tanga Cement) leo imeanza vibaya mashindano ya Shimuta baada ya kujikuta wakitandikwa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha Dar es Salaam (IFM) katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa uwanja wa CCM Mkwakwani.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali na wenye upinzani wa hali ya juu ambapo mpaka timu zote zinakwenda mapumziko IFM walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Yasin Mkumbo ambaye alitumia uzembe wa mabeki wa Tanga Cement na kupachika wavuni bao hilo.
 
MKUU WA WILAYA YA MUHEZA,SUBIRA MGALU AKIIKAGUA TIMU YA TANGA CEMENT LEO
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo kila timu iliingia uwanjani hapo zikiwa na lengo la kuhakikisha zinapata matokeo mazuri kwenye ngwe hiyo ya lala salama iliyokuwa ikichezwa na mwamuzi Ibrahimu Kidiwa.

Wakionekana kujipanga baada ya kuwa nyuma bao 1-0,Tanga Cement waliweza kufanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa IFM na kufanikiwa kuandika bao la kufutia machozi kupitia mchezaji wake Daud Izack.

Baada ya bao hilo Tanga Cement waliweza kujipanga na kuendeleza mashambulizi mfululizo langoni mwa IFM bila mafanikio yoyote kutokana na wachezaji wake kupata mipira na kuipiga nje ya lango la wapinzani wao.


Kutokana na shambulio hilo,IFM waliweza kucharuka na kupeleka mashambulizi langoni mwa Tanga Cement na kufanikiwa kuandika bao la pili ambalo lilifungwa na Steven Shekiondo ambaye aliamsha shangwe na nderemo kwa mashabiki wao.

DKT. SHEIN AZINDUA TAMASHA LA VIJANA BWAWANI UNGUJA,ZANZIBAR LEO

November 22, 2014

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein akisalimiana na Viongozi wakiwemo wawekezaji Kampuni na wadau wa maendeleo wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar”uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein akisalimiana na Viongozi wa mbali mbali wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar”uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein akizungumza na Waziri wa Ofisi ya Rais,Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman kabla ya uzinduzi wa Tamasha la Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar”uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Baadhi ya Viongozi wa Idara za Serikali ya Mapinduzi walioshiriki katika uzinduzi wa Tamasha la Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar”uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Vijana walioshiriki katika uzinduzi wa Tamasha la Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein alipozungumzanao leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Tamasha la Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein akipata maelezo kutoka kwa Taki Dewji wa banda la Shell wakati alipotembelea mabanda mbali mbali mara baada ya kuzindua rasmi Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein akipata maelezo kutoka kwa Rose Tesha Meneja Vipindi katika banda la VSO wakati alipotembelea mabanda mbali mbali mara baada ya kuzindua rasmi Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” uzinduzi uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Ameir Ali Ameir katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma wakati alipotembelea banda la maonesho baada ya kuzindua rasmi Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” uzinduzi uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein akipata maelezo kutoka kwa Mussa Ngwali Ahmed, katika banda la TUPOMOJA wakati alipotembelea mabanda mbali mbali baada ya kuzindua rasmi Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” uzinduzi uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein akipata maelezo wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Uwezaji Wananchi Kiuchumi katika maonesho ya ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” baada ya uzinduzi uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein akipata maelezo kutoka kwa Kirtikumar B.Dave Meneja katika kampuni ya maziwa ya Azam wakati alipotembelea katika maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” baada ya uzinduzi uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja. [Picha na Ikulu.]

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, ATUNUKU VYETI NA SHAHADA WAHITIMU ESAMI LEO

November 22, 2014


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Taasisi ya ESAMI iliyopo Njiro Hill Mkoani Arusha alipowasili kwenye Taasisi hiyo leo Novemba 22,2014 kuhudhuria Mahafali ya nane ya Taasisi hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal wa pili kulia na Viongozi wa Taasisi ya ESAMI iliyopo Njiro Hill Mkoani Arusha akiongoza maandamano ya mahafali ya nane ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo Novemba 22,2014 Njiro Hill Mkoani Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti Witness Steven mhitimu wa Shahada ya MBA katika Taasisi ya ESAMI Kampas ya Dar es salaam kwenye mahafali ya nane ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo Novemba 22,2014 Njiro Hill Mkoani Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti Leah Mumbua mhitimu wa Shahada ya MBA katika Taasisi ya ESAMI Kampas ya Nairobi kwenye mahafali ya nane ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo Novemba 22,2014 Njiro Hill Mkoani Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wahitimu wa fani mbalimbali kwenye Mahafali ya nane ya Taasisi ya ESAMI yaliyofanyika leo Novemba 22,2014 Njiro Hill Mkoani Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma George Yambesi kwenye Mahafali ya nane ya Taasisi ya ESAMI yaliyofanyika leo Novemba 22,2014 Njiro Hill Mkoani Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha pamoja na Viongozi na Wahitimu wa Fani mbalimbali kwenye Mahafali ya nane ya Taasisi ya ESAMI yaliyofanyika leo Novemba 22,2014 Njiro Hill Mkoani Arusha. (Picha na OMR)

TIMU YA CHUO CHA ARDHI WAIBUKA KIDEDE MCHEZO WA KUVUTA KAMBA DHIDI YA BODI YA MIKOPO,MASHINDANO SHIMUTA

November 22, 2014







DC MGALU AZINDUA MASHINDANO YA SHIMUTA LEO MKWAKWANI.

November 22, 2014
MKUU WA WILAYA YA MUHEZA,SUBIRA MGALU AKIZUNGUMZA LEO WAKATI AKIFUNGUA MASHINDANO YA SHIMUTA MKOANI TANGA


KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA MUHEZA,SUBIRA MGALU AKIZUNGUMZA NA WANAMICHEZO KULIA KWAKE NI KATIBU WA SHIMUTA AWARD SAFARI LEO,MASHINDANO HAYO YANASHIRIKISHA WANAMICHEZO 500.

KATIBU WA SHIMUTA,AWARD SAFARI AKIZUNGUMZA NA WANAMICHEZO WANAOSHIRIKI MASHINDANO HAYO LEO WAKATI WA UZINDUZI WAKE
MKUU WA WILAYA YA MUHEZA,SUBIRA MGALU AKISALIMIANA NA TIMU YA KIWANDA CHA CEMENT CHA TANGA CEMENT LEO

HAPA MKUU WA WILAYA YA MUHEZA,SUBIRA MGALU AKISALIMIANA NA TIMU YA SOKA CHUO CHA IFM
 





MASHINDANO ya Shimuta yamezinduliwa leo ramsi na Mkuu wa wilaya ya Muheza Subira Mgalu ambapo alizitaka mashirika yanayoshiriki mashindan o hayo kuhakikisha wanazingatia taratibu za michuano hiyo kwa kuchezesha wachezaji ambao watakuwa wafanyakazi na sio vyenginevyo.

Mashindano hayo yanashirikisha timu 20 ambazo ni Shirika la Utangazaji  Tanzania (TBC),Chuo Kikuu Huria(OUT),Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE),Kampasi za Mbeya na Dar es Salaam na Mwanza,Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO),Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM),Chuo Kikuu cha Ardhi.

Timu nyengine ambazo zinashiriki mashindano hayo ni Hifadhi ya Taifa Tanzania(TANAPA),Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini(IRDP),Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma(CDA),Chuo Kikuu cha Mzumbe,Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi(MOCU),Chuo kkikuu cha Muhimbili cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS),Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Wengine ambao watashiriki kwenye mashindano hayo ni Baraza la Hifadhi na Usimamizi na Mazingira (NEMC),Shirika la Mzinga,Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Arusha (AICC), Wenyeji wa Mashindano hayo,TANGA CEMENT na Timu mpya kwenye shirikisho hilo ya Bohari ya Madawa(Medical Stores Department(MSD).

Kauli mbiu ya Mashindano hayo msimu huu ni "Michezo kuboresha Afya za Wafanyakazi "Tufanye Michezo sehemu za Kazi.



CHUO IRDP DODOMA CHAADHIMISHA MAAFALI YA 28 KWA MAFANIKIO

November 22, 2014
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum wakati wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akimtukuku Shahada ya Uzamili katika Uchumi wa Maendeleo Amina Salum Mwanja wakati wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Baadhi ya wahitimu wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Mwanafunzi wa mwaka wa pili anayesomea Shahada ya kwanza ya Mipango ya Usimamizi wa Mazingira katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) Azizi Mshau akimweleza Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene namna bora ya kundaa mipango miji inayokuwa rafiki kwa mazingira.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akiagana na Mkuu wa kwanza wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) Askofu Dkt. Saimon Chiwanga mara baada ya sherehe ya mahafali ya 28 ya Chuo hicho.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene () akiwa katika picha ya pamoja na wahadhiri wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) mara baada ya mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma. (Picha zote na Eleuteri Mangi- Dodoma)

Na Eleuteri Mangi- Dodoma
Serikali imesema  inaendelea kushirikiana na sekta binafsi kuweka mazingira rafiki kwa kuboresha mifumo ya ajira katika sekta ya umma na ile ya binafsi ili kujenga uchumi wa kisasa unaozalisha ajira pamoja na kuwawezesha vijana wasomi nchini kujiajiri.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene kwa niaba ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum wakati wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) yaliyofanyika jana mjini Dodoma.

“Ninafarijika sana kusikia vijana wa chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini wameweza kuonesha njia kwa kuweka kwa vitendo waliyojifunza kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi katika sekta ya kilimo kama njia ya kujiajiri” alisema Mbene.

Naibu Waziri huyo aliwahakikishia vijana hao kuwa Serikali ipo tayari kusaidia juhudi hizo kupitia fursa mbalimbali za kuwasaidia vijana na wajasiriamali kupitia fursa zinazoendelea kutolewa na Serikali.

Naibu Waziri Mbene alisema kuwa ili kutekeleza lengo hilo, Serikali inaendelea kuhamasisha uwekezaji katika kilimo, uchimbaji wa madini na uwezo wa kuongeza thamani mazao yetu yanayozalishwa.

Mbene aliongeza kuwa maeneo yote hayo yanatoa fursa nyingi kwa wahitimu vijana nchini kuajiriwa katika ngazi mbalimbali za Serikali, sekta binafsi na kujiajiri.

Akimkaribisha Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo Dkt. Razack Lokina alitoa kilio cha chuo hicho cha kuomba kada ya mipango kupewa nafasi stahili katika mfumo wa ajira Serikalini.

Akifafanua suala hilo Dkt. Razack alisema kuwa kukosekana kwa kada ya Mipango kumesababisha kazi za kada hiyo kutotekelezwa ipasavyo kwa kiwango cha ufanisi unaotakiwa. 

Aidha, Dkt. Razack alisema kuwa taaluma ya Mipango inamtayarisha Afisa Mipango ambaye jukumu lake ni kubuni, kupanga, kufuatilia, kutathmini, kuratibu shughuli na rasilimali katika maeneo ya Mipango ili kufikia malengo ya maendeleo ya jamii kusudiwa tofauti na taaluma ya Uchumi ambayo inamuandaa Afisa kuwa na jukumu mahususi la kuchambua ili kutoa hali halisi ya mazingira ya kiuchumi kisekta.

Kwa upande wake Chuo hicho Constantine Lifuliro alisema kuwa wahitimu wa chuo chake wameandaliwa vya kutosha wapo tayari kutoa huduma katika nyanja mbalimbali kwenye maeneo waliyojifunza hasa katika kuandaa, kusimamia, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini mipango ya maendeleo katika maeneo mbalimbali  watakayofanyia kazi.

Naye mhitimu Baltazar Ngeze, kwa niaba ya wahitimu wa mwaka huu wa chuo hicho aliushukuru uongozi wa chuo kwa kuwaandaa vema kwenda kutekeleza majukumu yao ya taaluma ya Mipango katika jamii watakayokuwepo.

Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 1,909 waliotunukiwa tuzo zao katika kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo.

Kati ya wahitimu hao, wapo wanaume ambao idadi yao ni 1,003 sawa na asilimia 52 ya wahitimu wote na wanawake idadi yao ikiwa ni 906 sawa na asilimia 48 ya wahitimu wote.

Idadi hiyo ya wahitimu wa mwaka huu inaonesha wameongezeka wahitimu 63 sawa na silimia 3.4 zaidi ya wale waliohitimu masomo yao mwaka jana 2012/2013 ambao walikuwa 1,846 kati yao wakiwa wanaume 1,037 sawa na asilimia 56 na wanawake walikuwa 809 sawa na asilimia 44.