*KATIBU MKUU WA CCM, AMALIZA ZIARA YA MKOANI TABORA, ATINGA NA KUPATA MSOSI KWA MAMALISHE, AHITIMISHA ZIARA KWA MKUTANO WA HADHARA

May 19, 2014

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Stendi Kuu ya Zamani mjini Tabora, baada ya kumaliza ziara yake ya siku 11 katika mkoa huo, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata  Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi
Wakazi wa Mji wa Tabora Mjini  wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliondaliwa na CCM leo jioni,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana amehitimisha siku za ziara yake ya siku 11 mkoani humo,ya  ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata  Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.Kinana na msafara wake kwesho wataelekea mkoani Singida kwa ziara siku kadhaaa tena.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara wa CCM, Mjini Tabora leo, ambapo aliwafananisha Wapinzani na Boko Haramu wa waasi wa Nigeria kwa kuwachonganisha wananchi kwa maneno,hali ambayo imeeleza kuwa kinaweza kusababisha vurugu nchini.
 Katibu Mkuu wa CC,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM,Wilaya ya Tabora mjini mapema leo kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara,aidha Kinana katka ziara yake wilayani Tabora alikagua miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa umwagiliaji,kuweka jiwe la msingi katika ofisi za CCM,kukagua mradii wa ujenzi wa hospitali,kuzindua mradi wa matofali wa akina mama na mengineyo mengi. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa na Wazee waasisi wa chama cha TANU mjini Tabora leo.
 Kinana akinawishwa na Mamalishe kabla ya kupakuliwa msosi wa nguvu.
 Kinana akihudumiwa na Mama Lishe alipokwenda kula yeye na msafara wake kwa akina mama lishe eneo la Stendi Mpya Tabora mjini. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Munde Tambwe,kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Tabora, Aden Rage ukiungana na Kinana kula msosi kwa mamaLishe mjini Tabora leo.
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa wakipata mlo kwa Mama Lishe mjini Tabora leo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiapata mlo wa mchana kwa Mama ntilie katika stendi mpya ya mabasi mjini Tabora,Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini ,Mh Aden Rage,katikati ni  Mbunge wa viti maalum CCM mkoani Tabora,Mh.Munde Tambwe wakishiriki pamoja na naye katika mlo huo sambamba na vijana wa mjini Tabora.
 Naibu Waziri wa Maji,Mh.Amoss Makala akitoa ufafanuzi kwa wakazi wa Tabora mjini kuhusiana na suala zima la upatikanaji maji na mikakayi yake katika mkoa huo,ambapo imeelezwa kuwa mkoa huo una tatizo kubwa la maji
 Baadhi ya Wabunge mbalimbali walioshiriki kwenye mkutano huo wa Hadhara uliofanyika mjini Tabora,ikiwa ni siku ya mwisho ya kuhitimisha ziara ya siku 11 ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mkoani humo. 
Mbunge wa jimbo la Mtera,Mh.Livingstone Lusinde akiwahutubia wakazi wa mji wa Tabora mjini leo jioni kwenye mkutano wa hadhara uliondaliwa na chama cha CCM.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais,Mh. Ummy Mwalim akihutubia  katika mkutano wa hadhara na kuuponda Ukawa kwa kitendo chake cha kutoka bungeni kwa sababu zisizoeleweka wakati wa Bunge la Katiba,Mh.Ummy pia aliwatia shime akina mama kuwa na mshikamano katika suala zima la kujiletea maendeleo katika nyanja mbalimbali walizomo,na kuacha kubweteka wakisubiri waletewe maendeleo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa akihutubia katika mkutano wa hadhara wa CCM, ambapo alimpongeza Katibu Mkuu Kinana kwa kufanikisha ziara yake mkoani humo na kumaliza salama.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano ya Umma), Steven Wassira akihutubia katika mkutano wa hadhara na kuwaponda viongozi wa Ukawa wa kususia mkutano wa Bunge la Katiba bila kuwa na sababu za msingi.
MAFUNZO YA MAADILI NA KUANDIKA HABARI ZA JINSIA NA MIGOGORO YAFANYIKA MASASI, MKOANI MTWARA

MAFUNZO YA MAADILI NA KUANDIKA HABARI ZA JINSIA NA MIGOGORO YAFANYIKA MASASI, MKOANI MTWARA

May 19, 2014
SONY DSCMkurugenzi wa Fadhila FM Redio, Br. Edwin Mpokasye akiwakaribisha washiriki katika ufunguzi wa warsha ya Maadili na kuandika Habari za Jinsia na Migogoro kwa waandishi wa habari wa Redio za Jamii iliyofanyika Masasi mkoani Mtwara.
SONY DSCMkurugenzi wa Fadhila FM Redio, Br. Edwin Mpokasye akikabidhi risala aliyoitoa kwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi Farida Mgomi wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa warsha hiyo.
Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Bi. Rose Haji Mwalimu akitoa ufafanuzi kuhusu madhumuni ya warsha hiyo inayoendeshwa chini mradi wa Democratic Empowerment Project (DEP) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kutekelezwa na UNESCO. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Bi. Farida Mgomi.
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Bi. Farida Mgomi, akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Maadili na kuandika Habari za Jinsia na Migogoro kwa waandishi wa habari wa Redio za Jamii iliyofanyika Masasi mkoani Mtwara.
Mshiriki wa warsha Hassan Hassan kutoka Kituo cha Redio Micheweni FM, Pemba, akiwasilisha kazi ya kikundi kazi.
SONY DSC 
ichani juu na chini ni washirki kutoka Redio Jamii za Micheweni, Mtegani, Zenji, Pangani na Fadhila waliohudhuria warsha ya siku 10 iliyofanyika kwenye kituo cha Redio Fadhila FM Masasi.
Rais Kikwete aongoza kuaga mwili wa Mwakapugi Dar

Rais Kikwete aongoza kuaga mwili wa Mwakapugi Dar

May 19, 2014
D92A3800 D92A3809 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho na kufariji familia ya  aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini marehemu Arthur Mwakapugi huko nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam jana.Mwakapugi ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 64 alitumikia taifa kwa miaka 30 mfululizo katika nafasi mbalimbali.Marehemu baadaye alisafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwake Ilundo wilaya ya Tukuyu(picha na Freddy Maro).

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AANZA ZIARA YA KIKAZI NCHINI JAPAN

May 19, 2014

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Biashara, Uchumi na Viwanda wa Japan, Toshimitsu Motegi, (wa kwanza kulia) wakati alipofika ofisini kwa Waziri huyo kwa mazungumzo akiwa katika ziara yake nchini Japan, leo Mei 20, 2014. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibadilishana zawadi na Waziri wa Biashara, Uchumi na Viwanda wa Japan, Toshimitsu Motegi, baada ya mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa Waziri huyo akiwa katika ziara yake nchini Japan, leo Mei 20, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya JETRO, Hiroyuki Ishige, wakati walipokutana na kwa mazungumzo akiwa katika ziara yake nchini Japan, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibadilishana zawadi na Mwenyekiti wa Kampuni ya JETRO, Hiroyuki Ishige, baada ya mazungumzo yao wakati Makamu Dkt Bilal, akiwa katika ziara yake nchini Japan, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Rais wa JAICA, Akihiko Tanaka, yaliyofanyika wakati walipokutana kwa mazungumzo akiwa katika ziara yake nchini Japan, leo Mei 20, 2014. Kulia ni Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Rais wa JAICA, Akihiko Tanaka, yaliyofanyika wakati walipokutana kwa mazungumzo akiwa katika ziara yake nchini Japan, leo.
**********************************************
Na Sufianimafoto Reporter, Japan
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameanza leo ziara ya Kikazi nchini Japan, ziara inayolenga kuongeza ushirikiano baina ya Japan na Tanzania ikizingatia maeneo ya uwekezaji na ubadilishaji wa teknolojia baina ya nchi hizi mbili. Mheshimiwa Makamu wa Rais baada ya kuwasili nchini hapa na kukutana na viongozi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Japan ulio chini ya Balozi Salome Sijaona, alianza ziara hiyo kwa kutembelea Ofisi ya Wizara ya Biashara Uchumi na Viwanda na kukutana na Waziri wa Wizara hiyo Mheshimiwa, Toshimitsu Motegi, ambaye alimfahamisha Mheshimiwa Makamu wa Rais kuhusu maeneo ambayo Japan imekuwa ikishirikiana na Tanzania, sambamba na yale ambayo ingetarajia kushirikiana zaidi katika siku zijazo. 

Akiwa wizarani hapo Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata taarifa kuhusu makampuni ya Japan ambayo yana nia ya kuwekeza Tanzania na kuelezwa namna yalivyojipanga kushirikiana na Tanzania kutimiza azma zao za uwekezaji na pia akatumia nafasi hiyo kuwaeleza kuwa Tanzania inashukuru kuona Japan ikitangaza fursa za uwekezaji nchini Tanzania. 

Pia aliufahamisha uongozi wa wizara hiyo kuwa kwa sasa kuna ushindani mkubwa wa kiuwekezaji nchini Tanzania hasa katika sekta za mafuta na gesi na hivyo kazi ya Tanzania ni kutazama fursa ambazo zitakidhi matakwa ya Wananchi wake na kutoa nafasi kwa makampuni ya kigeni yanayotambua na kuthamini sera za uwekezaji zilizopo nchini huku yakiwa radhi kuchangia katika kupunguza umaskini nchini badala ya kutafuta faida peke yake. 

"Nafahamu kampuni kutoka Japan zina nia njema ya kustusaidia kukabiliana na umaskini wa wananchi wetu, tunashukuru sana kwa moyo huo na karibuni kuwekeza Tanzania," alisema.

Baada ya kikao hicho Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa JETRO, Hiroyuki Ishige, ambaye aliongozana na baadhi ya viongozi wa kampuni hi yo na kuzungumzia nia ya Japan kutanua uwekezaji wa makampuni yao nje ya Japan, sambamba na Makampuni ya Nje kuwekeza Japan. 

Uongozi wa JETRO ulieleza nia yake ya kufungua ofisi ya kuhamasisha uwekezaji nchini Tanzania na ukafafanua kuwa mazungumzo ya kufikia lengo hilo yanaenda vizuri huku wakimtaka Mheshimiwa Makamu wa Rais kuendelea kuwasaidia ili wafanikishe azma hiyo. Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, alifafanua kuwa ujio wa JETRO nchini Tanzania utafungua ukurasa mpya katika uwekezaji na pia utasaidia nchi hizi mbili kudumisha uhusiano wake ambao sasa unaakisi katika masuala ya teknolojia na uchumi.

Sambamba na hilo, Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata nafasi ya kukutana na Ujumbe kutoka JICA, ulioongozwa na Rais wake, Akihiko Tanaka,  ambao uliishukuru serikali ya Tanzania kukubaliana  na miradi mbalimbali wanayoitekeleza nchini Tanzania huku akisisitiza umuhimu wa kukuza ushirikiano baina ya nchi hizi mbili ili wananchi wa nchi zote wazidi kunufaika. 

Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais ambaye katika ziara hii ameambatana na Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe alifafanua kuwa, Tanzania inathamini uhusiano wake na Japan sambamba na mchango wake katika sekta mbalimbali na kwamba Tanzania ina tamaa kubwa ya kuona urekebishaji wa miundombinu yake hasa Reli ya Kati maeneo ambayo yamekabidhiwa kwa Japan yanafanyiwa kazi kwa wakati ili kukuza uchumi wa Tanzania na nchi jirani zinazotegemea Bandari ya Dar es Salaam katika kupitisha mizigo yake.

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI AKAMATWA NA BASTOLA YENYE RISASI 6 MKOANI MANYARA

May 19, 2014
 
JESHI la Polisi mkoani Manyara, linawashikilia watu watano kwa makosa tofauti, likiwemo la Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Chief Sarwati, akiwa na Bastola moja aina ya Chines iliyofutwa namba za usajili pamoja na risasi 6 zikiwa ndani ya magazine kinyume cha sheria

Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo leo Mei 16, 2014, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Deusdedit Nsimeki, amesema katika tukio la kwanza lilitokea Mei 14,2014 ambapo Polisi walimkamata, Said Shabani (16) mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule hiyo, na Lutemba John (22) mkazi wa mkoa wa Kigoma wakiwa na silaha hiyo kinyume na sheria.

PICHA MPYA ZA SUPER STAR KAJALA AKIWA MAFICHONI INASADIKIWA CHINA NA PEDESHJEE

May 19, 2014