*NSSF YATOA SEMINA KUHUSU MAFAO NA UTUNZAJI KUMBUKUMBU KWA MAOFISA UTUMISHI RAS, DED NA MANISPAA

April 25, 2014


 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Crescentius Magori akifafanua jambo wakati wa semina kuhusu mafao na utunzaji kumbukumbu kwa  maofisa utumishi RAS, DED na Manispaa kutoka mikoa yaote ya Tanzania Bara. Semina hiyo imeandaliwa na NSSF na kufanyika leo Mkoani Morogoro. Wa pili kushoto ni Ofisa Rasilimali Watu na Utawala, Chiku Matessa. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Crescentius Magori akitoa mada kuhusu mafao ya muda mrefu ya pensheni ya uzeeni, Pensheni ya ulemavu, pensheni ya urithi pamoja na mafao ya muda mfupi ambayo ni mafao ya matibabu, mafao ya kuumia Kazini, mafao ya uzazi na msaada wa mazishi. Semina hiyo iliandaliwa na NSSF kwa ajili ya maofisa utumishi RAS, DED na Manispaa kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
 Mshiriki wa semina ya maofisa utumishi wa manispaa akisoma kipeperushi cha taarifa za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kabla ya kuanza kwa semina ya maofisa utumishi ilifanyika mjini Morogoro na kuandaliwa na NSSF.
 Maofisa wa NSSF wakiwa katika semina hiyo.
 Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akiuliza maswali.
 Washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada.
 Baadhi ya maofisa Utumishi wakiwa katika semina hiyo.
 Meneja wa NSSF anayeshughulika na Idara za Serikali na Ofisi za Balozi, Rehema Chuma (kushoto), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Chiku Matessa.
 Mshiriki kutoka Kigoma akichangia mada katika semina hiyo.
Maofisa wa NSSF wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo.
 Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
 Mkurugenzi wa Uendesha wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (wa pili kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina kuhusu mafao na utunzaji kumbukumbu kwa  maofisa utumishi RAS, DED na Manispaa iliyofanyika leo mjini Morogoro.
Mkurugenzi wa Uendesha wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (wa pili kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina kuhusu mafao na utunzaji kumbukumbu kwa  maofisa utumishi RAS, DED na Manispaa iliyofanyika leo mjini Morogoro.
MKUU WA MAJESHI AFUTWA KAZI SUDAN KUSINI

MKUU WA MAJESHI AFUTWA KAZI SUDAN KUSINI

April 25, 2014

Generali James Hoth Mai amefutwa kazi na Salva Kiir ingawa Rais huyo hajatoa sababu ya hatua yake
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfuta kazi mkuu wa majeshi yake.
Amri iliyotolewa na Rais kupitia kwa televisheni, ilisema kuwa Generali James Hoth Mai ataondolewa katika wadhifa wake mara moja.
Hata hivyo Rais Kirr hakutoa sababu ya kumfuta kazi generali huyo.
Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na vurugu tangu mwezi Disemba.
Wiki jana waasi waliuteka mji ulio na utajiri mkubwa wa mafuta Bentiu.
Mbali na hayo, umoja wa mataifa ulitoa ripoti iliyohusisha wapiganaji waasi na mauaji ya kikabila.
Na pia imekosoa serikali kwa kutoa taarifa za kupotosha kuhusu mauaji ya halaiki yaliyofanyika mjini Bentiu punde waasi walipouteka mji huo. Mamia wanaaminika kuuawa.
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini,Michael Lueth, hakuwa mkweli alipowaambia wandishi wa habari kuwa wakazi waliokuwa wanatafuta hifadhi katika makao ya Umoja wa Mataifa walizuiwa kuingia katika hifadhi hiyo.
Baada ya waasi kuuteka mji wa Bentiu waliwalenga mamia ya raia wasio na hatia na ambao walikuwa wametafuta hifadhi ndani ya msikiti, kanisa na hospitali na kuwaua kwa misingi ya ukabila
Hata hivyo waasi wanaomuunga mkono makamu wa zamani wa Rais Riek Machar wamekanusha madai ya UN kuwa walihusika na mauaji ya mamia ya raia wasio na hatia huku vituo vya redio katika mji huo vikitumiwa kueneza chuki.

HII NDIYO NYUMBA ALIYOJENGA LULU MICHAEL INAYOTUMIKA KWA KUTAPELI WATU MAENEO YA HUKO KIMARA TEMBONI..!!

April 25, 2014
Mjengo wa staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliopo Mbezi Temboni-Salanga jijini Dar es Salaam umeingia kwenye lawama kufuatia madai kwamba, unatumika kwa kutapeli watu wanaotaka kununua nyumba maeneo hayo.
Mjengo wa staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliopo Mbezi Temboni-Salanga jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kina makazi jirani na nyumba hiyo, baadhi ya watu wanaojiita madalali wamekuwa wakiwapeleka wateja kwa siri kwenye nyumba hiyo ambayo haijaisha na kusema inauzwa na Lulu mwenyewe.
MCHEZO ULIVYO
“Baadhi ya madalali feki wamekuwa wakiwaleta wateja wanaotaka kununua nyumba maeneo haya. Wakifika wanasema Lulu anaiuza, wakiwa wameshaiona wanatoa fedha za usumbufu au za kuwapoza wasipeleke watej wengine na kutoa namba feki ya Lulu ili mteja ampigie.
“Wapo wateja walishanifuata na kusema wanampigia Lulu hapatikani, lakini waliponionesha namba yenyewe si ya Lulu.
“Siku moja mteja mmoja aliletwa na dalali kuiona nyumba, akaipenda, akampa dalali shilingi 300,000 za kumfanya asipeleke wateja wengine, akampigia Lulu hakupatikana. Alipokuja kwangu nikaiangalia namba hiyo ilisajiliwa kwa jina la Mwanahamis nani sijui,” kilisema chanzo hicho.
MAPAPARAZI WAJIFANYA WATEJA, MADALALI WASHTUKA
Mwishoni mwa wiki iliyopita, mapaparazi wetu walijifanya wateja wa kuinunua nyumba hiyo na kwenda kukutana na watu wawili waliodaiwa kuwa ndiyo madalali, Kitwana na Mambeze ‘Mchopa’.
Baada ya mazungumzo, madalali hao walidai kuwa, funguo za kuingia ndani ya nyumba hiyo anazo mama Lulu (Lucresia Karugila) na alisema angefika siku hiyo saa kumi jioni na kuwataka mapaparazi kurudi muda huo.
Wakati mapaparazi wetu wanaondoka, dalali mmoja alisema: “Nyie kama mmekuja kututega mmeliwa wenyewe, hapa hakuna mtoto wa kijijini. Wanaokuja hapa kutaka nyumba wanajulikana, nyie mmetumwa.”
LULU ALISHAFIKA, HAJUI KITU
Sosi mwingine alisema hivi karibuni alimuona Lulu akifika eneo hilo kwa ajili ya kuangalia nyumba hiyo ambayo imesimama ujenzi lakini hakuweka wazi kama alikuwa na nia ya kuiuza!
“Mimi mara ya mwisho nilimuona Lulu eneo hili na gari lake, naona alikuja kuangalia nyumba inaendeleaje na usalama pia. Mambo ya kuwa anaiuza hata siyajui ingawa kweli hata mimi nimekuwa nikiwaona watu wakija,” alisema sosi huyo ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini.
Juzi, gazeti hili lilimsaka Lulu kwa njia ya simu kwa ajili ya kumuuliza kuhusu suala hilo ambapo, awali aling’aka, akasema:
“Wewe ndiyo unaniambia kusema ukweli, sijui chochote. Naomba mnipe habari kwa upana ilivyo maana nyie waandishi mara nyingi mnakuaga wa kwanza kujua habari kuliko mhusika.”

Amani: Wewe Lulu sema ukweli tu, kama unaiuza. Nilichokwambia ndicho.”
Lulu: Kweli mimi siiuzi nyumba yangu wala sina wazo. Huyo aliyewapa habari awape kwa undani ili nijue.”
GPL via swahilitz


RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA HOSPITALI KUBWA NA YA KISASA YA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI KISASA KIJIJINI MLOGANZILA

April 25, 2014

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Balozi wa Korea nchini Mhe Chung IL wakiwa mbele ya mchoro wa mfano wa Hospitali ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe, Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini leo April 2014.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akifurahi na msanii Mrisho Mpoto baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe, Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini leo April 2014. leo April 2014.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chung IL  wakikata utepe kuashiria uwekaji wa  jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe, Kilometa 24 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini leo April 24,  2014.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chungh IL wakiweka udongo kwa pamoja wakati wa kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam,  April 2014.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chung IL na viongozi wengine  wakikata utepe kuashiria uwekaji wa  jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe  Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, April 24, 2014.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mkasi Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Mhe John Mnyika ili na yeye akate utepe na viongozi wengine kuashiria uwekaji wa  jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila mkoa wa Pwani leo April 24,  2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika sherehe za kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila mkoa wa Pwani leo April 2014.

MSEMAJI WA COASTAL UNION AJIUZULU NAFASI YAKE.

April 25, 2014
MIMI Hafidh Athumani Kido, nikiwa na akili timamu natangaza kutojihusisha na shughuli zote za Coastal Union, hasa usemaji wa klabu.

Miongoni mwa sababu nyingi zilizonifanya kutangaza uamuzi huo ni sintofahamu iliyozuka ndani ya klabu yetu, kwa taaluma yangu ya uandishi wa habari lazima niwe na msimamo juu ya mambo yanayoendelea kwenye jamii.

Ili niendelee kufanya kazi na klabu hii kwa wakati huu wa misuguano, lazima niwe na upande; kwa maana upande unaounga mkono uongozi ama upande usiokuwa na Imani na uongozi. Lakini mimi nimeamua kutounga mkono upande wowote.

Kwa hivyo basi, ili niwe katika mstari sahihi nimeamua kukaa pembeni nifanye shughuli zangu za uanahabari kwa furaha na amani.

Bado ni mwanachama halali wa Coastal Union Sports Club, namba yangu ya kadi ni 0013. Nitaendelea kutoa ushauri na kuishabikia klabu yangu ambayo nimekuwa nikimuona marehemu baba yangu na kaka zangu wakiishabikia tangu nikiwa mdogo.

Mtashangaa nimetangaza uamuzi huu wa kuachia ngazi bila kusema kuwa nimeandika barua ama la, kifupi sina mkataba wala taarifa yoyote ya kimaandishi juu ya kuajiriwa kwangu na klabu. Hivyo nimeamua kujiuzulu kienyeji kama nilivyoitwa kienyej