HII NDIO ILIKUWA KAULI YA WAFANYABIASHARA MKOA WA TANGA BAADA YA JOHNSON MINJA KUSHIKILIWA NA POLISI DAR

February 01, 2015



WAFANYABIASHARA mkoa wa Tanga wiki iliyoipita walilazimika kufunga maduka yao kuanzia asubuhi wakishinikiza kuachiwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Johnson Minja anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kuachiwa la sivyo wataendelea na mgomo huo.

Mwenyekiti huyo aliyekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es
Salaam wakati akitokea kwenye kikao cha kuwatetea wafanyabiashara hao kupinga mamlaka ya mapato nchin (TRA) kuwapandishia kodi asilimia 100 wakati wafanyabiashara hao walikubaliana asilimia 2.

Mgomo huo uliweza kuwaathiri wakazi mbalimbali wa jiji la Tanga ambao wanatoka wilayani kufungasha bidhaa na kujikuta wakishindwa kupata mahitaji ambayo yalikuwa wakitegemea kukutokana na hali hiyo.

Mwandishi wa gazeti hili aliweza kutembea kwenye maduka mbalimbali barabara ya kumi na tatu na kumi na mbili kujione namna wafanyabishara hao walivyokuwa nje ya maduka yao yakiwa wamefungwa wakiendelea kupiga soga.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mmoja kati ya wakazi hao,Athumani Jumanne kutoka wilaya ya Pangani alisema kuwa wamepata hasara kubwa kutokana na wao kuingia gharama za kutoka maeneo walipo mpaka kufikia mjini huku wakijua wataweza kufanikisha mipango yao lakini mambo yalikuwa ni tofauti.

Athumani alisema kuwa yeye tegemeo lake kubwa lilikuwa ni kuja kufanya biashara mjini Tanga na kurejea wilayani humo akitegemea malipo atakayoyapata ili aweze kujikimu kwenye usafiri na malazi ili siku inayofuata arejee alipotoka hivyo kufungwa kwa maduka hayo kumemuadhiri sana na hajua nini la kufanya.

Hali kadhalika mfanyabiashara,Alphonce Mboya alisema kuwa kushikiliwa kwa mwenyekiti huyo ni uonevu wanaofanyiwa hivyo kuitaka serikali kuangalia namna ya kumuachia ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku kwa sababu bila ya hivyo wataendelea na mgomo huo.

   “Sisi kama wafanyabiashara tunataka mwenyekiti wetu Taifa aachiliwe popote alipo ili aweze kurejea kwenye utendaji wake wa kila siku…kubwa zaidi tunaiomba serikali kuingilia kati suala hili kwa sababu wafanyabiashara tunanyanyasika “Alisema Alphonce Mboya ambaye ni mfanyabiashara barabara ya tatu jijini Tanga.

Kwa mfanyabiashara, Marry Shio aliiomba serikali kuangalia namna ambavyo wanaweza kuwasikiliza wafanyabiashara kuweza kunufaika na kazi wanazozifanya kuliko kitendo cha kushinikiwa kulipa kodi ambazo hazina maslahi kwao zaidi ya kuwadidimiza.

Shio alisema kuwa kitendo cha Mwenyekiti wao Taifa kushikiliwa na kutokujua mahali sahihi alipo kina wapa uchungu mkubwa kwa sababu serikali haiwezi kumkamata mtu kwa sababu anapiga mfumo wa mashine za mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)EFD.

Akizungumzia mfumo wa mashine za EFD alisema kuwa mashine hizo hazina faida kwao na wala hawatambui mfumo huo kwa sababu unawapa hasara kubwa hivyo wanaiomba serikali kuangalia upya mashine hizo.

    “Wamemkamata mwenyekiti wetu kwa sababu anatetea wanyonge na sisi hatutakubali tutahakikisha tunakuwa naye bega kwa bega mpaka hatua ya mwisho wao ndio walihisi yeye ndio anapinga agizo la kodi hiyo kumbe sivyo “Alisema Marry Shio.

Awali akizungumza kwenye mkutano huo na wafanyabiashara, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tanga(JWT) Peter Amosi alisema kuwa kitendo hicho ni uonevu zidi ya kiongozi huyo ambaye ameonekana kuwa mstari wa mbele kuwatetea wafanyabiashara ambao wanajitafutia ridhiki zao kwa njia ya halali.

Alisema kuwa wao kama wafanyabiashara wanacholalamikia ni tozo kubwa ya kodi kupanda mara mia jambo ambalo linawaumiza watu wengi na kushindwa kupiga hatua za maendeleo na kurudi nyuma kila siku.

Aidha alisema kuwa suala jengine ni malipo ya huduma za faya
extengisha ambapo kila mfanyabiashara ambay ana mlango anatakiwa kulipa elfu arobaini kila mwezi wakati ingeweze kukaa nyumba moja ikaweza kuhudumia maduka yote yanayozunguka nyuma hiyo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »