Waraghbishi wa kijiji cha Nyandekwa na Harakati za Kumkomboa Mwanamke

December 16, 2015
Baadhi ya waraghabishi wa kijiji cha Nyandekwa Wilayani Kahama wakiongea na waandishi wa habari waliofika kijijini hapo kwa ajili ya kujionea matokeo mbali mbali baada ya waraghabishi kuwasaidia wananchi hao kuchukua hatua katika kila jambo kwa maendeleo ya kijiji chao

Pichani nikihoji maswali kwa Dada Miriam Stefano  (Aliyejishika tama ) ambaye amekuwa mchango mkubwa kwa kutoa elimu ya uzazi na mabadilko ya mwili kwa vijana wa kike katika baadhi ya shule za sekondari na msingi katika kijiji hicho 


Picha ya pamoja nikiwa na waraghabishi wa kijiji cha Nyandekwa  Wilayani na waandishi wa habari tuliopata bahati ya kutembelea kijiji hicho na kujifunza namna gani wameweza kuwa chachu ya maendeleo katika kijiji hicho



Na Krantz Mwantepele ,KAHAMA

Mkutano mkuu wa Kijiji cha Nyandekwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga uliofanyika mwishoni wa mwezi wa tisa umeazimia kuwashikinikiza wazazi wa kijiji hicho kuwapeleka watoto wao shule  Azimio hilo Pia limeelekezwa  kwa vijana wanaokaa vijiweni kuwataka kushirki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na sio kukaa vijiweni pia kushiriki katika mikutano mbali mbali ya kijiji kujua maendeleo ya kijiji  Iikihusisha mapato na matumizi.

Mkutano huo umepitisha maazimio matano  yanayolenga kurejesha nidhamu Na heshima kijijini Nyandekwa hatua hiyo imefikiwa Kutokana Na wananchi wa kijiji hiki kutoona umuhimu wao kuchukua hatua za kujikwamua kiuchumi na pia Kuwa na ujasiri wa kuhoji mapato na matumizi kwa ajili ya kijiji chao .



Hali hiyo inatokana na juhudi za dhati bila kukata tamaa zilizofanywa waraghabishi  na watetezi wa haki za binadamu wa kijiji hicho akiwemo Miriam Stefano, Boniface Izengo , Matilda Peter ,Na Mwenyekiti Wa kitongoji cha  Busolwa Bi Ana Alphonce kuwapa ujasiri  na elimu ya uraia wananchi wenzao ili wawe chachu ya maendeleo.



Kwa mujibu wa bi Anna Alphonce ambaye pia ni mwenyekiti wa kitongoji cha   Busolwe aliweza kuongea na mtandao wa Mwanaharakati Mzalendo Blog alisema kupitia mikutano mbalimbali ya kijiji aliweza kutoa hamasa kwa wanawake na wanaume wa kijiji hicho kushiriki katika uchaguzi mkuu uliopita katika kusikiliza sera za viongozi na mwishowe kushiriki kupiga kura.Na kwa muda mfupi aliweza kufanikisha wanawake wengi kushiriki katika maamuzi ya kijiji pia kuwa na ujasiri wa kuhoji katika mikutano ya kijiji.

Wengi wa wanakijji ambao wamekuwa waraghabishi katika kijiji hiki waliweza kupata mafunzo haya ya uraghabishi ambapo waliweza kujua baadhi ya haki zao na kuwa na uajasiri wa kuhoji mapato na matumizi ya kijiji hicho ambapo mwanzoni walikuwa hawapati fursa hiyo kwa wakati .Waraghabishi hawa wamekuwa chachu ya maendeleo ya kijiji cha Nyandekwa katika sekta za kiuchumi ,kisiasa na kijamii kwa kuwaelimisha wanakijiji wenzao haki na wajibu wao kwa nafasi kubwa .

“Viongozi wa kijiji hiki hawakuweza kutupa mrejesho wa kila jambo linalofanyika kwa kijiji hcetu hasa katika mikutano ya kijiji na sisi tulipoanza kuhoji tulikosa ushirikiano kwao lakini mwishowe wananchi wengi waliona umuhimu wa kushirikishwa”   alinukuliwa  bw. Boniface Izengo mmoja wa waraghabishi wa kijiji hiki alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii.

Katika hatua nyingine mmoja wa waraghabishi wa kijiji hiki bi Matilda Peter amekuwa ni mmoja wa vijana wanaotoa elimu ya uzazi wa mpango kwa makundi rika ambapo hukutana na vijana hasa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari na kuwajuza kuhusu mabadiliko ya mwili yao na pia kuwashauri jinsi ya kuepuka maambukizi magonjwa ya ngono na mimba zisizotarajiwa.
 Maazimio yaliyopitishwa kuwa ni vijana wanaokaa au kusimama ovyo barabarani na maeneo mengine bila shughuli maalum kuwajibishwa na pia kuweza kuwawezesha kuwashirikisha katika shughuli za kijiji hicho ikiwemo kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji kijijini hapo
Pia mkutano wa kijiji hiki uliazimia kuwa mapato na matumizi kuweza kujadiliwa kwa uwazi na pia kubandikwa katika mbao za matangazo hapo kijijini kuwezesha wananchi hao kuweza kusoma na kuelewa kila kinachoendelea kijijini kwao katika swala la maendeleo ya uchumi .
.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO ATOA MWELEKEO WA UTENDAJI KAZI WA WIZARA

December 16, 2015

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akizungumza na watendaji wa Wizara ya Ujenzi pamoja na Taasisi zake kuhusu ufanyaji kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia maslahi ya jamii.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akisalimiana na baadhi ya watendaji wa Wizara ya iliyokuwa ya Uchukuzi wakati alipotembelea Wizara hiyo ambayo sasa imeunganishwa na Ujenzi na Mawasiliano.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara hiyo namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili na mikataba wanayoingia iwe kwa maslahi ya nchi.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akiweka sahihi katika kitabu cha wageni huku Katibu Mkuu wa aliyekuwa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi  na Teknolojia Bw. Yamungu Kayandabila akishuhudia.
MO DEWJI FOUNDATION YATOA MSAADA WA MIL. 110/- KWA TAASISI INAYOWASAIDIA WATOTO WENYE KANSA YA TUMAINI LA MAISHA

MO DEWJI FOUNDATION YATOA MSAADA WA MIL. 110/- KWA TAASISI INAYOWASAIDIA WATOTO WENYE KANSA YA TUMAINI LA MAISHA

December 16, 2015
IMG_8716
Meneja Mwendeshaji wa Taasisi ya MO Dewji, Francesca Tettamanzi (kulia) akitoa neno la ukaribisho kwa uongozi wa Taasisi ya Tumaini la Maisha inayohudumia watoto wenye kansa nchini na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kukabidhi msaada wa fedha kwa ajili ya watoto wenye kansa iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za MeTL Group jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mmoja wa Wakurugenzi wa Taasisi ya Tumaini la Maisha, Gerard Mongera na Wa pili kushoto ni Ofisa anayesimamia utekelezaji wa Programu wa Taasisi ya Tumaini la Maisha , Lilian Ndyetabula.
IMG_8726
Afisa Mahusiano wa Taasisi ya MO Dewji, Zainul Mzige (kulia) akisoma taarifa kuhusu madhumuni ya kuanzishwa kwa MO Dewji Foundation pamoja na kazi wanazofanya katika kusaidia jamii ikiwemo sekta ya Afya na Elimu.
IMG_8747
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Tumaini la Maisha, Gerard Mongera (kushoto) akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa MO Dewji Foundation na kuwaomba kuendelea kushirikiana nao wakati wa hafla ya kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 110 kwa ajili ya kusaidia watoto wenye kansa wanaohudumiwa na taasisi hiyo.
IMG_8785
Meneja Mwendeshaji wa Taasisi ya MO Dewji, Francesca Tettamanzi (kulia) akikabidhi mfano hundi ya Shilingi Milioni 110 kwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Tumaini la Maisha inayohudumia watoto wenye kansa nchini, Gerard Mongera (wa pili kushoto) kwa ajili ya kusaidia watoto wenye kansa wanaopata matibabu yao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kushoto ni Ofisa anayesimamia utekelezaji wa Programu wa Taasisi ya Tumaini la Maisha inayohudumia watoto wenye kansa nchini, Lilian Ndyetabula.
IMG_8770
Pichani juu na chini baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za MeTL Group jijini, Dar es Salaam.
IMG_8723
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Taasisi isiyo ya kiserikali ya MO Dewji iliyo chini ya makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group) inayojishughulisha na kusaidia jamii imetoa msaada wa Shilingi Milioni 110 kwa taasisi ya Tumaini la Maisha ambayo inajihusisha na kuwasaidia watoto wenye kansa kupata matibabu pamoja kuwahudumia kwa kipindi chote wanachokuwa katika matibabu.
Akizungumzia msaada huo, Afisa Mahusiano wa MO Dewji Foundation, Zainul Mzige alisema kuwa MO Dewji Foundation imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwa watoto ambao wanagundulika kuwa na kansa kuja Dar es Salaam kupata matibabu na msaada ambao wameutoa wanataraji kuwa utatumiwa vizuri na taasisi hiyo ili kuzidi kusaidia watoto.
Alisema wameshafanya kazi nyingi na Taasisi ya Tumaini la Maisha na wanawatambua katika utendaji wao wa kazi kusaidia watoto ambao wana kansa na msaada huo wa milioni 110 wanataraji utakuwa na faida kubwa kwa kutumika kusaidia watoto waliopo mikoani na hapa Dar ambao wanakutwa wakiwa na kansa na hivyo msaada huo utasaidia kuokoa maisha ya watanzania wengi.
“MO Dewji tumekuwa tukisaidia miradi mbalimbali ya kijamii na kama jinsi tunavyosaidia katika miradi hiyo na leo tunafuraha kutoa Shilingi Milioni 110 za kitanzania kwa Tumaini la Maisha tunaamini ni shirika linalotoa matumaini mapya kwa wagonjwa na familia zao,
“Tumekuwa tukishirikiana nao katika shughuli mbalimbali za kijamii tunafahamu ni jinsi gani wanavyosaidia watoto wenye kansa na kama jinsi tulivyokuwa tunashirikiana nao katika shughuli mbalimbali za kimatibabu na leo tunatoa msaada mwingine ili kuwawezesha kuzidi kuwasaidia watoto hao,” alisema Mzige.
Aidha Mzige alisema kuwa MeTL Group kupitia kwa MO Dewji Foundation wanatambua ni jinsi gani serikali imekuwa ikipambana na ugonjwa huo kwa kuwasaidia watoto wenye kansa na wao wanaahidi kuendelea kuwasaidia kwa kutoa misaada kwa watoto wenye kansa ili waweze kupata matibabu na kuokoa maisha yao.
Awali Afisa Mahusiano huyo alisema kuwa Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji aliamua kuanza kuwasaidia watoto wenye kansa baada ya kukutana na mtoto wa miaka 7 aliyetambulika kwa jina la Zakia mwaka 2012 wakati akiwa mbunge wa Singida Mjini ambaye alikuwa akisumbuliwa na kansa ambayo ilikuwa imeshasambaa mwili mzima.
Mzige alisema Dewji baada ya kukutana na mtoto huyo alimchukua na kumpeleka hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu lakini walikuwa wameshachelewa kutokana na kansa kusambaa mwilini na hivyo mtoto huyo kupoteza maisha hali ambayo ilimfanya Dewji kujitoa kusaidia watoto wenye kansa ili waweze kupata matibabu na kwa mapema kabla kansa haijasambaa zaidi.
Nae Gerard Mongera ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Tumaini la Maisha aliishukuru MO Dewji Foundation kwa msaada ambao wanaowapatia kwa kipindi chote ambacho wamekuwa wakishirikiana na kuitaja MO Dewji kama taasisi ambayo imekuwa ikiwasaidia zaidi hivyo kuwa na matarajio ya kuzidi kushirikiana
Mongera alisema msaada umetolewa na MO Dewji Foundation utatumika kuwasaidia watoto hao kupata matibabu na chakula kwa watoto wanaoumwa kansa walio katika hosteli za taasisi hiyo na walezi wanaowasimamia watoto hao kwa kuwanunulia chakula na mahitaji mengine muhimu ambayo yanahitajika kwa watoto hao.
“Tumekuwa tukishirikiana kwa muda mrefu na MO Dewji Foundation na natumia fursa hii kuwashukuru kwa msaada wanaotupatia wamekuwa wakitusaidia kwa muda mrefu na tunawaomba wazidi kuwa na moyo huo wa kuwasaidia watoto wenye kansa ambao wengi wao wanatoka mikoani na kwa kusaidiana nao tunaamini tutaweza kuwasaidia watoto wengi zaidi,” alisema Mongera.
Mongera aliongeza kuwa tangu mwaka 2013 walipoanza kufanya kazi na MO Dewji Foundation wamefanikiwa kuokoa zaidi ya asilimia 50 ya maisha ya watoto ambao wamekutwa na kansa na kutumia fursa hiyo kuyaomba makampuni mengine pamoja na watu binafsi kujitokeza kuisaidia taasisi hiyo ili kuwa na uwezo zaidi ya kuwahudumia watoto ambao wanakuwa wanasumbuliwa na kansa.

Kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi mjini Shinyanga chapigwa "Tafu " na Tigo

December 16, 2015
table align="center" cellpadding="0" cellspacing="0" style="background-color: white; color: #222222; margin-bottom: 0.5em; margin-left: auto; margin-right: auto; padding: 6px; text-align: center;">
Sehemu ya chakula mchele,unga na maharage tani 3.9,mafuta ya kupikia lita 100 na sabuni katoni 5,kilichotolewa   na kampuni ya mtandao wa simu za mkononi wa Tigo kwa kituo cha kulelea watoto yatima na wenye albinism cha  Buhangija mkoani  Shinyanga





Wafanyakazi wa kampuni ya mtandao wa simu za mkononi wa Tigo  wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto yatima na wenye  albinism katika kituo cha Buhangija mkoani Shinyanga,baada ya  kuwapa msaada,ambapo walitoa mchele,unga na maharage tani   3.9,mafuta ya kupikia lita 100 na sabuni   katoni  5



Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Ali Maswanya akiwakabidhi sehemu ya msaada kwa watoto yatima na wenye albinism katika  kituo cha Buhangija mkoani Shinyanga,ambapo walitoa  mchele,unga na maharage tani 3.9,mafuta ya kupikia lita 100  na sabuni katoni  5

Watoto yatima na wenye albinism cha Buhangija mkoani  Shinyanga,wakicheza kwenye tufe la tigo,baada ya kupokea  msaada wa chakula,ambapo wafanyakazi wa tigo walitoa
mchele,unga na maharage tani 3.9,mafuta ya kupikia lita 100  na sabuni katoni 5




Watoto yatima na wenye albinism cha Buhangija mkoani 
Shinyanga,wakiwa wamevaa fulana za tigo,baada ya kupokea 
msaada wa chakula,ambapo wafanyakazi wa tigo walitoa 
mchele,unga na maharage tani 3.9,mafuta ya kupikia lita 100 
na sabuni katoni 5
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Ali Maswanya akizungumza na  watoto yatima na wenye albinism katika kituo cha Buhangija  mkoani Shinyanga  wakati wa kutoa msaada kwenye kituo cha  kulelea ,ambapo mchele,unga na maharage tani 3.9,mafuta ya  kupikia lita 100 na sabuni katoni 5,kushoto ni Meneja wa Tigo  mikoa ya Shinyanga,Tabora na Kigoma Kamara Kalembo na Meneja  Huduma kwa wateja kanda ya ziwa Beatrice Kinabo(kulia)

Waatalam Wajadili mbinu za kupambana na magonjwa ya mlipuko Arusha

December 16, 2015
Dokta Mwele Malecela wa Kituo cha Utafiti wa Madawa (NIMR) Tanzania akifanya mahojiano jana na baadhi ya vyombo vya habari vilivyoshiriki katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama ukiwemo ugonjwa wa Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko duniani.Warsha hiyoimeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa.
Wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali za barani Afrika na Ulaya wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama kama Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko duniani. Warsha hiyo imeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa. -- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

MAKAMPUNI YA MAWASILINANO YA SIMU YATAKIWA KUBORESHA HUDUMA BORA KWA WATEJA WAO ILI KUONDOA MALALAMIKO

December 16, 2015
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akifungua semina ya kuwaelimisha na kuwahamasisha watumiaji wa Huduma za Mawasiliano  iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC) katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya Desemba 15 -2015 ).Picha Emanuel Madafa  

Mwenyekiti Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za  Mawasiliano (TCRA-CCC)Ndugu Stanley Mwabulambo (kulia) pamoja na Meneja wa Mawasiliano TCRA Kanda ya Nyanda za juu kusini Mhandisi Lilian Mwangoka wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katika ufunguzi wa semina ya kuwaelimisha na kuhamasisha watumiaji wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

Wananchi na baadhi ya watumishi wa serikali na mashirika binafsi wakisikiliza kwa Makini Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro katika semina ya kuwaelimisha na kuwahamasisha watumiaji wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

Watumiaji wa huduma za mawasiliano Mkoa wa Mbeya wakifatilia kwa makini hotuba ya mkuu wa mkoa wa mbeya Abbasi Kandoro.

Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Mariam Mtunguja akizungumza katika semina ya kuwaelimisha na kuhamasisha  watumiaji wa wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 Mwaka huu katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Ndugu Stanley Mwabulambo akitoa neo katika semina hiyo ya kuelimisha na kuhamasisha watumiaji wa Huduma za mawasiliano  Mkoa Mbeya Desemba 15-2015 katika ukumbi wa Mkapa jijini mbeya.

Wadau wakifuatilia mkutano 

Kaimu Katibu mtendaji Baraza la Ushauri watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA-CCC Ndugu  Mary Msuya akiwasilisha maada kwa wanasemina juu ya haki na wajibu wa Mtumiaji wa huduma za Mawasilino  katika semina hiyo yenye lengo la kuelimisha na kuhamsisha watumiaji wa huduma hizo Desemba 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano Mkapa jijini Mbeya.


Mhandisi toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Nyanda za juu kusini Mbeya ( TCRA( Asajile Mwakisisile akitoa maada katika semina hiyo.

Mmoja wa washiriki katika semina hiyo akichangia katika semina .

Mjumbe wa Baraza la Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC) Ndgugu Nyanda Shuli akitoa Maada juu ya Muundo ,Kazi na Majukumu ya Baraza la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano katika semina ya kuelimisha na kuhamasisha watumiaji wa huduma za mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya.

Washiriki wa semina hiyo ya Uhamasishaji na uelimisha wa huduma za Mawasilino wakifuatilia kwa Makini semina hiyo.


Picha ya pamoja na Meza Kuu.

Na EmanuelMadafa,Mbeya(jamiimojablogu )
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameyaasa Makampuni ya  huduma za Mawasiliano ya Simu Nchini kuhakikisha yanaboresha huduma zao  kwa kuhakikisha yanaondoa kero zote anazo kutana nazo mtumiaji wa mawasilino hayo.
Amesema moja ya changamoto inayowakwaza watumaiji wa mawasilino hayo ni pamoja na kuweka matangazo ya simu (Miito ya simu)ambapo hukatwa kiasi cha pesa pasipo makubalino.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro ametoa kauli hiyo jijini Mbeya wakati akifungua semina ya kuelimisha na kuhamasisha watumiaji wa huduma za mawasiliano iliyondesha na Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za mawasilino TCRA-CCC katika ukumbi wa Mkapa jijini humo.
Amesema pamoja na kutambua mchango wa makampuni yanayotoa huduma hizo za mawasiliano katika kuleta maendeleo ,nivyema makampuni hayo yakahakikisha yanatoa huduma zenye ubora wa hali ya juu unaonekana na thamani inayolipwa na watumiaji wa huduma hizo sanjali na kutimiza majukumu yao kwa watumiaji kama yalivyo ainishwa katika sheria na kanuni za leseni.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya amewataka watumiaji huduma hizo za mawasiliano ya simu kujikita katika matumizi bora ya mitandao ya simu badala ya kujingiza katika matumizi yasiyo sahihi ambayo yamekuwa yakichangia kwa kiwango kikubwa kuondoa maadili katika jamii pamoja na uchochezi.
 Amesema kuwa sheria ya makosa ya mitandao nchini namba 14 inaweka wazi juu ya adhabu atakayo weza kutolewa  dhidi ya mtu au kikundi kitakacho husika na upotoshwaji wa aina yoyote .
Amesema sheria ya makosa ya mitandao inaanisha makosa na adhabu zinazohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na teknolojia ya habari na mawasilino.
Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa wa mbeya ametumia fursa hiyo kulitaka baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano TCRA- TCCC  kuendelea  kuhamasisha ,kuelimisha pamoja na kutambua na kuelewa  kero na matalajio ya watumiaji wa huduma za mawasiliano nchi.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano Ndugu Stanley Mwabulambo ametoa wito kwa Makampuni yote yaliyojikita katika uwekezaji wa mawasiliano ya simu ,huduma za utangazaji na huduma za posta kuhakikisha wanaendelea kujenga mitandao ya huduma zao nchi nzima ili kuwawezesha wananchi kushiriki katika maendeleo.
Aidha Mwenyekiti huyo ameviomba vyombo vya habari nchini kusaidia kulitangaza Baraza hilo na shughuli zake ili wananchi wajue ni wapi pa kupata ushauri na kutatua matatizo yao yanayohusiana na huduma za mawasiliano.
Katika semina hiyo pamoja na kutoa elimu kwa watumiaji Baraza pia limeunda kamati ya watumiaji  wa huduma za mawasililiano kwa mkoa wa mbeya ambapo wajumbe wa kamati hiyo walichaguliwa kutoka miongoni mwa wanasemina ambapo majukumu yao yatakuwa ni kuelimishajamii juu ya haki wajibu na utaratibu wa kuwasilisha malalamiko sanjali na kupokea toka kwa watumiaji na kuyawasilisha kwa baraza.

Mwisho.
KAWAIDA