HII NDIO KAULI YA MKUU WA WILAYA YA MUHEZA,SUBIRA MGALU ALIFUNGUA MASHINDANO YA SHIMUTA.

November 24, 2014
TANGA.

MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Subira Mgalu amezionya timu ambazo zinashiriki kwenye michuano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Kampuni Binafsi Nchini (SHIMUTA) kuacha kuchukua wachezaji ambao sio wafanyakazi  kwani kufanya hivyo wanapunguza ladha ya mashindano hayo.

Mgalu aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizundua mashindano ya Shimuta yanayofanyika kwenye viwanja vya Mkwakwani mkoani hapa na kushirikisha wanamichezo wapatao 500 kutoka mashirika na makampuni mbalimbali hapa nchini.

Alisema kuwa michezo hujenga undugu na furaha baina ya wanamichezo hivyo kuwaingia wachezaji ambao sio wafanyakazi kwenye mashindano hayo wataondoa maana halisi ya mashindano hayo jambo ambalo linaweza kuwafanya kushindwa kufikia malengo yao waliojiwekea

  “Mashindano haya ni ya wanamichezo wafanyakazi…kuna wale wanamichezo ambao sio wafanyakazi ambao wanajulikana kama mamluki au wavamizi kwamba hapa sio mahala pao nawasihi tuchezeshe wafanyakazi halisi ili mshindi apatikane kihalali na sio vyenginevyo….. kwa sababu ni hatari sana kumleta mwanamichezo ambaye sio mfanyakazi kwenye michezo hii anaweza kuvunjika mguu au akifa kwa mfano hatuombei itokee hiyo itakuwaje “Alisema DC Mgalu.

Aidha alizitaka timu hizo kuacha kuwatumia wachezaji wa aina hiyo kwani wana madhara makubwa hasa pale yanapokuwa yakijitokeza kwa kuzitaka timu zenye utamaduni huo kuhakikisha wanaondokana nao.

Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya alionekana kukerekwa na baadhi ya menejimenti za Taasisi,Mashirika na makampuni mbalimbali kuwa na utashi wa kutokupenda michezo na wengine kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha kuacha kufanya hivyo badala yake wamuunge mkono Rais Jakaya Kikwete katika jitihada zake za kuinua na kuendeleza michezo hapa nchini.

Akizungumzia waamuzi wanaochezesha mashindano hayo,DC Mgalu aliwataka kuchezesha kwa haki bila upendeleo kwa kufuata sheria za mchezo husika ili mshindi aweze kupatikana kihalali kwa sababu wakienda kunyume chake wanaweza kusababisha tafrani na manung’uniko kwa baadhi ya timu shiriki.

Hali kadhalika aliwataka kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu wakati wote wa mashindano ikiwemo kukubaliana na matokeo pindi watakapojikuta wamefungwa wakati wa mashindano hayo.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu huyo wa wilaya, Mwenyekiti wa Shimuta, Khamis Mkanachi alisema kuwa mashindano hayo msimu huu yanashirikisha timu 20 pungufu ya 22 zilizoshiriki mwaka jana mkoani Dodoma ingawa walijiwekea lengo la kuwa na timu 25 hadi 30 mwaka huu .

Alisema kuwa kupungua kwa idadi ya timu shiriki kunatokana na baadhi ya mashirika kubinafsishwa hali ambayo imepelekea timu nyingi kushindwa kupata nafasi ya kupeleka washiriki wake lakini pamoja na kuwepo hali hiyo shirikisho hilo limendelea na jitihada za ziada kuhakikisha idadi ya timu hizo haipungui bali kuongezeka.

Aidha alizitaja timu hizo kuwa ni  Shirika la Utangazaji  Tanzania (TBC),Chuo Kikuu Huria(OUT),Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE),Kampasi za Mbeya na Dar es Salaam na Mwanza,Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO),Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM),Chuo Kikuu cha Ardhi.

Timu nyengine ambazo zinashiriki mashindano hayo ni Hifadhi ya Taifa Tanzania(TANAPA), Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini(IRDP),Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma(CDA),Chuo Kikuu cha Mzumbe,Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi(MOCU),Chuo kkikuu cha Muhimbili cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS),Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Wengine ambao watashiriki kwenye mashindano hayo ni Baraza la Hifadhi na Usimamizi na Mazingira (NEMC),Shirika la Mzinga,Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Arusha (AICC), Wenyeji wa Mashindano hayo,TANGA CEMENT na Timu mpya kwenye shirikisho hilo ya Bohari ya Madawa(Medical Stores Department(MSD).

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YAKUTANA NA WADAU WA MADINI YA SHABA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YAKUTANA NA WADAU WA MADINI YA SHABA

November 24, 2014

unnamedKamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja (katikati) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa madini ya Shaba. Wengine kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Dominick Rwekaza, Kamishna Msaidizi wa Madini na Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje, Kaimu Kamishna Msaidizi sehemu ya Uongezaji Thamani Madini, Latifa Mtoro na Mwakilishi wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA), John Mvumula.
unnamed2Mfanyabiashara wa madini ya Shaba kutoka Kanda ya Kati Doreen Kisia, akisistiza jambo wakati akichangia hoja katika mkutano huo.
unnamed3Mmoja wa washiriki wa mkutano huo, akiongea jambo wakati akichangia mada kuhusu madini ya Shaba.
unnamed4Kamishna Msaidizi  Kamishna Msaidizi wa Madini na Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje, akisalimiana na baadhi ya wadau wa madini ya Shaba waliohudhuria mkutano huo.
unnamed5Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Dominick Rwekaza, (kulia) akiongea jambo wakati wa mkutano huo

………………………………………………………………………….
Na Asteria Muhozya, Dare s Salaam
Wizara ya Nishati na Madini imekutana na wadau wa madini ya Shaba katika mkutano wa siku mbili ulioanza tarehe 24- 25 Novemba, 2014 na kuwashirikisha wafanyabiashara wa madini hayo, wachimbaji wadogo, viwanda vya kuyeyusha madini ya Shaba, Makamishana Wasaidizi wa Madini kutoka Kanda mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya Maafisa Madini Wakaazi.
Akifungua mkutano huo, unaolenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ndogo ya madini ya Shaba na namna ya kuyaongezea thamani madini hayo, Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja amewataka wachimbaji wadogo nchini kutumia fursa zinazotolewa na Wizara ya Nishati na Madini ikiwemo kupata ruzuku ili waweze kuendeleza shughuli za uchimbaji wa madini jambo ambalo litasaidia kuyaongezea thamani madini hayo.
Aidha, Kamishna Masanja ametumia fursa hiyo, kuwataka wachimbaji na wafanyabiashara kuacha kufanya biashara kinyume na sheria na taratibu kwa kuwa jambo hilo linaikosesha Serikali mapato ikiwemo kuchangia madini hayo kutokupata thamani halisi.
Vilevile Kamishna Masanja ameeleza kuwa, Serikali itaendelea kuzuia usafirishaji madini ghafi ya Shaba na kueleza kuwa, “Haturuhusu madini ghafi ya shaba kutoka nje, tunataka yatoke yakiwa tayari ni madini, kwasababu kuna zaidi ya shaba hivyo tunapoteza, tunataka kuyaongeza thamani madini yetu hapa hapa nchini”, alisisitiza Masanja.

KINANA ATINGA MASASI, ATAKA CCM IENDELEE KUIBANA SERIKALI JUU YA WAFUJAJI WA FEDHA ZA UMMA

November 24, 2014

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi na kuwaambia kila mtu kwenye utumishi wa serikali inabidi awajibike katika kufanikisha lengo na asiyeweza inabidi aachie ngazi alisema lazima tutangulize utumishi kwa umma.
 Kadi zilizorudishwa kutoka kwa wananchama wa vyama pinzani ambao kwa hiyari yao leo wamerudi na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi ya aliyekuwa Katibu Mwenezi wa chama cha NLD Taifa Ndugu Frank Rashid Maulano aliyejiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa jimbo la Lulindi wilayani Masasi.
Wanachama wapya waliojiunga na CCM pamoja na jumuiya zake wakinyoosha kadi zao juu wakati wa kula kiapo cha uanachama mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Chiungutwa wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Machombe ambapo alipita kukagua ujenzi wa Bwawa la maji litakalo saidia kaya 150 kata ya Marika jimbo la Lulindi wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
 Wananchi wa Kijiji cha Machombe wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara wakishangilia wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana anayetembea nchi nzima kukagua miradi mbali mbali ambayo zilikuwa ahadi za CCM.

 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Bwawa la maji akiongozana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mh. Farida Mgomi pamoaja na wanakijiji cha Machombe kata ya Marika.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizorudishwa na wapinzani wakati wa kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Marika wilayani Masasi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Marika ikiwa sehemu ya kujenga na kukiimarisha chama cha Mapinduzi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Chiungutwa jimbo la Lulindi wilayani Masasi ambapo alikagua maendeleo ya mradi wa maji wa Chiungutwa mradi ambao utasaidia vijiji 27,tarafa 3 ambapo watu zaidi ya elfu 60 watanufaika na mradi huo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Chiungutwa wilaya ya Masasi ambapo aliwapongeza kwa kutambua utapeli wa vyama vya upinzani katika kijiji chao na kuamua kujitenga nao kabisa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Chiungutwa ambapo aliwapongeza kwa kuwa na Mbunge mchapa kazi anayejali wananchii wake,Kinana aliwaambia wananchi hao wahakikishe wanajiandikisha tayari kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa.
 Mbunge wa Jimbo la Lulindi ( CCM ) Jerome Bwanausi akihutubia wakazi wa kijiji cha Chiungutwa na kuwaeleza maendeleo ya utekelezaji wa ahadi za CCM kwenye jimbo lake wakati wa mkutano wa hadhara ambao mgeni wa heshima alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Mbunge wa zamani wa mkoa wa Mtwara John Aidi aliyekuwa mbunge wa Mtwara miaka ya 75 mpaka 85 na aliwahi kuwa mbunge wa Masasi miaka ya 65 mpaka 70 akifuatilia kwa makini mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.

NAIBU WAZIRI UMMY MWALIMU ACHANGIA VIFAA VYA UJENZI WA MAABARA KATIKA WILAYA ZA PANGANI NA MKINGA

November 24, 2014

 NAIBU Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga,Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi mabati 50 Mkuu wa wilaya ya Pangani,Hafsa Mtasiwa ikiwa ni jitihada za kuunga mkono ujenzi wa maabara unaondelea maeneo mbalimbali hapa nchini.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Viti Maalumu(CCM)mkoa wa Tanga,Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi kadi Bi Halima Kassim mmoja wa wanachama wapya kwenye kata ya Maramba wilayani Mkinga.

Naibu Waziri  Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM),Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa UWT mara baada ya kuwakabidhi kadi zao waliosimama kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Tanga,Mkuu wa wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga,Al-Shymaa Kwegir

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu ya Rais na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga,Ummy Mwalimu wa nne kutoka kulia akipata maelekezo ya ujenzi wa maabara kutoka kwa mwalimu Cyprian Taabani kutoka Shule ya Sekondari ya Daluni wilayani Mkinga wa kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya Daluni,Mwanakombo Gobeto
Na Amina Omari,Mkinga
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Ummi Mwalimu ametoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya sh Milioni moja na nusu kwa wilaya mbili za Mkinga na Pangani kusaidia ujenzi wa maabara.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na mifuko 70 ya saruji kwa wilaya ya Mkinga na mabati 50 kwa wilaya ya Pangani.
Akikabidhi vifaa hivyo Naibu waziri alisema kuwa lengo kubwa ni kuunga mkono agizo la Rais la ujenzi wa maabara kwa shule zote za sekondari nchini.
"Nimeona na mimi kama waziri mwenye thamana na mwananchi wa Mkoa wa huu kusaidia kuharakisha ujenzi wa maabara katika wilaya hizi mbili"alisema Naibu waziri Mwalimu.
Pia aliongeza kuwa nia ya serikali kuagiza ujenzi wa maabara ni kutaka wanafunzi wanaochukuwa masomo ya sayansi kupata fursa ya kufanya mazoezi kwa vitendo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mkinga Mboni Mgaza alishukuru kwa msaada wa mifuko ya saruji na kusema utasaidi kuharakisha ujenzi huo.
Pia aliongeza kuwa tayari ujenzi wa vyumba vya maabara katika wilaya hiyo umefikia katika hatua nzuri kwani ziadi ya asilimia 70 ya ujenzi imekamilika.
Vile vile mkuu wa wilaya ya Pangani Hafsa Mtasiwa alimpongeza Naibu waziri kwa juhudi zake za kuwaunga mkono kwenye ujenzi huo.
"Kwa msaada huu kwa wilaya ya Pangani tutakuwa tumekamilisha kuezeka vyumba vilivyokuwa havijaezekwa na tunaimani tutakamilisha kwa wakati ujenzi wa maabara"alisema Dc Mtasiwa.
Picha kwa Hisani ya Katibu wa Naibu Waziri,Lulu Mussa
TARATIBU ZA TIBA YA RAIS MH. JAKAYA MRISHO KIKWETE ZAKAMILIKA

TARATIBU ZA TIBA YA RAIS MH. JAKAYA MRISHO KIKWETE ZAKAMILIKA

November 24, 2014

D92A4106
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns
Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika
mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita.Rais Kikwete
anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa
maendeleo ya kidonda na ushauri .Kulia kwake ni Daktari wa Rais
Profesa .Mohamed Janabi
………………………………………………………………….
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI LEO
Taratibu za matibabu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, zimekamilika leo, Jumatatu, Novemba 24, 2014.
Taratibu hizo za matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zimekamilika kiasi cha saa 12 asubuhi ya leo wakati madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, walipomfanyia hatua ya mwisho ya tiba.
Hata hivyo, Rais Kikwete ataendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana na Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku mbili hadi tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.
Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa na madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 29, 2014.
Rais Kikwete aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba 6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake lakini madaktari katika Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya Novemba 8, 2014.
Rais Kikwete anaendelea kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona haraka na kurejesha afya njema katika kipindi chote cha ugonjwa wake.
Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu – Dar es Salaam. 24 Novemba,2014
 WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO

WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO

November 24, 2014


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika  picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa SACCOS ya Katoro, Geita waliotembelea Bunge  mjini Dodoma kwa mwaliko wa  Mbunge wao wa jimbo la Busanda Lolesia Bukwimba  (wapili kushoto kwake)  Novemba 24, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
unnamed1 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza  na baadhi ya wanachama wa SACCOS ya Katoro , Geita waliotembelea Bunge mjini Dodoma Novemba 24, 2014 kwa mwaliko wa Mbunge wao, Lolesia Bukwimba. (Pichana Ofisi ya Waziri Mkuu)

KIWANDA CHA SARUJI,SIMBA CEMENT CHANOGESHA MASHINDANO YA KISASA YA SAMAKI

November 24, 2014
                 





NA SALUM MOHAMED,Tanga.
WIZARA ya Mifugo na Uvuvi Tanga imetakiwa kuongeza doria katika pwani ya bahari ya Hindi  kuzuia vitendo vya uvuvi haramu wa mabomu na utupa  lengo likiwa ni kulinda rasilimali za viumbe hai baharini.

Rai hiyo imetolewa  na washiriki wa mashindano ya wavuvi wa samaki yaliyodhaminiwa na kiwanda cha Saruji cha Simba Cement (TCCL)  na kusema kuwa samaki wengi wametoweka  kufuatia  kushamiri kwa uvuvi haramu.

 Alisema samaki wengi wamepotea na viumbe hai vya baharini kufa kufuatia uvuvi huo ambao umekuwa ukifanyika nyakati za usiku na hivyo kuitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kulikomesha

“‘Boti yetu imeweza kutembea hadi karibu na pwani ya wavuvi kisiwani Pemba na tumerejea na samaki  mmoja tu kwa kweli ni aibu---tulikuwa na vifaa vya kisasa vya kuvulia” alisema na kuongeza

“Sababu ni kuwa bado vitendo vya uvuvi haramu vipo jambo linaloashiria miaka mitano Tanga haitakuwa na samaki na hivyo ni wajibu ya mamkala kulikomesha” alisema Asif Ganighee

Alisema kipindi cha nyuma Tanga ilikuwa kituo kikuu cha uvuaji wa samaki na kuwavitia wachuuzi wa ndani na nje ya nchi na hivyo kuitaka kurejeshwa kwa hali hiyo na kuwezesha uchumi wa Mkoa na wananchi kupanda.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Mtanga Noour, aliwataka washiriki hao kuwa mabalozi wazuri kwa wavuvi wengine ili kuwaweka pamoja na kuzungumza changamoto zinazowakabili.

Alisema wavuvi wengi wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi  za baharini na nje ya bahari na hivyo kuyataka mashindano hayo kuwa chachu ya kuwashirikisha wengine mwakani.

“Sekta ya uvuvi iko na changamoto nyingi na nadhani hakuna kiwakutanishacho kama hiki cha leo----kwa kweli kama tutakuwa na utaratibu kama huu sekta hii itakuwa ni yenye maendeleo” alisema Mtanga

Alisema kiwanda cha Saruji kimekuwa kikisaidia makundi mbalimbali ya kijamii pamoja na sekta ya uvuvi kwa kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuwa wavuvi bora na wa kisasa.

Aliwashauri kila mmoja kuwa askari wa mwenzake katika kukabiliana na uvuvi haramu wa upigaji wa mabomu na utumiaji wa nyavu aina ya kokoro pamoja na utupa ili kuurejesha Mkoa huo katika uvuvi wake wa asili.
DAKTA SHEIN AKIWA KATIKA MKUTANO WA CCM MFENESINI

DAKTA SHEIN AKIWA KATIKA MKUTANO WA CCM MFENESINI

November 24, 2014

IMG_2308  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (kulia) Mwenyekiti wa Wilaya ya Mfenesini Kichama Mjumbe Msuri wakiwa katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha  Mwalimu Nyerere Bububu Kihinani Mkoa wa Magharibi Kichama nje ya Mji wa Unguja katika mkutano maalum wa kuimarisha Chama kwa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani,{Picha na Ikulu.]IMG_2372
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani  katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha  Mwalimu Nyerere Bububu Kihinani Mkoa wa Magharibi Kichama akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM katika Wilaya ya Mfenesini, {Picha na Ikulu.]

Machenja alipania tamasha la NSSF Handeni Kwetu 2014

November 24, 2014

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MSANII wa muziki wa mashairi, Said Machenje, amesema ameanza mazoezi rasmi kwa ajili ya kuhakikisha kuwa anakuwa mmoja wa wasanii watakaotoa burudani kali katika tamasha la NSSF Handeni Kwetu, linalotarajiwa kufanyika katika Desemba 13 mwaka huu, katika Uwanja wa Azimio, mjini Handeni, mkoani Tanga.

Machenje anayeshindana vilivyo na mkali wa muziki huo, Mrisho Mpoto alisema kuwa maandalizi yake yanakwenda sambamba na shauku ya kutembelea kwa mara ya pili wilayani Handeni.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Machenje alisema kwamba mwaka jana alipanda jukwaani kuimba kwa kushirikiana na kikundi cha Naukala Ndima, ila msimu huu amefanikiwa kupata mwaliko wake binafsi.

Mwimbaji huyo wa 'Kajenge kwa Mumeo' na 'Mila', alisema kwa kualikwa binafsi, kunamfanya apate hamu ya kujiandaa kwa ajili ya kufanya mambo makubwa zaidi ili kuonyesha umahiri wake katika tasnia ya muziki wa mashairi.
 
“Nashukuru Mungu kwa kupangwa kuwa mmoja wa wasanii watakaotoa burudani katika tamasha la NSSF Handeni Kwetu 2014, wilayani Handeni mkoani Tanga kwakuwa ni mwelekeo mzuri katika maisha yangu ya sanaa.

“Nafanya mazoezi makali kwa ajili ya kujiweka sawa ili nifanye shoo nzuri Desemba 13, katika Uwanja wa Azimio, ukizingatia kuwa nina uzoefu sasa na jukwaa la tamasha hili la aina yake,” alisema.

Wadhamini tamasha hilo ni Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na Phed Trans, SmartMind & Partners iliyopo chini ya Anesa Co. Ltd kwa kupitia kitabu cha ‘Ni Wakati wako wa kung’aa, Handeni Kwetu Foundation, Wait & Watch Film Company Ltd, Qs Mhonda J Apex Group of Companies Ltd na Skyblue Security and Risk Mgt Ltd na Michuzi Media Group.
 

NSSF YAENDESHA SEMINA KWA WAAJIRI, WANACHAMA

November 24, 2014

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu, amewataka waajiri na wanachama wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kujadili changamoto zinazokabili shirika hilo na kuzitatua. Mkwizu aliyasema hayo mjini Bagamoyo katika semina iliyoandaliwa na NSSF ikiwa ni utaratibu wa shirika hilo kukutana na wadau wake.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu (katikati), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (kulia) na Meneja Idara za Serikali na Balozi NSSF, Rehema Chuma wakiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wakati wa semina ya wadau wa Kada ya Utumishi wa Idara na Asasi za Serikali iliyoandaliwa na NSSF mjini Bagamoyo.


Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori  akitoa akifafanua jambo wakati wa semina ya wadau wa Kada ya Utumishi wa Idara na Asasi za Serikali iliyoandaliwa na NSSF na kufanyika mjini Bagamoyo, mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu, Meneja wa Idara za Serikali na Balozi NSSF, Rehema Chuma  na Meneja wa NSSF Mkoa wa Kibaha, Ummy Lweno. 
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa semina ya wadau wa Kada ya Utumishi wa Idara na Asasi za Serikali iliyoandaliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kufanyika mjini Bagamoyo.
 Meneja wa Idara za Serikali na Balozi NSSF, Rehema Chuma akizungumza katika semina hiyo.
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori  akitoa mada wakati wa semina ya wadau wa Kada ya Utumishi wa Idara na Asasi za Serikali iliyoandaliwa na NSSF na kufanyika mjini Bagamoyo.
 Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
 Washiriki wa semina wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwakilishwa.
 Wadau wa NSSF wakiwa katika mkutano huo.
 Maofisa wa NSSF wakiwa katika mkutano huo.
 Maofisa wa NSSF wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
Meneja wa Idara za Serikali na Balozi NSSF, Rehema Chuma (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Chiku Matesa.
 Mgeni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu akiagana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori mara baada ya kufungua semina ya wadau wa Kada ya Utumishi wa Idara na Asasi za Serikali iliyoandaliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kufanyika mjini Bagamoyo jana. Katikati ni Meneja Idara za Serikali na Balozi NSSF, Rehema Chuma.