Mama Samia Azindua Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS)

Mama Samia Azindua Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS)

June 24, 2017
unnamed
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu cha picha kutoka kwa Kamishna wa Utalii Zanzibar Javed Jafferji wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam.
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha kitabu cha picha alichokabidhiwa na Kamishna wa Utalii Zanzibar Javed Jafferji (kulia) wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia  Kamishna wa Utalii Zanzibar Javed Jafferji alipokuwa akisaini katika kitabu cha picha alichomkabidhi Makamu wa Rais wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam.
3
Mwanzilishi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS), Bw. Abdulsamad Abdulrahim akitoa maelezo kuhusu malengo ya jumuiya hiyo mbele ya mgeni rasmi Makamu Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi rasmi wa Jumuiya hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Mwanzilishi huyo alitoa mchango wa shilingi milioni 25 kama mtaji wa kuanzia wa ATOGS.
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiomba dua wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS).Kutoka kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage na Mwanzilishi wa Jumuiya hiyo Bw. Abdulsamad Abdulrahim.
5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue(kushoto) wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo jana Jijini Dar es Salaam,kulia ni Mwanzilishi wa Jumuiya hiyo Bw. Abdulsamad Abdulrahim. Hafla hiyo iliambatana na uzinduzi rasmi wa Jumuiya hiyo ambayo lengo lake ni kushirikiana na Serikali katika kuwahamasisha wazawa kujihusisha na masuala ya gesi na mafuta ili kuongeza mnyororo wa katika sekta hiyo.
6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Jumuiya ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) mara baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Lengo la Jumuiya hiyo ni kushirikiana na Serikali katika kuwahamasisha wazawa kujihusisha na masuala ya gesi na mafuta ili kuongeza mnyororo wa katika sekta hiyo.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO

MAFUNZO YA SIKU TANO KWA MADAKTARI YALIYOANDALIWA NA WCF YAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM

June 24, 2017

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi Dkt.Kezia, cheti cha ushiriki wa mafunzo ya tathmini ya ajali na majeraha kwa mfanyakazi aliyeumia wakati akitekeleza majukumu yake mahala pa kazi, wakati wa kilele cha mafunzo ya siku tano kwa madaktari kutoka hospitali za umma na binafsi za jijini Dar es Salaam. Jumla ya madaktari 70 kutoka hospitali 35 walishiriki.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAFUNZO ya siku tano kwa madaktari yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), ili kuwajengea uelewa wa namna ya kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi yamemalizika kwa washiriki kutunukiwwa vyeti.
Mafunzo hayo yaliyofunhga na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba makao makuu ya Mfuko huo, jingo la GEPF barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, Juni 23, 2017, yaliwaleta pamoja madaktari 70 kutoka hospitali mbalimbali za umma na binafsi jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yaliyogusa maeneo mbalimbali pia yaliwawezesha madaktari hao kujifunza Muongozo mpya unaohusu namna ya kufanya tahmini kabla ya kumlipa fidia stahiki Mfanyakazi aliepata madhara mahala pa kazi.
Akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw Masha Mshomba, alisema kuwa ni iani ya Mfuko kuwa Madaktari hao wamefaifika na mafunzo hayo na yatawezesha ufanisi katika kjutoa huduma hizo kwa wafanyakazi waliopata magonjwa au kuumia wakati wakiwa

MASHAURI 18 YA MADAI YA KODI YA ARDHI YENYE THAMANI YA BILIONI 1.1 YAWASILISHWA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA WILAYA YA TANGA

June 24, 2017
Mwakilishi wa Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya
Kaskazini, Ardhi Mwandamizi Thadeus Riziki akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu Baraza la Ardhi Mkoani Tanga kupokea mashauri 18 yenye thamani ya Bilon 1.1 ambayo yamefikishwa kutokana wamiliki wa nyumba ,makazi na viwanda  kushindwa kulipa kodi ya ardhi kwa wakati

 Afisa Ardhi Mteule Halmashauri ya jiji  la Tanga Straton Thobias akielezra mkakati wa  mwaka wa fedha wa 2016/7 halmashauri imeweka lengo la  kukusanya kodi ya ardhi kiasi cha shilingi bilioni 2.5 ambapo hadi sasaimefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 2.3
Mwanasheria wa  Ofisi ya Kamishina wa Ardhi Kanda ya Kaskazini  Rosemery Mshana akiwataka wamiliki wa ardhi wanatakiwa kilipa kodi bila shuruti na kwamba kinyume chake watafikishwa mahakamani  mujibu wa kifungu cha  50  cha sheria ardhi namba nne(4
 Mashauri 18 ya madai ya kodi ya ardhi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.1 yamewasilishwa katika Baraza  la ardhi na nyumba  wilaya ya Tanga ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuwabana wamiliki wa viwanja wanao kwepa kulipa kodi.

Akizungumza mara baada ya kuwasilishwa kwa mashuari hayo mwakilishi wa afisa ardhi msaidizi kanda ya kazikazini Thadeus Riziki amesema hatua ya kuwafikisha mahakamani wamiliki wa viwanja  hivyo ni kupata kibali kitakacho wezesha wizara kulipwa makusanyo ya madeni

Amesema baada ya halmashauri kuwapelekea wamiliki hati ya madai na kushindwa kulipa hatua inayofuata ni kuwafikisha mahakamani ili kupata ridhaa ya kisheria ya kukamata mali za wadaiwa.

Kwa upande wake afisa ardhi mteule Halmashauri ya jiji  la Tanga Straton Thobias amesema katika mwaka wa fedha wa 2016/7 halmashauri imeweka lengo la  kukusanya kodi ya ardhi kiasi cha shilingi bilioni 2.5 ambapo hadi sasaimefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 2.3

Akizungumzia zoezi hilo mwanasheria ofisi ya kamishina wa ardhi  Rosemery Mshana amesema wamiliki wa ardhi wanatakiwa kilipa kodi bila shuruti na kwamba kinyume chake watafikishwa mahakamani  mujibu wa kifungu cha  50  cha sheria ardhi namba nne(4)

SHUJAAZ WAWAFUNDA WAANDAAJI WA MASHINDANO YA EAST AFRICA CUP 2017

June 24, 2017
Mkuu wa utafiti wa Kampuni ya Well Told Story,Dkt Anastasia Mirzoyants akitoa maelezo kwa washiriki wa Warsha iliyoandaliwa na  Mradi wa Shujaaz  iliyofanyika Hotel ya Uhuru mjini Moshi.
Baadhi ya Washiriki wa Warsha iliyoandaliwa na watayarishaji wa Mradi wa Shujaaz kwa ajili ya kutoa eimu juu ya maswala mbalimbali ikiwemo Ujasiliamali pamoja na Kilimo,Warsha ambayo inafanyika sambamba na Mashindano ya Kimataifa ya Vijana kwa vijana wa nchi za Afrika Mashariki.
Mkuu wa utafiti wa Kampuni ya Well Told Story,Dkt Anastasia Mirzoyants akitoa maelezo kwa washiriki wa Warsha iliyoandaliwa na  Mradi wa Shujaaz  iliyofanyika Hotel ya Uhuru mjini Moshi
Washiriki katika Warsha hiyo.
Mkuu wa utafiti wa Kampuni ya Well Told Story,Dkt Anastasia Mirzoyants akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumalizika kwa Warsha iliyoandaliwa na  Mradi wa Shujaaz  iliyofanyika Hotel ya Uhuru mjini Moshi

MUFTI MKUU WA TANZANIA AWASILI MKOANI KILIMANJARO KWA AJILI YA SWALA YA EID EL FITRI.

June 24, 2017
Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akiwa katika lango la kutokea eneo la watu mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) alipowasili jana mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya Swala ya Idd El- Fitr inayotaraji kufanika kitaifa mkoani humo.
Mufti wa Tanzania ,Sheakh Abubakary Zubery akitia aini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kilimajaro (KIA).
Mufti Mkuu wa Tanzania ,Sheakh Abubary Zubery akiteta jambo na Sheakh Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Msafara wa Mufti ukitoka katika uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) .
Mufti wa Tanzania ,Sheakh Abubary Zubery akiwa na viongozi pamoja na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wanawake wa Dini ya Kiislamu walipofika kwa ajili ya kumpokea Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery.
Mufti wa Tanzania ,Abubakary Zubery akiwasili katika mmoja wa miskiti iliyopo wilayani Hai kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi. 
Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akifungua kitambaa katika jiwe la Msini kuashiria kuendelea kwa ujenzi wa jingo hilo litakalo tumika kama Madrasa.

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imekabidhi msaada kituo cha watoto yatima mkoani Dodoma

June 24, 2017
Mlezi wa kituo cha watoto cha Rahman Ophanage Centre  cha mjini Dodoma  Shekhe Mohamed Thabiti (kushoto) akipokea masaada wa vyakula kutoka kwa Meneja wa Tigo kanda ya kaskazini inayojumuisha mikoa ya Dodoma ,Singida na Manyara Aidan Komba (kulia)  jana kampuni hiyo iliandaa futari  kwa Watoto wa kituo hicho na  kukabidhi msaada wa vyakula ,mafuta na sabauni vyote vikiwa na  thamani zaidi ya milioni 1.5.


Meneja wa tigo kanda ya kaskazini inayojumuisha mikoa ya Dodoma ,Singida na Manyara Aidan Komba (kulia) akimkabidhi msaada mtoto Halima Bakari kwa niaba ya watoto wa kituo cha kulelea watoto cha Rahman Ophanage Centre  cha mjini Dodoma  jana usiku wakati kampuni hiyo ilipoandaa futari   kwa Watoto wa kituo hicho na  kukabidhi msaada wa vyakula ,mafuta na sabauni vyote vikiwa na  thamani zaidi ya milioni 1.5.

MBOWE AFUTURISHA MISIKITI MINNEJIMBONI KWAKE,WAISLAMU WILAYA YA HAI WAMTUNUKU CHETI.

June 24, 2017
Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Helga Mchomvu wakati wa Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Mbunge huyo katika miskiti minne tofauti.
Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakipata Futari katika msikiti wa Kibaoni wilayani Hai.
Sheakh Mkuu wa wilaya ya Hai,Omar Mohamoud akizungumza wakati wa hafla ya kupata Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Imamu wa Msikiti wa Kambi ya Nyuki ,Fahad Lema akisoma Risala kwa Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe mara baada ya kumalizika hafa ya kupaa futari kwa pamoja katika msikit wa Kibaoni wilayani humo.
Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe akisalimiana na Imamu wa Msikiti wa Kambi ya Nyuki Fahad Lema mara baada ya kuwasilisha ombi la kusaidiwa ujenzi wa vyumba vya madrasa ambapo Mh Mbowe alichangia kiasi cha Sh Mil,2 kwa ajili ya kununua mbao za kuezekea Paa.  
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akisalimana na Waumini katika Msikiti wa Kibaoni uliopo Bomang'ombe wilayani Hai ,mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kupata futari iliyoandaliwa na Mbunge huyo katika miskiti minne tofauti katika jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akipata Futari na waumini wengine katika Msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani Hai baada ya kushiriki pia katika miskiti mingine mitatu .
Mmoja wa viongozi wa Dini ya Kiislamu Mwl Mohamed Mbowe akizungumza wakati akimkaribisha Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe katika Msikiti wa Lambo .
Mjumbe wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaji ,Habib Nasiwa akikabidhi Cheti cha Heshima kwa Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe kwa jitihada zake za kuleta umoja katika Dini na Madhehebu mbalimbali katika wilaya hiyo.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akionesha zawadi ya Cheti alichokabidhiwa na Waislamu katika wilaya ya Hai.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akikabidhi zawadi ya Cheti kwa Diwani wa kata ya Machame Kaskazini,Clement Kwayu ili afungue na kusoma kilichoandikwa ndani.
Diwani wa kata ya Machame Kaskazini,Clement Kwayu (Mwenye suti) akisoma maneno yaliyoandikwa katika Cheti kilichotolewa na Waislamu wa wilaya ya Hai,kwa Mbunge wa jimbo hilo Freeman Mbowe. 
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akishiriki Dua mara baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari iliyoandaliwa katika misikiti minne tofauti ukiwemo msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani Hai.
Baadhi ya wauimini wa Dini ya Kiislamu wakiwasiliza viongozi mara bada ya kushiriki hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Msikiti wa Lambo uliopo Machame ambao Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe amechangia kwa kiasi kikubwa ujenzi wake.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
MBUNGE wa Jimbo la Hai na Kionozi wa Kambi rasmi Bungeni,Mh ,Freeman Mbowe ametunukiwa cheti cha heshima na jamii ya Waislamu katika wilaya ya Hai kutokana na jitihada zake zisizo na ukomo katika kuleta umoja katika Dini na Madhehebu mbalimbali.
“Tunaamini katka Uhuru wa kuabudu na kujieleza ,malumbano ya hoja na mijadala ,Kuvumiliana na kusamehe, Vitisho ,ugandamizaji  na uonevu wa aina yoyote vinaweza kuendelea lakini havitaweza kushinda jamii yetu. Uhuru ni tunu ya sili tuliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu” yalieleza maeno yaliyopo katika Cheti hiycho.
Mh Mbowe alikabidhiwa cheti hicho na Mjumbe wa Baraza Kuu la Waisalmu (BAKWATA) Alhaji Habib Nasiwa , katika msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla ya kushiriki futari iliyoandaliwa na mbunge huyo katika misikiti minne tofauti ya Modio ,Rundugai,Kibaoni na Lambo.
Cheti hicho kilichosainiwa na Sheakh Mkuu wa wilaya ya Hai,Sheakh ,Omary Mahmoud ambaye pia ni katibu wa msikiti wa Kibaboni Bomangombe kimetolewa ikiwa ni ni ishara ya kutambua mchango mkubwa unatolewa na Mbunge huo kwa Waislamu.
AkIzinunguza mara baada ya kukabidi cheti hMjumbe wa Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaji Habib Nasiwa alitoa shukrani kwa niaba ya waislamu wa jimbo la Hai kwa namna ambavyo ameendelea kujitoa pamoja na kuchangia ujenzi wa msikiti wa Lambo.
“Nimehemewa sana ,sidhani kama naweza kusema kiasi cha kutoshereza ,nimehemewa na kujaaa furaha ya kufikiwa na Mh Mbowe,halikua jambo rahisi la kumpata leo ,kwanza tukijua Bunge linaendelea kadharika tukijua kwamba ana majukumu mengine mengi lakini akaona ashiriki na sisi wilaya ya Hai.”alisema Nasiwa.
“Jambo fupi la kukushirikisha jioni ya leo,mheshimwa tunakupongeza kwa kujua umuhimu wa ramadhan kwa kuacha shughuli zako na kuja kushiriki nasi katika kutufuturisha,tunakupa asante sana na mungu akubariki sana,”aliongeza Alhaji Nasiwa.
Katika hafla hiyo ya kufuturisha ,Mh Mbowe alishiriki katika misikiti yote minne ambapokatika msikiti wa Mudio alitoa mifuko 100 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya msingi inayomilikiwa na msikiti huo na pia alikabidhi kiasi cha sh Mil moja kwa msikiti wa Rundugai kwa ajili ya mwalimu anayefundisha masomo ya dini katika shule ya Msingi na Sekondari za Rundugai .