Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, atimiza ahadi kwa wananchi wa Nyamongo

November 06, 2013

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifafanua jambo wakati wa kikao maalum cha ndani na wakazi wa eneo la Nyamongo, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa wakieleza kero zao na wamiliki wa mgodi wa North Mara .
 Ndugu Elizabeth Malembela akielezea jinsi utaratibu ulivyombovu wa kuwahamisha na kuwalipa fidia wakazi wanaoishi kando kando ya mgodi wa North Mara.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisikiliza kwa makini malalamiko ya wananchi wa Nyamongo juu ya ukiukwaji wa utaratibu na mikataba baina ya wawekezaji na Wanavijiji.
 Mkuu wa Wilaya ya Tarime Ndugu John Henjewele akiwaelezea wakazi wa Nyamongo kazi za kikosi kazi (Task force) katika kurahisisha shughuli za kutathimini ardhi na kuchukua malalamiko ya wananchi dhidi ya wawekezaji wa mgodi wa North Mara.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye akiangalia moja ya eneo linaloaminika kutiririsha maji yenye kemikali kutoka kwenye Mgodi wa North Mara kwenda kwenye mto Mara na kuhatarisha afya za wananchi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia kwa karibu kabisa maji ya kemikali kutoka machimbo ya mgodi wa North Mara kuelekea mtoni.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma jiwe la msingi la ofisi ya Kikundi cha Bodaboda Nyamongo mara baada ya kuzindua ofisi hiyo.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Ndugu Amos Sagara Nyabikwi akihutubia wakazi wa Nyamongo wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliwaelezea wananchi wa eneo hilo hatua za awali za kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao zilivyoanza.
 Mkurugenzi wa Kushughulikia Malalamiko dhidi ya Jeshi la Polisi,Magereza,Uhamiaji,Zimamoto na Uokoaji Ndugu Agustine D. Shio akihutubia wananchi wa Nyamongo na kuwaambia amesikia malalamiko yao dhidi ya Jeshi la Polisi na atalifanyia kazi mapema iwezekanavyo na haki zitapatina.
 Sehemu ya Wakazi wa Nyamongo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi nape Nnauye.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nauye akihutubia wakazi wa Nyamongo wilayani Tarime na kuwaelezea jinsi alivyoanza rasmi kazi ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili wananchi wa Nyamongo

MATUKIO YA PICHA KATIKA MKUTANO WA WADAU WA MFUKO WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA UKIJUMUISHA WADAU TOKA NHIF NA CHF .

November 06, 2013

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Ole Kuyan akimkabidhi mashuka 150 Sister Magldlena Moro  wa kituo cha Afya cha Tumaini cha mjini Tanga baada ya kufanyika kongamano la wadau wa Mfuko wa Bima ya Afya lililofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga


Mwanachama wa Bima ya Afya mkazi wa Kilindi Mkoani Tanga, Thomasi Mzinga akitoa mchango wake wa kuboreshwa kwa huduma za Afya hasa vijijini katika kongamano la wadau wa Bima ya Afya lililofanyika jana katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Mwanachama wa mfuko wa Bima ya Afya Mustafa Beloka mkazi wa Mikanjuni Mkoani Tanga akichangia katika kpongamano la wadau wa Bima ya Afya lililofanyika jana katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, Mboni Mgaza akizungumza katika kongamano la wadau wa mfuko wa Bima ya Afya lililofanyika jana katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

WAZEE WAIOMBA SERIKALI KUWAONGEZEA FEDHA ZA PENSHENI

November 06, 2013


WAZEE wastaafu  ambao walikuwa watumishi wa Umma wameitaka Serikali kuwaongezea  fedha  za  Pensheni kutokana na kwamba  gharama za maisha zimepanda hivi sasa.

Sambamba na hilo pia wastaafu hao wapatao 5000 katika wilaya hiyo wameitaka Serikali kuwaeleza kwa nini wanacheleweshewa malipo yao ya pensheni hawapati  kwa wakati unaotakiwa.

Hayo yamesemwa na wastaafu hao katika kikao chao kilichofanyika katika ukumbi wa Bomani ambapo mgeni rasmi alikuwa Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) wilayani Muheza, Laick Gugu.

Akizungumzia kuhusu ongezeko la Pensheni Ibrahim Shemdoe amesema kuwa Serikali ilishatoa agizo kule hazina toka mwaka 2009 kwamba wastaafu waongezewe pensheni lakini mpaka sasa hawajapata kitu.

Shemdoe amesema kuwa Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo pamoja na Rais Jakaya Kikwete walishatoa agizo wastaafu hao waongezewe pensheni lakini maagizo yao yamedharauliwa.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika mkutano huo, Gugu amesema kuwa kama wataanzisha umoja huo wa wazee wastaafu basi waanzishe Chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) na atawachangia sh.milioni 1 ya kufungua akaunti huku akisema pia itakuwa rahisi kuchangiwa na watu wengine.