Tigo wafanya usafi mkoani Morogoro

February 06, 2017


 Meneja wa mauzo -  Tigo mkoa wa morogoro, Abbas Abdulrahman(aliyeshika fagio mbele kushoto)  akishiriki zoezi la usafi na wafanyakazi wa tigo sambamba na wa Redio Africa swahili fm  katika eneo la stendi ndogo ya daladala  mkoani Morogoro juzi.


Wafanyakazi wa Tigo Morogoro na wafanyakazi wa Redio Africa swahili fm wakishiriki katika usafi wa pamoja kwenye stendi ndogo ya daladala mkoani Morogoro juzi.

Vyama vya Siasa Vyatakiwa Kutoa Fursa za Uongozi kwa Wanawake

February 06, 2017
Afisa Programu na Uchambuzi wa TGNP, Deogratius Temba (kulia) akiwasilisha mada katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni. Semina hiyo liyofanyika Mabibo Jijini Dar es Salaam iliandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Afisa Programu na Uchambuzi wa TGNP, Deogratius Temba (kulia) akifafanua jambo katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni. Semina hiyo liyofanyika Mabibo Jijini Dar es Salaam iliandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakichangia mada anuai katika Semina hiyo Sehemu ya washiriki wa semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakifuatilia mada anuai. Semina hiyo liyofanyika Mabibo Jijini Dar es Salaam iliandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakiwasilisha kazi za vikundi baada ya majadiliano. Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakichangia mada anuai katika Semina hiyo. Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakichangia mada anuai katika Semina hiyo.

 BAADHI ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya Tatu za Mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wameviomba vyama vya siasa kutoa fursa za uongozi kwa wanawake ili waongezeke katika nafasi za uongozi ngazi mbalimbali. 

Ombi hilo limetolewa na viongozi hao katika maoni yao walipokuwa katika semina kuangalia usawa wa kijinsia katika nafasi mbalimbali za uongozi iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). 

Baadhi ya viongozi hao na watendaji walisema kumekuwa na changamoto nyingi ndani ya vyama vya siasa ambazo zinaendelea kuwa vikwazo kwa wanawake kushiriki katika nafasi za uongoni katika vyama anuai, hivyo kama zikiangaliwa zinaweza ongeza hamasa kwa wanawake kupata nafasi za uongozi.

CCM KIGOMA YAVUNA WANACHAMA WAPYA 868 AKIWEMO MWENYEKITI WA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO NA CUF WILAYANI KAKONKO

February 06, 2017





CHAMA Cha CCM Mkoa wa Kigoma kimevuna jumla ya Wanachama wapya 868 kutoka vyama mbalimbali vya siasa akiwemo mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo Venasi Busunzu wa wilaya ya Kakonko na Mwenyekiti wa CUF Kilembwe Omari mgombea udiwani kata ya Sinuka wamekabidhiwa kadi ya chama hicho jana, katika hitimisho ya sherehe za madhimisho ya kutimiza miaka 40 ya CCM.

Akihitimisha sherehe hizo jana zilizo fanyika Kimkoa Katika kijiji cha Mwakizega Wilayani Uvinza Mwenyekiti wa CCM kigoma Amani Kabourou , alisema katika maazimisho waliyafanya Mkoa mzima katika Wilaya zote walipatikana wanachama wapya 726 na kutoka vyama vya upinzani ni wanachama 146 ambao walikabidhiwa kadi katika sherehe za maazimisho zilizo fanyika jana katika Kijiji cha Mwakizega kata ya Mwakizega Wilaya ya Uvinza.

Alisema wanachama hao Waliamua kurudi katika Chama hicho kutokana na Shughuli kubwa zinazo fanywa na chama hicho , ambapo mpaka sasa kuna Maendeleo Makubwa yaliyo fanyika katika Kipindi cha Mwaka mmoja cha uongozi wa serikali unaongozwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Kabourou alisema Kwa sasa Viongozi wa chama hicho wameweka mikakati wa kukisafisha chama hicho kwa kuondoa viongozi wote wasio na sifa wanaokichafua sana na kuifanya CCM kuwa mpya na Serikali mpya kutokana na Misingi iliyo wekwa na waanzirishi wa Chama hicho.
Akizungumzia hatua hiyo, aliyekuwa mwenyekiti wa ACT wazalendo Bususnzu alisema amegundua mapungufu makubwa katika chama cha awali hali ,iliyomshawishi kujiunga na ccm ni pamoja na viongozi kuhamasisha misuguano kwa jamii ,ili nchi isitawalike lakini kwa awamu ya serikali ya wamu ya tano ya John Magufuli ni kigezo cha upinzani kukubali uwajibikaji wake wenye tija kwa wananchi.

Akizungumzia hilo Kilembwe Omari alisema amerudi kundini akiwa na wananchama 34 kutoka chama cha ACT wazalendo ,akidai amerudi kwa baba na mama yake akiwa na wenzake hao,sababu aminiye na kubatizwa ameokoka na anatumaini atakuwa mumini mzuri wa chama hicho.

Akiongezea hilo Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF,wilaya ya Kakonko Amana Ramadhani alisema anapokea kadi kwa hiari japokuwa amekulia katika upinzani akiwa mwenyekiti wa kina mama kwa miaka 15 wa chama cha CUF,kwa sababu ya sera zake akijua kitawakomboa wananchi,kumbe kipo kwa ajili ya kupata ruzuku ya serikali.

Alisema tangu mwaka 1990 wapo wanachama wawili hali inayokwamisha jitihada za kuleta maendeleo ,awali aliamini ujio wa UKAWA ni kuimarisha vyama lakini kilichotokea ni ubaguzi wa udini na kugombea maslai binafsi na si wananchi,hivyo hana budi kujiunga na ccm ili kutimiza ndoto za kuinua uchumi .

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Emanuel Maganga alisema kwa awamu ya tano ya serikali ya leo,imetatua kero mbalimbali za wananchi,hususani katika sekta ya elimu kigoma imepiga hatua 2015/16 wilaya ya kakonko ilishika nafasi ya kwanza matokeo ya kidato cha pili na kidato cha sita kigoma ilishika nafasi ya kwanza kitaifa.

Maendeleo hayo ni pamoja na sekta ya miundombinu ya barabara ,miradi ya maji zimetengwa kiasi cha sh.milioni 10 kwa kila wilaya ya kigoma kwa ajili ya kukamilisha miundombinu ya maji iliyokuwa ikisuasua sanjari na umalizwaji wa barabara ya Kidahwe hadi kasulu na nyakanazi Kakonko huku Uvinza hadi Tabora fungu la fedha zimepangiwa bajeti katika mwaka wa 2016/17.

SALAMU ZA POLE NA RAMBIRAMBI KUTOKA CCM

February 06, 2017
SALAMU ZA POLE NA RAMBIRAMBI
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu saba wakiwemo viongozi na wanachama wanne wa CCM ambao ni Ndg Ally Mmbaga, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa, Ndg Arnold Swai, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Hai, Ndg Anastazia Innocent Malamsha, Mwenyekiti wa UWT Tawi la Chuo Kikuu cha Ushirika (Moshi) na Ndg Edwin Msele, Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Kilimanjaro vilivyosababishwa na ajali ya barabarani katika eneo la Mwika, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoa wa Kilimanjaro siku ya Jumapili ya tarehe 05th Februari 2017.

Ajali hiyo ilitokea majira ya jioni ikihusisha gari ya mizigo aina ya Fuso na Toyota Hilux Surf iliyokuwa imewabeba Viongozi wa CCM waliokuwa wakitoka katika kutekeleza majukumu ya Chama ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya Kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kimkoa Wilayani Rombo na kusababisha vifo vyao.

Kutokana msiba huo, Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Ndugu Iddy Juma, familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wanachama wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro kufuatia vifo vya Viongozi wetu. 

Wana CCM nchi nzima, tunawaombea majeruhi kupona haraka, na tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke mahali pema roho za Marehemu.  Amina.
Imetolewa na,

HUMPHREY POLEPOLE
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA, ITIKADI NA UENEZI
06/02/2017.