KAMPENI YA KUTOKOMEZA MARADHI YA FISTULA YATUA WILAYA YA KIBONDO

May 31, 2015

Mkazi wa Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma Esther Batolomea akisoma kipeperushi chenye ujumbe wa maradhi ya Fistula wakati wa kampeni ya kutokomeza maradhi hayo iliyofanyika wilayani hapo. Hospitali ya CCBRT kwa kushirikiana na Vodacom Foundation zinatoa elimu kwa Umma kupitia kampeni inayozunguka mikoa mitatu nchini kuwasisitiza wanawake wajitokeze wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wa kujifungua.
Wakazi wa Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma wakisoma vipeperushi vyenye ujumbe wa maradhi ya Fistula wakati wa kampeni ya kutokomeza maradhi hayo iliyofanyika wilayani hapo. Hospitali ya CCBRT kwa kushirikiana na Vodacom Foundation zinatoa elimu kwa Umma kupitia kampeni inayozunguka mikoa mitatu nchini kuwasisitiza wanawake wajitokeze wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wa kujifungua.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kumwamba iliyopo Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma walijumwika na wakazi wa wilaya hiyo katika viwanja vya Community Centre wakimsiliza Meneja Biashara wa Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Grace Lyon wakati alipokuwa akiwafafanulia jambo kuhusiana na maradhi ya Fistula. Wakati wa kampeni ya kutokomeza maradhi hayo inayoendelea kufanyika katika mikoa mitatu nchini,Kampeni hiyo inaendeshwa na Hospitali ya CCRBT kwa kushirikiana na Vodacom Foundation. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wa kujifungua.
Balozi wa maradhi ya Fistula nchini Msanii Mrisho Mpoto alimaarufu”Mjomba” akitoa elimu kwa wakazi wa Kibonda kuhusiana na maradhi ya fistula na kuwasihi wakina baba kuwaruhusu wake zao wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Alitoa elimu hiyo wakati wa kampeni inayoendeshwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na CCBRT ya kutokomeza maradhi hayo inayoendelea katika mikoa mitatu nchini. Inakadiriwa wastani wa wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wanapojifungua.

MWANAHABARI DEOGRATIAS MONGELA ALIVYO UKACHA UKAPERA

May 31, 2015

 Mwanahabari Deogratias Mongela wa Kampuni ya Global Publishers Ltd.
 Bibi Harusi, Elizabeth Sanga.
 Deogratias Mongela akiwa na mke wake Elizabeth Sanga wakati wa hafla ya ndoa yao iliyofanyika Hoteli ya Atriums iliyopo Sinza Afrikasana baada ya kufunga ndoa Katika Kanisa la Katoliki, Parokia ya Mbezi Luis Dar es Salaam jana.
 Maharusi hao (katikati) wakiwa na wapambe wao kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Cobson Nzige na mke wake Subira Nzige (kulia), 'hakika wamependeza si mnawaona'.
 Bibi harusi Elizabeth Sanga akiteta na mpambe wake Subira Nzige.

AFRICAN SPORTS KUINGIA KAMBINI JUNI 3.

May 31, 2015
KLABU ya African Sports “Wanakimanumanu”inatarajiwa kuingia kambini Juni 3 mwaka huu kwa ajili ya kujiwinda na Michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao baada ya kupanda kucheza daraja hilo.

 Akizungumza jana, Katibu wa timu hiyo, Khatib Enzi aliliambia gazeti hili kuwa wameamua kuingia kambini mapema ili kuhakikisha wanakiandaa vema kikosi chao kwa ajili ya kuhimili mikimiki ya Ligi kuu ikiwemo kupata matokeao mazuri.

Enzi alisema kuwa wachezaji wa timu hiyo waliopo nje ya mkoa wa Tanga kwa sasa watalazimika kutua mkoani hapa Juni Mosi mwaka huu tayari kuungana na wenzao katika kambi yao itakayokuwepo Kata ya Usagara jijini Tanga.

     “Kuanza kambi mapema ni miongoni mwa mipango yetu ya kuhakikisha tunakiandaa kikosi chetu vyema kwani Ligi kuu sio lelemama hivyo inahitajika kujipanga vema “Alisema Enzi.

Katika hatua nyengie,Enzi alisema kuwa usajili ambao wataufanya kabla ya kuanza michuano hiyo utakuwa ni katika nafasi za mlinda mlango, kiungo wa kati na washambualiaji ambao tayari kamati ya usajili ya timu hiyo imeshaanza kazi ya kuhakikisha nafasi hizo zinapata wachezaji makini watakaoiletea maendeleo.

Alisema kuwa msimu ujao wamepania kufanya usajili wa nguvu ambao utawawezesha kurudisha enzi zao za zamani wakati walipopanda daraja na kuchukua ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara.

Hata hivyo alisema kuwa klabu hiyo imekwisha kuwafungashia virago wachezaji sita ambao ni Gerary Samburu, Khasim Mkele, Eddy Zaharani, Nyanda Kazioba, Shingwa na Evarist Mujwahuki ambao wapo huru.

SERIKALI YAKARIBISHA WAWEKEZAJI BINAFSI KWENYE SEKTA YA UCHUKUZI

SERIKALI YAKARIBISHA WAWEKEZAJI BINAFSI KWENYE SEKTA YA UCHUKUZI

May 31, 2015

uc1
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2015/2016 bungeni mjini Dodoma leo.
uc2
 Mbunge wa Kisarawe (CCM) Bw. Suleiman Jafo akichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya uchukuzi leo bungeni mjini Dodoma.
…………………………………………………………….
Na Fatma Salum – Maelezo
Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imesema inakaribisha wawekezaji binafsi kwenye miradi mbalimbali ili kuboresha sekta za uchukuzi na hali ya hewa hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. Charles Tizeba wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge zilizowasilishwa kwenye mjadala wa bajeti ya wizara hiyo leo bungeni mjini Dodoma.
“Serikali inawakaribisha wawekezaji binafsi kuwekeza kwenye miradi ya kuboresha miundombinu ya uchukuzi na hali ya hewa kwa kuwa Serikali peke yake haiwezi kukamilisha miradi yote bila ya ushirikiano na wengine”
Dkt. Tizeba alisema Serikali ina mipango madhubuti ya kuboresha miundombinu nchini ikiwemo reli, bandari na barabara na kupitia dhana ya ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi (Public Private Partnership) itaweza kufanikisha mipango hiyo kwa ufanisi na kwa wakati.
Aidha Dkt. Tizeba aliongeza kuwa kupitia juhudi za Serikali baadhi ya miradi ipo katika hatua za awali ikiwemo uboreshaji wa viwanja vya ndege 11 kwenye mikoa mbalimbali nchini ambapo wataalamu wameshafanya upembuzi yakinifu (Feasibility Study) na fedha zikipatikana vitafanyiwa matengenezo mara moja.
Akizungumzia upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam Dkt. Tizeba alibainisha kuwa taratibu za kumpata mzabuni zinaendelea na akipatikana ujenzi wa gati namba 13 na 14 za bandari hiyo utaanza.
Leo Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta aliwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2015/2016 ambapo bunge lilikubali kupitisha zaidi ya shilingi bilioni 452.9.