KENYA,SHELISHELI KUSHIRIKI BONANZA LA MCHEZO WA BAISKELI JIJINI TANGA

April 04, 2018



WAENDESHA Baiskeli kutoka nchini za Kenya na Visiwa vya Shelisheli wanatarajiwa kushiriki kwenye bonanza la mchezo huo ambalo litafanyika mkoani Tanga mwanzoni mwa mwezi wa sita mwaka huu.

Akizungumza na Tanga Raha Blog, Mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli Mkoani Tanga (CHABATA) Dege Masoli alisema licha ya nchi hizo kushiriki lakini pia mikoa mbalimbali ya Tanzania bara nayo itashiriki.

Alisema lengo la bonanza hilo litakuwa ni kunua na kusaka vipaji vya wachezaji wachanga wa mchezo huo ili kuweza kuona namna ya kuwajengea uwezo waweze kuwa wachezaji wazuri siku zijazo.

“Kwa kweli kama unavyojua sisi kama chama tumeona tuanzisha bonanza hili na kuzialika nchi jirani na mikoa kwa lengo la kuweza kuinua mchezo huo mkoani hapa na hili tunadhani linaweza kutupa mafanikio siku zijazo”Alisema Dege Masoli.

Hata hivyo alisema kwenye bonanza hilo zaidi ya wachezaji 300 wanatazamiwa kushiriki ambao watapata fursa ya kuweza kuonyesha vipaji vyao huku akiyaomba makampuni mbalimbali kujitokeza kufadhili.

COASTAL UNION KUTUMIA MILIONI 200 KUSAJILI WACHEZAJI

April 04, 2018


MABINGWA wa Ligi kuu soka Tanzania bara mwaka 1988 Coastal Union wanatarajiwa kutumia milioni 200 kwa ajili ya kufanya usajili wa wachezaji wa ndani na kigeni ili kuweza kukitumikia kikosi hicho.

Akizungumza na Tanga Raha Blog,Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa timu hiyo,Hafidhi Kidoh alisema wanakusudia kutumia kiasi hicho cha fedha ili kuwea kukithi mahitaji ya kikosi chao msimu ujao.

Alisema fedha hizo ni nyingi hivyo wanakusudia kuangalia namna ya kusaka wadhamini ambao watawasaidia kwenye mchakato huo wa kupata wachezaji watakaowasajili kwa ajili ya kuichezea timu hiyo kongwe hapa nchini.

“Kama unavyojua hivi sasa tupo kwenye harakati za kusajili wachezaji lakini pia kusaka wadhamini ambao watatuwezesha kutimiza malengo hayo kwani kwa makadirio yetu tunatarajia kutumia milioni 200 kusajili Alisema.


Hata hivyo aliwataka wadau mbalimbali kujitokeza kuiunga mkono timu hiyo ili iweze kutimiza malengo yao waliojiwekea ya kushiriki vema michuano hiyo na hatimaye kuweza kuchukua Ubingwa.

WAZIRI KIGWANGALLA KUONGOZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA UPANDAJI MITI KITAIFA KESHO MKOANI SHINYANGA

April 04, 2018

Wateja 676 wa Tigo wajinyakulia simu janja za TECNO R6 na bonasi za intaneti bure baada ya kununua bando za intaneti kupitia *147*00#

April 04, 2018
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) na Mtalaam wa Bidhaa wa Tigo,  Jacqueline Nnunduma (kulia) wakiongea na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi zawadi za simu janja aina ya Tecno R6 kwa washindi wa promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu 676 bure pamoja na bonasi za intaneti hadi GB 1 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00#. 



Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (aliyesimama kulia) akimkabidhi Gladness Mori (alieyeketi)

zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus huku akitazamwa na baadhi ya washindi wengine wa promosheni hiyo. Tigo imetoa jumla ya simu 676 bure pamoja na bonasi za intaneti hadi GB 1 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00#.


Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (aliyesimama kulia) akimkabidhi Diana Pumpuni zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus huku akitazamwa na baadhi ya washindi wengine wa promosheni hiyo. Tigo imetoa jumla ya simu 676 bure pamoja na bonasi za intaneti hadi GB 1 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00#.



Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (aliyesimama kulia) akimkabidhi Charles Shabani zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus huku akitazamwa na baadhi ya washindi wengine wa promosheni hiyo. Tigo imetoa jumla ya simu 676 bure pamoja na bonasi za intaneti hadi GB 1 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00#.


Nyaka Nyaka Bonus - Promosheni ya Tigo Inayoongeza Matumizi ya Intaneti Nchini

Zaidi ya simu 400 na bonasi za intaneti bado zinashindaniwa!

Dar es Salaam, Aprili 5, 2018 – Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini ya Tigo Tanzania inazidi kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma za intaneti nchini baada ya kuwazawadia wateja wake 676 simu janja aina ya Tecno R6 katika promosheni yake inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus.

Katika promosheni hii murwa ambapo Tigo inatoa jumla ya simu janja 12 kila siku, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za intaneti za kuanzia TSH 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# pia wanapata bonasi ya hadi GB 1 bure kwa matumizi ya mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Twitter.

‘Ofa hii kabambe ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na maslahi na mahitaji ya wateja ili kuwezesha kila mtu kufurahia maisha bora ya kidigitali kupitia mtandao wetu mpana wa Tigo,’ Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi simu zao jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumza katika hafla kama hiyo iliyofanyika mjini Morogoro leo, Mtalaam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza alisema kuwa kupitia promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo inafanikisha azma yake ya kuwaunganisha wananchi wote na mtandao wake wenye kasi ya juu na mpana zaidi nchini wa Tigo 4G.

‘Tunataka kila mtu awe sehemu ya mabadiliko makubwa yanayotokana na kuunganishwa na mtandao wa intaneti na pia kufurahia huduma bora zenye uwezo wa kubadili maisha zinazotopatikana katika mtandao wetu wenye kasi ya juu na mpana zaidi nchini wa Tigo 4G unaopatikana katika miji 24 nchini,’ alisema.

Takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonesha kuwa asilimia 45% tu ya Watanzania ndiyo waliofikiwa na huduma za kimtandao, huku asilimia 84% ya wale waliofikiwa wakitumia simu zao za mkononi kama njia kuu ya kupata huduma hizo za mtandao. Ubunifu huu wa Tigo utahakikisha kuwa idadi ya watumiaji wa huduma za mtandao inaongezeka nchini.

‘Tunawaasa wateja wetu kuchangamkia fursa hii kubwa ya kuwa sehemu ya mageuzi ya ulimwengu wa kisasa wa kidigitali kwa kununua bando intaneti kupitia *147*00# ili wajipatie bonasi za intaneti pamoja na nafasi ya kujishinidia simu janja aina ya Tecno R6 kutoka Tigo.’ Woinde alibainisha.

FRUITS AND VEGETABLES ARE KEY ANGLES TO FOOD SAFETY

April 04, 2018

Food safety is one of the most important angle of human survival, Scientific research over the last decades has shown that a diet rich in fruits and vegetables is protective against many cancers and lowers the occurrence of coronary heart disease. This has contributed to substantial increase in consumption of fresh fruits and vegetables.

The importance of fresh fruits and vegetables for human health, together with their marked increase in the year-round availability from a global market, has contributed to the substantial increase of their consumption.



However, the recent increase in reports of food borne illness and outbreaks linked to fresh fruits and vegetables as a result of microbial infection has raised concerns from public health agencies and consumers about the safety of these products, more the less due to a higher rate of fruits and vegetables consumption a threat towards the consumers raised eyebrows of COLEACP and SOLIDARIDAD to gather key number of stakeholders to mention few among them being Tanzania Bureau of Standards (TBS), Tropical Pesticides Research Institute (TPRI) and farmers discuss about fruits and vegetables threats and safety as whole in Dar es salaam and together agreed on the following points as a measure


a) importance of good health and hygiene for personal health and food safety;

b) importance of hand washing for food safety and the importance of proper hand washing techniques;



c) importance of using sanitary facilities to reduce the potential for contaminating fields, produce, other workers, and water supplies; and

d) techniques for hygienic handling and storage of fresh fruits and vegetables by transporters, distributers, storage handlers and consumer

e) importance of tidy and developed environment



But also vowed each stakeholder at a respected area of technicality to make sure they be ambassadors and key participants to make sure the goal having safe food including fruits and vegetables is achieved.

Blogs za Mikoa Tanzania Network Email: blogzamikoa@live.com Facebook/instagram/twitter @blogszamikoa Website: www.blogszamikoa.co.tz

MBUNGE ROSE TWEVE AMBANA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA JUU YA FIDIA ZA MAJERUHI WA AJALI ZA BARABARANI

April 04, 2018


Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiuliza swali la nyongeza kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba juu ya idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo ili kupunguza ajali hizo


Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiwa makini kuandika hoja ambazo anajibiwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba.


Na Fredy Mgunda,Dodoma.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve amelibana jeshi la polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabani kwa kutaka kujua idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo ili kupunguza ajali hizo

Mbunge Rose Tweve mapema hii leo bungeni aliuliza swali kwa wizara ya mambo ya ndani ya nchi kwa kutaka kujua idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo.

Akijibu swali la mbunge Rose Twelve Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba alisema kuwa jeshi la polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabani limeweza kupunguza ajali za barabarani kwa asilimia 43 kwa mwaka 2017

Mwigulu alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2016-2017 kulitokea ajali 9856 ambazo zilisababisha vifo 3256 na majeruhi 2128 ambapo kwa mwaka 2017 kulitokea ajali 5310 na kusababisha vifo 2533 na majeruhi 5355.

Waziri Mwigulu ameongeza kuwa kwa kipindi cha januari hadi februari 2018 kumetokea ajali 769 na kusababisha vifo 334 na majeruhi 698.

Akiuliza swali la nyongeza mbunge Rose Tweve alimtaka waziri kutoa idadi ya wahanga wa ajali waliolipwa fidia na mwaka 2009 bunge ilipitisha sheria ndogo namba 10 ya bima ya kuwalinda wahanga wa ajali hizo,sasa mheshimu waziri hawa wenzetu wa TIRA wanaonyesha wanamapungufu mengi na watanzania wamekuwa wanahanga wakubwa kwenye swala hilo na kwanini tusianzishe idara maalum ambayo itakuwa inatoa elimu kwa wahanga wa ajali pindi inapotekea na kujua nini cha kufanya.

Akijibia swali la Nyongeza la Mbunge Rose Tweve la kuhusu idadi ya wahanga wa ajali waliolipwa fidia, Waziri Nchemba amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2016-2018 jumla ya wahanga wa ajali 1583 wakilipwa fidia takribani Bilioni 7 kutoka makampuni mbalimbali ya bima.

Katika hatua nyingine Mwigulu Nchemba amekiri kuwepo kwa matukio ya ajali 1500 yanayosababishwa na uzembe wa madereva huku serikali ikipanga kuwachukulia hatua madereva wenye tabia hizo.

“Ni kweli serikali itahakikisha inawachukulia hatua madereva wazembe ikiwemo kuwanyang’anya leseni ili kupunguza idadi ya madereva ambao wamekuwa wakisababisha ajali zinazoweza kuepkukika” alisema Mwigulu nchemba.