AWESO AKERWA NA WAKANDARASI WASIO NA UWEZO

AWESO AKERWA NA WAKANDARASI WASIO NA UWEZO

December 02, 2017
1
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiangalia kilula cha maji cha mradi wa Liula, Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
2
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akitoa maagizo kwa watendaji mara baada ya kukagua Tenki la maji la mradi wa Parangu katika Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
3
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akitoka kukagua chanzo cha maji cha Masimeli, kinachotumika kuzalisha maji kwa ajili ya mradi wa Lipaya katika  Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
4
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa kwenye tenki la mradi wa Matimila, Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
……………………………………………………………………………….
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesema kuwa anakerwa na wakandarasi wasio na uwezo, ambao wamekuwa wakitekeleza miradi bila kuzingatia mikataba, ama kutoikamilisha kwa wakati au kutekeleza chini ya kiwango kwa kukosa thamani halisi ya fedha iliyotumika.
Aweso alisema hayo wakati akikagua utekelezaji wa miradi ya maji katika Wilaya ya Songea Vijjini, katika ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma na kusikitishwa na mwenendo wa utekelezaji usioridhisha wa baadhi ya miradi.
Naibu Waziri alisema kuwa ipo haja ya kufutiwa usajili na kutokupewa kazi yoyote nchini wakandarasi wote wababaishaji, baada ya kutoridhishwa tendaji wao katika baadhi ya miradi wilayani humo.
‘‘Hatutawavumilia wakandarasi wasio na uwezo ambao wanatuangusha, tutawafuatilia na ikiwezekana wafutiwe usajili kabisa nchini ili wasiendelee kufanya kazi mahali popote nchini, tubaki na wakandarasi wenye uwezo’’, alisema Aweso.
Akiwa mkoani Ruvuma, Aweso ametembelea miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa  katika wilaya za Tunduru, Namtumbo, Songea Mjini, Songea Vijijini na Madaba lengo likiwa ni kuweka msukumo katika utekelezaji wa miradi kwa nia ya kuhakikisha inakamilika kwa wakati na wananchi wa  mkoa huo wanapata huduma ya maji  ya uhakika
TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO MAJIMBO 3 NA KATA 6

TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO MAJIMBO 3 NA KATA 6

December 02, 2017

Hussein Makame-NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya Uchaguzi Mdogo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini na kata sita za Tanzania Bara ambao utafanyika tarehe 13 Januari mwaka 2018.

Akitoa taarifa kwa umma jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa NEC, Mhe. Jaji Mkuu (Mst. Zanzibar) Hamid Mahmoud Hamid, alisema Tume imetangaza uchaguzi huo kufuatia kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kuwepo nafasi wazi ya jimbo la Singida Kaskazini kufuatia kuvuliwa uanachama wa CCM mbunge wa jimbo hilo Lazaro Nyalandu na hivyo kupoteza sifa ya kuwa mbunge.

Kwa upande wa Jimbo la Songea Mjini, Jaji Mst. Hamid alisema kuwa Spika aliitaarifu Tume kuwepo nafasi wazi ya jimbo hilo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Leonidas Gama huku Tume ikipokea Hati ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ikithibitisha kuwa Jimbo la Longido kuwa wazi baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo.

Aliongeza kuwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, aliitaarifu Tume kuwepo nafasi wazi za madiwani katika kata sita Tanzania Bara.

Mhe. Jaji Mst. Hamid alizitaja kata zinazohusika katika uchaguzi huo kuwa ni Kimandolu (Halmashauri ya Jiji la Arusha), Kihesa (Halmashauri ya Manispaa ya Iringa), Bukumbi (Halmashauri ya Wilaya ya Uyui), Kurui (Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe), Keza (Halmashauri ya Wilaya ya Ngara) na Kwagunda (Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe).

Alisema utoaji fomu za uteuzi katika majimbo hayo na kata hizo sita utakuwa ni kati ya tarehe 12 hadi 18 Desemba, 2017 wakati katika jimbo la Songea Mjini utoaji fumo utakuwa kati ya tarehe 14 hadi 20 Desemba, 2017.

“Uteuzi wa wagombea katika majimbo ya Singida Kaskazini na Longido na kata za Keza, Kimandolu, Kwagunda, Bukumbi, Kurui na Kihesa utafanyika tarehe 18 Desemba, 2017 na uteuzi wa wagombea katika jimbo la Songea Mjini utafanyika tarehe 20 Desemba, 2017” alisema Jaji Mst. Hamid.

Alifafanua kuwa kwa upande wa kampeni za uchaguzi huo katika majimbo ya Singida Kaskazini na Longido na kata zote sita zitaanza tarehe 19 Desemba, 2017 na kumalizika tarehe 12 Januari, 2018.

Katika jimbo la Songea Mjini, alisema kuwa kampeni za zitaanza tarehe 21 Desemba, 2017 na kumalizika tarehe 12 Januari, 2018 wakati siku ya uchaguzi katika majimbo yote matatu na kata zote sita itakuwa tarehe 13 Januari, 2017.

Mhe. Jaji Mst. Hamid alivikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi wazingatie Sheria, Kanuni, Taratibu, Miongozo na Maelekezo yote wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo wa majimbo hayo na kata Sita.

MHE MWANJELWA AELEKEZA UONGOZI WA MKOA WA RUVUMA KUHAMASISHA WAKULIMA KUJIUNGA NA VYAMA VYA MSINGI VYA USHIRIKA

December 02, 2017
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akikagua Maghala ya Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma, Wengine Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe Pololet Kamando Mgema (Kushoto) Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba (Katikati) na Meneja NFRA Kanda ya Songea Ndg Amos Mtafya, Jana Novemba 2, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na kina mama waliojipatia kibara kwenye ujenzi wa Kituo cha mafunzo ya kilimo OTC Lilambo kitakachojihusisha na uchakataji wa mahindi kilichopo Mtaa wa Namanditi, Kata ya Lilambo, Wilaya ya Songea wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Ruvuma, Jana Novemba 2, 2017. 
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Wa tatu Kushoto) akitembelea na kukagua Maghala ya Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma, Wengine Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe (Kushoto) Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba (Wa Pili kulia) na Meneja NFRA Kanda ya Songea, Jana Novemba 2, 2017. 
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alipotembelea Kijiini Likuyu Fusi, Kata ya Lilambo, Wilaya ya Songea Mjane Bi Ester Gama ambaye ni mke wa Marehemu Leonidas Gama akimvisha kitenge ikiwa ni ishara ya upendo na faraja. Gama alifariki Dunia Novemba 23, 2017 katika Hospitali ya Mtakifu Joseph ya Peramiho.
Jana Novemba 2, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mahindi ili kubaini alipotembelea Maghala ya Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma, Jana Novemba 2, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akikagua Maghala ya Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma, Jana Novemba 2, 2017.

Na Mathias Canal, Ruvuma

Uongozi Wa Mkoa Wa Ruvuma leo Disemba 1, 2017 umeelekezwa kuwahamasisha wakulima kujiunga na vyama vya msingi vya ushirika kwani kupitia vikundi ndio njia muhimu na mkombozi kwa manufaa ya mkulima mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Amebainisha hayo Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akizungumza na baadhi ya wakulima sambamba na viongozi Wa wakulima katika Mkutano Wa hadhara ulifanyika katika eneo la Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea.

Pamoja na kuwasisitiza wakulima hao kujiunga katika vikundi vya vyama vya msingi vya ushirika, Mhe Naibu Waziri ameelekeza uongozi Wa Mkoa Wa Ruvuma kutilia msisitizo umuhimu Wa Vyama hivyo kwani ni maelekezo ya ilani ya Ushindi ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi cha miaka mitano 2015-2020 inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano ikiongozwa na Mhe Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

WAVIU WASHAURI WATEMBELEA VITUO VIKUBWA VYA CTC HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO NA SEKOTOURE JIJINI MWANZA

December 02, 2017

Waviu Washauri kutoka mkoa wa Mwanza wametembelea vituo vikubwa vya tiba na matunzo katika hospitali ya Rufaa ya Bugando na Sekotoure jijini Mwanza ili kujifunza kwa kuona huduma mbalimbali zinazotolewa katika maeneo hayo.

DK. KIGWANGALLA AAGIZA NDANI YA SIKU 30 KUJITOKEZA WAMILIKI WA MAGOGO YALIKAMATWA BANDARINI DAR

December 02, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) ametoa mud wa siku 30 kwa wahusika ambao ni wamiliki wa magogo yaliyokamatwa katika bandari ya Dar e s  Salaam (TPA) ambayo yalikuwa yasafirishwe nje ya Nchi, kujitokeza haraka kueleza wameyato wapi na walikuwa na lengo gani baada ya kuyatelekeza bandarini  hapo kwa muda wa miaka 10 sasa huku mengine yakitelekezwa pasipo kuwa na vibali maalum.
Dk.Kigwangalla ametoa kauli hiyo baada ya kufanya ziara ya ghafla bandarini hapo kukagua mali na bidhaa zinazoshughulikiwa na Wizara yake hiyo ambapo katika zkukagua kwake huko alibaini uwepo wa makontena hayo 55 ambayo yapo  kwa miaka 10 sasa yakihifadhiwa huku wahusika wakishindwa kujitokeza.
“Naagiza mamlaka zilizo chini ya wizara yangu kuhakikisha wanahakiki magogo yote yalipo hapa bandarini. Mwenye huu mzigo lazima ajulikane hasa haya magogo 938, Ndani ya siku 30 mwenye haya magogo atangaziwe na ajitokeze vinginevyo itabaki kuwa mali ya Serikali” alisema Dk. Kigwangalla.
Hata hivyo aliagiza pia kontena 55 zilizokutwa bandarini hapo zenye magogo pia nazo wahusika wajitokeze na nyaraka zao kamili ili waeleze kama kweli wameyatoa  Zambia magogo hayo ama sehemu gani hivyo wajitokeze na wasipofanya hivyo ndani ya siku hizo 30, magogo hayo yatataifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Katika ziara hiyo, Waziri Dk.Kigwangalla aliweza kutembelea bandari ya Dar es Salaam pamoja na maeneo yanayohifadhiwa magogo hayo zikiwemo bandatri ya nchi kavu ya NASACO, Malawi (Malawi Cargo) na baadae eneo hilo la bandari ya Dar es Salaam.

DC SHINYANGA ATEMBELEA VITUO VYA HUDUMA YA MTOTO VYA MAKANISA YENYE USHIRIKA NA COMPASSION KLASTA YA SHINYANGA

December 02, 2017
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ametembelea vituo sita vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa ya Shinyanga yenye vituo tisa.