Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini akiwasili uwanja wa Ndege wa
Mwanza leo Juni 26, 2014 kwa ziara ya kikazi Magereza Mkoa wa Mwanza.
Aidha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza atahudhuria pia Kikao cha
26 cha Bodi ya Taifa ya Parole ambacho kimeanza leo katika Ukumbi wa
Mwanza Hoteli, Jijini Mwanza(kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa
Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Goleha Masunzu.
Afisa
Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Remegius
Pesambili(wa pili kulia) akimlaki Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza
Nchini, John Casmir Minja(Kaunda Suti nyeusi) alipowasili leo Juni 26,
2014 katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ziara ya Kikazi Magereza Mkoa
wa Mwanza.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akisaini kitabu
cha Wageni mapema leo jioni Juni 26, 2014 alipowasili Jijini Mwanza kwa
ziara ya Kikazi(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).