NAMA RC MPYA WA MKOA WA TANGA MARTINI SHIGELLA ALIVYOLAKIWA

March 18, 2016




 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela, akipokewa na aliekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Mwantumu Mahiza, mara baada ya kuwasili  na kupokewa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali Leo  ikiwa ni siku yake ya kwanza kuwasili na kukabidhiwa ofisi.




 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mboni Mgazza wakati akiwasili na kupokewa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali ikiwa ni siku yake ya kwanza kuwasili ofisini kwake  leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela, akisalimia na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali mara baada ya kuwasili kwa makabidhiano ya ofisi na mtangulizi wake Mwantumu Mahiza leo.


NAIBU WAZIRI MAZINGIRA LUHANGA MPINA AFANYA ZIARA YA KUSHUTUKIZA TANGA

March 18, 2016


 Naibu Waziri Ofisi ya Makamo wa Rais Mazingira na Muungano, Luhanga Mpina, akisaini kitabu cha wageni ofisni kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga jana.kabla ya kuanza kutembelea ukuta wa Pangani ambao unahatarisha maji kuingia mitaani.
Katika ziara hiyo Waziri Mpina alikifungia kiwanda cha Rhino Cement kwa uharibifu wa mazingira pamoja na kutoa maelekezo kabla ya kuanza uzalishaji.


 Naibu wa Waziri Ofisi ya Mkamo wa Rais Mazingira na  Muungano, Luhanga Mpina, akiangalia ukuta mto Pangani ukiwa umeanguka na kuhatarisha maji kuingia mitaani na kutoa ufafanuzi kuwa fungu la pesa la kuanza ujenzi wa ukuta huo liko tayari na kuwataka wananchi wa Pangani kuupokea mradi huo na kutoa ushirikiano.

 Afisa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jacob Kingazi akimsaidia Naibu Waziri Luganga Mpaina kutoka ufukweni na kupanda ukuta wa mto Pangani ulioangukla baada ya kumaliza kuukagua jana wakati wa ziara yake ya kuangalia mzingira Mkoani humo.


 Mji wa Pangani ambao uko na historia nyingi . Moja ya majengo ya kale ufikapo Wilayani humo utakutana nayo

 Pia Naibu huyo aliweza kufanya ziara kiwanda cha Saruji cha Simba Cementi na kujionea kiwanda hicho kinavyodhibiti uharibufu wa mazingira ikiwa na pamoja na kutembeleza sehemu ya uzalishaji saruji na Sehemu ya uchimbaji udongo wenye madini utumikao katika uzalishaji wa Saruji.


 Naibu Waziri Mazingira Ofisi ya Makamo wa Rais akipata maelekezo kutoka kwa Injnia wa kwianda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement) Saimon Kakote wakati wa ziara yake jana.


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA DULA LA MSD WILAYANI CHATO

March 18, 2016

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Laurean Bwanakunu (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kabla ya Waziri Mkuu hajafungua duka la dawa la MSD Wilayani Chato juzi.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim M. Majaliwa (wa tatu kushoto), akizungumza wakati akifungua dula la Bohari ya Dawa (MSD), Wilayani Chato.


Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amefungua dula la Bohari ya Dawa (MSD), la Wilayani Chato duka litakalotoa huduma kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa duka hilo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu alisema duka hilo ni mfano kwa Wilaya nyingine na mikoa,ambapo tayari Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa(Tamisemi) mikoa na Wilaya kuanzisha maduka hayo,na kisha MSD itatoa ushauri wa kitaalam.


Bwanakunu alisema kwa kuanza,duka la dawa la Halmashauri ya Chato linaendeshwa na MSD,lakini baada ya muda watalikabidhi kwa Halmashauri ya Chato. 

KATIBU MKUU IKULU AKABIDHI GARI JIPYA LA WAGONJWA KWA HOSPITALI YA WILAYA YA CHALINZE KWA NIABA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

KATIBU MKUU IKULU AKABIDHI GARI JIPYA LA WAGONJWA KWA HOSPITALI YA WILAYA YA CHALINZE KWA NIABA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

March 18, 2016

riz1
Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo akimkabidhi funguo za gari jipya la wagonjwa Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya shughuli ya  kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze. Tukio hilo lilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
riz3
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akipokea na kuangalia nyaraka za gari hilo la kubebea wagonjwa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo.
riz4
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwasha gari jipya la Wagonjwa lililotolewa na na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze.
riz5
Sehemu ya Ndani ya gari hilo kama inavyoonekana .
riz6
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiendesha gari hilo la wagonjwa lililotolewa na na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze.
riz8
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akifurahia mara baada ya kukabidhiwa Gari hilo la Wagonjwa.
SPIKA ATEMBELEA HOSPITALI YA CCBRT

SPIKA ATEMBELEA HOSPITALI YA CCBRT

March 18, 2016

cc1
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw. Erwin Telemans (kushoto) wakati alipotembelea hospitali hiyo kwa mara ya kwanza akiwa ni Mlezi wa Hospitali hiyo.Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mpoki Ulisubisya.
cc2
Mkurugenzi wa Hospitali ya Walemavu CCBRT, Bi. Brenda Msangi akimueleza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) kuhusu namna ya utendaji kazi hospitalini hapo. Spika alitembelea hospitali hiyo kuangalia utendaji kazi kama mlezi wao.
cc3
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akipata maelekezo juu ya namna ya wagonjwa wa macho wanavyowekewa macho bandia (artificial eyes) wakati alipotembelea hospitali hiyo kwa mara ya kwanza akiwa ni Mlezi wa Hospitali hiyo. Kulia ni ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mpoki Ulisubisya.
cc4
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya nchini pamoja na Menejimenti ns Madaktari wa CCBRT alipowatembelea kama mlezi wa Hospitali hiyo.
cc5
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (mwenye tai nyekundu) akipokea machapisho yanayohusu masuala ya walemavu kutoka kwa Afisa Mtetezi CCBRT wa masuala ya walemavu, Bw. Fredrick Msigala wakati alipotembelea hospitali hiyo kwa mara ya kwanza akiwa ni Mlezi wa Hospitali hiyo.
KILA LA KHERI AZAM FC, JKU, YANGA SC

KILA LA KHERI AZAM FC, JKU, YANGA SC

March 18, 2016
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezitakia kila la kheri vilabu wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, timu za Azam FC, JKU na Yanga SC katika michezo yao watakayocheza wikiendi hii.
Katika salamu hizo, TFF imezitakia kila la kheri timu hizo kuhakikisha zinafanya vizuri katika michezo yao ili ziweze kusonga mbele katika hatua inayofuata, na kuwapa furaha washabiki wa mpira wa miguu pamoja na watanzania wote.
Timu ya JKU ya visiwani Zanzibara leo Ijumaa watakua kibaruani kuchuana na SC Villa ya Uganda, mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Amani mjini Zanzibar.
Kesho Jumamosi, Yanga SC watakua wenyeji wa APR ya kutoka nchini Rwanda katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa (CAF CL) kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, mchezo utakaochezeshwa na mwamuzi Bernard Camille, akisaidiwa na Eldrick Adelai, Gerard Pool na Allister Bara kutoka nchini Shelisheli.
Jumapili Azam FC watakua wakicheza dhidi ya Bidvest FC kutoka nchini Afrika Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho (CAF CC) kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, mwamuzi wa mchezo huo ni Gait Oting akisaidiwa na Abdallah Gassim, Casim Dehiya, mwamuzi wa akiba Ariel James wote kutoka Sudan Kusini
 

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA NHC

March 18, 2016


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na  Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda (kushoto kwake), wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara kwenye miradi miwili ya Shirika la Nyumba la Taifa ya NHC Mwongozo na NHC Eco Residence uliopo Kinondoni Hananasif. Kwa ujumla Kamati ya Bunge imeridhishwa sana na utendaji mzuri wa Shirika la Nyumba la Taifa na imeahidi kuyavalia njuga masuala ya Double Taxation kwa serikali ili lifanyiwe kazi na Watanzania wengi zaidi wapate nyumba za kuishi na suala la Mamlaka husika kufikisha huduma za kijamii katika nyumba za NHC zinakojengwa kama za Maji, Umeme na Barabara. Picha Zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii cha NHC.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wilfred Lwakatare akiongozana na Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina  Mabula wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda na Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina  Mabula wakiwasili kwenye eneo la mradi wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula na Mkurugenzi wa nyumba kutoka Wizara wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Michael Mwalukasa wakijadiliana jambo katika ziara hiyo
Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozana na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Mikoa, Raymond Mndolwa  wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozana na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki, Hamad Abdallah wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na  Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda (kushoto kwake), wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara kwenye miradi miwili ya Shirika la Nyumba la Taifa ya NHC Mwongozo na NHC Eco Residence uliopo Kinondoni Hananasif.
Mradi wa Mwongozo unavyoonekana kwa juu 
Kamati ya Bunge ikisikiliza maelekezo wa Mhandisi Anna Mrema anayesimamia Jengo la Eco Residence kwa niaba ya NHC huku Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akifuatilia mazungumzo hayo wakati Kamati hiyo ilipotembelea jengo la Nyumba za makazi za NHC Eco Residence la Shirika la Nyumba la Taifa kujua utekelezaji wa miradi ya Shirika hilo. Jengo hilo linajengwa na mkandarasi mahiri Estim Construction Limited.
Kamati ya Bunge ikisikiliza maelekezo wa Mhandisi Anna Mrema anayesimamia Jengo la Eco Residence kwa niaba ya NHC huku Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akifuatilia mazungumzo hayo wakati Kamati hiyo ilipotembelea jengo la Nyumba za makazi za NHC Eco Residence la Shirika la Nyumba la Taifa kujua utekelezaji wa miradi ya Shirika hilo. Jengo hilo linajengwa na mkandarasi mahiri Estim Construction Limited.