COASTAL UNION YAANZA KUIPIGIA HESABU KAGERA SUGAR

October 21, 2014
TIMU ya Coastal Union ya Tanga imeanza maandalizi ya kuelekea mechi yao na Kagera Sugar itakayopigwa wikiendi hii kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ikiwa ni muendelezo wa Ligi kuu soka Tanzania bara.

Kauli hiyo ilitolewa na Kocha Mkuu wa Coastal Union,Yusuph Chippo mara baada jana wakati akizungumza na gazeti hili mara baada ya kumalizika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye viwanja wa shule ya Sekondari Popatlaly mjini hapa.

Alisema kuwa kikosi chake kipo imara kuweza kuwavaa wakata miwa wa bukoba kutokana na kuimarisha sehemu mbalimbali kwenye timu hiyo hasa mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi yao na Mgambo Shooting ambapo Coastal ilishinda bao 2-0.

Kocha huyo alisema kuwa wembe uliotumika kuwanyoa timu hiyo ya Mgambo Shooting ndio ambao watautumia ili kuweza kupata pointi tatu muhimu wakiwa ugenini lengo likiwa kuweza kuwa kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi kuu .

“Tunamshukuru mungu kwa kupata pointi tatu muhimu kwenye mechi hii na hili linatokana na kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi yetu iliyopita lakini kubwa ni umoja na mshikamano uliopo “Alisema Chippo.

Hata hivyo aliwataka wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha wanapambana vilivyo kila mchezo ili waweze kupata matokeo mazuri yatakayowawezesha kuirudishia heshima timu hiyo yenye maskani yake barabara 11 jijini Tanga.

Katika hatua nyengine,Timu hiyo inatarajiwa kutumia usafiri wa ndege kuelekea mkoani Kagera kucheza mechi yake ya Ligi kuu wikiendi hii dhidi ya Kagera Sugar mechi itakayochezwa uwanja wa Kaitaba.

TANZANIA NA CHINA WAFANYA PAMOJA MAZOEZI YA KIJESHI

October 21, 2014

Wanajeshi wa Tanzania wakifanya mazoezi
Mkuu wa operesheni na utendaji kivita wa JWTZ, Meja Jenerali James Mwakibolwa, (Wapili kulia), akitazama silaha ya kivita, wakati wa maonyesho ya zana za kijeshi na uzinduzi wa mazoezi ya pamoja kati ya majeshi ya wanamaji kutoka China na Tanzania yaliyopewa jina la "Surpassing 2014" kwenye kamandi kuu ya wanamaji wa JWTZ, Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.
RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AANZA ZIARA RASMI YA CHINA

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AANZA ZIARA RASMI YA CHINA

October 21, 2014

1a
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali
Davis Mwamunyange na IGP Ernest Mangu wakati akiondoka katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa
kuamkia leo tayari kuanza  ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya
Watu wa China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping.
2a
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe
Raymond Mushi wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo tayari kuanza
 ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaliko
wa Rais Xi Jinping.
3a
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na maafisa wa Ubalozi wa China
nchini Tanzanioa  wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo tayari
kuanza  ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya Watu wa China kwa
mwaliko wa Rais Xi Jinping.
PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Oktoba 21, 2014, anaanza ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping, ikiwa ni ziara yake ya pili nchini humo akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Baada ya China, Rais Kikwete atafanya ziara rasmi ya siku tatu nchini
Vietnam kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo.
Wakati wa ziara yake nchini China, Rais Kikwete ambaye aliondoka
nchini usiku wa jana, Jumatatu, Oktoba 20, 2014, atatembelea majimbo matatu ya nchi hiyo, atafanya mazungumzo na viongozi wakuu wa China, atashuhudia utiaji saini mikataba muhimu ya shughuli za maendeleo, atatunukiwa shahada za heshima na atashiriki katika sherehe za miaka 50 tokea kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania na China.
Rais Kikwete amepangiwa kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Xi Jinping; Waziri Mkuu Mheshimiwa Li Keqiang pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Zhang Dejiang.
Rais Kikwete pia atashuhudia utiaji saini wa mikataba ya miradi ya
maendeleo ya Tanzania ambayo inasaidiwa ama inagharimiwa na fedha kutoka China na pia atakutana kwa mazungumzo na wakuu wa taasisi muhimu zinazogharimia baadhi ya miradi mikubwa ya maendeleo katika Tanzania zikiwamo China-Africa Development Fund (CADB) na China Development Bank (CDB).
Akiwa Beijing, Rais Kikwete atakutana na Mabalozi wa Afrika
wanaoziwakilisha nchi zao katika China, atafungua Mkutano wa Tatu wa Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na China na atazindua rasmi Kijiji cha Kiafrika.
Aidha, Rais Kikwete atatunukiwa uprofesa wa heshima na Chuo Kikuu cha Kilimo cha China cha China Agricultural University na Chuo Kikuu cha East China Normal University na pia atakuwa mwenyeji wa hafla maalum ya kusherehekea miaka 50 ya uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania na China. 
Uhusiano huo ulitimiza miaka 50, Aprili 26, mwaka huu, siku
ambako Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia ilitimiza miaka 50 ya
kuzaliwa kwake.
Baada ya kumaliza ziara yake Beijing, Rais Kikwete atatembelea Jimbo la Jinan ambako atashuhudia maonyesho rasmi ya kijeshi ya Jeshi la Ukombozi la Wananchi wa China la Chinese People’s Liberation Army (PLA) lililoandaliwa rasmi kwa heshima yake. Hiyo itakuwa mara ya kwanza katika historia kwa heshima ya namna hiyo kutolewa kwa kiongozi wa nchi yoyote duniani, nje ya China.
Akiwa Jimbo la Jinan, Rais Kikwete pia atakutana na viongozi wa Jimbo hilo na pia atakutana kwa mazungumzo na madaktari wa Kichina ambao wamefanya kazi katika Tanzania katika miaka 50 iliyopita.
Baada ya Jimbo la Jinan, Rais Kikwete atakwenda  Jimbo la Shenzhen ambako atatembelea makao makuu ya taasisi na makampuni makubwa ya China ya Shenzhen Economic Zones Authority, China Merchants Holdings International (CMHI), Huawei na ZTE. Shenzhen ndiko Watanzania wengi wanaonunua bidhaa kutoka China hufanyia biashara zao.
Mara ya mwisho, Rais Kikwete alitembelea China mwaka 2008 wakati
alipoliwakilisha Bara la Afrika katika Mkutano wa Kwanza wa
China-Afrika katika nafasi yake wakati huo kama Mwenyekiti wa Umoja wa
Afrika (AU).
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
21 Oktoba,2014

MATUKIO KATIKA PICHA JINSI AFRICAN SPORTS ILIVYOWACHAPA POLISI DAR "WATOTO WA KOVA"MABAO 2-1 MKWAKWANI JUZ

October 21, 2014

KIKOSI CHA AFRICAN SPORTS KILICHIOBAMIZA POLISI DAR MABAO 2-1

KIKOSI CHA POLISI DAR KIKITOKA UWANJANI MARA BAADA YA KUMALIZIKA MECHI YA LIGI DARAJHA LA KWANZA KATI YAO NA AFRICAN SPORTS AMBAO WALIFUNGWA MABAO 22-1

KOCHA MKUU WA AFRICAN SPORTS ALLY MANYANI WA PILI KULIA AKITETE NA WACHEZAJI WAKE WAKATI MECHI HIYO IKIENDELEA

VIONGOZI WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA TANGA(TRFA) WA KWANZA KUSHOTO NI MWENYEKITI SAIDI SOUD,WA PILI KUTOKA KUSHOTO NI KHALID ABDALLAH MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI TFF TAIFA,KATIBU WA CHAMA CHA SOKA MKOA BEATRICE MGAYA NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAKOCHA MKOA WA TANGA JUMA MNGUNDA WAKIFUATILIA MECHI HIYO JUZI

KIKOSI CHA AFRICAN SPORTS KIKISHEREKEA USHINDI HUO MARA BAADA YA KUMALIZIKA KWA MECHI HIYO


 KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA MINJA AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA AFISA MNADHIMU MKUU MSAIDIZI WA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DARES SALAAM

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA MINJA AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA AFISA MNADHIMU MKUU MSAIDIZI WA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DARES SALAAM

October 21, 2014
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(suti nyeusi) akiwa amesimama wakati mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen Nzawila ulipowasili tayari kwa kuuagwa rasmi nyumbani kwake Ukonga, Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2014(wa kwanza kushoto) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Nicas Banzi(wa pili kushoto) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Jumanne Mangara(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
m1 
Mchungaji wa Kanisa la Moravian lililopo Ukonga, Banana Relini Hansi Mwakijoja akiwaongoza Waombolezaji kwa sala kabla ya kuuaga rasmi mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza ambaye amefariki Jumapili Oktoba 19, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam. image_2 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza ambaye amefariki Jumapili Oktoba 19, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
image_3 
Baadhi ya Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa wamejipanga katika mstari tayari kuuaga mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza leo Oktoba 20, 2014 Ukonga, Jijini Dar es Salaam. Mwili wa Marehemu unatajiwa kusafirishwa kesho kuelekea Tutuo Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora kwa Mazishi. image_4 
Mke wa Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza akiwa na majonzi makubwa na waombolezaji kabla ya kuuaga rasmi mwili wa  mume wake ambaye amefariki Jumapili Oktoba 19, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
image_5 
Sehemu ya Waombolezaji waliojitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza kwa makini wasifu wa Marehemu kabla ya kuuaga rasmi leo Oktoba 20, 2014 Ukonga, Dar es Salaam.
image_6 
Bendi ya Jeshi la Magereza ikitumbuiza katika hafla fupi ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen Nzawila ambaye amefariki Jumapili Oktoba 19, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza). m2 
Mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen Nzawila ukiwa umebebwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kabla ya kuagwa rasmi leo Oktoba 20, 2014 nyumbani kwake, Ukonga Dar es Salaam.

DC MGAZA AWAFUNDA WAZAZI WILAYANI MKINGA KUHUSU CHANJO

October 21, 2014
MKUU WA WILAYA YA MKINGA,MBONI MGAZA AKIZUNDUA KAMPENI YA CHANJO WILAYANI HUMO JUZI

MGANGA MKUU WA WILAYA YA MKINGA,JUSTICE MUNISI AKISOMA RISALA KWENYE UZINDUZI WA KAMPENI HIYO JUZI


MKUU WA WILAYA YA MKINGA MBONI MGAZA AKIMEZA VIDONGE MARA BAADA YA KUZINDUA KAMPENI HIYO JUZI

Picha ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza kulia akimpatia chanjoya surua na rubella mtoto Albertina Siza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika jana kwenye kata ya Duga wilayani hapa kushoto ni
Muunguzi wa Kituo cha Afya Duga Maforoni Ester Kingu


WANANCHI WA MAENEO MBALIMBALI WILAYANI MKINGA WAKIMSIKILIZA MKUU WA WILAYA YA MKINGA MBONI MGAZA AMBAYE HAYUPO PICHANI WAKATI WA UZINDUZI WA KAMPENI HIYO
MKINGA.

WAZAZI na Walezi wilayani Mkinga mkoani Tanga wametakiwa kuondokana na imani za kushirikina badala yake wahakikisha wanawapeleka watoto wao kwenye vituo vya afya ili waweze kupatiwa chanjo ambazo zitawasaidiakuwakinga na magonjwa mbalimbali.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza mwishoni mwawiki wakati akizundua kampeni ya chanjo ya surua-rubella vitaminiA,Mebendazole na dawa za magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbelekwenye wilaya hiyo.

Alisema kuwa lazima wananchi watambue kuwa ili kuweza kuwakinga watotowao wadogo na maradha mbalimbali wanapaswa kuwapeleka kwenye vituo vya afya ili waweze kupata chanjo ambao ni mkakati muafaka wa kupunguzamadhari kwa watoto wenye umri mdogo hasa katika kipindi chao cha
ukuaji.

Aidha alisema kuwa katika wilaya ya Mkinga jumla ya watoto wapatao19711 wanatarajiwa kupatiwa chanjo hiyo ambapo aliwataka wazazi wawalezi kuhakikisha wanawapeleka kwenye vituo vya afya ili wawezekupatiwa chanjo hiyo muhimu.

Aliongeza kuwa lazima jamii iondokane na dhana potofu badala yakewahakikisha wanawapeleka watoto wao kwenye vituo vya afya ili kuwezakupata chanjo kutoka kwa wataalamu walipo.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo,Mganga Mkuu wa wilaya yaMkinga,Justice Munisi alisema kuwa kampeni ya kitaifa ya chanjo yasurua rubella itawafikia watoto wote ambao  hawakupatiwa kingakikamilifu ili kuzuia mlipuko wa ugonjwa huo wa surua.

Munisi alisema licha ya utoaji huo lakini wanakabiliwa n achangamoto mbalimbali kwenye katika kuendesha zoezi hilo ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara ambao unachangia uharibifu wa mipira ya magari wakati wa kufuatilia chanjo mkoba hasa katika maeneo ya wafugaji.

Alisema kuwa suala lengine ni ucheleweshwaji wa fedha za kampeniumechangia mafunzo ya watoa huduma na uendeshaji wa vikao muhimu kufanyika kabla  bila malipo.

Hata hivyo waliomba fedha za kampeni ziwasilishwe mapema ili
maandalizi yaweze kufanyika kwa usahihi pamoja na marekebisho yabajeti /mipango iliyowasilishwa yafanyike mapema kwenye ngazi zawilaya ijulishwe kwa wakati wanapokuwa wamefanya marekebisho.

Tamasha la Handeni Kwetu lawapigia magoti wadhamini

October 21, 2014

 
Na Mwandishi Wetu, Handeni
WADAU wa mambo ya utamaduni yakiwamo mashirika, makampuni na watu mbalimbali wameombwa kujitokeza kuliwezesha tamasha la Handeni Kwetu 2014, lililopangwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Tamasha hilo linafanyika huku mwaka jana likiwezeshwa kwa kiasi kikubwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ushirikiano na wadau mbalimbali walioliwezesha tamasha hilo kwa mara ya kwanza katika Historia ya Mkoa wa Tanga.

Akizungumza mjini hapa, Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa wadhamini wakijitokeza kwa wingi kutaongeza chachu ya maendeleo ya nchi, sanjari na sanaa ya utamaduni inayotakiwa kuungwa mkono na watu wengi.

Alisema kuwa kitendo cha wadhamini kuendelea kuliunga mkono Tamasha hilo kutachangia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa nchi pamoja na kutangaza utamaduni wa Mtanzania.

“Mwaka jana wadau wengi walijitokeza kuliwezesha tamasha la Handeni, wakiwamo NSSF, hivyo tunaomba msimu huu pia tuendelee kushirikiana kuliwezesha Tamasha la Handeni Kwetu litakalofanyika Desemba 13 mwaka huu, Handeni Mjini.

“Hadi wakati huu, walioonyesha nia ya kulisaidia tamasha la Handeni Kwetu 2014 ni pamoja na SmartMind & Partners iliyopo chini ya Anesa Co. Ltd kwa kupitia kitabu chao cha Ni Wakati wako wa Kung’aa, Phed Trans, chini ya Yusuphed Mhandeni, Handeni Kwetu Foundation, Wait & Watch Film Company Ltd, Qs Mhonda J Apex Group of Companies Ltd na Skyblue Security and Risk Mgt Ltd,” alisema Mbwana.
 
Tamasha la Handeni Kwetu ni miongoni mwa matukio makubwa ya kiburudani mkoani Tanga, ambako zaidi ya watu 500 walihudhuria tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu mipango kabambe ya kuhakikisha kuwa linafanyika kwa mafanikio.