Menejimenti Ya DCC Yapongezwa kwa Kurejesha Uhai wa Shirika

Menejimenti Ya DCC Yapongezwa kwa Kurejesha Uhai wa Shirika

May 26, 2017
PIX1a
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akipokelewa na wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam alipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC).Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Sipora Liana na Mstahiki Meya wa Jiji hilo Isaya Mwita.
PIX0b
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akizungumza na menejimenti za Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) wakati wa ziara  yake katika ofisi za mashirika hayo leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana  Bohela Lunogelo.
PIX0a
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora Liana akifafanua jambo wa mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (mbele) alipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.
PIX1b
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akisisitiza jambo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo katika Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana  Bohela Lunogelo.
PIX1c
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana  Bohela Lunogelo akielezea jambo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo katika Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo. Katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.
PIX1d
 Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam(DDC) wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni(hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi katika Mashirika ya Masoko Kariakoo na Shirika la Maenedeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC).
PIX2a
 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko la Kariakoo Hetson Msalale Kipsi akiwasilisha taarifa fupi ya Shirika hilo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa ziara ya yake kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.
PIX2b
Meneja Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC), Rwandiko Manumbu akiwasilisha taarifa fupi ya Shirika hilo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya yake kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.Katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
PIX3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akipokelewa na baadhii ya wajumbe wa Bodi za Mashirika ya Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) NA Shirika la Masoko Kariako alipowasili katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.
PIX4
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akisalimiana na mmoja wa wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo Shimoni wakati wa ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.
PIX5
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita (kushoto) akimuongoza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni(mwenye suti nyeusi) kuelekea katika Ofisi za Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) wakati wa ziara ya kikazi kutembelea Shirika hilo pamoja na Shirika la Masoko Kariakoo  leo Jijini Dar es Salaam.
PIX6
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akizungumza na wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama Machinga wanaopanga bidhaa zao mbele ya Ofisi za Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi kutembelea Shirika hilo pamoja na Shirika la Masoko Kariakoo  leo Jijini Dar es Salaam.
Picha zote: Frank Shija – MAELEZO
………………….
Nuru Juma – MAELEZO.
Serikali imeipongeza Bodi na Menejimenti nzima ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) kwa juhudi zao zakurejesha uhai wa Shirika hilo richa ya changamoto wanazo kumbana nazo.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI), George Simbachawene wakati akipokea taarifa fupi ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) na Shirika la Masoko Kariakoo  alipokutana na menejinti ya mashirika hayo leo.
Waziri Simbachawene alisema kuwa amepitia taarifa ya Shirika hilo na kuridhika nayo hivyo hana budi kuipongeza timu nzima ya uongozi kwani kwa muda mfupi imeweza kufanya mabadiliko na kuweza kuliinua tena Shirika hilo.
“Pamoja na kuipongeza bodi hii lakini napenda kuwashauri kuangalia maeneo mengine ya kuwekeza kama kufungua maeneo mengi zaidi ya burudani kwani hilo ndilo lilikuwa lengo la kuanzishwa kwa DDC,ikiwa ni pamoja na kuweka mahali ambapo watoto wataweza kucheza ili kuhakikisha shirika linajiongezea kipato na kuiongezea Serikali kipato pia,” alisema Waziri Simbachawene.
Simbachawene alitumia nafasi hiyo kuwaagiza Wakuu wa Mashirika ya Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanaandaa taarifa nyingine itakayohusisha mali zote za mashirika hayo.
Aidha ameutaka uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo kuwa wabunifu kwa kuanzisha masoko sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni mkakati wa kusogeza huduma kwa wananchi na njia ya kuongeza ajira kwa vijana.
Alilitaka Shirika hilo kuachana na mawazo ya kizamani na badala yake wajipange kimkakati ili kuendana na wakati ikiwemo kufikiria namna ya  kuwaza kushusha mizigo katika soko hilo kwani serikali haitaweza kuruhusu maroli ya mizigo kufika katika soko hilo ili kupunguza ya kuepuka msongamano katikati ya jiji.
Aliushauri uongozi huo uandae mikakati ya kuwezesha soko hilo kuwa la kiwango cha juu (Super Market) na kuwalipisha wafanyabiashara kiwango kinachoendana na bei halisi ya soko kama ambavyo wapangishaji wengine wamekuwa wakitoza ili kukuza kipato kwa Taifa.
Waziri Simbachawene ameahidi kushirikiana na mashirika hayo katika kutatua changamoto ambazo zinahitaji msaada wa uongozi na kuwataka wafanye kazi kwa bidii kwani Serikali ya Awamu ya Tano inahitaji watu wanaojituma na kuchapa kazi.
Awali akiwasilisha taarifa fupi ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam Meneja Mkuu wa Shirika hilo Rwandiko Manumbu alisema kuwa pamoja na changamoto wanazokumbana nazo Shirika limefanikiwa kutoa shilingi milioni 140/- kama gawio kwa mwanahisa wake ambaye ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
“Mhe. Waziri, kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Shirika hili tumeweza kutoa gawio la kiasi cha shilingi milioni 140/- kwa Halmashauri ya Jiji na haya ni mafanikio makubwa kwetu,” alisema Manumbu.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amempongeza Waziri Simbachawene kwa utayari wake wa kushughulikia changamoto zinazo yakabli mashirika hayo ikiwa ni pamoja na kutenga muda wake kuja kusikiliza matatizo yao.
Pamoja na pongezi hizo Mwita alishauri Shirika la Maendeleo la Dar es Salaam (DDC) kuangalia uwezekano wa kurejesha bendi za muziki kama ambavyo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alivyokuwa amedhamiria wakati wa uanzishwaji wa Shirika hili.
Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) na Shirika la Masoko Kariakoo ni mashirika ya Umma yanayoongozwa na Serikali kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam chini ya Sheria za Makampuni namba 2012 ya mwaka 1971 na Sheria ya Bunge namba 36 ya mwaka 1974, “The Kariakoo Market Corporation Act, 1974

WIZARA TATU KUSHIRIKIANA KUKABILIANA NA UVUVI HARAMU

May 26, 2017
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi kutoka Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Fatuma Sobo akizungumza wakati wa kikao baina yao na madiwani wa halmashauri  Jiji la Tanga,Mkurugenzi na wakuu wa idara ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha rasilimali za bahari zinatunza na kulindwa kilichofanyika mjini hap
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi kutoka Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Fatuma Sobo akielekeza jambo wakati wa kikao baina yao na madiwani wa halmashauri  Jiji la Tanga,Mkurugenzi na wakuu wa idara ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha rasilimali za bahari zinatunza na kulindwa kilichofanyika mjini
hap
 baadhi ya washiriki wa kikao cha pamoja yao na madiwani wa halmashauri  Jiji la Tanga,Mkurugenzi na wakuu wa idara ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha rasilimali za bahari zinatunza na kulindwa.
 Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga (CUF) Mohamed Haniu akiuliza swali kwenye kikao hicho
Picha ya pamoja
WIZARA tatu zinatarajiwa kushirikiana ili kuweza kukabiliana na wimbi la uvuvi haramu ambalo limekuwa tishio kubwa kwenye ukanda wa bahari ya hindi na maziwa hapa nchini  inayotishia usalama wa rasilimali zilizopo.
Hayo yalibainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi kutoka Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Fatuma Sobo wakati wa kikao baina yao na madiwani wa halmashauri  Jiji la Tanga,Mkurugenzi na wakuu wa idara ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha rasilimali za baharibzinatunza na kulindwa.

Wizara ambazo zitashirikiana ni za Maliasili na Utalii,Nishati na
Madini,Sheria na Katiba na Ofisi ya Rais kutokomeza suala hilo kwenye maeneo ya bahari na maziwa.

Alisema kupitia mpango huo wanaweza kufanikiwa kukabiliana na vitendo vya uvuvi haramu ambavyo vimekuwa vikifanyika kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini na kusababisha uharibifu wa mazalia ya samaki lakini pia kuleta madhara kwa viumbe.

Fatuma ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi upande wa wa Idara ya
Maendeleo ya Uvuvi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
anayeshughulikia masuala ya uendelezaji wa rasilimali za uvuvi
 
Aidha alisema anaamini kupitia kikao hicho madiwani wanaweza kutumia elimu walioipata kuifikisha kwa wananchi hao juu ya athari za uvuvi haramu ili kusaidia kupunguza wimbi la tatizo hilo hasa kwenye maeneo ya ukanda wa bahari ya hindi kwani wao ndio wanajua mabomu yanapigwa kwenye maeneo gani.
 
“Ninaamini kikao hiki kitakuwa mwanga mzuri kwenu nyingi kuona namna ya kusaidia harakati hizi za kupambana na suala la uvuvi haramu kwani limekuwa na athari kubwa lakini sisi kama wizara hivi sasa tunashirikiana na wizara nyengine kwa lengo la kuzibiti suala hilo“Alisema Fatuma.

Akizungumzia suala la wavuvi wan chi jirani kuingia kuvua hapa nchini alisema ni kosa la kisheria kwani sheria hairuhusu wao kuingia na kuacha kufanya shughuli za namna hiyo kwenye maeneo yetu hivyo wanapaswa kuacha kujihusisha na jambo hilo.
 
“Sheria haiwahurusu wavuvi kutoka nchi jirani kuvua kwenye nchi
nyengine zilizopo jirani bila kuwa na idhini ya mamlaka husika hivyo niwatake wenye tabia za namna hiyo kuacha mara moja “Alisema.
 
Akizungumza kwa upande wake, Naibu Meya wa Jiji la Tanga (CUF) Mohamed Haniu alisema anaamini kupitia elimu hiyo itawasaidia kushirikiana na kamati za BMU kupambana na uvuvi haramu.
 
“Nisema tunashukuru elimu hii ambayo ni muhimu kwa kutunza na
kuvilinda viumbe vya baharini hivyo tutashirikiana na kamati za BMU kuona namna ya kukabiliana na suala hilo “Alisema Naibu Meya huyo.

 Naye Mratibu wa Mradi wa Swiofish katika Halmashauri ya Jiji la Tanga Nkana Mwagala alitoa wito kwa jamii kutunza rasilimali za bahari kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.
 
Alisema kupitia kikao hicho wanaamini madiwani watakaa na wananchi hao ili kuweza kuwaelimisha madhara ya kufanya uvuvi haramu ikiwemo kuachana na suala hilo .

“Kwa sababu madiwani wanakundi kubwa la wananchi kwenye maeneo yao hivyo kupitia kikao hiki wanaweza kusaidia kuipa jamii uelewa kuhusu athari za uvuvi haramu lakini pia waweze mabalozi wazuri kuzilinda rasilimali za bahari kwa manufaa ya sasa na kizazi kijacho “Alisema.


ZINGATIA HAYA UNAPOTAKA KUENDESHA GARI UMBALI MREFU

May 26, 2017

Na Jumia Travel Tanzania

Linaweza kuwa si jambo la kushangaza kuwaona watu wakisafiri kwenye usafiri wao binafsi kuelekea mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Na hii ni kutokana na maendeleo na mabadiliko ya kiuchumi miongoni mwa watanzania wengi ambapo hapo awali walikuwa wanategemea usafiri wa umma.

Sababu za kusafiri zinaweza kuwa nyingi kama vile kifamilia, kutembelea ndugu na jamaa au vivutio mbalimbali vya kitalii. Lakini je ni wangapi wanayafahamu mambo ya kuzingatia kabla ya kuamua kuingia barabarani na usafiri binafsi kwenda umbali mrefu? Jumia Travel imekukusanyia masuala muhimu ambayo usipokuwa makini kuyafuata basi safari yako itakuwa ni shubiri badala ya asali huko njiani.

Jipange kwa safari nzima. Sidhani kama kuna jambo ambalo unaweza kufanikiwa bila ya kujipanga. Vivyo hivyo unapotaka kusafiri ni lazima uweke mipango madhubuti tangu mwanzo mpaka mwisho wa safari yako. Kwa mfano, safari itachukua muda gani, hoteli gani mtafikia, gari utakalolitumia litawatosha watu wangapi, gari litahitaji mafuta kiasi gani mpaka kumaliza safari, nini cha kufanya inapotokea dharura na kadhalika.   

Chunguza usafiri wako. Barabarani kuna mengi yanatokea ingawa kuna mengi unaweza kuyadhibiti endapo utachukua tahadhari kabla. Kwa mfano suala la gari kuharibika njiani linaweza kuepukika endapo utachukua muda wako kulipeleka kwa fundi kufanyiwa uchunguzi na matengezo pale yatakapohitajika. Huwezi jua inawezekana injini isingeweza kukupeleka hata nusu ya safari yako au jaribu kuvuta picha gari linapokuharibikia katikati ya msitu wenye wanyama wakali bila ya msaada.
Hakikisha usafiri wako umekidhi vigezo vyote vya kuwa barabarani. Kusafiri umbali mrefu hususani kutoka katikati ya jiji haimaanishi kwamba huko barabarani sheria hazifuatwi. Kwa hiyo hakikisha kuwa usafiri wako umekidhi vigezo vyote vya kuwepo barabarani kama vile leseni ya udereva, bima ya gari, leseni ya barabarani na sheria nyinginezo. Usipofanya hivi unaweza kujikuta unalipishwa faini, kukamatwa na hivyo kupotezewa muda ambao ilibidi uutumie kukufikisha huko uendako. Kwa mfano sio umefika Bagamoyo tu askari wa barabarani wanakukamata na kukuambia vibali vya gari lako kuwa barabarani vimekwisha muda wake.

Tarajia changamoto mbalimbali barabarani. Ni mara chache kusafiri barabarani bila ya kukutana na changamoto zozote kama vile foleni, njia kuwa mbovu, ukaguzi wa mara kwa mara, ajali na kadhalika. Hivyo lazima ujiandae kiakili wewe kama dereva pamoja na watu unaosafiri nao.
Usibebe mizigo mingi sana. Sawa mizigo ni muhimu kwa kuwa unasafiri umbali mrefu lakini kwa kufanya hivyo unaweza kujinyima fursa ya kubeba vitu vingine utakavyovutiwa navyo njiani. Hivyo basi hakikisha unabeba mizigo ambayo ni muhimu kwako kwani unaweza kupita sehemu na ukakuta vitu vya gharama nafuu ambavyo unaweza kununua.

Beba ramani ya kukusaidia huko uendako. Wengi wetu huwa tunapenda kwenda sehemu ambazo tunazifahamu hivyo inakuwa sio lazima sana kuwa na ramani ya kukupa mwongozo. Lakini siku hizi maendeleo ya teknolojia yamekuwa ni makubwa kwani sehemu nyingi zimewekwa kwenye ramani kupitia vifaa mbalimbali kama vile kompyuta, tabiti na simu. Mbali na teknolojia kurahisisha hilo lakini unashauriwa kubeba ramani ya karatasi, kwa mfano kama unanda Zanzibar unaweza kuwa na ramani inayokuonyesha sehemu zote za kule.
Kuwa na nyimbo au vitu vya kukuburudisha njiani. Kazi na dawa huwa wanasema Waswahili. Haimaanishi kwa sababu unasafiri umbali mrefu basi ndiyo uwe makini na usukani pasipo kujiburudisha. Beba vitu kama vile CD za muziki zenye nyimbo uzipendazo pamoja na michezo mbalimbali kwa ajili ya watoto wako kama unasafiri nao. Lakini pia hata vinywaji na vitafunwa vinaweza kuifanya safari iwe ni fupi na ya kuifurahia.

Beba pesa ya akiba. Unaposafiri njiani unaweza kukutana na changamoto ambazo zitahitaji pesa ya papo kwa papo ili kuweza kuzitatua. Hivyo hakikisha unakuwa na kiasi cha pesa taslimu kwani mara nyingi sehemu za kuzipata huwa ni nadra. Pia itakusaidia hata kununua vitu vya njiani, kwa mfano Morogoro kuna bidhaa nyingi sana kutoka kwa wakulima.  

Jaribu kuipumzisha simu yako kwa muda. Itakuwa haileti maana kuwa upo kwenye usafiri pamoja na wenzako au familia yako lakini unawasiliana na watu uliowaacha ulipotoka. Lengo la safari za namna hii mara nyingi ni kujaribu kubadili na kufurahia mazingira mapya. Basi jaribu kuendana na mazingira hayo kwa kuzungumza na wenzako ndani ya gari ninaamini kutaifanya safari kuwa ni ya kusisimua zaidi.  

Piga picha kwa ajili ya kumbukumbu. Ni muhimu kuwa na kumbukumbu ya baadhi ya matukio unayoyaona. Siku hizi kamera inapatikana kwenye simu za mkononi hivyo kurahisisha kuhifadhi kumbukumbu ya matukio mbalimbali. Basi hakikisha unapiga picha za sehemu na matukio utakayovutiwa nayo au hata wewe mwenyewe ukiwemo ili iwe kama ni ukumbusho kwako. Kwa mfano haiwezekani ukapita mbuga ya Mikumi bila ya kupiga picha ya Tembo au pundamilia wanaokatiza barabarani.
Kusafiri kwa kutumia gari binafsi hususani umbali mrefu ni starehe kubwa ambayo wengi bado hawajaigundua. Wapo wengine wanapanda ndege ili kuwahi kufanya vitu vingi huko waendapo pamoja na kuepuka uchovu. Lakini Jumia Travel inasisitiza kwamba kusafiri kwa njia ya barabara kunakupa fursa kubwa ya kujionea ni jinsi gani nchi yako imebarikiwa na fursa ya kujifunza mengi zaidi.

Fid Q, Snura, Madee kutumbuisha matamasha ya Taifa Moja Jumamosi hii

May 26, 2017
Wasanii wa kizazi kipya Fid Q, Snura, Madee, Dogo Njaja, Stamina na Navy Konzo wanatarajia kutoa burundani katika matamasha ya Taifa Moja ambayo yatafanyika kesho (Jumamosi) kwenye mikoa mine tofauti hapa nchi. 
 
Burandani hio itaenda sambasamba na kutoa elimu kwa Wananchi wa mikoa husika juu ya uhuru wa kutuma pesa bila mipaka ambayo ni ushirikiano wa makampuni matatu ya simu za mkononi kupitiia huduma zao Tigo Pesa, Airtel Money na Ezy Pesa. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Liginiku Milinga ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Fern Tanzania ambao ndio waratibu na waandaaji wa matamasha hayo alisema wasanii wote washathibitisha kushiriki kwao kwenye matamasha hayo na kwamba maandalizi yote yamekamilika huku akiwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kupata burundani toka kwa wasanii wakali hapa nchini na pia kupata elimu juu ya kutuma na kupokea pesa kwenda mtandao wowote hapa Tanzania kwa gharama ile ile.
Wasanii Stamina na Fid Q watambuiza kwenye tamasha litakalofanyika kwenye uwanja wa Mwembetongwa mjini Iringa wakati Dogo janja na Baba Levo wakifanya ya kwao kwenye uwanja wa Community Center grounds uliopo mjini Kigoma huku Snura na Madee wakiwashika vilivyo wakazi wa mji wa Tanga kwenye uwanja wa Tangamano. Navy Kenzo huku akitamba na wimbo wake wa kamati ya chini, atakuwa kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Sabasaba iliyopo mjini Morogoro.
Tangu tuanze kampeni yetu ya Taifa Moja tumekuwa tukitumia wasanii wetu kutoa elimu kwe Wananchi kupitia burudani na tumetapata mafanikio makubwa sana ya kufikisha ujumbe wetu wa uhuru wa kutuma pesa bila mipaka kupitia burudani kwa Watanzani. Naomba nitoe wito wangu kuwaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi kesho kushuhudia wasanii wetu ambao wamehaidi kutoa burundani ya uhakika.
Bali na kupata burundani, Watanzania wataweza kufahamu jinsi ya kujikwamua kiuchumi kwani kwa njia ya kutuma pesa kwenda mtandao wowote ule kwa gharama ile ile imetoa urahisi kwa kuongeza watumiaji wengi wa huduma ya kutuma pesa na hivyo kuwa rahisi Wananchi kupata huduma za kifedha.
Taifa Moja ni kampeini ambayo imedhaminiwa na taasisi za Financial Sector Deepening Trust of Tanzania (FSDT) pamoja na Bill & Melinda Gates Foundation huku ikiratibiwa na International Finance Corporation (IFC) chini ya muungano ya makampuni matatu ya simu za mkononi za Airtel Tanzania, Tigo Tanzania na Zantel kupitia huduma zao za Airtel Money, Tigo Pesa na Ezy Pesa.
BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA ARDHI KWA MWAKA WA FEDHA 2017/18

BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA ARDHI KWA MWAKA WA FEDHA 2017/18

May 26, 2017
NGEN1
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Naibu wake; Angeline Mabula wakiwa na watendaji wa Wizara na Taasisi katika picha ya pamoja baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.
NGEN2
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akipongezwa na baadhi ya Watendaji wa Wizara baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.
NGEN3
Waziri wa ardhi; Mhe. William Lukuvi na viongozi wakuu wa Wizara; Naibu wake; Angeline Mabula, Katibu Mkuu; Dkt. Yamungu Kayandabila na Naibu Katibu Mkuu; Dkt. Moses Kusiluka wakijadili jambo nje ya ukumbi wa bunge, baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.
NGEN4
Waziri wa ardhi; Mhe. William Lukuvi wakifurahia na watendaji wa Wizara na Taasisi baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.
NGEN5
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini; Edwin Ngonyani akipata elimu ya matumizi ya vifaa vya upimaji Ardhi vya kampuni ya Surveying Equipment Service Centre (EA) LTD/ SESC (EA) LTD katika eneo la bunge baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.
…………………………………………………
Waziri Lukuvi aahidi kasi ya Upimaji Nchini.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi aahidi ongezeko la Upimaji wa Ardhi Nchini baada ya kuwasilisha bajeti ya Wizara – Bungeni.
Akitoa ufafanuzi kuhusu kupatikana kwa vifaa zaidi vya upimaji, baada ya hoja za wabunge; Mhe. Lukuvi amesema Wizara imejipanga kutoa mafunzo kwa wapima wa Ardhi nchini na hivyo kasi ya upimaji itaongezeka nchini kwani vifaa hivyo vya aina ya RTK vina uwezo wa kupima ekari elfu 30 kwa wakati mmoja. Alisema, vifaa hivyo vitatolewa kwa Halmashauri nchini bila gharama. Aliongeza kuwa Serikali itanufaika kwa kupata ongezeko la mapato ya Kodi ya Pango la Ardhi zaidi.
Aidha, katika mwaka wa fedha 2016/17, Serikali iliahidi kuidhinisha ramani za Upimaji zenye viwanja 200,000 na mashamba 400. Hadi kufikia 15 Mei, 2017; ramani za upimaji zenye jumla ya viwanja 118,502 na mashamba 374 ziliidhinishwa. Katika mwaka wa fedha 2017/18 Wizara itaidhinisha ramani za upimaji zenye jumla ya viwanja 200,000 na mashamba 400.

WAFANYAKAZI MAHIRI WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI WATUNZWA

May 26, 2017
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima (wa kwanza kulia), akimkabidhi zawadi Afisa Mambo ya Nje, Bi. Eva Ng'itu kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa. Bi. Ng'itu amekuwa Mfanyakazi Hodari wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. Dkt. Mlima aliwapongeza na kuwasihi wafanyakazi waliofanya vizuri kuwa zawadi walizokabidhiwa iwe chachu ya kuongeza juhudi na ufanisi katika utumishi wao. 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akimpongeza Bi. Ng'itu kwa kuwa mfanyakazi Hodari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Bw. Mohammed Kheri kutoka Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar akipokea zawadi yake kwa kuwa mfanyakazi bora wa Idara hiyo. 
Bw.Joseph Mlingi akipokea zawadi kwa kuwa mfanyakazi bora kwa upande wa madereva wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Bw. Emannuel Luangisa akipokea zawadi yake ya kuwa mfanyakazi bora wa Idara ya Asia na Australasia. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora na Mratibu wa Mafunzo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Tagie Daisy Mwakawago naye akipokea zawadi ya ufanyakazi bora wa Idara ya Diaspora 
Bi Eva Kaluwa kutoka Idara ya Sera na Mipango akipokea zawadi yake kutoka kwa Dkt. Mlima. 
Bi. Kisa Mwaseba akipokea zawadi ya Mfanyakazi bora wa Idara ya Mashariki ya Kati. 
Bi. Upendo Mwasha akipokea zawadi ya mfanyakazi bora wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda. 
Bi. Nelusigwe kutoka Kitengo cha Ununuzi na Ugavi akipokea zawadi baada ya kuibuka mfanyajkazi bora wa Kitengo hicho. 
Bw. Erick Ngilangwa kutoka Idara ya Afrika akipokea zawadi ya mfanyakazi bora wa Idara hiyo 
Afisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Rose Mbilinyi akipokea zawadi yake kutoka kwa Dkt. Mlima. 
Katibu Mkuu Dkt. Mlima akizungumza katika kikao cha baraza la wafanyakazi la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Mambo ya Nje, Zanzibar akichangia jambo katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi. 
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza kwa makini Katibu mkuu alipo kuwa akizungumza nao 
Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu, Dkt. Mlima na wafanyakazi bora kutoka kwenye Idara na Vitengo vya Wizara. Mwanamke pekee aliyeketi ni Bi. Eva Ng'itu ambaye ameibuka mfanyakazi hodari wa Wizara nzima kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.

MBUNGE AWESO AMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUIPATIA VIFAA TIBA WILAYA YA PANGANI

May 26, 2017
Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kulia akimkabidhi vitanda moja kati ya 25 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Sabas Chambasi ambavyo ni miongoni mwa mgao wa vifaa tiba walivyopewa na Rais John Magufuli kwa ajili ya wilaya ya Pangani kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Issa
Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kulia akimkabidhi Mgao wa mashuka 50 kutoka kwa Rais John Magufuli Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Sabas Chambasi kwa ajili ya kusaidia huduma za afya kwenye wilaya ya Pangani katika halfa iliyofanyika kwenye hospitali ya wilaya ya Pangani juzi wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Issa
 Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kushoto akiwa ameambatana na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa wakitembelea hospitali ya wilaya ya Pangani kabla ya kukabidhi Msaada wa vifaa tiba ambavyo vimetolewa na Rais John Magufuli
 Mganga Mkuu wa wilaya ya Pangani,Dkt Juma Mfanga kulia akimueleza Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Changamoto zinazowakabili wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba ambavyo vimetolewa na Rais John Magufuli kwa Mbunge huyo kwa ajili ya wilaya ya Pangani ambayo ni mashuka 50 na vitanda 25
 Mganga Mkuu wa wilaya ya Pangani,Dkt Juma Mfanga kulia akielezea Changamoto zinazowakabili wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba ambavyo vimetolewa na Rais John Magufuli kwa Mbunge huyo kwa ajili ya wilaya ya Pangani wa pili kutoka  kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso
 Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso akizungumza katika halfa hiyo ambapo alimshukuru Rais John Magufuli kwa kuona umuhimu wa kusaidia vifaa ntiba wilaya ya Pangani
 Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa akizungumza katika halfa hiyo kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akizungumza katika makabidhiano hayo
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Sabasi Chambasi akizungumza katika halfa hiyo

Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso mara baada ya hafla hiyo kwa kumshukuru Rais John Magufuli kwa kuona umuhimu wa kusaidia vifaa tiba kwenye wilaya hiyo
 Picha ya pamoja baada ya makabidhiano hayo