ANGALIA PICHA MAMBA MKUBWA WA AINA YAKEAKAMATWA NIGERIA

May 01, 2014


Mamba huyu anaurefu wa miter 7 na Inakadiriwa kuwa na umri zaidi ya miaka 85, inasemekana kuwa mamba huyu amekula watu zaidi ya 200 katika umri wake.Kilio cha wanakijiji ndio kimesababisha mamba huyu kutegwa na kukamatwa kitaalam, hatahiyo 

SHEREHE ZA MEI MOSI ZAINGIA DOSARI, MFANYAKAZI WA IKULU AFIA UWANJANI DSM

May 01, 2014

Baadhi ya jamaa aliyoambatana nao wakimwangalia mara baada ya kufikishwa chumba cha huduma ya kwanza.

Akiingizwa kwenye gari la wagonjwa tayari kwa kupelekwa hospitali kwa hatua zaidi.

Mmoja wa watu aliokuwa nao ambaye yaelekea ni mfanyakazi mwenzake akiwa anaingia katika gari hilo huku akiwa amebeba nguo na viatu vya Rashid John Chilwangwa.

Gari la wagonjwa lililombeba likiondoka uwanjani kuelekea hospitali.
MAADHIMISHO ya Siku ya Wafanyakazi Kitaifa, maarufu kama Mei Mosi yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam yameingia dosari baada ya mmoja wa wafanyakazi kufariki dunia uwanjani kwa ghafla akiwa katika maadhimisho hayo.

Mfanyakazi huyo anayedaiwa kufanyakazi Ikulu alizidiwa ghafla akiwa katika maandamano na kupatiwa huduma za kwanza lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya na hatimaye kudaiwa kupoteza maisha akipatiwa huduma na madaktari na wahudumu kutoka kikosi cha msalaba mwekundu waliyokuwa katika maadhimisho hayo.

Thehabari.com ilishuhudia mfanyakazi huyo akiletwa katika kambi ya watu wa huduma ya kwanza iliyokuwa katikati ya uwanja wa Uhuru, kisha kupatiwa huduma ya kwanza bila mafanikio na baadaye alifariki dunia. Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika kundi ambalo lilimleta mfanyakazi huyo baada ya kuzidiwa ghafla lilimtaja kuwa jina lake ni Rashid John Chilwangwa.

Mmoja wa wafanyakazi waliyokuwa wameandamana na mfanyakazi huyo ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa yeye si msemaji akisimulia tukio hilo, alisema John Chilwangwa (45) walikuwa naye katika sherehe za maadhimisho na hali yake ilibadilika kabla ya kuingia uwanjani na aliomba aende kujisaidia haja ndogo baada ya hapo alianza kuishiwa nguvu.

“…Si tulishangaa alikaa muda kidogo akijisaidia baada ya kumfuata tulimkuta ametoka ndani ya choo na kuja nje na kisha kukaa kwenye tofali huku akisema anajisikia kuishiwa nguvu na hali ilibadilika ndo tukamleta hapa,” alisema shuhuda huyo.

Alipoulizwa hali yake kwa sasa ambapo alikuwa ameingizwa kwenye hema la huduma ya kwanza kwa wahudumu kutoka kikosi cha msalaba na madaktari alisema wamejaribu kumuhudumia lakini bahati mbaya amefariki dunia tayari. “…Tumeambiwa na madaktari kuwa ameshafariki tayari,” alisema shuhuda huyo ambaye alikuja na mgonjwa huyo.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia madaktari wakijaribu kumtundikia dripu huku wakijaribu kurudisha mapigo ya moyo kwa kushtua mara kadhaa lakini juhudi ambazo hazikuzaa matunda. Baada ya kubaini amefariki dunia walisita kumwekea dripu ambayo ilikuwa inaandaliwa na badaye walimfunika kwa shuka nyeupe na kuita gari la wagonjwa tayari kwa kumpeleka hospitali kwa uchunguzi zaidi. Hata hivyo hakupatikana mara moja daktari kuzungumzia kilichomsibu Chilwangwa.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AWASILI MJINI BUKOBA MKOA WA KAGERA JIONI HII KUWASHA MWENGE WA UHURU KESHO

May 01, 2014


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba jioni hii kwa ajili ya kuwasha Mwenge wa Uhuru kesho katika hafla itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Mkoa wa Kagera.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Skafu na Vijana wa 'Scout' wa mkoa wa Kagera, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba jioni hii kwa ajili ya kuwasha Mwenge wa Uhuru kesho katika hafla itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Mkoa wa Kagera.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi, waliompokea kwenye uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba leo jioni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhingo Rweyemamu, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba jioni hii kwa ajili ya kuwasha Mwenge wa Uhuru kesho katika hafla itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Mkoa wa Kagera.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili ya kabila ya Wahaya baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba jioni hii kwa ajili ya kuwasha Mwenge wa Uhuru kesho katika hafla itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Mkoa wa Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu, Fabian Masawe, akisoma Taarifa ya Mkoa mbele ya Makamu wa Rais Dkt. Bilal.

MAJI MAREFU MGENI RASMI MASHINDANO YA AWESO CUP

May 01, 2014
NA OSCAR ASSENGA, KOROGWE.
MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani “Maji
Marefu”anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa pazia la mashindano ya Vijana ya Kombe la Aweso Cup yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai Mosi mwaka huu kwenye kata ya Mswaha darajani wilayani hapa.

Mashindano hayo yameanzishwa na diwani wa kata ya Mswaha Darajani, Aweso Omari lengo likiwa kuinua vipaji vya soka kwa vijana ikiwemo kuwaepusha kukaa vijweni ambapo hutumia muda mwingi kufikiria kufanya vitendo viovu ambavyo sio vya kiungwana kwenye jamii husika.

Akizungumzia maandalizi ya mashindano hayo jana, Aweso alisema msimu huu mashindano hayo yanashirikisha timu kumi na tano tofauti na msimu uliopita ambapo kati ya hizo timu 10 zinatoka ndani ya kata hiyo na nyengine 5 zinatoka kwenye kata za jirani.

Alizitaja baadhi ya timu ambazo zitashiriki mashindano hayo kuwa ni kutoka vijiji vya Makuyuni, Kiloza, Gereza, Karekwa na Mgobe ambapo mshindi wa kwanza mpaka wa tatu watapata zawadi kutoka kwa muandaaji huyo ambapo yatafanyika kwenye uwanja wa soka wa kijiji cha Mswaha darajani.

Alisema mshindi wa kwanza atapata Mbuzi na Jezi seti tatu, mshindi wa pili atapata jezi seti mbili na mshindi wa tatu apate jezi seti moja na kila timu itakayoshiriki itapata mpira mmoja.

Hata hiyo alisema siku ya ufunguzi atawaalika madiwani kutoka kata nyengine lengo likiwa kuwapa hamasa ya kwenda kuanzisha mashindano kama hayo kwenye kata yao ili waweze kutimiza malengo yao ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya soka wilayani humo.

IGP, DCI WALA KIAPO CHA KUWA WAJUMBE WA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA

May 01, 2014

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akila kiapo cha kuwa mjumbe wa Tume ya utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji wa Mahakama kuu Mhe. Njengafibili Mwaikugile jijini Dar es Salaam jana .Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari polisi na Magereza.Katikati ni Msajili wa Mahakama kuu Bw.Benedict Mwingiwa (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Issaya Mngulu akila kiapo cha kuwa mjumbe wa Tume ya utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji wa Mahakama kuu Mhe. Njengafibili Mwaikugile jijini Dar es Salaam jana .Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari polisi na Magereza.Katikati ni Msajili wa Mahakama kuu Bw.Benedict Mwingiwa (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

Kamishna wa Utawala na Utumishi wa Jeshi la Polisi, Thobias Andengenye akila kiapo cha kuwa mjumbe wa Tume ya utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji wa Mahakama kuu Mhe. Njengafibili Mwaikugile jijini Dar es Salaam jana .Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari polisi na Magereza.Katikati ni Msajili wa Mahakama kuu Bw.Benedict Mwingiwa (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

WEMA, NAJMA WALINIFILISI SANA,AFUNGUKA MR BLUE

May 01, 2014

NYOTA wa Bongo Fleva, Herry Samir maarufu kama Mr. Blue amesema wasichana warembo, Wema Sepetu na Najma ambao aliwahi kutoka nao kimapenzi kwa nyakati tofauti miaka ya nyuma, walimfilisi kutokana na matumizi makubwa ya fedha alipotoka nao viwanja.

Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Mr. Blue, msanii aliyeanza kupata umaarufu akiwa bado kijana mdogo, alisema alilazimika kutumia fedha nyingi akiwa nao, kwani vinginevyo wangemuona hana pesa, kitu ambacho hakuwa tayari kuona kinatokea.

“Mademu wengi walikuwa wanapenda sana starehe, kila day (siku) wanataka twende kiwanja, ndiyo maana kama unakumbuka niliyumba kimuziki.

“Wanawake wengi niliotoka nao hawajulikani, ila kuna Wema na Najma, ilikuwa ukizama nao dukani lazima ufanye shopping (manunuzi) ya nguvu, kuanzia laki saba, nane na kuendelea ili wakuone unazo na mademu wengi wakisikia tu umepiga shoo, sms hazikauki kuomba uwatumie mawe (pesa),” alisema.

Kuhusu maisha yake ya sasa, Mr. Blue alisema yamebadilika sana, kwani hivi sasa ameoa mwanamke mwenye asili ya Kiarabu na amejaliwa kupata mtoto mmoja, hivyo ni baba wa familia ambaye pia anakaribia kumaliza mjengo wake siku si nyingi.

Hata hivyo alisema mkewe siyo maarufu, ana malengo na upendo kwani amekuwa akimuaga kila safari anayofanya na kwamba hata yeye anaporejea nyumbani, hupokelewa vizuri.

Mr. Blue ni mmoja kati ya wasanii wa muda mrefu ambao bado wanafanya muziki na wenye mashabiki wengi ndani na nje ya Bongo.
 
credit gpl

RAIS MSTAAFU MH. MKAPA AKABIDHI NYUMBA 30 MKOANI SINGIDA

May 01, 2014



7722 Email: drweyunga@gmail.com
NYUMBA MBILI ZA WATUMISHI WA AFYA KATIKA KIJIJI CHA SENENENFURU HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA AMBAZO ZIMEKABIDHIWA KATI YA NYUMBA 30 MKOANI SINGIDA NA NYINGINE 70 ZILISHA KABIDHIWA KATIKA MIKOA YA MTWARA NA RUKWA KATI YA NYUMBA ZINAZO JENGWA 310 NCHI NZIMA.
RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU MHE.BENJAMIN WILLIAM MKAPA AKABIDI NYUMBA 30 ZA WATUMISHI WA AFYA ZILIZOJENGWA NA TAASISI YA MKAPA KWA UFADHILI KUTOKA MFUKO WA DUNIA WA KUPAMBANA NA UKIMWI,KIFUA KIKUU NA MALARIA( GLOBAL FUND ) MKOANI SINGIDA ,AMBAZO ZIMEGARIMU JUMLA YA SHILINGI BILIONI 1,945,187,143/=.

RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU WA TANZANIA MHE. BENJAMIN WILLIAM MKAPA AKISUBIRIA KUVISHWA SKAFU NA GWARIDE LA VIJANA WA CHIPUKIZI BAADA YA KUWASILI KATIKA KIJIJI CHA SENENENFURU KWENYE HAFLA YA KUKABIDHI NYUMBA 30 ZA WATUMISHI WA AFYA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA , WA KWANZA KUSHOTO MKUU WA MKOA WA SINGIDA AKISHUHUDIA.

RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU WA TANZANIA MHE. BENJAMIN WILLIAM MKAPA AKIVISHWA SKAFU NA VIJANA WA CHIPKIZI BAADA YA KUWASILI KATIKA KIJIJI CHA SENENENFURU KWENYE HAFLA YA KUKABIDHI NYUMBA 30 ZA WATUMISHI WA AFYA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA.

RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU WA TANZANIA MHE. BENJAMIN WILLIAM MKAPA AKIKATA UTEPE KUASHIRIA KUZIFUNGUA NYUMBA 30 MKOANI SINGIDA.

RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU WA TANZANIA MHE. BENJAMIN WILLIAM MKAPA AKIWA NJE YA MOJA YA NYUMBA HIZO BAADA YA KUZI KAGUA.
RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU WA TANZANIA MHE. BENJAMIN WILLIAM MKAPA AKIPOKEA ZAWADI YA MBUZI WAWILI NA MAFUTA YA ALIZETI KUTOKA KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI WA KIJIJI CHA SENENENFURU WAKATI WA SHEREHE ZA MAKABIDHIANO YA NYUMBA 30. 

                                                                   Credit:Rweyunga Blog Singida

RC TANGA AONGOZA KUTUNDIKA MIZINGA YA NYUKI KOROGWE.

May 01, 2014




Mkuu wa mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu Chiku Gallawa jana aliongoza mamia ya wakaazi wa kijiji cha Kwamzindawa kilichopo kata ya Mnyuzi, Korogwe vijijini kutundika mizinga ya nyuki pembezoni mwa milima inayopakana na hifadhi ya asili ya Amani katika
kuadhimisha siku ya kutundika mizinga nchini ambapo kitaifa shughuli hiyo ilifanyika mkoani Katavi .
Maadhimisho hayo ya kimkoa yaliyoratibiwa na Wakala wa misitu Tanzania (TFC) kwa ushirikiano na Halmashauri ya wilaya ya Korogwe yalifanikisha utundikaji wa mizinga 45 iliyotolewa na TFC shughuli iliyofanywa kwa umakini na viongozi mbalimbali kwa ushirikiano na Wananchi wakiongozwa na Mkuu wa mkoa.
Katika hotuba yake mara baada ya zoezi hilo Mkuu wa mkoa alikipongeza kikundi cha ufugaji nyuki cha Malkia cha kijijini hapo ambacho ndiyo kimekuwa chachu ya kuendeleza ufugaji nyuki  waliouanzisha kwa jitihada zao binafsi na baadaye kupatiwa msaada wa vifaa vya kufugia na kurinia asali ikiwemo mizinga hiyo.
Gallawa aliongeza kuwa ni vyema kikundi hicho kikajenga mtandao wa ulinzi na utunzaji wa mazingira ili kuwavutia zaidi nyuki kuingia katika mizinga hiyo na kumwagiza Mkurugenzi Mtendaji kuwaandalia mafunzo ya kitaalamu wafugaji hao ili ufugaji huo ukue na kufikisha mizinga 100 hatimaye uweze kuwa na tija kwenye uchumi endelevu.
“Agizo la mkoa ni kila kikundi cha ufugaji nyuki kuwa na mizinga 100 hapo ndipo mnaweza kuona tija ya ufugaji nyuki ambao mtaji na uwekezaji wake ni mdogo,lakini faida ni kubwa.” Aliongeza Gallawa.
Kadhalika aliwashauri wafugaji hao kulima zao la alizeti ambalo huvutia nyuki hivyo itapelekea kupata faida mara zaidi hatimaye kufanikisha kipaumbele cha mkoa cha kumfanya mkazi wa Tanga kuongeza pato hadi kufikia  Tsh ml 1.5 kwa mwaka.
Awali katika risala yao iliyosomwa na Fatuma Kipara, kikundi cha ufugaji nyuki cha Malkia walimweleza Mkuu wa mkoa kuwa wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wataalamu wa sekta ya nyuki jambo linalowaathiri kwa kuwa hawatembelewi mara kwa mara.
Naye Afisa nyuki wa wilaya Vicent Mhezi, akisoma taarifa ya ufugaji nyuki alisema Wilaya ina vikundi vya ufugaji wa nyuki 38,vyenye wanachama 602, vikundi  vilivyosajiliwa ni 13 na kuongeza kuwa Korogwe imefanikiwa kuanzisha  ofisi ya usindikaji wa Mazao ya Nyuki iliyopo Bungu,ambapo kwa mwaka 2013,wamefanikiwa kusindika asali lita 500 yenye thamani ya Tshs 5,000,000/-
Diwani wa kata ya Mnyuzi Rajab Muhidin akitoa maelezo ya awali kuhusu kata yake kwa  Mkuu wa Mkoa.

Afisa Nyuki wilaya Vicent Mhezi akieleza teknolojia iliyotumika kutengeneza mizinga hiyo kwa Mkuu wa Mkoa

 Shughuli ya kutundika mizinga ikiendelea mara baada ya Mkuu wa Mkoa kuzindua zoezi hilo.
 Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga  Edith Mallya akiungana na Mkuu wa Mkoa katika kutundika mizinga
 Baada ya "tundikatundika" , tuliacha eneo hilo likionekana namna hii
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luten Mstaafu Chiku Gallawa akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Mzindawa
 Wananchi wa Mzindawa walioshiriki tukio hilo wakimsikiliza Mh.Mkuu wa Mkoa
  Mwisho Mkuu wa Mkoa alihitimisha shughuli hiyo kwa kutembelea banda la maonesho la kikundi cha Malkia kujionea  mazao yatokanayo na Nyuki

MAKORORA WAFANYIA BIASHARA CHAKULA CHA MSAADA.

May 01, 2014


MBUNGE wa Korogwe vijijini Stephen Ngonyani juzi aliiweka kikaangoni serikali ya kijiji cha Makorora akihoji uhalali wa kuwauzia wananchi chakula cha msaada kwa kwa bei ya Tsh
100/= kwa kilo badala ya Tsh 50/= zilizoelekezwa na serikali vitendo ambavyo vimewakera wananchi.

Hatua hiyo ya kuhojiwa kwa serikali ya kijiji hicho iliyotakiwa kutoa maelezo ilikuja baada ya risala kusomwa kwa mbunge huyo na mwenyekiti wa vijana wa tawi la CCM Ringo Mjenga aliyesema,haki haikutendeka kutokana na kuuziwa mahindi ya msaada kwa bei iliyo kinyume na  utaratibu.

Baada ya mwenyekiti wa serikali Aziza Shemkunde kujitetea kuwa  kutokuwepo wakati maamuzi yakifanywa ili kuongeza nguvu ya kupata fedha za kusukuma miradi mingine,mbunge Ngonyani alisema ameisamehe serikali hiyo kwa vile ni kosa la kwanza akiwaasa kutorudia makosa.

“Kuhusu chakula cha msaada serikali ya kijiji ilikosea,kwa kuwa mwenyekiti wa kijiji ni mgeni nimemsamehe vinginevyo ningeondoka naye”alisema Ngonyani huku akitoa Tsh 80,000/= ili ziweze kurejeshwa kwa wananchi ambao walinunua chakula hicho kwa bei ya Tsh 100/=.

Aidha alimtaka afisa mtendaji wa kijiji hicho Bakari Zayumba kusimamia vizuri urejeshwaji wa fedha hizo kwa waathirika wa tukio hilo bila ya kuwepo kwa malalamiko ya aina yeyote ile miongoni mwao.

Pamoja na kutoa fedha hizo ili kuweza kurejeshwa kwa wananchi ambao waliuziwa chakula kwa bei kubwa kama walivyomlalamikia mbunge huyo aliwasisistiza viongozi kutokukiuka maagizo yaliyowekwa na serikali.

Mbali na maelekeo hayo Ngonyani aliwaasa wananchi wa kijiji hicho cha Makorora kutokushabikia mambo kwa kuwasilishabaadhi ya kero ambazo hawana ushahidi nazo huku akiwataka kuendelea kumpatia ushirikiano yeye pamoja na diwani wao njia itakayosaidia kuharakisha maendeleo.

Vilevile alikemea vikali tabia tabia za baadhi ya wananchi kutokuwa tayari kushiriki misalagambo kwenye miradi ya maendeleo ambapo alimtaka afisa mtendaji wa kijiji hicho kuendelea kuona hamasa watu kushiriki kazi hizo sanjari na kuwashughulikia wakaidi.

“Atakayezuia misalagambo jina lake liorodheshwe lifikishwe kwenye vyombo vya kisheria,ili miradi yetu ifanye vizuri tuna haja wote kushiriki pindi tunapohitajika,kusiuwepo kwa visingizio”alisema Ngonyani  akisisitiza umuhimu wa viongozikukosoana wakitumia vikao.

Akielezea sakata hilo Afisa kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe Kakulu Lugembe alisema ni kinyume cha Sheria Serikali ya kijiji kujipangia bei ya chakula cha msaada kinyume na mwongozo wa bei ya Serikali na kuahidi kulifuatilia suala hilo kwa hatua zaidi


Mbunge wa Korogwe vijijini Stephen Ngonyani akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Makorora kata ya Magoma mwishoni mwa wiki. (Picha na mtandao)

JK AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI KITAIFA LEO

May 01, 2014


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wa serikali na wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA)  wakiangalia maandamano ya wafanyakazi wakati wanaingia uwanjani hapo leo katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) leo Mei 1, 2014 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, Naibu Rais TUCTA, Notburga Masikini na Katibu Mkuu wa TUCTA, Nicolaus Mgaya na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
 Mdundiko ulioendelea
 Benki ya Twiga Bancorp ilishiriki maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya wafanyakazi kwa chini ya Chama chao cha Wafanyakazi TUICO na kujumuika na wafanyakazi webnzao duniani kopte katika maandamano kama inavyoonekana pichani.
 Wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania wakishiriki katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Kitaifa Jijini Dar es Salaam leo.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali TSN, nao walishiriki katika maandamano hayo.
Wafanyakazi wa Uhuru FM nbao walishiriki Kikamilifu katika maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Steve Gannon akionesha sha furaha kwa siku ya wafanyakazi
 
 Kampuni ya Bia ya Serengeti nayo ilishiriki katika maadhimisho hayo na pichani ni wafanyakazi wake wakiwa uwanjani hapo.
Benki ya Posta Tanzania (TPB) ni moja ya taasisi za fedha zilizo shiriki maadhimisho hayo. 
 Askari wa Wanyama Pori wakishiriki katika maadhimisho hayo na katika gari ni ngozi ya Mamba