DC DENDEGO AWAFUNDA WAZAZI TANGA.

April 17, 2014
NA SALUMU MOHAMED,TANGA.
MKUU wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego amekemea vikali tabia ya baadhi ya wazazi wilayani hapa ambao huwaoza mabinti zao wakati bado wapo masomoni kwa kuwataka kuacha mara moja la sivyo watachukuliwa hatua kali zidi yao ili kukomesha vitendo hivyo kwenye jamii.

Aliyasema hayo  wakati wa mahafali ya 12 shule ya sekondari ya St.Christina iliyoko Kange Maziwa mjini hapa na kusema kuwa tabia ya wazazi kuwapa waume mabinti zao wakati wakiwa shuleni inasikitisha na hivyo ofisi yake imeadhimia kuikomesha.

Alisema kitendo hicho kinawanyima mabinti hao haki ya kupata elimu na kuweza kumkomboa mwanamke katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii hasa kwa wakati uliopo  sasa wa sayansi na teknolojia ulimwenguni.
Dendego alisema kupitia mahafali hayo wazazi na walezi ikiwemo wakina mama na wababa kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja ili kuweza kutokomeza vitendo vya wanafunzi wa kike kupewa wanaume wakati wakiwa masomoni.
“Nadhani hao wazazi wenye tabia hii kwa kweli  wako na jambo kama sio maslahi ni shida za papo kwa papo---sera ya mwanamke kuongoza na kuweza bila kuwezeshwa haijawafika baadhi ya wazazi na hivyo nawataka kuelimika” alisema Dendego
 

Alisema ofisi yake haitomvumilia mzazi wala mlezi yoyote atakaebainika kumuoza binti yake wakati yuko katika masomo na hivyo atahakikisha tabia hiyo inakomeshwa ili kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu na kuweza kuleta mapinduzi ya ukombozi wa wanawake katika kujiletea maendeleo.

Akizungumzia wazazi kuwabidiisha watoto wao katika elimu, Dendego aliwataka kuwa na ada ya kuwafuatilia maendeleo yao shuleni na kuacha kuwaruhusu kushiriki katika shughuli ambazo zinaweza kumtoa kimawazo katika masomo yake.
 

Alisema kuna baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwatumia vibaya watoto vipindi vya likizo kwa kuwapa kazi ambazo ziko nje ya uwezo wao pamoja na kuwashirikisha katika biashara na kusahau kuwa vipindi hivyo ni vya maandalizi ya kujiandaa na masomo yalioko mbeleni kwao.
“Ni jambo la kushangaza kuona vipindi vya likizo kwa wanafunzi wazazi wanafurahia kama wamepata kitu kizuri---kumbe furaha yao ni kuwatumikisha katika kazi ambazo ziko nje ya uwezo wao na kusahau kuwa nihatari” alisema Dendego
Alisema ili kuwawezesha watoto kufanya vizuri vipindi vyote vya masomo yao ni jukumu la wazazi kuwabidiisha katika masomo vipindi vya likizo ili karo wanazolipa faida yake iweze kuonekana na kuacha kuzilaumu shule kuwa hazisomeshi.

MBUNGE MTATA WA ZANZIBAR AFUNGUKA KWENYE FACEBOOK YAKE KUHUSU KUSUSIA BUNGE NA SABABU UCHWARA NA ZA KITOTO ONA HAPA LIVE!!

April 17, 2014

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba tunaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) tumefanya uamuzi wa hekima na busara wa kuondoka kwenye Bunge la Katiba baada ya kutoridhishwa na mambo yafuatayo:

1. CCM kupindua Rasimu ya Katiba ya Wananchi na kupenyeza Rasimu yao yenye lengo la kuwalinda watawala na mafisadi.

2. Waziri William Lukuvi kutumia Kanisa kupandikiza chuki na kuchochea vurugu kwa kurejea kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba ukipitishwa muundo wa Muungano wa Shirikisho la Serikali Tatu, jeshi litachukua madaraka na kwamba Zanzibar itaunda Dola ya Kiislamu dhidi ya Wakristo.

3. Mjadala wa Bunge la Katiba kugeuzwa jukwaa la kuhubiri matusi, chuki, ubaguzi wa rangi na ukabila.

Tunawaomba wananchi watulie na wasubiri kauli za viongozi wao juu. Wasiwe na khofu. Kwa kupitia njia za amani na demokrasia, Katiba ya Wananchi itapatikana.
Na Ismai Jussa Facebook
MPANGO MKAKATI WA NATIONAL HOUSING CORPORATION MKOA WA KATAVI/RUKWA 2010/2011

MPANGO MKAKATI WA NATIONAL HOUSING CORPORATION MKOA WA KATAVI/RUKWA 2010/2011

April 17, 2014


9 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Katavi  Ndugu Nehemia Msigwa juu ya miradi ya ujenzi wa nyumba itakayofanyika ndani ya mkoa wa Katavi.Pichani ni Michoro ya Nyumba zitakazojengwa mkoani Katavi na Shirika la Nyumba ya Taifa,ambapo wilaya ya Mlele ,Shirika la Nyumba linajenga nyumba 60 na zitachukua  miezi nane kukamilika. 
…………………………………………………………………………….
Shirika la Nyumba Mkoa wa Katavi/Rukwa  umejizatiti katika kutekeleza mpango Mkakati wa Shirika wa miaka mitano yaani 2010/2011 hadi 2014/2015 kama ilivyokwa mikoa mingine katika Shirika la Nyumba la Taifa. Mpango huu umekuja wakati mwafaka kushughulikia tatizo la uhaba wa nyumba za makazi na biashara kwa Mkoa huu wa Katavi/Rukwa. Katika Mpango Mkakati huu, Shirika limejiwekea Dira, Dhima, Maadili ya Msingi, Malengo na Matarajio ya Shirika.
Wakati  Utekelezaji wa Mpango huu unaendelea kwa sasa,  unasaidia sana katika kukuza uchumi kwa katika mkoa wetu kwa njia ya kuongeza Ajira mbalimbali pamoja na kodi, na hili linatokana na uwezo mkubwa wa sekta ya Nyumba katika kukuza uchumi katika eneo husika. Zaidi sana ni Msisitizo wetu NHC-Katavi/Rukwa kuwa,  Maendeleo ya Mikoa hii, lazima yaendane na Ujenzi wa Nyumba Bora za Makazi na za Biashara. Na kwa hili NHC tunaelekea kukamilisha malengo yetu mawili ya kuwa Kiongozi Mahiri katika Kuendeleza Milki na Pia kuwa Msimamizi Mahiri wa Miliki si hapa Katavi tu bali Tanzania Nzima.
Kwa sasa kuna miradi Mitano ambayo ipo katika hatua mbalimbali ambayo inatekelezwa na Shirika katikakufikia malengo shirika tuliyojiwekea.
Kuna Mradi wa Ilembo ambao unatarajiwa kukamilika 30/Mei/2014. Mradi huu una jumla ya nyumba 90. Ni mradi mkubwa kwa eneo kama la Mpanda ambao utakuwa name gharama ya said I ya Tsh. 3.1 Bil. kuwepo na umesaidia sana kutia hamasa kwa wananchi wa Mpanda kuongeza kasi katika sekta ya ujenzi wa Nyumba, pia umesaidia kuleta mandhari bora ya makazi. Ni matarajio yetu,  kwa kuwa tumeshaanza kuuza nyumba hizo,  Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma, Mashirika Binafsi, Halmashauri za Miji ambazo katika mkoa wa katavi watumishi wake wengi wanakosa Nyumba bora za kuishi watazichangamkia Nyumba hizi kwa kuzinunua na kuwapangiza watumishi wake. Vilevile ni matarajio yetu kuwa Wananchi nao kila mmoja binasfi watajitokeza kwa wingi kununua Nyumba hizi ambazo ni Bora kwa makazi.
Katika Wilaya Mpya ya Mlele, Mradi wa nyumba za Gharama nafuu upo katika hatua za awali, ni mmatarajio yetu mara baada kukamilika kwa Mradi huo tatizo la uhaba wa nyumba Bora za Kuishi pale Inyonga, ambapo ndipo makao makuu ya Wilaya, litakuwa limedhibitiwa kwa kiasi kikubwa, rai yetu ni ileile kwa taasisi za serikali, Mashirika ya Umma, pamoja na Mashirika Binasfi zichangamkie fursa hiyo ya kupata nyumba kwa ajili ya Watumishi wake.
Miradi kama hii ya Ilembo-Mpanda pamoja na Inyonga tunatarajia pia kuipeleka katika Wilaya za Kalambo pamoja na Nkasi mkoa wa Rukwa na Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi. Miradi katika wilaya hizi itaanza mara tu taratibu husika zitakapo kamilika. Ninatoa Ari kuwa halmashauri ambazo zitatoa ushirikiano chanya kwa NHC katika kutatua tatizo hili la uhaba wa nyumba bora za makazi kwa wafanyakazi wake na wananchi kwa ujumla ndio itakayofikiriwa zaidi, hii ni pamoja na changamoto za bei kubwa za Viwanja tunazokumbana nazo kutoka kwa halmashauri husika.
Katika orodha ya Miradi ambayo ipo katika Mkoa huu ni pamoja na Mradi wa Jengo la Biashara litajengwa katika eneo la Paradise-Mpanda hapa Mkoani Katavi na Mradi wa Nyumba za Makazi katika eneo la Jangwani-Sumbawanga Mkoani Rukwa.  Miradi hiyo yote imeshatangazwa kwa ajili ya Kupata wakandarasi watakao jenga miradi hiyo, hivyo muda si mrefu miradi hiyo itaanza rasmi.
Katika hatua nyingine, ili kutatua tatizo la uhaba wa kumbi za mikutano, Shirika la Nyumba la Taifa kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji ya Mpanda watajenga Ukumbi wa Kisasa wa Mikutano katika eneo la madini (Madini Plot). Huu ni mradi mwingine katika Mji wa Mpanda ambao si tu utaleta mandhari nzuri kwa Mkoa wa Katavi bali pia Utafanya Mkoa wa Katavi kuwa Kitovu cha mikutano muhimu ya Ushirikiano kwa mikoa ya kanda hii ya ziwa Tanganyika na Nchi jirani, hivyo pia kuchangai ukuaji wa uchumi katika mkoa huu.
Napenda pia kuchukua fursa hii kuzishauri Halmashauri za Miji taasisi za serikali, mashirika ya umma yote yanao jiusisha na utoaji wa huduma za miundo mbinu (Maji, Umeme pamoja na Barabara) kuwa sisi NHC ni wabia wao wakubwa kwani tunachangia kwa kiasi kikubwa kuwatafutia wateja wapya katika kila Mradi husika. Hivyo pindi tunapoanza ama hata kabla ta kuanza mradi husika huduma zao zinahitajika.
MPANGO WA SHIRIKA LA NYUMBA WA KUSAIDIA VIJANA KWENYE HALMASHAURI ZA WILAYA NA MIJI MASHINE ZA KUFYATULIA MATOFALI
Katika kuunga mkono jitihada za dhati zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  kuongeza ajira za vijana na kupunguza umaskini hapa nchini na hasa Mikoa ya Katavi na Rukwa, Shirika limeamua kutoa mashine za kufyatulia matofali kwa Halmashauri zote zilizoko katika Mikoa hii, zikiwemo Halmashauri za Mlele, Nsimbo, Mpanda Mji pamoja na Halmashauri ya Mpanda Vijijini kwa Mkoa wa Katavi, Pia Halmashauri Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi-Namanyere Pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo katika Mkoa wa Rukwa.
Mashine hizo zitatumiwa na vikundi vya vijana vitakavyoundwa na Halmashauri kwa kushirikiana na Meneja wa Mikoa wa NHC. Kila kikundi cha vijana kitapewa msaada wa mashine nne (4) ambazo, kila mashine itakuwa ikihudumia vijana wapatao 10 hivyo vijana 40 katika kila Halmashauri.  Pamoja na msaada wa mashine, Shirika litatoa Shilingi laki tano (500,000/=) kwa kila kikundi kama kianzio cha vijana hao kununua vifaa muhimu vya kuwezesha kazi ya kufyatua matofali kuanza. Aidha, vikundi hivyo vya vijana vitaweza baadae kuunda SACCOS zao na hivyo kupanua shughuli zao za kiuchumi.
Ili kufanikisha mpango huo,  Shirika kwa kushirikiana na Wakala wa Utafiti wa Vifaa Bora vya Ujenzi wa Nyumba (NHBRA) iliyo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, pamoja na Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) litatoa mafunzo ya siku 21 kati ya mwezi Desemba 2013  na Januari 2014 kwa wakufunzi wapatao 50, ya namna ya kutumia mashine hizo. Wataalam hawa ndio watakaotumika katika kuvifundisha vikundi vya vijana katika Halmashauri kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2014.
Shirika la Nyumba la Taifa linatanguliza Shukrani kwa kutuunga mkono katika kufanikisha jambo hili muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.
“KATAVI  BILA UMASIKINI INAWEZEKANA, KWA KUWA MAISHA NI NYUMBA” 
MAISHA YANGU NYUMBA YANGU 
 IMETOLEWA NA 
NEHEMIA L. MSIGWA
MENEJA WA MKOA
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

WACHEZAJI MABORESHO STARS WATAJWA

April 17, 2014

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza majina ya wachezaji 16 waliochaguliwa katika maboresho ya timu ya Taifa Taifa Stars kwenye hoteli ya Hill View jijini Mbeya.

Wachezaji hao ni kipa Benedicto Tinoko Simwanda (Temeke), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).

Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).

Washambuliaji ni Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga) na Bayaga Atanas Fabian (Mbeya).

Alisema mpango huu wa kuboresha timu ya Taifa ambayo inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ni endelevu na kusisitiza kuwa hata wale 18 walioachwa watafuatiliwa na TFF na kuitwa panapokuwa na mahitaji.

“Hawa wote wapo kwenye database ya TFF na hawataachwa tu hivi hivi wapotee,” alisema kocha Mayanga.

Wachezaji ha0 waliingia kambini mjini Tukuyu, Machi 21 mwaka huu na wamefanya mazoezi kwa pamoja kwa karibu wiki nne sasa kabla ya kuchujwa.

Wachezaji 16 waliochaguliwa wanatarajiwa kuondoka Tukuyu kesho (Aprili 18 mwaka huu) na kwenda kwenye kambi ya Taifa Stars katika Hoteli ya Kunduchi ambapo wataungana na wachezaji wa Taifa Stars wa siku zote.

Baadaye watachujwa tena ili ipatikane timu moja ya Taifa iliyoboreshwa.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjro Premium Lager inaunga mkono utaratibu huu wa maboresho ya Taifa na imewekeza zaidi ya dola milioni 2 kwa mwaka kudhamini Taifa Stars. Huu ndio udhamini mkubwa zaidi ambao Stars imewahi kupata tangu kuanzishwa kwa TFF.

LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA MEI 10
Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) itakayochezwa kwa ligi ya mkondo mmoja katika vituo vitatu vya timu tisa kila kimoja inatarajia kuanza Mei 10 mwaka huu.

Timu ya kwanza kutoka katika kila kituo ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015. Kwa vile ligi hii haina mdhamini, hivyo timu zitajigharamia kwa kila kitu.

Vituo vitakavyotumika kwa ajili ya RCL, kanuni pamoja na ratiba vitatangazwa kabla ya kuanza kwa ligi hiyo. Pia kituo kitakachoteuliwa kwa ajili ya ligi hiyo, timu yake haitapangwa katika kituo husika ikiwa ni moja ya njia ya kuhakikisha kanuni ya mchezo wa kiungwana (fair play) inazingatiwa.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)