COASTAL UNION NA MTIBWA SUGAR NGOMA SARE,YASHINDWA KUFUNGANA MKWAKWANI LEO

January 31, 2015
WACHEZAJI WAKISALIMIANA KABLA YA KUANZA MPAMBANO HUO LEO

KIKOSI CHA COASTAL UNION KILICHOCHEZA NA MTIBWA SUGAR LEO UWANJA WA CCM MKWAKWANI

KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR KILICHOCHEZA NA COASTAL UNION LEO





LICHA YA CHANGAMOTO NYINGI BARA LA AFRIKA LINAPIGA HATUA - ZUMA

January 31, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisoma makabrasha ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU unaofanyika kwa siku mbili jijini Addis Ababa kuanzia leo. Nyuma ya Mhe. Rais ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb). Waziri wa Jinsia na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Sophia Simba (Mb) na Balozi wa Tanznia nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz (mwenye ushungi).






Na Ally Kondo, Addis Ababa
Wakuu wa Nchi za Afrika wamekumbushwa kuwa, Mwaka 2015 umeingia lakini Bara la Afrika bado linakabiliwa na changamoto nyingi ambazo kama hazitapatiwa ufumbuzi ustawi wa bara hilo utaendelea kudumaa. Kauli hiyo ilikuwa inarudiwa mara kwa mara na viongozi waliopata fursa ya kuhutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa siku ya Ijumaa tarehe 30 Januari 2015.

Changamoto hizo ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi, ugaidi, migogoro ya kutumia silaha, ukatili wa kutisha, biashara haramu ya binadamu, umasikini na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. Walishauri katika mwaka wa 2015 lazima matatizo hayo yajadiliwe kwa kina kwa madhumuni ya kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu.

Alipokuwa anahutubia mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Nkosazana Zuma alisema kuwa, licha ya changamoto hizo, Bara la Afrika linapiga hatua kimaendeleo na kwamba Agenda 2063 inayowasilishwa katika Mkutano huo inatoa wito kwa Serikali na sekta nyingine kushirikiana kwa pamoja ili kukuza uchumi kwa kuweka mkazo kwenye ubunifu katika sekta ya kilimo, usindikaji wa mazao na ujenzi wa miundombinu.

Mhe. Zuma alisisitiza umuhimu wa kutumia fedha za ndani kwa ajili ya kugharamia miradi ya kipaumbele ambayo imezingatiwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka 10 ambao nao utawasilishwa katika mkutano huo. Alieleza kuwa Sekretarieti imefanyia kazi pendekezo la kutafuta vyanzo mbdala vya fedha ambapo Mawaziri wa Fedha walijadili na ripoti yao itawasilishwa wakati wa mkutano huo. Umoja wa Afrika pia umeanzisha Mfuko Maalum utakaozinduliwa wakati wa mkutano huo kwa ajili ya kuhifadhi fedha hizo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Ban Ki-moon alieleza kuwa mwaka 2014, AU na UN zilishirikiana kutafuta amani katika nchi zenye migogoro. Alisema mafanikio makubwa yalipatikana na hivyo kusisitiza kuwa pande zilizosaini mikataba ya amani lazima zitekeleze vipengele vya mikataba hiyo. Alitoa mfano wa Mkataba wa Arusha na kusema kuwa pande zinazohusika zitekeleze makubaliano ya kugawana madaraka. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kukitokomeza kikundi cha waasi cha FDLR kinachoendesha uasi wake Mashariki mwa DRC.

Mhe. Ban Ki-moon pia aliwakemea viongozi wa Afrika wanaong’ang’ania madaraka. Aliwashauri viongozi hao waache tabia hiyo na kuruhusu demokrasia ichukue mkondo wake.
Rais wa Kikao cha 69 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Sam Kutesa pamoja na mambo mengine, alizungumzia mabadiliko ya mfumo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Alisema katika uongozi wake atafanya jitihada kuhakikisha kuwa mfumo wa Baraza hilo, chombo ambacho alikitaja kama kisichokuwa na demokrasia kuliko vyombo vyote duniani unafanyiwa mabadiliko.

Viongozi hao pia walihimiza juhudi za kutafuta tiba na chanjo ya ugonjwa wa Ebola na kusisitiza kuwa kampeni ifanywe ili nchi zilizoathirika na ugonjwa huo zisamehewe madeni.

MEYA MANISPAA MOROGORO, WAANDISHI WA HABARI WAPATA AJALI

January 31, 2015

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ( wa kwanza kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro , Said Amanzi , wakipita eneo ambalo gari la namba SM 4151 Nissan iliyokuwa ikitumiwa na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo , ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30 alasiri eneo la Mzambarauni Darajani -Msamvu barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .Meya huyo na watu wengine watatu walijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kulazwa wakindelea kupatiwa matibabu.
Gari la Meya likiwa halitamaniki.
Wasamalia wakimuwahisha Hospital,Mmoja wa majeruhi mara baada ya kupata ajali eneo la Mzambarauni Darajani -Msamvu barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .
Hili ndilo basi lililogongana na Gari ya Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo ,(45) akiwa amelazwa wodi namba tano ya daraja la kwanza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kujeruhiwa kufuatia gari yake SM 4151 ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30 alasiri eneo la Mzambarauni Darajani , Msamvu Barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam ,mbali na Meya huyo na watu wengine watatu ,Dereva Mwambala Ally (55), na waandishi wa habari , Anita Chali (30) pamoja na HUSSEIN Nuha (28) pia walijeruhiwa na kulazwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu. ( Picha na John Nditi).
Mwandishi wa habari,Anita Chali akiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kujeruhiwa kufuatia gari waliyoipata,walipokuwa kwenye kazi na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe akionesha eneo ambalo gari la namba SM 4151 Nissan iliyokuwa ikitumiwa na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo , ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30 alasiri eneo la Mzambarauni Darajani , Msamvu Barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .Meya huyo na watu wengine watatu walijeruhiwa na kupimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kulazwa wakindelea kupatiwa matibabu.

Na John Nditi ,Morogoro
MEYA wa Halmashauri ya Manispaa Morogoro , Amir Nondo (45), dereva  na waandishi  wa habari wawili wamepata ajali   baada ya  gari walilokuwa wakisafiria kugongwa na basi la abiria lenye namba za usajili T 831 CEH, aina ya Scania mali ya kampuni ya Happy Africa na kujeruhiwa  sehemu mbalimbali za miili yao na kulazwa  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Tukio hilo lilitokea Januari 30, mwaka huu majira ya saa 9: 30 alasiri , eneo la Msamvu Mzambarauni darajani katika barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam, ambapo basi hilo lilikuwa likotokea mkoani Njombe.

Majina ya watu hao wengine waliojeruhiwa na kulaza katika wodi za daraja la kwanza katika hospitali ya rufaa ya mkoa , ni dereva wa gari la Meya, Mwambala Ally (55) , na waandishi wa habari ambao ni wapigapicha vituo vya televisheni , Anitha Chali (30) pamoja na Hussein Nuha (28).

Mstahiki meya huyo  aliyekuwa kwenye gari ya Halmashauri ya Manispaa hiyo  yenye namba za usajili SM 4151, ikiendeshwa na Mwambala  ambamo pia walikuwemo waandishi wa habari hayo na alikuwa katika msafara wa ziara ya kikazi ya mkuu wa mkoa huo,Dk Rajab Rutengwe.

Meya Nondo akizungumzia  ajali hiyo, akiwa wodini akipatiwa matibabu  ,sambamba na majeruhi wengine alisema baada ya kufika eneo la Mizambarauni, Darajani, lilichomoka pembeni basi la abiria ililokuwa likitokea Njombe kuelekea  Dar es  salaam, na kuligonga kwa mbele gari alilokuwemo.

Mashuhuda wa ajali hiyo  waliwaambia waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio,  kuwa  chanzo cha ajali hiyo ni basi la abiria mali ya kampuni ya Happy Africa, kuingilia msafara huo wa mkuu wa mkoa uliokuwa ukielea mjini baada ya kukagua shughuli za ujenzi wa vyumba vya maabara na kuzungumza na wananchi wa Kata ya Bigwa katika  Shule ya Sekondari Sumaye.

Mkuu wa mkoa kwa takribani wiki mbili amekuwa katika ziara katik halmashauri saba za mkoa huo kwa ajili ya kukagua shughuli za ujenzi na umaliziaji wa maabara tatu kwa kila shule ya skondari ya Kata na pia kutumia fursa hiyo kujitambulisha , kusikiliza kero na kuzipatia majawabu ya msingi.

Januari 29 na 30 mwaka huu ilikuwa ni zamu ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na Shule ya sekondari Sumaye kilikuwa ni kituo chake cha mwisho katika ziara hiyo na baadaye kufanyika kwa majumuisho ya ziara hiyo Januari 31, mwaka huu mjini Morogoro.

Hata hivyo baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa ya mkoa , viongozi mbalimbali walifika kuwajulia hali  wakati wakiendelea kupatia matubabu na madaktari mbingwa wa hospitali hiyo, akiwemo Mganga mkuu wa mkoa , Godfrey Mtei.

Mstahiki Meya Nondo ameumia sehemu ya kichani na mkononi , wakati na mpiga picha Anita Chali, ameumia  kichwani, huku dereva pamoja na  Hussein wakiumia zaidi  kwenye paji la uso na kichwani huku Hussein akisaidiwa na mashine ya kupumulia (oxygen).

 Kufuatia tukio hilo Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa mkoa imesema itatoa taarifa ya ajali hiyo  jumamosi ya  Januari  31, mwaka huu.

SIMBA YAITUNGUA JKT RUVU BAO 2 - 1 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO

January 31, 2015

 Beki wa timu ya Simba,Hassan Isihaka (26) akiangalia namna ya kumzuia Mshambuliaji wa Timu ya JKT Ruvu,Jabir Aziz katika mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi pinde kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.Simba imeshinda Bao 2-1.
 Nyanda wa Timu ya Simba,Ivo Mapunda akiwania mpira wa juu na Mshambuliaji wa timu ya JKT Ruvu,Samuel Kamuntu katika mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi pinde kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.Simba imeshinda Bao 2-1.
 Weeee.........
 Wachezaji wa Timu ya JKT Ruvu wakishangilia goli lao la kusawazisha dhidi ya Simba,katika mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi pinde kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.Simba imeshinda Bao 2-1.
Kiungo wa JKT Ruvu akiruka daruga .
 Kocha wa Timu ya Simba akiwapa mawaidha wachezaji wake.

CHIPUKIZI WA UVCCM WAJIFUA VIKALI TAYARI KWA KILELE CHA MIAKA 38 YA CCM KESHO

January 31, 2015

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mratibu wa Maadhimisho ya Miaka 38 ya CCM, Emmanuel Nchimbi, walipokuwa wakikagua mazoezi ya vijana wa Chipukizi wa CCM ya paredi na halaiki kwa ajili ya Maadhimisho ya Kilele cha Miaka 38 ya CCM, yatakayofanyika Kitaifa kesho kwenye Uwanja wa majiMaji mjini Songea.
 Vijana wa Chipukizi wa CCM waliopo katika mazoezi ya halaiki na paredi kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 38 ya CCM mjini Songea, wakikipiga saluti wakati wa mazoezi ya mwisho leo kwenye uwanja wa Majimaji
 Kijana wa Chipukizi wa CCM Mbaraka Ngonyani akionyesha umakini wake wakati akipiga saluti wakati wa mazoezi hayo ya mwisho leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa  UVCCM Sixtus Mapunda wakitazama mazoezi ya mwisho ya Chipukizi hao
 Mshika bendera ya CCM kwenye kikosi cha Bendera cha Gwaride la Umoja wa Vijana wa CCM, Sharif Mohammed na wenzake wakipita kwa ukakamavu mbele ya jukwaa kuu wakati wa mazoezi ya mwisho ya gwaride na halaiki kwa ajili ya Kilala cha Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM yanayofanyika kesho Kitaifa kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma 
 Vijana wa Chipukizi wa CCM wakionyesha ukakamavu wakati wa mazoezi yao ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea
 Vijana wa Chipukizi wa CCM wakionyesha ukakamavu wakati wa mazoezi yao ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea
 Vijana wa Chipukizi wa CCM wakionyesha ukakamavu wakati wa mazoezi yao ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea
 Vijana wa Chipukizi wa CCM wakionyesha ukakamavu wakati wa mazoezi yao ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea
 Vijana wa Chipukizi wa CCM wakionyesha mazoezi ya ukakamavu wakati wa mazoezi yao ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea
 Vijana wa Chipukizi wakionyesha ohodari wao wa mazoezi ya 'kikomandoo' wakati wa mazoezi yao ya mwisho ya paredi na halaiki kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya miaka 38 ya CCM kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea
 Chipukizu hao wakiwa kwenye mazoezi ya halaiki
Mmoja wa Chipukizi wa CCM waliokuwa katika mazoezi hayo akisaidiwa baada ya kuanguka kutokana na mazoezi hayo ya mwisho kupamba moto. Alipata ahueni baada ya kupatiwa huduma ya kwanza. (Picha zote na Bashir Nkoromo)
 MATUKIO BUNGENI- MJINI DODOMA

MATUKIO BUNGENI- MJINI DODOMA

January 31, 2015
1
Spika wa Bunge la Jamhuri, Anne Makinda akieleza jambo Januari 31, 2015  Bungeni mjini Dodoma ambapo mkutano wa 18 wa Bunge hilo unaendelea.
2
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji George Masaju akitoa ushauri kwa Bunge la Jamhuri.
3
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Dkt. Festus Limbu, akijibu hoja za wabunge waliochangia kwenye taarifa yake.
4
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akijibu hoja za kamati zilizoelekezwa katika wizara yake.
5
Mbungge wa Kawe, Halima Mdee akitoa mchango wakati wa kujadili taarifa za kamati za Bunge, bungeni mjini Dodoma.
Habari Picha na Hussein Makame-MAELEZO, Dodoma
………………………………………………………………………………………..
KAMATI za Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) na ile ya Hesabu za Serikali (PAC), zimeridhishwa na mafanikio na hatua zilizochukuliwa na Serikali kwa kuongeza mapato yake na kushughulikia changamoto zinazoikabili katika kutekelza majukumu yake.
Kufuatia hali hiyo, Bunge limepitisha taarifa za kamati hizo na nyingine tatu, huku Serikali ikiahidi kufanyia kazi yale yote yaliyopendekezwa kwenye taarifa hizo ili kulipeleka Taifa kule kunakotakiwa.
Taarifa za Kamati ambazo Bunge limezipitishwa jana na juzi usiku ni za Kamati ya Bajeti, Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Hesabu za Serikali (PAC), Miundombinu na Nishati na Madini.
Akihitimisha hoja yake, Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC  Rajabu Mbarouk   aliipongeza Serikali na Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia kwa hatua alichokua kwa watendaji wa Serikali waliobainika kutumia vibaya fedha za umma.
“Mimi ni mpinzani lakini kwa hili, kwa kweli nimpongeza Waziri kwa sababu jana aliniletea list (orodha) karibu ya halmashauri zote nchini ambazo wakurugenzi amewachukulia hatua, kilichobaki ni mimi kuichukua ile taarifa na kumpelekea kwa CAG kwa ajili ya kuihathibitisha” alisema Mbarouk.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Zitto Kabwe aliipongeza Malmalaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuongeza mapato na kwamba wameiomba iongeze mapatao katika miaka ijayo ili kuifanya mamlaka hiyo iwe na tija kwa taifa.
“Ni lazima tuwe wakweli, Mamlaka ya Bandari imeongeza sana sana ufanisi katika kazi zake, mapato yameongezeka kutoka shilingi Bilioni 320 mpaka shilingi Bilioni 537 katika kipindi cha miaka miwili” alisema Zitto.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba aliithibitishia kamati na wabunge waliotoa michango yao kuwa wamepokea michango yao na wataifanyia kazi.
“Kwanza nisema ndugu Mwenyekiti, tumewasikia wabunge, tumepokea waliyoyasema na tutayafanyia kazi, tupo kwa ajili hiyo” alisema Naibu Waziri Nchemba.
Alisema tangu mwaka wa fedha ulipoanza, mkakati wa Wizara chini ya usimamizi wa Waziri wa Fedha ilikuwa ni kuhakikisha kila fedha inapokusanywa inakwenda pale ilipokusudiwa.
Alifafanua kuwa hata hoja za baadhi ya wabunge kuwa kuna miradi imepata mgawo sifuri, inawezekana hiyo sifuri ni ya fedha zile zinazotoka nje.
“Naongea hili kwa uhakika, mwaka wa fedha uliooanza tu tulitoa Bilioni 500 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na mpaka wizara zingine wakashangaa wakauliza hizi fedha mmekosea au ndivyo kweli zinatakiwa zije” alisema na kuongeza:
“Walidhani ni za mishahara, haikuzoeleka kutokea fedha nyingi ndani ya mwezi wa kwanza wa bajeti kwa ajili ya shughuli za maendeleo”
Hivyo aliwaomba wabunge wazingatie mambo mamwili, moja Waziri ameweka utaratibu kwamba kila taasisi inapopokea fedha za maendeleo ni lazima ipeleke mrejesho imetumia fedha zile kwa shughul gani na mradi ule uonekane kabla fedha zingine hazijakwenda.
Alisema jambo la pili ni nia ya Serikali kuhakikisha kwamba fedha zilizotengwa kwa ajili ya mifuko na matumizi maalum ya miradi ya maendeleo na kwamba kuanzia mwezi Februari wanarekebisha utaratibu wa kutengeneza mchanganuo wa fedha kuhakikisha fedha hizo zimekwenda kwenye miradi ya maendeleo.
Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri unatarajiwa umeahirishwa hadi Jumatatu ambapo bunge hilo linataraji kupokea taarifa za Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji.
MAFUNZO YA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII (SOCIAL MEDIA) YAFANYIKA MJINI ZANZIBAR

MAFUNZO YA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII (SOCIAL MEDIA) YAFANYIKA MJINI ZANZIBAR

January 31, 2015

1
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Elimu Zanzibar (ZEDO) Ussi Said Suleiman akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Social Media huko Chuoni kwao Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
2
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis (alie simama) akiwahutubia washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya matumizi ya Mitandao ya kijamii (Social Media), hawapo pichani yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu Zanzibar kwa kushirikiana na Kigamboni Community Centre KCC kutoka Dar es Salam, huko Chuoni kwao Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
3
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimskiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis (hayupo pichani).  
4
Mgeni rasmin Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis (wakatikati) waliokaa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya matumizi ya Mitandao ya kijamii (Social Media).
Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.