WAGONJWA 3000 WANUFAIKA NA HUDUMA YA KUPATIWA MATIBABU YA MACHO TANGA.

May 24, 2015


WAGONJWA wapatao 3000 kutoka maeneo mbalimbali mkoani Tanga wenye matatizo ya macho wameanza kunufaika na huduma za kufanyiwa uchunguzi wa  pamoja na matibabu kwenye Hospital ya Shifaa Charitable Health Centre iliyopo mjini hapa.

Matibabu hayo yaliyoanza kutolewa Mei 16 mwaka huu ambayo yalimalizika jana yakiwa na lengo la kuwafanyia upasuaji wa aina mbili wananchi wenye matatizo ya macho ili kuweza kubaini matatizo wanayokabiliana nayo na kuyapatia huduma.

Akizungumza jana, Naibu Mudir wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Center,Sheikh Salim Bafadhil alisema kuwa upasuaji huo unalenga kwenye mambo makuu mawili yakiwemo ya kuondoa mtoto wa jicho na utandu uliopo ndani ya macho ambayo inaendesha na hospitali hiyo chini ya udhamini wa Al Basar International Foundition kutoka Saudi Arabia.

Alisema kuwa zoezi hilo linaendeshwa na madaktari kumi na mbili waliotoka nchini Pakistani wakiongozwa na daktari Fakhruddin Dakhan ambapo kwa siku wanahudumia wagonjwa wa macho wapatao 300 ambayo wanakwenda kwao kwa ajili ya matibabu.

   “Mpaka jana(juzi) tumeweza kufanya upasuaji zaidi ya wagonjwa 130 na kubwa ni kuangalia matatizo makubwa kwenye macho kama vile kuondoa motto kwenye jicho na kuondoa utandu  kwenye macho kwa kushirikiana na madaktari hao “Alisema Naibu Mudir huyo.

Aidha alisema kuwa lengo kubwa lao ni kuhakikisha wanatoa huduma kwa jamii ya wananchi wenye matatizo hayo ili waweze kupata nafuu na kuweza kufanya kazi mbalimbali za kijiingizia vipato kama ilivyokuwa kawaida yao kabla ya kukumbana na changamoto hizo.

JK AKIONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU ya CCM Taifa (NEC) MJINI DODOMA

May 24, 2015

Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kwenye ukumbi wa NEC ,Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
………………………………………………..
Angalia picha za mkutano wa halmashauri kuu ya ccm mei 23 mjini dodoma.





BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, LIU DONG AZINDUA TAMTHILIA YA TUOANE 'LETS GET MARRIED'

May 24, 2015

 Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Tamthilia mpya ya Tuonae ,Lets Get Married iliyichezwa na wachina na kutafsiriwa kwa kiswahili. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar e Salaam jana. Kulia ni Ofisa kutoka ubalozi wa China, ambaye alikuwa ni mkalimani wa balozi huyo, Yetianfa Attache.
  Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong (kulia), akipeana mkono na Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal 'Shetta' wakati wa uzinduzi wa Tamthilia hiyo.

Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong (kulia), akipeana mkono na Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal 'Shetta' wakati wa uzinduzi wa Tamthilia hiyo.

 Maofisa wa Kampuni ya StarTimes wakifurahia jambo kwenye uzinduzi huo.
 Wanahabari wakichukua tukio hilo.
 Warembo wa StarTimes wakiwa tayari kwa zoezi la kuzindua Tamthilia hiyo. Kutoka kulia ni Hadija Saidi, Nyachilo Bunini na Fausta Mushi.
 Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal 'Shetta'  (katikati), akiwa na wadau wengine kwenye uzinduzi huo.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale


BALOZI wa China nchini Tanzania, Liu Dang amesema ushiriano wa kirafiki baina ya Tanzania na China ni muhimu sana katika ukuzaji wa sekta ya utamaduni.


Kauli hiyo aliitoa wakati akihutubia katika uzinduzi wa Tamthilia ya Tuonane 'Lets Get Married iliyochezwa na wachina baada ya kutafsiriwa kwa lugha ya kiswahili.


"China na Tanzania ndugu na ushirikiano na ubadishilianaji katika sekta mbalimbali hasa sekta  ya kiutamaduni zinahistoria ndefu hivyo zinapaswa kudumishwa" alisema Balozi Dong.


Alisema Rais wa China Xi Jingping alipotembelea Tanzania mwaka jana serikali za hizi nchi mbili zilipeana vizuri mawazo na kusaini mikataba mingi mbalimbali ya ushirikiano ambapo ziara hiyo iliziletea nchi hizi mbili mafanikio makubwa na kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya historia ya uhusiano baina yao.


Akizungumza katika uzinduzi huo Mchambuzi wa Vipindi wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Rehema Kisyombe alisema kutokana na ushiriano mzuri wa nchi hizo kwa upande wao StarTimes wameadhimia kuudumisha kwa njia ya burudani kwa kuleta vipindi mbalimbali kutoka china.


Alisema kwa kutambua hilo StarTimes imekuwa ikileta tamthilia mbalimbali za kichina zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ambapo mpaka hizi sasa wamekwisha onesha nne kupitia chaneli ya Kiswahili ijulikanayo kwa jina la Star Swahili.


Kisyombe alizitaja tamthilia hizo kuwa ni Mapambano, Ujana wangu, Matumaini ya Baba na Hot Mom ambazo zilipokelewa vizuri na watamazaji wa chaneli hiyo na sasa wanawaletea tamthilia hiyo ya Tuoane. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

TANZANIA KATIKA UMOJA WA MATAIFA WIKI HII

May 24, 2015

Na  Mwandishi Maalum, New York
Umoja wa Mataifa wiki hii, umekamilisha mikutano  muhimu miwili kati ya mingi, ambapo  ujumbe wa Jamhuri ya  Muungano  wa Tanzania ulioshiriki majadiliano  ya mikutano hiyo waliiwakilisha vema nchi yao.
Moja ya mikutano hiyo  ni ule   wa  marejeo  ya Mkataba wa kuzuia usambaaji na uzalishaji   wa silaha za nyukilia, matumizi yake, ikiwa ni pamoja na silaha nyingine za maangamizi ( NPT),   Mkutano huu ambao umefanyika kwa mwezi  mzima,  ukitawaliwa na majadiliano   makali  juu ya  mada mbalimbali muhimu zinazohusiana na  marejeo  ya mkataba huo. Bado hadi siku ya mwisho  ya mkutano ( Ijumaa) wajumbe wamemaliza mkutano pasi kufikia makubaliano ya  pamoja ya vipengele kadhaa vya tamko la mwisho la mkutano.
Katika kile kilichooneka wazi  kwamba wajumbe wamekubali kuto kukubaliana,  ni kwa  baadhi ya  mataifa  hasa yale ya magharibi na yenye silaha za nyukilia kutoonyesha utayari na utashi wa kisiasa wa  kuungano  mkono  baadhi ya  mambo kadhaa  likiwamo  la  kufanyika kwa mkutano   wa Ukanda Huru  usio na  silaha za Nyukilia katika Eneo la Mashariki ya  Kati .
Mataifa kama vile Marekani,  Uingereza na Canada yalisimamia kidete misimamo yao ya kupinga kuingizwa katika   tamko  la mwisho la mkutano wa NPT sehemu inayopendekezwa kufanyika kwa mkutano huo huko  Mashariki ya Kati, kwa kile walichodai kwamba baadhi ya  mataifa yamelipenyeza suala hilo  bila ya   ushirikishwaji wa nchi  nyingine ikiwa Israel jambo ambalo wamesema hawakubaliani  nalo.
 Mkutano  kuhusu ukanda huru usio wa silaha za nyukilia katika  eneo la Mashariki ya Kati,  umeshindikana kufanyia kwa muda mrefu sasa licha  ya maazimio mbalimbali yanatoaka  ufanyika.
Kushindwa kwa mkutano huo ambao unaelekezwa kama muhimu kwa mustakabali wa hali ya  amani na usalama  katika eneohilo,  unatokana kwa kiasi kikubwa kukosekana kwa uungwaji mmono  usio na shaka kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwamo Israeli ambayo imekuwa ikilalamikwa na baadhi ya mataifa ya Kiaarabu.
Israel si mwanchama wa NPT. lakini pia inasadikiwa   inamiliki silaha za nyukilia  ingawa  haijatamka hadharani.  Mataifa mengi yakiwamo yakiiarabu yamekuwa yakilitaka  taifa hilo kutamka mbele ya   Jumuiya ya Kimataifa kwamba inamiliki  silaha hizo lakini imekuwa ikikingiwa kifua na baadhi ya  mataifa makubwa.
Eneo jingine ambalo  wajumbe wameshindwa kukubaliana kwa kauli moja ni pendekezo   la kuingizia kwenye mkataba huo    sehemu itakayozungumzia  madhara ya kibinadamu yatakayo na  matumizi ya silaha za nyukilia.  Eneo hili nalo  limezua mjadala mzito kiasi kwamba licha ya  umuhimu  wake kwa uhai wa mwanadamua na viumbe hai likashindwa pia kufikia  makubaliano  ya pamoja.
 Rasmu ya tamko  la mwisho la mkutano  huo  limepitishwa kwa  vifungu kutokana na kile ambacho wajumbe wamesema ni kutoridhishwa kwa maudhui mazima ya  tamko hilo huku wengine wakieleza kwamba, baadhi ya vifungu ambayo vilipitishwa kwa  makubaliano wakati wa majadiliano ya wiki nne  havikuingizwa katika  tamko hilo

Wazungumzaji wengi  katika siku ya mwisho ya mkutano huu ambao ulikwenda hadi saa tatu  usiku, siku ya  ijumaa, wameelezea masikitiko yao  ya kukosekana kwa fursa ya  kusukuma mbele utekelezaji wa  NPT kwa sababu tu ya baadhi ya nchi kusimamia maslahi binafsi badala ya maslahi ya jumla.
Mkutano wa pili  ambao nao ulikuwa na mvutano wa aina yake  ni ule uliokuwa ukijadili  maandalizi ya  ajenda na malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 ( SDGs). Mkutano huu wa wiki moja na ambao  pia ulimalizika  siku ya ijumaa, wajumbe licha ya kukubaliana na  maudhui mazima ya  haja na umuhimu wa  kufanyika kwa tathmini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa  SDGs,  wajumbe walishindwa kukubaliana kwa kauli moja mada au ajenda  zitakazo jadiliwa wakati wa mkutano wa  Kisiasa wa Ngazi ya Juu wa  viongozi  Wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika  mwezi Septemba  2015
Mkutano huo wa Kilele wa Kisiasa wa viongozi  unatarajiwa  kupokea na kupitisha ajenda na malengo ya  maendeleo endelevu baada ya 2015,   mkutano ambao pia utakuwa na  miduara ya  majadiliano   ya maada mbalimbali.
 Katika  maandalizi ya   mkutano huo, Rais wa Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa aliziomba nchi wanachama  kuunda  mada zikazojadiliwa katika mkutano huo, maanda mabazo kimaudhui zinatakiwa kwenda na  SDGs.
Kwa wiki kadhaa  nchi wanachama   kupitia makundi yao ya kikanda  walikuwa na kazi kubwa ya kubuni mada hizo,  kuzijadilia na kisha kukubaliana zile ambazo wanaamini  ndizo muhimu.
Mada ambazo zimependekezwa  ni  pamoja na mada itakayojadili   kumaliza umaskini na tatizo la njaa, kukabiliana na ukosefu wa  usawa,  uwezeshwaji wa wanawake na wasichana bila kuacha mtu nyuma, kukuza  uchumi endelevu na  kuleta mabadiliko katika   uzalishaji na kiwango cha matumizi  na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi  ili kuilinda dunia.
Mada nyingine zinazopendekezwa ni  kujenga ufanisi, uwajibikaji ili kufikia maendeleo endelevu, kukuza ushirikiano wa kimataifa, kujenga misingi imara ya uwajibikaji na taasisi jumuishi ili kufikia maendeleo endelevu na  kukuza ushirikiano wa kimataifa.
Pamoja na kukuballiana juu ya mada hizo,  washiriki wa mkutano  huu walishindwa kukubaliana juu ya maudhui pana   iliyoainisha kila  mada. Kutokana nakwamba  kila nchi au kundi wakilishi lilikuwa na  tafsiri tofauti ya maelezo ya  ziada ya  mada hizo.
 Matokeo ya  kushindwa kukubaliana   kuhusu maudhui pana au maelezo yakina ya baadhi  mada na baada ya majadiliano ya kujaribu kupata muafaka kati ya pande zinazopinga kushindwa kuafikiana,   Wenyeviti- wenza wa majadiliano hayo  walieleza kwamba kutokana na wajumbe  kutokubaliana basi mada hizo zitapelekwa  kwa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa maamuzi.
Ilikubaliwa katika mkutano huo kwamba  mada hizo ziwasiliwe kwa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, bila  ya maelezo ya ziada kuhusiana na  mada zenyewe kwa vile nchi wanachama zilishindwa kukubaliana.