BENKI YA NMB KUENDELEA KUTOA MIKOPO KWA WAENDESHA BODABODA NA BAJAJI LENGO KUWAEPUSHA NA MIKATABA YA KINYONYAJI

May 25, 2023



Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga akizungumza wakati wa halfa hiyo


Sehemu ya Waendesha pikipiki alimaarufu Bodaboda na Bajaj wakimsikiliza kwa umakini Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Madaraka Elizaberth Chawinga katika kikao ambacho kiliitishwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga


Na Oscar Assenga,TANGA

BENKI ya NMB tawi la Madaraka Jijini Tanga limeadhimia kuendelea kutoa Mikopo kwa waendesha Bodaboda na Bajaji kwa lengo la kuwaepusha kujiingiza kwenye mikataba ya kinyonyaji hatua ambayo imechangia kudoofisha jitihada zao za kujikwamua kiuchumi.


Meneja wa NMB tawi la Mdaraka Jijini Tanga, Elizabeth Chawinga akieleza mipango ya benki hiyo kuwakwamua kiuchumi waendesha bodaboda na bajaji  kwenye kikao maalum kilichowahusisha Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, viongozi wa bodaboda,bajaji na wamiliki kilichofanyika katika Bwalo la Polisi Mkoani Tanga.

Katika kikao hicho, Meneja huyo wa NMB alisema, benki yake tayari imeshaanza utaratibu wa kutoa mikopo kwa waendesha bodaboda hatua ambayo lengo lake ni kuwakwamua kiuchumi na kuwaondoshea changamoto ya kuingia kwenye mikopo yenye mikataba migumu.

“ NMB tunaendelea kutoa mikopo kwa bodaboda na bajaji, tayari tumetoa bajaji na guta,hivyo karibuni sana, wahusika lazima wafuate taratibu ikiwemo kuwa na leseni ya kutumia chombo cha moto,uthibitisho wa wenyeviti wa mitaa na taratibu nyingine muhimu”alisema Chawinga.

Meneja huyo wa Benki ya NMB tawi la Madaraka aliendelea kusema kwamba, kupitia utaratibu huo wa utoaji mikopo ya vitendea kazi hivyo wataweza kuwakomboa wajasiriamali hao huku akiwasihi kufungua Akaunti kwenye taasisi hiyo ya fedha ili kupata huduma stahiki kirahisi.

Kwa mujibu wa Chawinga, mikopo hiyo inaendelea kutolewa kwa waendesha Bajaji na Bodaboda ni yenye masharti nafuu na mkopaji atakuwa akilazimika kulipa kwa Wiki hadi pale atakapokuwa amefanikiwa kumaliza deni lake kwenye benki hiyo ya NMB tawi la Madaraka.

Aidha Chawinga alisema kwamba,huduma hiyo kwa wajasiriamali hao itakuwa endelevu huku akitoa wito kwa kuwataka kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo inayopatikana kwenye benki hiyo ambayo imejipambanua katika kuwakomboa Wananchi wenye kipato cha chini.

NMB mbali na kuhusika kuwawezesha kwa kuwapatia mikopo yenye Masharti nafuu wafanyabiashara wadogo lakni pia imekuja na huduma mbalimbali likiwemo suala la utoaji wa Bima hatua ambayo lengo lake ni kulipa fidia kwa wahanga pindi majanga yanapowakuta,

Mwisho.



RPC TANGA AWATAKA WAENDESHA BODABODA KUTII SHERIA

May 25, 2023

 

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Henry Mwaibambe akizungumza na wamiliki,waendesha bodaboda na bajaji,viongozi wa Serikali za mitaa na viongozi wa vyama vya waendesha Bodaboda katika Halmashauri ya Jiji la Tanga,

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Henry Mwaibambe akizungumza na wamiliki,waendesha bodaboda na bajaji,viongozi wa Serikali za mitaa na viongozi wa vyama vya waendesha Bodaboda katika Halmashauri ya Jiji la Tanga,

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Henry Mwaibambe akizungumza na wamiliki,waendesha bodaboda na bajaji,viongozi wa Serikali za mitaa na viongozi wa vyama vya waendesha Bodaboda katika Halmashauri ya Jiji la Tanga,
MKUU wa Polisi wilaya ya Tanga(OCD) Enock Ngonyani akizungumza wakati wa kikao hicho
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga akizungumza wakati wa kikao hicho
Sehemu ya wamiliki,waendesha bodaboda na bajaji,viongozi wa Serikali za mitaa na viongozi wa vyama vya waendesha Bodaboda katika Halmashauri ya Jiji la Tanga wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe
Sehemu ya wamiliki,waendesha bodaboda na bajaji,viongozi wa Serikali za mitaa na viongozi wa vyama vya waendesha Bodaboda katika Halmashauri ya Jiji la Tanga wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe


Na Oscar Assenga,TANGA

WAENDESHA Bodaboda Jijini Tanga wametakiwa kutii sheria na kutambua kuwa shughuli wanayoifanya ni halali kama ilivyo kwa kazi nyingine na kwamba kazi wanayoifanya siyo kama waganga wa kienyeji ambayo kila mmoja hutumia mtindo ‘Style’ ya aina yake katika kuagua.

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Henry Mwaibambe alitoa Wito huo wakati akizungumza na wamiliki,waendesha bodaboda na bajaji,viongozi wa Serikali za mitaa na viongozi wa vyama vya waendesha Bodaboda katika Halmashauri ya Jiji la Tanga,

Katika kikao hicho kilicholenga,kukumbushana na kuelimishana juu ya umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani na suala zima la ulinzi na Usalama Jijini Tanga,Kamanda Mwaibambe alisema Bodaboda na Bajaji wanapaswa kujitambua na kuzingatia Sheria.

Alisema kwamba, kazi hiyo ya Bodaboda inapaswa kufanywa kwa kuzingatia misingi ya sheria huku akiwataka ,kuzingatia suala la kufahamiana baada ya kuwa kila mmoja amesajiliwa katika Chama husika hatua ambayo itasaidia kudhibiti vitendo vya uhalifu kwenye Jiji hilo la Tanga,

“Usalama kwetu Bodaboda ndio kila kitu, mshirikiane vizuri na wenyeviti hawa wa mitaa, msikae na wahalifu kwenye vijiwe vyenu…”alisema Kamanda Mwaibambe huku akilaani tabia za baadhi ya Bodaboda kujihusisha na vitendo vya uporaji wa Simu na uhalifu mwingine.

Kamanda huyo wa Jeshi la Polisi Mkoani Tangaaliwataka waendesha bodaboda hao kujali maisha yao kwa kutokubali kutumbukia kwenye vitendo vya uhalifu kwa maelezo kuwa wako wanaoingia bila kujua na hata pale wanapobaini wamekuwa wazito katika kutoa taarifa.

“ Tuishi maisha ya kufahamiana, tujali maisha yetu tunapokutana na mtu hatu muelewi kwenye vituo vyetu tuone taarifa. Uporaji Simu imekuwa ni changamoto hivyo tufahamiane na Tanga tuna deni kubwa kuendelea kudumisha amani na usalama”alisema SACP Henry Mwaibambe.

SACP Henry Mwaibambe amewaasa waendesha bodaboda ba bajaji hao kutohusika katika kusafirisha madawa ya kulevya kama vile Mirungi, Bangi n ahata wahamiaji haramu na kwamba ikitokea vyombo vyao vikikamatwa kuhusika na matukio hayo ni Dhahiri kuwa vitataifishwa.

Amewataka wajasiriamali hao kujitahidi kuwa wakweli ili kuiwezesha Tanga kuzidi kustawina kwamba wawe tayari kumfichua yeyote yule atakayekwenda kinyume huku akiahidi kusdhirikiana na kila mmoja kwa maelezo kuwa milango ya ofisi yake iko wazi muda wote.

Awali katika kikao hicho Uongozi wa Bodaboda ulieleza kuwa kuna changamoto ubebaji wanafunzi zaidi ya wanne kwenye vyombo hivyo vya usafiri jambo ambalo ni hatari kwa usalama kero ambayo ilidaiwa kuchangiwa na wasafirishaji hao ikiwa ni pamoja na wazazi.

Katika hoja hiyo Zakaria Bernard ambaye ni Mkuu wa Operesheni za Jeshi la Polisi Mkoani Tanga alisema, hali ngumu ya maisha isiwe kisingizio cha waendesha bodaboda ama wazazi kuruhusu watoto wao ambao ni wanafunzi kupakizwa mshikaki kwenye vyombo vya usafiri.

Aidha waendesha bodaboda na bajaji walilalamikia kufanyiwa vurugu na madereva wa Hiace pindi wanapotaka kupakia abiria jambo ambalo limesababisha jamii hizo kupigana mara kwa mara ambapo wameliomba Jeshi la Polisi kuingilia kati ili kulipatia ufumbuzi suala hilo.

Changamoto nyingine waliieleza kuwa ni waendesha bodaboda kupigwa faini nyingi,kukamatwa kwenye maeneo yenye kona ambapo Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga SACP Henry Mwaibambe alisema amezichukua kero zote hizo huku akiahidi kwamba atazifanyia kazi.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Tanga, Abel Nyalecha aliwataka Wenyeviti wa mitaa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria waendesha bodaboda ambao wanapasua bomba za pikipiki makusudi ili kupiga kelele.

Alisema kwamba, wenyeviti hao wanaweza kuwasiliana na Jeshi la Polisi pindi yanapotokea matukio ya aina hiyo ambayo husababisha vurugu kubwa miongoni mwa jamii akisema kwamba viongozi hao wanahusika katika kulinda usalama huku wakishirikiana kwa karibu na jeshi hilo.

Mwisho.

RAIS SAMIA PAMOJA NA RAIS MUSEVENI WAZINDUA MRADI WA KUFUA UMEME WA KIKAGATI – MURONGO, MBARARA NCHINI UGANDA

May 25, 2023

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kamba pamoja na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023. Mradi huo wa umeme utanufaisha nchi zote mbili katika masuala ya Nishati ya umeme.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Uganda mara baada ya uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Kikagati - Murongo, Mbarara nchini humo tarehe 25 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Mradi wa Umeme wa Kikagati - Murongo, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati alipotembelea mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo (Megawatt 16), Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

Eneo la mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo pamoja na Mitambo kama linavyoonekana pichani, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.