KESHO NI KESHO TANZANIA V IVORY COAST

KESHO NI KESHO TANZANIA V IVORY COAST

August 25, 2016
Mchezo wa kwanza wa mpira wa miguu wa ufukweni, kati ya Tanzania na Ivory Coast unatarajiwa kufanyika kesho kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja uliotengenezwa maalumu kwa ajili ya mchezo huo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Tanzania imepania kufanya vema dhidi ya Ivory Coast iliyoingia Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Jumanne kwa ajili ya mchezo huo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika ambako fainali zake zitafanyika Lagos, Nigeria.

Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Ali Sharif ‘Adolph’, licha ya kupania mchezo huo, anakiri anakutana na timu ngumu ambayo inashika nafasi ya pili barani Afrika, lakini watatumia uzoefu kupata ushindi ili kuweka historia katika mchezo huo nchini.
Mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi kutoka Uganda ambao ni Shafic Mugerwa atakayepuliza kipyenga na wasaidizi wake ni Ivan Bayige Kintu na Muhammad Ssenteza, Mtunza muda atakuwa Adil Ouchker wa Morocco huku Kamishna akiwa ni Reverien Ndikuriyo wa Burundi.
Timu hizo zinatarajiwa kucheza mechi mbili za kuwania kufuzu kwani mara baada ya mchezo wa Dar es Salaam, zitarudiana tena Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa amefanikiwa kufuzu kwa fainali.
Kwa upande wa Tanzania, Kocha Mkuu wa timu hiyo, John Mwansasu, anaendelea na mazoezi na wachezaji wake 16 aliowatangaza wiki iliyopita. Kikosi hicho kinaundwa na wachezaji sita kutoka Zanzibar na 10 Tanzania Bara.
Wanaounda kikosi hicho ni Talib Ame, Ahamada, Mohammed Makame, Ahamed Rajab (golikipa) Khamis Said na Yacob Mohamed wote kutoka Zanzibar. Wengine ni Ally Raby, Mwalimu Akida, Khalifa Mgaya, Rolland Revocatus, Juma Sultan, Rajab Ghana, Samwel Salonge, Kashiru Salum, Juma Juma na Kevin Baraka.
MAJALIWA: WAKURUGENZI WAHAMASISHENI WALIMU KUJIENDELEZA KIELIMU

MAJALIWA: WAKURUGENZI WAHAMASISHENI WALIMU KUJIENDELEZA KIELIMU

August 25, 2016

index 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wa halmashauri na Maofisa Elimu nchini kutowaondoa katika nyadhifa zao Waratibu wa Elimu Kata na Wakuu wa shule za sekondari wasiokuwa na shahada, walimu wakuu wa shule za msingi wasiokuwa na diploma badala yake wawahamasishe kwenda kusoma.
“Maofisa Elimu na Wakurugenzi msije mkawaondoa wale walimu wakuu kwa zile sifa nilizosema bado muda ukifika tutatangaza.Msije mkawakurupusha sasa hivi waacheni waendelee na kazi zao tutatoa muda ili wajipange viziri,” aliema.
 Agosti 20 mwaka huu Waziri Mkuu alisema Waratibu wa Elimu katika ngazi ya Kata na Wakuu wa shule za sekondari wanatakiwa kuwa na shahada huku walimu wakuu kwenye shule wanatakiwa kuwa na diploma.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Agosti 24, 2016) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha Mandela katika jimbo la Sumbawanga mjini.
Alisema Mratibu wa Elimu katika ngazi ya Kata ni lazima awe na shahada ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kusimamia utolewaji wa elimu katika shule za sekondari na msingi.
“Wakuu wa shule za sekondari na waratibu wa elimu kata wasiokuwa na shahada wasiondolewe katika nafasi zao kabla ya kupewa nafasi ya kwenda kujiendeleza kwa masomo ili waweze kuwa na vigezo vya kuendelea kushika nyadhifa hizo,” alisema.
Alisema katika kuboresha maslahi ya walimu Serikali imetenga zaidi ya sh. bilioni tano kwa mwezi ambazo ni posho ya madaraka. Waratibu Elimu Kata wanapewa sh 250,000 kwa mwezi huku Wakuu wa shule za sekondari na walimu wakuu katika shule za msingi wanapewa sh. 200,000.
Waziri Mkuu alisema badala ya kuwaondoa kwenye nyadhifa hizo ni vema Wakurugenzi wakawahamasisha walimu hao kwenda kusoma ili na wao wanufaike na posho ya madaraka iliyoanza kutolewa na Serikali hivi karibuni.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka wazazi na walezi kwenda kuwaandisha watoto wenye umri wa miaka mitano katika shule za awali ambapo watapata fursa ya kujengewa msingi mzuri wa masomo kabla ya kuanza darasa la kwanza.
Pia aliagiza shule zote za msingi nchini zisizokuwa na madarasa ya awali kuhakikisha waanzisha madarasa hayo haraka na kuanza kutoa elimu hiyo.
BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI LAKUTANA KUJADILI MAENDELEO YA MKAKATI WA KUPUNGUZA AJALI

BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI LAKUTANA KUJADILI MAENDELEO YA MKAKATI WA KUPUNGUZA AJALI

August 25, 2016
BAR01
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani nchini  ambae pia ni Naibu Waziri  wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kudhibiti Ajali za Barabarani , ambao ulizinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwezi wa nane,ukiwa na lengo la kupunguza ajali kwa asilimia kumi  ifikapo mwezi Februari, mwakani. Kikao  kilifanyika katika ukumbi wa wizara,jijini Dar es Salaam.
BAR1
Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, wakiongozwa na Mwenyekiti wa baraza ambae pia ni Naibu Waziri  wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati),  katika kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kudhibiti Ajali za Barabarani , ambao ulizinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwezi wa nane,ukiwa na lengo la kupunguza ajali kwa asilimia kumi  ifikapo mwezi Februari, mwakani.Wa kwanza mkono wa kulia kwa Naibu Waziri ni Katibu  Mtendaji  wa  baraza ambae pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani ,  Mohamed Mpinga. Kikao  kilifanyika katika ukumbi wa wizara,jijini Dar es Salaam.
BAR02
Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ASP  Deus Sokoni, akizungumza wakati wa  kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kudhibiti Ajali za Barabarani, ambao ulizinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwezi wa nane,ukiwa na lengo la kupunguza ajali kwa asilimia kumi  ifikapo mwezi Februari, mwakani. Kikao  kilifanyika katika ukumbi wa wizara,jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
BAR2
Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Henry Bantu, akizungumza wakati wa  kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kudhibiti Ajali za Barabarani , ambao ulizinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwezi wa nane,ukiwa na lengo la kupunguza ajali kwa asilimia kumi  ifikapo mwezi Februari, mwakani. Kikao  kilifanyika katika ukumbi wa wizara,jijini Dar es Salaam.

TEA KUFADHILI UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU KATIKA MAENEO YASIO RAHISI KUFIKIKA

August 25, 2016

Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Joel Laurent (wa kwanza kushoto) akijadiliana suala  na viongozi wa Halmashauri ya Kilosa, Mamlaka ya Elimu  Tanzania inatarajia kutekeleza na kufadhili mradi wa kujenga nyumba za walimu kupitia Watumishi Housing Ltd katika Ujenzi katika maeneo yasio rahisi kufikika, katika shule ya Sekondari Uleling'ombe iliyopo Wilaya ya Kilosa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Joel Laurent akiongea na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, kamati ya shule ya Uleling'ombe,uongozi wa kijiji cha Uleling'ombe wakijadilana utekelezaji wa Mradi wa kujenga nyumba za walimu katika maeneo yasio rahisi kufikika, katika shule ya Sekondari Uleling'ombe iliyopo Wilaya ya Kilosa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Joel Laurent akioneshwa eneo lililotengwa kwa ajili ya kujenga nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Uleling'ombe mradi unaotekeleza na kufadhili na Mamlaka ya Elimu Tanzania ikiwatumia Watumishi Housing Ltd katika Ujenzi katika maeneo yasio rahisi kufikika.
Picha ya pamoja.
Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Laurent amesisitiza kuwa taasisi yake itaendelea kutafuta rasilimali ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanosoma katika maeneo ambayo ni magumu kufikika wanajengewa miundombuni ili kupata elimu bora.
Mkurugeni Mkuu huyo alisema hayo wilayani Kilosa wakati akikagua eneo la ujenzi wa nyumba ya walimu wa shule ya sekondari ya Uleling’ombe utakaogharimu zaidi ya 148m/- ambayo walimu sita watakaa katika nyumba hiyo.
Alisema mamlaka hiyo imetiliana saini mkataba na Watumishi Housing wa ujenzi wa nyumba za walimu 40 nchi nzima katika maeneo ambayo ni magumu kufikika ili kuhakikisha kuwa walimu wapya wanaopangiwa katika maeneo hayo ambao wengi wamekuwa wakikimbia kufundisha wanapata sehemu nzuri za kuishi.
Aliongeza kuwa katika mwaka huu wa fedha mamlaka yake imetenga bajeti ya kujenga nyumba 30 mwaka huu ambapo ujenzi wa kila nyumba ni miezi mitatu.
“Nyumba hii itakapokuwa tayari na tunategemea ikamilike ifikapo Desemba mwaka huu, itakuwa na uwezo wa kuwaweka walimu sita kuishi katika nyumba hiyo ila tunazitaka halmashauri kuangalia uwezekano wa kuwawekea samani za ndani” alisema.
 
Na pia alisisitiza juu ya umuhimu wa ushiriki wa wananchi na halmashauri hizo katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa nyumba hizo unazingatia ujenzi ili ziweze kutumika kwa muda mrefu na hivyo kuwanufaisha wanafunzi wengi zaidi.
TEA ilibuni mradi huo baada ya kugundua kuwa kuna uhitaji maalum wa makazi ya walimu katika mazingira ambayo ni vigumu kufikika ambapo wengi ambao wamekuwa wakipangiwa kufundisha hutafuta uhamisho na hivyo wanafunzi wa maeneo hayo ufaulu wao umekuwa mdogo kutokana na kukosa walimu.
“Walimu wanaokusudiwa kuishi katika nyumnba hizi ni wale wanaoanza kazi ndiyo maana ni chumba na sebule kwa kila mwalimu kwani tunaamini baada ya muda watakuwa wameishazoea na kuweza kujipatia makazi uraiani pale watakapokuwa tayari kuanza familia” Alisema Bw Laurent.
Aliongeza kuwa mamlaka hiyo inajadiliana na wadau mbali mbali ili kuona kama wataweza kuwezesha upatikanaji wa internet na ving’amuzi katika sebule ya pamoja ya nyumba hizo ili wale watakaopangiwa maeneo hayo wasijione kuwa wamepangiwa katika mazingira ambayo si rafiki au wameonewa.
Akizungumza katika ukaguzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Bw Rwegerela Katabaro alisema kuwa wako tayari kushirikiana na TEA japo rasilimali fedha imekuwa ni changamoto kubwa.
Aliomba kuwa katika miradi mingine halmashauri zipewe taarifa za awali ili ziweke kutenga fungu katika bajeti zaona hivyo kuchangia katika juhudi za maendeleo.
Alimhakikishia Mkurugenzi Mkuu huyo juu ya ushiriki wa halmashauri kusimamia kwa karibu ujenzi wa nyumba hiyo ili kupata nyumba ambayo inalingana na thamani ya fedha zilizotengwa.
Aidha ili kuondoa mgongano alishauri TEA itoe muongozo ili kila taasisi ijue jukumu lake katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa nyumba hiyo unakuwa bora na kwa viwango walivyokubaliana.
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Uleling’ombe, Magashi Shimba alishukuru kwa kupatiwa mradi huo kwani walimu wengi wanaopangiwa huko huwa hawarudi kutokana na mazingira hasa upatikanaji wa makazi.