MAOFISA WAFAWIDHI NCHINI WAPIGWA MSASA

September 11, 2015

Tangakumekuchablog
KATIBU Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Erick Shitindi, amewagiza Maofisa Kazi Wafawidhi nchini kupiga vita utumikishaji kazi kwa watoto wadogo maeneo ya kazi ikiwa na pamoja na kuwafikisha wahusika katika vyombo vya sheria.
Akifungua kongamano la siku tatu lililoitishwa na Wekeza Mkoani hapa na kuwashirikisha Maofisa Kazi  Wafawidhi kutoka Mikoa mbalimbali nchini jana, Shitindi alisema tabia ya utumikishaji watoto bado ni tatizo nchini.
Alisema tabia hiyo imekuwa ikitumiwa na matajiri na kuwalipa ujira mdogo na hivyo kuwataka kuhakikisha kila Ofisa anasimama katika nafasi yake na kuweza kutokomeza hali hiyo ambayo inakuwa kila kona ya nchi.
“Utumikishaji kazi watoto wadogo kunawaathiri mambo mengi ikiwemo kuwaharibia maisha yao ya mbeleni-----elimu na malezi wanakoseshwa na baadae kuwa watoto wa mitaani” alisema Shitindi na kuongeza
“Unapomtumikisha kazi mtoto mdogo utambue kuwa umemuharibia mfumo mzima wa maisha yake---na hii mara nyingi mtoto anakuwa katika makuzi mabaya na kuweza kujitumbukiza katika vitendo vya uporaji na ujambazi” alisema
Alisema ili kuweza kumaliza tatizo la utumikishaji kazi kwa watoto ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha eneo lake hakuna kero hiyo ambayo kadri ya siku linaelekea kukua kwa kasi kila Mkoa.
Akizungumza katika kongamano hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Masha Mshomba, amewataka waajiri kuwawekea mazingira mazuri wafanyakazi wao ikiwemo ajali kazini.
Alisema waajiri wengi wamekuwa hawawekei mazingira mazuri wafanyakazi wao hasa pale itokeapo ajali pamoja na kifo jambo ambalo limekuwa likisababisha kesi na kupotezeana muda.
“Waajiri wengi hawana utaratibu mzuri kwa wafanyakazi wao na kusababisha malumbano hasa wakazi wa ajali au kifo------hili limekuwa tatizo kubwa sana kila kona” alisema Mshomba
Alisema ili kuwawezesha wafanyakazi kufanya kazi kwa weledi ni vyema waajiri kuhakikisha wanawawekea mazingira mazuri na salama na kuweza kutokomeza kero na usumbufu kwa mwajiri na mwajiriwa.
         
Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Erick Shitindi, akifungua mafunzo ya siku tatu ya Maofisa Kazi Wafawidhi kutoka Mikoa mbalimbali nchini yaliyoandaliwa na WEKEZA ikiwa na lengo la kupunguza kutumikishwaji kazi  kwa watoto pamoja na fidia kwa wafanyakazi, katikati ni Kamishna wa kazi Wizara ya Kazi na AJIRA Saul Kinemela, kushoto ni  Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wekeza Yuonne Prempeh Furgerson .

 Maofisa Wafawidhi kutoka Mikoa mbalimbali wakishiriki katika Semina ya siku tatu juu ya kupiga vita utumikishwaji kazi kwa watoto iliyoanza jana hoteli ya Tanga Beach

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YAZINDUA MFUMO WA UTUNZAJI WA TAARIFA ZA VITUO VYA AFYA TANZANIA BARA

September 11, 2015

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando (kulia), akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mfumo wa taarifa ya vituo vya afya nchini uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama wa   wizara hiyo, Hermes Rulagirwa na Ofisa wa Tehama, Kenani Mwansasu.
 Hapa ni kupongezana baada ya uzinduzi huo.
 Mkuu wa Kitengo cha Tehama wa   wizara hiyo, Hermes Rulagirwa (kulia), akizungumza na wanahabari.
 Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya wakiwa kwenye uzinduzi huo uliofanyika Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Jengo la Ubungo Plaza.
  Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya wakiwa kwenye uzinduzi huo uliofanyika Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Jengo la Ubungo Plaza.

 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya afya wakati wa uzinduzi huo.
………………………………..
Na Dotto Mwaibale
 
SERIKALI imezindua mfumo mpya wa kuhifadhi  taarifa za vituo vya huduma ya afya vya Serikali na binafsi katika ngazi ya kanda, mtaaa kijiji na mkoa nchini.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizindua mfumo huo , Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando alisema kupitia mfumo huo watumiaji watapata taarifa za vituo sahihi na namna vinavyotoa huduma.
Alisema mfumo huo utatumik kama chanzo pekee cha taarifa za vituo na mwisho utumiwe na wananchi kupata taarifa za huduma zinazotolewa na kituo husika.
“Mpango huu wa kielektroniki wa kuandaa mipango na kufanya maamuzi madhubuti wa sekta ya afya nchini, tunaomba na tunahitaji sana kushirikiana katika kuboresha huduma za afya na kuwatendea haki Watanzania,” alisema.
Aliongeza kuwa utatengeneza namba maalum kwa kila kituo kitakachoingizwa na namba hiyo haitarudiwa hata kama kituo hicho kitafungwa.
Dk.Mmbando aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Serikali kwa kuhakikisha wanaleta maendeleo nchini na kuwaaagiza waganga kuhakikisha wanafanya update kila wakati ili kuendana na wakati.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha  Tehama Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Hermes Rulagirwa alisema kupitia mfumo huo utatawawezesha kujua sehemu ya kituo kilipo na huduma wanazozitoa.
Alisema kabla ya kuzinduliwa kwa mfumo huo wapo waganga kutoka vituo mbalimbali nchini walipatiwa mafunzo.
 
JIMBO LA IRINGA MJINI LILIKOSA MBUNGE MAKINI SASA NI ZAMU YANGU UBUNGE -MWAKALEBELA

September 11, 2015

Mgombea   ubunge  jimbo la  Iringa mjini Frederick Mwakalebela  akiomba kura kwa  wananchi wa kata ya Mshindo  leo  wakati wa mkutano wake wa kampeni
Wananchi   wakiwa katika  mkutano  huo wa kampeni leo
Aliyekuwa  mgombea  ubunge  katika mchakato wa ndani ya  chama Michael Mlowe  akimnadi Mwakalebela
Katibu  wa CCM Iringa mjini Bw Elisha Mwampashi  akimnadi  Mwakalebela
Wana CCm na  wananchi wa kata ya  Mshindo   wakisukuma  gari alipopanga mgombea  ubunge wa CCM Bw  Mwakalebela na mgombea  udiwani wa kata  hiyo Bw Ibrahim Ngwada leo
Wanananchi  na  wana CCm wakisukuma gari la Mwakalebela
………………………… Na matukiodaima Blog

MGOMBEA Ubunge wa jimbo la Iringa kupitia chama cha mapinduzi ( CCM) Frederick Mwakalebela amesema jimbo la Iringa Mjini limekosa kunufaika na fursa za maendeleo kwa kuwa halikuwa na mbunge makini wa kuleta maendeleo .

Hivyo amewataka wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kuecha kujutia kukosa maendeleo na badala yake kumchagua kuwa mbunge wao ifikapo Octoba 25 mwaka huu.
Mwakalebela ametoa kauli hiyo leo wakati wa mkutano wake wa kampeni za Ubunge kwenye kata ya Mshindo  alisema iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha anasogeza maendeleo ya haraka kwa wananchi wa Jimbo la Iringa ambao kwa miaka mitano wamekosa kupata maendeleo hayo .
Kwani alisema hakuna sababu ya kujutia na badala yake kutumia nafasi hiyo kujutia miaka mitano ambayo wamepumzika pasipo kushuhudia maendeleo yoyote katika jimbo hilo la Iringa mjini.
Kuhusu nini atafanya baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge alisema ni pamoja na kuboresha miundo mbinu ,kuanzisha saccos ya vijana ,kuanzisha mfuko wa elimu wa jimbo kwa kutumia sehemu ya mshahara wake ,kuwawezesha wazee kupata matibabu ya bure na kuboresha sekta ya michezo.
Wakati aliyekuwa Mgombea Ubunge katika mchakato wa kura za maoni Balozi Augustino Mahiga alisema matumaini mapya ya jimbo la Iringa yatapatikana kwa kuchagua diwani ,mbunge na Rais toka CCM .
Kwani alisema kuwa majuto ya wanajimbo la Iringa ambayo wanayo kwa sasa ni kutokana na kukosa mbunge Makini wa kuwatumikia wananchi na badala yake kuwa na mbunge wa maandamano na fujo bungeni.

Samia Suluhu Afunika Mkutano wa Kampeni Kibaha

September 11, 2015

WanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe, ambapo mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (hayupo pichani) alihutubia.

Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) uliofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani leo.

Mmoja wa wasanii wa kugani mashairi akiwaburudisha wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe, ambapo mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (hayupo pichani) alihutubia.

Mjumbe wa Kamati ya kampeni Taifa ya CCM, Anjela Kairuki, akizungumza kumnadi mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (hayupo pichani) kwenye mkutano wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe.

Kikundi cha akinamama wajasiliamali na utamaduni kutoka Temeke kikitoa burudani kwa umati na mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais,  katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe.

Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (kulia) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani, Subira Mgalu katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe leo.

Wasanii Bongo Movie Wanogesha Kampeni za Mgombea Mwenza CCM

September 11, 2015

Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.

Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akisalimiana na baadhi ya viongozi na wananchi baada ya kuwasili katika eneo la mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani jana.
Baadhi ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
Mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Kibaha Vijijini, akizungumza na wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
Baadhi ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
Baadhi ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
 *Imeandaliwa/www.thehabari.com

PPF YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI, SHULE YA MSINGI YA JESHI LA WOKOVU JIJINI DAR ES SALAAM

September 11, 2015

 Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, (kushoto), na Afisa wa Fedha Mwandamizi wa Mfuko huo, Angel Mukasa, (kulia), na Mfanyakazi mwingine wa Mfuko huo, Omari Bundile, (wapili kushoto), wakigawa mafuta maalum yanayotumiwa na watu wenye ulemavu wa ngozi, pamoja na sare za shule na viatu kwa wanafunzi hawa wenye ulemavu wa ngozi wa shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam leo Septemba 11, 2015. Katika kutekeleza sera ya mfuko ya kusaidia jamii, PPF, imetoa vifaa mbalimbali ikiwemo, sare za snhule, viatu na mafuta hayo maalum, Meneja Uhusiano wa Mfuko huo Lulu Mengele aliwaambia waandishi wa habari. 
(Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
 Latifa Musa,(kulia), akitoa shukrani kjwa niaba ya wenzake baada ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wa shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam, kupatiwa msaada na Mfuko wa Pensheni wa PPF
 Watoto wenye ulemavu wa ngozi kwenye shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa msaada kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF, shuleni hap oleo Ijumaa Septemba 11, 2015
Watoto wenye ulemavu wa ngozi, wakiteta jambo, baada ya kupatiwa msaada wa vifaa yakiwemo mafuta maalum yanayotumiwa na watu wenye ulemavu wa ngozi
 Picha ya pamoja ya maafisa wa PPF, Walimu na wanafunzi wa shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu
 Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi ya Jeshi la Wokovu, Flora Millinga, akizungumza kwenye hafla hiyo
 Lulu akiwa na baadhi ya watoto
 Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, akizungumza na watoto hao wakati wa kutoa msaada wa vitu mbalimbali Septemba 11, 2015
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Janet Ezekiel, (kulia), akizungumza jambo na baadhi ya watoto hao
 Kikundi cha Kwaya kikitoa burudani
Angel Mukasa, akizungumza na baadhi ya watoto