RC KINDAMBA AHIMIZA JAMII KUTILIA MKAZO LISHE BORA KWA WATOTO

August 17, 2023
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza wakati  akifungua kikao cha nusu mwaka cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu.


MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza wakati  akifungua kikao cha nusu mwaka cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu





Na Oscar Assenga, Tanga


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba, amehimiza jamii kutilia mkazo lishe bora kwa watoto hususani wa chini ya miaka mitano, ili kuwa na kizazi chenye afya na tija katika uzalishaji na utoaji huduma.


Ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua kikao cha nusu mwaka cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu.


Mkuu wa Mkoa amesema ombwe katika masuala ya lishe linaanzia utotoni pale watoto wanapokosa lishe bora hivyo kuathiri ukuaji na afya zao.


‘’Tukiwaacha wakue hovyo hovyo ndio baadaye wataleta matatizo kwenye nchi. Tunasema hakuna madaktari wazuri, hakuna wakandarasi wazuri…ni kwa sababu hatukuwangalia wakati wakiwa watoto walikuwa wanakula chakula gani,’’ amesema.


Amesema hitihada za uboreshaji lishe kwa watoto zinapaswa kutilia mkazo kwa wazazi na walezi kutambua aina ya chakula, kazi na umuhimu wake kwa mtoto.


‘’ Hapa suala lisiwe mtoto kula kwa lengo la kushiba, bali kutambua chakula kinakwenda kufanya kazi gani mwilini,’’ amesema.


Kindamba amesema pamoja na changamoto zilizopo, mkoa huo umefanikiwa kuongeza wastani wa jumla kwa Shilingi 100 zinazotengwa na halmashauri kwa kila mtoto mwenye umri wa chini ya miaka mitano, kutoka Shilingi 794.3 katika kipindi cha Julai hadi Disemba, 2022 kufikia Shilingi 1,272.3 kwa Januari hadi Juni, 2023.


Pia amesema kumekuwepo ongezeko la asilimia ya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa afua za lishe kutoka 57.7 kwa Julai hadi Disemba, 2022 kufikia 96.79 katika kipindi cha Januari hadi Juni, 2023.


Mkuu wa mkoa amesema lishe bora kwa jamii ni kichocheo cha maendeleo katika nyanja zote zikiwemo afya, elimu, biashara, kilimo na uchumi.


Hivyo, amesema ni pale ambapo athari za lishe duni na utapiamlo zitakazodhibitiwa au kutokomezwa, malengo ya maendeleo katika nyaja hizo yatafikiwa kwa ufanisi.
Mwisho














JESHI LA POLISI TANGA LAIPONGEZA SHIRIKA LA AMED TANZANIA KWA HATUA WALIZOCHUKUA KUKABILIANA NA AJALI ZA BARABARANI

August 17, 2023

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga William Mwamasika akizungumza  baada ya kumaliza kwa uendeshaji kesi katika Mahakama ya Watoto( Mahakama Kifani) kwa madereva waliovunja sheria za usalama barabarani kwa kutosimama maeneo yenye alama za watembea kwa miguu yanayotumiwa kuvuka wanafunzi.
Meneja wa Shirika la  Amend Tanzania Simon Kalolo akizungumza 









Na Oscar Assenga, Tanga

JESHI la Polisi Mkoani Tanga Kitengo cha Usalama Barabarani limepongezwa kwa hatua walizochukua kukabiliana na ajali za barabarani na hivyo kupelekea mpango kazi wa Usalama Barabarani kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga uliokuwa unatekelezwa na Shirika la Amend Tanzania kufikia asilimia 90

Pongezi hizo zilitolewa leo na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani William Mwamasika baada ya kumaliza kwa uendeshaji kesi katika Mahakama ya Watoto( Mahakama Kifani) kwa madereva waliovunja sheria za usalama barabarani kwa kutosimama maeneo yenye alama za watembea kwa miguu yanayotumiwa kuvuka wanafunzi.

Mahakama ya Watoto ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kazi huo sambamba na kuweka alama na michoro ya barabarani zinazopita kwenye baadhi ya Shule za msingi katika Jiji la Tanga.

Alisema mpango huo ulikuwa ni Shirika la Amend Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani huku akisema bodaboda katika Jiji la Tanga zinachangia ajali kwa kiwango kikubwa

“Hivyo niwaombe waendesha vyombo vya moto kuheshimu sheria za usalama barabarani kwani kufanya hivyo kutasaidia kupunguza ajali za barabarani au kuzitokomeza kabisa”Alisema

Mkuu huyu wa Kikosi cha Usalama barabarani pia alitoa rai kwa wazazi na walezi kutokubali wanafunzi kupakiwa mishikaki kwenye bodaboda aidha wakati wa kwenda shule au kurudi nyumbani kwani ikitokea ajali msiba wake utakuwa mkubwa na wenye kuumiza.

Awali akizungumza Meneja wa Amend Tanzania Simon Kalolo baada ya kumaliza kwa uendeshaji kesi katika Mahakama ya Watoto (Mahakama Kifani) kwa madereva waliovunja sheria za usalama barabarani kwa kutosimama maeneo yenye alama za watembea kwa miguu yanayotumiwa kuvuka wanafunzi.

Mahakama ya Watoto ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kazi huo sambamba na kuweka alama na michoro ya barabarani zinazopita kwenye baadhi ya Shule za msingi katika Jiji la Tanga.

Alisema Amend imekuwa ikijishughulisha na usalama barabarani nchini tangu mwaka 2009 na kwa ufadhili wa Shirika la Fondation Botnar jijini Tanga,wanashirikiana na Halmashauri ya Jiji hilo kuboresha miundombinu ya barabara maeneo ya shule.

Aidha alisema wamekuwa wakitoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi, kuanzisha klabu za usalama barabarani na mahakama kifani za watoto, mafunzo kwa madereva pikipiki , kuandaa makongamano ya wadau wa usalama barabarani, kufanya tafiti huhusu ajali za barabarani, na kuandaa Mpango Kazi wa usalama barabarani kwa Jiji hilo.

Alisema mpango kazi huo wa usalama wa usalama barabarani ulikuwa na lengo la kuboresha safari salama na endelevu kwa Jiji la Tanga uliozinduliwa Novemba 11, 2022 na tangu ulipozinduliwa kuna mambo kadha yametekelezwa.

" Baada ya uzinduzi huo tumefanikiwa kuzindua miundumbinu katika shule tatu za msingi za Shaaban Robert, Mabawa na Majengo. Pia kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi 3,501 wa shule za msingi Mabawa, Majengo na Shabaan Robert na wengine 3,247 wa shule za sekondari Toledi, Kihere na Kiomoni.

Hata hivyo alisema kupitia mpango huo wameanzisha klabu mbili za shule za usalama barabarani katika Shule ya Msingi Usagara na klabu ya usalama wa baiskeli katika Shule ya Sekondari Usagara, yenye watoto 20 katika kila klabu.

“Tumetoa mafunzo ya usalama barabarani kwa watoto hawa, baada ya kuhitimu kuwa mabalozi, wakipokea vyeti katika hafla ndogo.Shughuli za vilabu hivi zimejumuisha mafunzo, midahalo ya usalama barabarani," Alisema.

Pia alisema wametoa mafunzo ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki 350 kufanya jumla ya madereva waliopata mafunzo haya kufikia 950.

Kalolo alisema Februari mwaka huu wamesambaza vifaa vya kufundishia usalama barabarani kwa maofisa maendeleo ya jamii katika kata 22 kati ya 27 za Jiji la Tanga.

Aliongeza Juni mwaka huu maofisa maendeleo ya jamii walikuwa wamezungumza kuhusu usalama barabarani katika zaidi ya mikutano au matukio 50 tofauti, na kuelimisha jumla ya takriban wananchi 6,600.

Hata hivyo alisema wamekamilisha uwekaji wa miundombinu ya waenda kwa miguu katika eneo moja lenye shule tatu za msingi na kwamba lengo kuu ilikuwa kupunguza mwendo wa vyombo vya moto hadi chini ya 30km/h na kuwapa watoto mahali salama pa kutembea na kuvuka."

Awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Majengo Mayasa Said amesema baada ya wanafunzi na walimu kupatiwa elimu ya usalama barabarani sambamba na kuwekwa kwa alama zinazowawezeha wanafunzi kuvuka kwa usalama ajali zimepungua, hivyo wanaishukuru Amend kwa kupeleka mpango huo jijini Tanga.

Mwisho

RC KINDAMBA AFUNGUA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MATOKEA YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022

August 17, 2023
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza wakati akifungua mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya Watu na makazi yam waka 2022 kwa viongozi, watendaji, wawakilishi na viongozi wa vyama vya siasa mkoani humo ikiwemo makundi maalumu kwa Halmashauri za mkoa huo .
Mratibu wa Sensa Mkoa wa Tanga Tony Mwanjota akizungumza wakati  wa  mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya Watu na makazi yam waka 2022 kwa viongozi, watendaji, wawakilishi na viongozi wa vyama vya siasa mkoani humo ikiwemo makundi maalumu kwa Halmashauri za mkoa huo .
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akizungumza wakati wa mafunzo hayo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba katikati akiwa meza kuu na viongozi wengine kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akifuatiwa na Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo kulia akiwa na washiriki wengine wakifiuatilia kwa umakini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo kulia akiwa na washiriki wengine wakifiuatilia kwa umakini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga wakiwa kwenye mafunzo hayo
Washiriki wa mafunzo hayo

Na Oscar Assenga,TANGA

MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amefungua mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya Watu na makazi yam waka 2022 kwa viongozi, watendaji, wawakilishi na viongozi wa vyama vya siasa mkoani humo ikiwemo makundi maalumu kwa Halmashauri za mkoa huo .

huku akieleza kuwa yatawajengea uwezo wakufunzi kuchambua na kutumia matokeo ya sensa ili yawe mwanzo wa dira ya kuwaongoza katika utekelezaji wa majukumu na malengo yao ya kila siku.

Kindamba aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Regail Naivera Jijini Tanga ambapo alisema mafunzo haya yatawajengea uwezo wa kutafsiri, kwahiyo nawaomba sana wakati mafunzo yakiendelea kuwa watulivu, ili yaweze kwenda kuwa msaada kwenye ngazi ya chini.

Alisema kwa mujibu wa takwimu ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 idadi ya watu Mkoa wa Tanga idadi imeongezeka lakini siyo kwa idadi kubwa ya watu tofauti na Mikoa mingine Kitaifa.

Aidha alisema Idadi hiyo inaonesha kwamba kiwango cha kuongezeka kimetoka asilimia 2.2 mwaka 2012 na kufikia asilimia 2.5 2022, lakini pamoja na hayo, Mkoa wa Tanga inaonesha kwamba kasi yetu ya kukua iko chini sana ikilinganishwa na takwimu za sensa za Kitaifa ambazo sasa ipo asilimia 3.2.


Katika hatua nyengine Mkuu huyo wa Mkoa alitoa wito kwa viongozi wa halmashauri kuwa makini katika kuhakikisha wanaweka mikakati madhubuti na endelevu itakayowahakikishia wananchi huduma bora na za kiuchumi ili kuimarisha ustawi wao na maendeleo ya Mkoa.

Hata hivyo alisema ni muhimu kutambua Mkoa huo umefunguka kutokana na uwepo wa fursa mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo mradi mkubwa wa bomba la mafuta nao utakuja na watu wake hivyo wao wameamua Tanga iwe kituo cha kuvutia watu waje na hivyo wanapokuja na wenyeji nao wapo.

Awali akizungumza katika mafunzo hayo Meneja wa Takwimu Mkoa wa Tanga Tonny Mwanjota alisisitiza umuhimu wa wadau wa sensa na wananchi kwa ujumla kuwa wavumilivu kwa baadhi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, kusubiria majibu ya matokeo kwa upande wa watu wenye hali ya ulemavu.

Mwanjota amesema matokeo ya sensa bado yanaendelea kutolewa kwa awamu hivyo kwa ugumu wa takwimu kwa wenye ulemavu hivyo nayo yapo miongoni mwa yale ambayo yanaendelea kufanyiwa kazi.

WANAFUNZI 350 TANGA WANUFAIKA NA ELIMU YA USALAMA BARABARANI CHINI YA SHIRIKA LA AMEND

August 17, 2023
 Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Tanga (RTO) Wiliam Mwamasika akizungumza wakati kuelezea mpango kazi wa Usalama barabara kwa Jiji la Tanga unaendeshwa na Shirika la Amend Tanzania ambao umefikia asilimia 90.
Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo akielezea  Mpango Kazi wa Usalama Barabarani
Mmoja wa madereva waliokiuka sheria za usalama barabara Avishai kushoto akiandika maelezo ya kutokurudia kosa la kutokusimama kwenye kivuko cha waenda kwa miguu baada ya kukamatwa kwa kosa hilo leo na kufikishwa kwenye mahakama ya watoto iliyokuwa ikishikiliza kesi za madereva waliovunja sheria za barabarani kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Tanga William Mwamasika
Mahakama ikiendelea


Elimu ikitolewa kwa waendesha bodaboda
Wanafunzi wakifiatilia mahakama hiyo





Na Oscar Assenga,TANGA

WANAFUNZI 350 wa Shule ya Msingi katika Halmashauri ya Jiji la Tanga wamenufaika na mpango wa elimu ya usalama barabarani inayotolewa na Shirika la Amend Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani humo 

Kabla ya kueleza mpango huo kulishuhudiwa uendeshaji kesi katika Mahakama ya Watoto( Mahakama Kifani)kwa madereva waliovunja sheria za usalama barabarani kwa kutosimama maeneo yenye alama za watembea kwa miguu yanayotumiwa kuvuka wanafunzi.

Hayo yalibainishwa leo na Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo alisema hilo limetekeleza Mpango Kazi wa Usalama Barabarani kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa asilimia 90 huku likitumia nafasi hiyo kueleza hatua mbalimbali za kuutekeleza mpango.

Alisema Shirika hilo linajishughulisha na usalama barabarani nchini tangu mwaka 2009 na kwa ufadhili wa Shirika la Fondation Botnar jijini Tanga, shirika hilo limekuwa likishirikiana na Halmashauri ya Jiji katika kuboresha miundombinu ya barabara kwenye maeneo ya shule.

“Pia kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi,kuanzisha klabu za usalama barabarani na mahakama kifani za watoto, mafunzo kwa madereva pikipiki , kuandaa makongamano ya wadau wa usalama barabarani, kufanya tafiti huhusu ajali za barabarani, na kuandaa Mpango Kazi wa usalama barabarani kwa Jiji hilo”Alisema

Akizungumzia Mpango Kazi huo wa usalama barabarani wenye lengo la kuboresha safari salama na endelevu kwa jiji la Tanga alisema ulizinduliwa Novemba 11 ,2022 na tangu ulipozinduliwa kuna mambo kadha yametekelezwa.

Alisema baada ya uzinduzi huo amesema shirika la Amend limefanikia kuzindua miundumbinu katika shule tatu za msingi za Shaaban Robert, Mabawa na Majengo.

“Mpaka sasa tumetoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi 3,501 wa shule za msingi Mabawa, Majengo and Shabaan Robert na wengine 3,247 wa shule za sekondari Toledi, Kihere and Kiomoni”Alisema

“Tumeanzisha klabu mbili za shule za usalama barabarani katika Shule ya Msingi Usagara na klabu ya usalama wa baiskeli katika Shule ya Sekondari Usagara, yenye watoto 20 katika kila klabu na tumetoa mafunzo ya usalama barabarani kwa watoto hawa, baada ya kuhitimu kuwa mabalozi, wakipokea vyeti katika hafla ndogo”Alisema

"Shughuli za vilabu hivi zimejumuisha mafunzo, midahalo ya usalama barabarani, michezo, mijadala ya mezani na kushiriki katika kampeni za vyombo vya habari na mafunzo ya msasa kwa madereva wa pikipiki 350 kufanya jumla ya madereva waliopata mafunzo haya kufikia 950."

Kalolo alisema Februari mwaka huu wamesambaza vifaa vya kufundishia usalama barabarani kwa maofisa maendeleo ya jamii katika kata 22 kati ya 27 za Jiji la Tanga.


Awali akizungumza Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Tanga (RTO) William Mwamasika Alisema kwamba mkoa huo una changamoto kubwa ya matukio ya ajali hususani kwa watoto na wanafunzi wanapotoka majumbani kwenda shuleni na wanaporejea.


Alisema mpango huo umekwenda sambamba na kufadhili mafunzo kwa waendesha bodaboda 300 katika Jiji la Tanga ili kuweza kuzijua sheria za usalama barabarani na namna ya kuweza kuziepuka.

Alisema mara nyingi ajali hizo zimekuwa zikisababishwa na waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kutokana na baadhi yao kushindwa kufuata sheria za usalama barabarani

Alisema kufuatia uwepo wa changamoto hiyo, Jeshi hilo limendelea kujipanga na kuimarisha usalama hususani kwenye vivuko wavyovukia wanafunzi nyakati za asubuhi wanapovuka ikiwa ni mkakati wa kutokomeza ajali ambazo zimekuwa zikipoteza ndoto zao.

“Kwa kweli sisi kama Mkoa wa Tanga tumejipanga vizuri kuhakikisha tunatokemeza ajali za barabarani hususani kwa watoto na wanafunzi kwa kuhakikisha kila siku hususani nyakati za asubuhi kuna kuwa na askarti wa usalama kwenye vivuto vya watembea kwa miguu kwa lengo kuondosha ajali hizo”Alisema

Alisema watumiaji wa vyombo vya moto wamekuwa wakipuuzia sheria za usalama barabarani licha ya kuzifahamu hivyo ni jukumu la kila mwananchi sasa wahakikishe wanazingatie na kufuata sheria za usalama ili kuweza kupunguza ajali