MCHUNGAJI NATSE AWAAGA JIMBO LA KARATU ,QAMBALA KUPEPERUSHA BENDARA YA CHADEMA

July 25, 2015

Mbunge mstaafu wa Jimbo la Karatu mkoa wa Arusha,Mchungaji Israel Natse akizungumza katika mkutano mkuu wa Jimbo hilo ambao ulifanya uchaguzi wa madiwani na Wabunge wa  Viti Maalumu mgombe Ubunge wa Jimbo la Karatu,katikati ni Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha,Kalisti Lazaro na Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Karatu,Thomas Darabe.

Mbunge wa Viti Maalumu wilaya ya Karatu,Cecilia Paresso akizungumza katika mkutano huo ambao alichaguliwa na wajumbe wanawake kuwania nafasi hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya hosteli ya KKKT Karatu na kumpongeza mch.Natse kwa kuamua kuachia nafasi wanachama wengine.

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya hosteli ya KKKT Karatu na kumpongeza mch.Natse kwa kuamua kuachia nafasi wanachama wengine.

Mwanamke wa kwanza kuwahi kujitokeza kuomba ridhaa ya wanachama kumchagua kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Karatu,Fransisca Duwe akijinadi kwa wajumbe.

Willy Qamballa mmoja wa wagombea akijinadi kwa wajumbe

Aliyekua Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Karatu,Lazaro Maasay akiomba kura kwa wajumbe

Mshindi wa kura za maoni za Ubunge Jimbo la Karatu,Willy Qamballa akiwashukuru wajumbe baada ya kujizolea kura 217 na mpinzani wake wa karibu Lazaro alipata kura 84.

Mshindi wa kura za maoni za Ubunge Jimbo la Karatu,Willy Qamballa akifurahia na wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi.
TTCL yaunganisha Ofisi na Kanda za MSD kwenye Mkongo

TTCL yaunganisha Ofisi na Kanda za MSD kwenye Mkongo

July 25, 2015

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto) hati ya makubaliano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania. Hafla hiyo ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania imefanyika leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD Dar es Salaam. Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto) hati ya makubaliano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania. Hafla hiyo ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania imefanyika leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania inayotolewa na kampuni ya TTCL. Ofisi za Kanda za MSD zimeunganishwa na Makao Makuu na huduma za mkongo wa mawasiliano ili kufanya kazi zake kwa haraka na ufanisi zaidi.  Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania inayotolewa na kampuni ya TTCL. Ofisi za Kanda za MSD zimeunganishwa na Makao Makuu na huduma za mkongo wa mawasiliano ili kufanya kazi zake kwa haraka na ufanisi zaidi.Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD Dar es Salaam, kulia ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akishuhudia. Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD Dar es Salaam, kulia ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akishuhudia.Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kulia) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD), kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akishuhudia kabla ya kukabidhiwa. Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kulia) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD), kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akishuhudia kabla ya kukabidhiwa.Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (wa tatu kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (wa nne kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa kampuni ya Simu Tanzania na Bohari ya Dawa Nchini katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania na kampuni ya TTCL. Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (wa tatu kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (wa nne kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa kampuni ya Simu Tanzania na Bohari ya Dawa Nchini katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania na kampuni ya TTCL.

 KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) leo imekabidhi mradi mkubwa wa Mkongo wa Mawasiliano ambao umeyaunganisha matawi yote ya Bohari ya Dawa Nchini (MSD) na Makao Makuu ili kufanya kazi zake kwa haraka na kwa ufanisi. Hafla ya kukabidhi mradi huo imefanyika leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD zilizopo jijini Dar es Salaam. 

 Akikabidhi mradi huo, kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura, Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania, Peter Ngota alisema kampuni hiyo inajisikia fahari kufanikiwa kuunganisha ofisi zote za kanda za MSD na Makao makuu kupitia mkongo wa mawasiliano ambao ni salama na wauhakika katika utendaji wa kazi. 

 Alisema MSD ni moja ya wateja wake wakubwa ambao wameunganishwa kihuduma kupitia mkongo wa mawasiliano ambao ufanisi wake ni mkubwa na salama kwa wateja tofauti na teknolojia nyingine za mawasiliano. Alisema huduma za mkongo wa mawasiliano zinazotolewa na TTCL kwa wateja wake ni salama na zenye ubora katika ufanisi jambo ambalo limevuta idadi kubwa ya wateja kuongezeka kila uchao. 

 Alisema kwa sasa TTCL inatoa huduma hizo kwa makampuni ya simu, taasisi mbalimbali za umma na binafsi, mabenki, hospitali kadhaa, vyombo vya habari, wateja binafsi pamoja na mataifa kama Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Zambia na nchi ya Malawi. 

 Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani alisema MSD ilianza kufungiwa mawasiliano ya mkongo Mwezi Mei, 2011 kwa kuunganisha ofisi za makao makuu na baadaye ofisi mpya za mauzo zilizopo Muleba zilizounganishwa mwaka 2013. 

 Alisema MSD ilifanya uamuzi wa kuhamia kwenye teknolojia ya Mkongo baada ya kuona uwepo wa matatizo makubwa yaliyokuwepo katika teknolojia ya awali ambayo ni waya wa jadi yaani shaba ambayo pia ilitolewa na kampuni ya TTCL. 

 "...Bohari ya Dawa iliamua kuhamia katika teknolojia hii baada ya kufanya utafiti wa kina na kuona faida ambazo zinaweza kupatikana kwa kutumia teknolojia hii (mkongo) na hivyo kuachana na matatizo yanayosababishwa na teknolojia ya shaba. Hii ina maana mkongo unaweza kubeba habari zaidi na kwa ubora mkubwa kuliko waya wa shaba," alisema Mwaifwani. 

 Alisema kwa sasa MSD imeanza kupata mafanikio makubwa baada ya kuanza kutumia huduma za mkongo na tayari TTCL imeyaunganisha Ofisi 10 za MSD ambazo ni Kanda nane (8) pamoja na vituo viwili vya mauzo; alizitaja Kanda zilizounganishwa ni pamoja na Dar es Salaam, Moshi, Iringa, Mbeya, Mwanza, Tabora, Dodoma, Mtwara, Muleba, Tanga, Makao Makuu ya Muda Jamana na Ofisi za Keko Mwanga. 

 "...Tunasema kwamba Bohari ya Dawa imedhamiria kuokoa maisha ya Watanzania kwa kutumia teknolojia ya Mkongo yenye kasi zaidi, usalama, na gharama nafuu zaidi katika kuhakikisha dawa zenye ubora zinamfikia kila Mtanzania kwa wakati na kupunguza kero ya kusubiri huduma zetu kwa muda mrefu kwani sasa huduma zinapatikana kwa wakati kwa kuwa teknolojia inayotumika ni ya kisasa na yenye ubora wenye kukidhi viwango vinavyohitajika na bohari ya dawa," alisema Mkurugenzi Mkuu, Mwaifwani.

Kadama Malunde Achaguliwa Mwenyekiti Mpya wa Wanahabari Shinyanga

July 25, 2015
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza muda wake, Shija Felician akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde (mwenye suti) baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa Klabu hiyo. Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza muda wake, Shija Felician akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde (mwenye suti) baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa Klabu hiyo. Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga waliomaliza muda wao wakijiuzuru nyadhifa zao kabla ya uchaguzi mkuu kupata viongozi wapya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club- SPC) Msimamizi wa uchaguzi mkuu wa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga David Nkulila akizungumza jambo wakati wa uchaguzi mjini Shinyanga   Mwenyekiti mpya wa SPC Kadama Malunde, ambaye pia ni Mkurugezi wa Malunde1 blog akipongezana na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Shija Felician (kulia) Viongozi wapya wa SPC wakiwa meza kuu Katibu mkuu mpya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ndugu Stephen Wang'anyi akizungumza baada ya uchaguzi, kushoto ni mweka hazina aliyetetea kiti chake bi Stella Ibengwe Baadhi ya viongozi wa SPC wakiwa katika picha ya pamoja.