MKUU wa wilaya ya Korogwe,Hafsa Mtasiwa amelitaka Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoani Tanga kushirikiana na Halmashauri kuweka mpango katika ujenzi wa viwanda vya nyama na matunda ambavyo vitaboresha,kuinua kipato na kuongeza ajira kwa wanachama wa mfuko huo.
Mtasiwa aliyasema hayo jana wakati akifungua semina ya wajasiriamali, waajiri na wadau wa Mfuko huo wilayanai Korogwe ambapo alisema ujenzi huo utasaidia kuwakwamua wakulima sambamba na wafugaji ambao wanakabiliwa na soko la uhakika wa kuuzia bidhaa zao.
Alisema kuwa uwepo wa viwanda hivyo utaweza kusaidia kuwapunguzia adha wananchi wanayokumbana nayo wakati mazao yao na mifugo inapokuwa tayari kwa ajili ya kuuzwa na hivyo kukuta baadhi ya bidhaa ikiwemo matunda kuozea mashambana kwa kukosa soko.
Aidha alisema kuwa sambamba na hilo wilaya hiyo ina auhitaji mkubwa wa nyumba kwa ajili ya watumishi na wakazi wa wilaya hiyo hivyo kulitaka shirika hilo kuangalia eneo hilo kwa njia ya uwekezaji na kuwapatia makazi bora kwa bei nafuu wananchi.
“Katika jambo hili ni matumaini yangu kwamba mtaharakisha taratibu husika ili kuhakikisha uwekezaji huo unafanyika mapema na kwa kiwango cha juu ili kumpa mwanachama wenu Faida na pia kunufaisha jamii ya wakazi wa Korogwe na Taifa kwa ujumla “Alisema DC Mtasiwa.
Hata hivyo alilitaka shirika hilo kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha wanaandikisha wanachama katika maeneo ya vijijini na mijini wanaostahili ili waweze kupata fursa ya kujiunga na kunufaika na huduma za mfuko huo hasa kwa mafao ya matibabu.
“Nitumie nafasi hii kusisitiza kwamba nyie ambao ni waajiri na
wanachama wa mfuko huu milifanya uchaguzi sahihi na hilo ni jambo la kupongezwa kwani ipo mifuko mingi ambayo mngeweza kujiunga nayo lakini mlipima na kuona NSSF ni mfuko sahihi “Alisema.

Mkuu huyo wa wilaya alitoa wito kwa waajiri kuhakikisha wafanyakazi
wao wanaandikishwa na kupata huduma za mfuko na kutekeleza wajibu wao
kuwasilisha michango sahihi na kwa wakati ili waweze kunufaika kupitia
mfuko huo.
Awali akizungumza, Meneja wa NSSF Mkoani Tanga,Dkt Frank Maguda alisema kuwa shirika hilo limekuwa na mpango madhubuti wa kutoa elimu kwa wanachama na wasio wanachama ili kuweza kuzijua na kuzitumia fursa zilizopo kwenye mfuko wa Taifa ya Hifadhi za Jamii zikiwemo za matibabu,pensheni mbalimbali, mafao ya muda mrefu na muda mfupi.
“Katika kuwaelezea juu ya fursa pia tunaonyesha wajibu wao ili
kuwapa uwezo wa kukidhi vigezo au sifa za kupata mafao na huduma mbalimbali zitolewazo na shirika hilo vikiwemo pia mikopo,msaada wa mazishi,mafao ya uzazi,kuumia kazini,ulemavu “Alisema Meneja Maduga