Mahakama ya Rwanda mjini Arusha yathibitisha vifungo vya viongozi wa zamani wa Rwanda

September 29, 2014
Mahakama ya Rwanda inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ilioko mjini Arusha Tanzania, imethibitisha hukumu ya kifungo cha maisha kwa viongozi wa zamani wawili kwa uhalifu wa mauaji ya kimbari yaliofanywa mwaka wa 1994. 

Matthieu Ngirum-patse na Edouard Karemera, mwanachama wa zamani na naibu kiongozi wa chama kilichotawala wakati huo, walihukumiwa kifungo cha maisha mwaka wa 2011. 

Walishitakiwa kuhusiana na mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya binaadamu na kwa kutozuwiya mauaji  au kulaani uhalifu huo uliotekelezwa na wanamgambo wa chama hicho wanaojulikana kama Interahamwe. 

Viongozi hao wawili walikuwa wamekata rufaa katika kesi hiyo. Watu wanaokadiriwa kufikia 800,000 wengi wao kutoka kabila la wachache la watutsi waliuwawa katika mapigano hayo yaliodumu siku 100 mauaji yaliosemakana kuwa ya kasi mno kuliko yale ya wayahudi yaliotokea katika vita vya pili vya dunia. 

Viongozi hao wawili wa zamani nchini Rwanda watabakia kizuizini wakisubiri kuhamishwa katika magereza ya nchi nyengine watakapotumikia vifungo vyao. Serikali ya Rwanda imepongeza uamuzi huo.
*MATUKIO YA PICHA BUNGE MAALUM LA KATIBA LEO 29 SEPTEMBA, 2014 MJINI DODOMA.

*MATUKIO YA PICHA BUNGE MAALUM LA KATIBA LEO 29 SEPTEMBA, 2014 MJINI DODOMA.

September 29, 2014
image
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiongoza mjadala ndani ya Bunge hilo leo 29 Septemba, 2014 mjini Dodoma. 
image
Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Andrew Chenge akisoma taarifa Bungeni hap oleo 29 Septemba, 2014 mjini Dodoma. 
 .image 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Evod Mmanda akisoma taarifa yake bungeni hapo leo 29 Septemba, 2014 mjini Dodoma. 
image 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mjumbe ndani ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mizengo Pinda akifafanua kuhusu suala la Mahakama ya Kadhi bungeni hap oleo 29 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

*TANZANIA YAENDELEA KUNUFAIKA NA UHUSIANO MWEMA BAINA YAKE NA TAIFA LA CHINA

September 29, 2014

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Uwekezaji na Uwezeshaji) Dkt. Mary Nagu  na Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lui Youqing wakikata Keki  wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji na Uwezeshaji Dkk. Mary Nagu akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
 Picha ya Keki kwa ajili ya hafla ya maadhimisho ya miaka 65 tokea kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lui Youqing (katikati) akiteta jambo na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya kuadhimisha miaka 65 tokea kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana na Afisa anayeshughulikia masuala ya Menejimenti na Programu wa Aga Khana Development Network Bw. Navroz Lakhani
 Msanii wa Jamhuri ya Watu wa China akicheza mchezo wa Wushu wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
 ya wageni wakisoma vitabu wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni wakifuatilia michezo mbalimbali kutoka kwa wasanii wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija, WHVUM
*************************************************
Na: Daud Manongi,    WHVUM
Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2013 China imetoa msaada wa zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 1.943 kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ushirikiano wa kibiashara  dola bilioni 3.7 na uwekezaji dola bilioni 2.5 na jumla ya makampuni 500 yamewekeza nchini Tanzania.
Haya yamebainishwa na Waziri wa Nci ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya miaka 65 ya toka kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.

Dkt Nagu amesema kuwa msaada huo utasaidia katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwema Bandari ya Bagamoyo, mradi wa EPZ, usambazaji wa umeme ukanda wa Kaskazini – Mashariki, Elimu kwa njia ya mtandao,Serikali Mtandao kwa ajili ya Zanzibar na Umeme wa upepo katika mkoa wa Singida.
Aliongeza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutafungua njia za uchumi na kusababisha Tanzania kuwa na uchumi imara na endelevu.

“Najisikia faraja kusema kuwama pamoja na mafanikia chanya tunayopata Tanzania bado ina miradi mingi ambayo inahitaji msaada wa kifedha na kitaalam kutoka kwa Jamhuri ya Watu wa China na ni imani kuwa wataendelea kutoa ushirikiano katika kufanikisha miradi hiyo” Alisema Dkt. Nagu.

Kwa upande wake Balozi wa China hapa nchini Balozi Lui Youqing amesema kuwa nchi yake itaendelea kuisaidi Tanzania kwa kuwa kumekuwa na mahusiano mazuri nay a muda mrefu baina ya nchi hizi mbili.

Balozi Youqing ameongeza kuwa Tanzania inavutia wakezaji kwa kuwa na mazingira salama ya kisiasa na kijamii ambapo anashawishika kuunganisha wawekezaji wa China kushirikiana na wawekezaji wengine katika kupunguza umasikini na kuleta maendeleo akitolea mfano ushirikiano katika sekta ya majengo.
“Tanzania ni nchi kubwa yenye maono na inayovutia zaidi kimataifa kutokana na uimara wake katika Nyanja za siasa na uchumi jamii, imekuwa na ushawishi wa hali ya juu katika anga za kikanda na kimataifa, hali inafanya wawekezaji kutoka sehemu kama EU, US, Japana na kwingineko waongeze uwekezaji, ata mimi binafsi nashawishika kuwashawishi wawekezaji wa China kuwekeza zaidi katika nchi hii” Alisema Balozi Youqing.

China inasherehekea miaka 65 toke kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1949, wkati huo huo ni miaka 50 sasa tokea Taifa kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia kati yake na Tanzania uhusiano ambao umeasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mao Zedong.

Kweingoma waahidi uhondo wa ngoma ya selo tamasha la Handeni Kwetu

September 29, 2014

NA MWANDISHI WETU, HANDENI
KIKUNDI cha ngoma cha selo kilichopo katika kijiji cha Kweingoma, wilayani Handeni, mkoani Tanga, kimesema kimepania vikali Desemba 13 mwaka huu kufanya balaa katika tamasha la Handeni Kwetu 2014, litakalofanyika wilayani hapa.

Shauku ya kikundi hicho imetolewa na Kiongozi wao Zaina Selemani, alipozungumzia umuhimu wa tamasha hilo, ambalo mwaka jana walishindwa kushiriki kutokana na wasanii wake wengi kukabiliwa na mambo ya kifamilia, ikiwamo kuugua na kuuguliwa.

Akizungumza kwa furaha kubwa, Zaina alisema ngoma ya selo ni nzuri inayoshawishi kuangalia wasanii wanapokuwa jukwaani, hivyo mashabiki na wadau wote watapata burudani nzuri.

“Mwaka huu tutashiriki kwa nguvu zote kwasababu ni tamasha lililoanza vizuri kwa mkoa huu wa Tanga, maana vikundi vingi kutoka sehemu mbalimbali za Handeni na mkoa wa Tanga vinashiriki,” alisema.

Naye Mratibu Mkuu wa tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa kwa siku kadhaa walikuwa wakifanya ziara kadhaa katika vijiji ambavyo vina vikundi vya ngoma za asili ili vishiriki, hususan vile ambavyo mwaka jana havikushiriki.

“Tunataka kuongeza wigo wa vikundi kutoka ndani ya Tanga na nje pia, ukizingatia kuwa tunahitaji tamasha lenye nguvu na mguso pia ili kukuza sekta ya utamaduni na uchumi wa nchi yetu,” alisema Mbwana.

Tamasha la Handeni Kwetu lililopangwa kufanyika Desemba 13 katika Uwanja wa Azimio (Kigoda Stadium), ni moja ya matukio makubwa mkoani Tanga yanayokutanisha mamia ya watu kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania.

Tibaijuka aombwa kuingilia kati mgogoro eneo la viwanda Kange Tanga

September 29, 2014
Wamiliki wa  eneo la viwanda la Kange Jijini Tanga wamemuomba
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi,Profesa Anna Tibaijuka kuingilia kati mgogoro wa uvamizi eneo lao  ili kuepusha
uwezekano wa kutokea uvunjifu wa amani.

Walisema eneo lao ambalo walimilikishwa na Halmashauri ya Jiji la
Tanga tangu 2008 ,limevamiwa na Serikali ya Kijiji cha Kichangani na kugawa  kwa wananchi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kinyume cha sheria.

Katibu wa kamati ya  walimiki hao wa viwanda ya kushughulikia mgogoro huo,Kassim Salim alisema jana kuwa umefikia hatua mbaya  na sasa kuna hatari ya kumwagika damu  kwa sababu vijana wa Kichangani wanazuia wamiliki wa viwanda kujenga hapo.

“Baadhi tunataka kujenga viwanda lakini kuna vijana wamekuwa wakizuia magari kumwaga mawe na mchanga,ina maana wamejipanga kwa vurugu  sasa hii hali inatakiwa kuingiliwa kati”alisema Salim.

Katibu huyo alisema tayari wamiliki hao wamefikisha malalamiko yao
katika ngazi mbalimbali za Halmashauri ya Jiji na Serikali Wilaya ya
Tanga lakini kuna hali ya kutegeana kutoa maamuzi jambo ambalo
linaweza kuhatarisha hali ya amani katika eneo hilo.

Alisema ili kuleta hali ya amani katika en eo hilo wameona ni vyema kumuomba Waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi,Anna Tibaijuka kuingilia kati.

Mwenyeikiti wa Serikali ya Kijiji cha Kichangani,Rajab Mbalazi alisema kimsingi katika eneo hilo hakuna mgogoro kwa sababu ni mali ya Kijiji na imeamua kugawa kwa wananchi kwa kufuata taratibu zake na kwamba,wamiliki hao waligawiwa kinyume cha sheria kwani si mali ya Halmashauri ya Jiji.

“Mwaka 2008 Halmshauri ya Jiji la Tanga kupitia idara yake ya mipango ilichukua ardhi hiyo kinyemela bila ridhaa ya kijiji ndipo mwaka 2012 kupitia mkutano mkuu wa kijiji ukaamua kurejesha ardhi yake”alisema Mbalazi.

Mwenyekiti huyo alisema kuanzia Julai 28 mwaka 2012 Serikali ya kijiji iliamua kutekeleza kwa vitendo na karibu asilimia 90 ya ardhi
iliyokuwa imechukuliwa na halmashauri ya jiji kinyemela tayari
imeshagawa kwa wananchi.

Hata hivyo gazeti hili  linayo nakala ya tangazo lililotolewa na
Halmashauri ya Jiji la Tanga lililosainiwa na Mkurugenzi
Mtendaji,Juliana Malange likitahadharisha kwamba kumejitokeza watu au kikundi chenye tabia  ya uvamizi katika viwanja  katika maeneo ya Kange  A,B,C,D,E,F  na Kange eneo la Viwanda ,Masiwani shamba,Mwakidila,Mwahako,
Magaoni,Mwambani,Mbugani na EPZ.

Tangazo hilo liliwatahadharisha wananchi kuepuka kununua ovyo viwanja ambavyo havina  nyaraka  halali huku likiwahimiza wenye viwanja kuvilinda.