SHAKA HAMDU SHAKA AKUTANA NA MKUU WAMKOA WA SIMUYU

October 14, 2016
 
 Mkuu wa Mkoa Simiyu Mhe:Antony Mtaka akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Mapema
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akikagua Banda na kupatamaelezo Mbali mbali juu ya Shughuli mbali mbali zinazofanywa Jeshi laKujenga Taifa Kambi ya Msange
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akipata Maelezo katika Banda la NHIF
 
 Kaimu katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akimweleza jambo  Mkuu wa Mkoa Simiyu Mhe Antony Mtaka  kwa Msisitizo

Viongozi wakishikilia bidhaa zinazozalishwa na Vijana Mkoani Simiyu    
Na Woinde Shizza wa Globu  ya jamii
 
Katimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu  (MNEC)   amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu
wa  Mkoa wa Simiyu Mhe, Antony Mtaka  ofisini kwake Bariadi Mkoa wa Simiyu katika mazungumzo yao waligusia Nyanja mbali mbali za kuimarisha mfumo wa kuwawezesha vijana kumudu kujiajiri ikiwa ni kupunguza malalamiko ya kilio cha ukosefu wa ajira kwa vijana. Kaimu Katibu Mkuu amempongeza Mkuu huyo wa Mkoa kwa
kuitikia na kutekeleza kwa vitendo agizo la  Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, John Pombe Magufuli kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda ili kutoa fursa kwa vijana kupata ajira.
Amesifu mpango mkakati na utekelezaji wake unaojulikana Wilaya mmoja kiwanda moja ni kampeni ambayo
imeanza kuonyesha matukio ambapo vijana wanaonekana kuanza kuchangamkia fursa hiyo ndani ya wilaya za mkoa wa Simiyu, ametoa wito kwa wakuu wa Mikoa wengine kuiga mfano mzuri ulioaznishwa na Mkoa wa Simiyu ili kuendana kwa pamoja na kasi na lengo la Rais la HAPA KAZI ambapo kinadharia linahimiza maendeleo
endelevu nay a haraka katika sekta zote za kiuchumi  na kijamii hususan kwa Vijana.
Kwa upande wake  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amemueleza Kaimu katibu Mkuu Shaka kuwa wamejipanga vizuri katika kubuni na kuendeleza mipango yao sio kwa maneno bali kwa vitendo ili kuufanya mkoa huo kuwa  kitovu
cha viwanda vidodogo na vya kati na viwanda vikubwa . Kwasasa Simiyu imeanzisha kiwanda cha maziwa Wilaya ya Meatu na kiwanda cha Wilaya ya Maswa
Wakati huo Kaimu Katibu Mkuu ametembelea na kukagua mabanda ya Maonyesho yaliyozinduliwa tarehe 7 mwezi huu ikiwa ni miongoni mwa shuhuli za wiki ya Vijana kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu.Kaimu Katibu Mkuu ameridhishwa na muamko wa vijana katika kuonyesha muamko wa kuitikia wito wa Serikali wa kuwekeza katika miradi yao ya kijamii ili kumudu kujiari na kupunguza kilio cha ukosefu wa ajira sambamba na kuwanusuru wasijiingize katika matendo maovu.
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN MINJA ATEMBELEA ENEO LITAKALOJENGWA KIWANDA KIPYA CHA KUTENGENEZA VIATU, MJINI MOSHI

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN MINJA ATEMBELEA ENEO LITAKALOJENGWA KIWANDA KIPYA CHA KUTENGENEZA VIATU, MJINI MOSHI

October 14, 2016
g1
Kamishna Jenerali wa Magereza – CGP. John Casmir Minja(vazi la kiraia) akiwa ameongozana na Mkuu wa Gereza  Karanga, Moshi, ACP. Hassan Mkwiche (kushoto) pamoja na Kaimu Mkuu wa Kiwanda cha Viatu Karanga, ASP. Michael Minja(kulia) alipotembelea Kiwanda hicho ili kuona eneo lililotengwa kwa ajili ya  ujenzi wa Kiwanda kipya cha kisasa cha viatu leo Oktoba 14, 2016. Wengine pichani ni Maafisa wa Jeshi la  Magereza Mkoani Kilimanjaro.
g2
Kamishna Jenerali wa Magereza – CGP. John Casmir Minja(vazi la suti) akiangalia eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda kipya cha viatu .
g3
Kamishna Jenerali wa Magereza – CGP. John Casmir Minja(vazi la suti) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Magereza Mkoa Kilimanjaro, ACP. Anderson Kamtearo(kulia) alipokagua moja ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho kipya cha kutengeneza viatu.
g4
Eneo litakalojengwa kiwanda kipya cha kisasa cha kutengeneza bidhaa mbalimbali za ngozi. Kiwanda hicho kitakuwa cha ubia baina ya Shirika la Magereza na Mfuko wa jamii wa PPF.
g5
Kamishna Jenerali wa Magereza – CGP. John Casmir Minja akiangalia kiatu aina ya buti ndefu zinazotengenezwa kiwandani hapo kwa ajili ya Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kama inavyoonekana katika picha
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

KONGAMANO LA KUMUENZI MWALIMU J.K NYERERE LAFANYIKA WILAYANI IKUNGI

October 14, 2016
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwa amembeba mmoja ya mwanafunzi wa shule ya Msingi Ikungi mchanganyiko
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikabidhi mahitaji kwa wanafunzi walemavu mara baada ya kuwasili shule ya msingi Ikungi mchanganyiko
 Baadhiya washiriki wa Kongamano wakisikiliza kwa makini mada zikiwasilishwa kwenye mdahalo

BARABARA YA DODOMA-MAYAMAYA KUKAMILIKA NOVEMBA

October 14, 2016
Muonekano wa Barabara wa Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65 ikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake. Barabara hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi Novemba Mwaka huu.
Meneja Mradi wa Barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65 Eng. Yusuf Karera, akitoa maelezo ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa barabara hiyo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kushoto), alipokagua ujenzi wake, Mkoani Dodoma.
Muonekano wa tabaka la kwanza la Barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65 ambayo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiweka mchanga katika tabaka la kwanza la ujenzi wa barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65 alipokagua mkoani Dodoma.
RAIS WA ZANZIBAR DK ALI MOHAMED SHEIN AONGOZA SHUGHULI ZA UZIMAJI MWENGE MKOANI SIMIYU LEO

RAIS WA ZANZIBAR DK ALI MOHAMED SHEIN AONGOZA SHUGHULI ZA UZIMAJI MWENGE MKOANI SIMIYU LEO

October 14, 2016
mibi
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar SMZ na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Ali Mohamed Shein akipokea mwenge kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu George Mbijima wakati wa sherehe za uzimaji wa Mwenge wa Uhuru Bariadi mkoani Simiyu leo  baada ya kukimbizwa nchi nzima huku kiongozi huo akikagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuhimiza wananchi katika uwajibikaji kwa taifa ambapo sherehe hizo zimefanyika kitaifa mkoani humo.
WAZIRI MKUU APOKEA MSAADA WA SH. MILIONI 27.62

WAZIRI MKUU APOKEA MSAADA WA SH. MILIONI 27.62

October 14, 2016

shivyata
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa  akisalimiana na Ahmed Olotu(Mzee Chilo) mara baada ya kupokea shilingi laki sita na ishirini kutoka kwa Mtandao wa wasanii(SHIWATA) ikiwa ni msaada wa kusaidia waathirika wa tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.Wengine pichani ni Mkurugenzi  Idara ya uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Gen.Mbazi Msuya na Caasim Taalib(wa tano kushoto)  ambaye ni Mwenyekiti wa mtandao wa wasanii.
shivyata1
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara ndogondogo solo la kariakoo  mara baada ya kupokea msaada wa nguo mchanganyiko,midoli na kanzu wenye thamani ya  shilingi milioni 2 ikiwa ni msaada wa kusaidia waathirika wa tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.
……………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea fedha taslimu sh. milioni 25.62 pamoja na nguo zenye thamani ya sh. milioni mbili  kutoka kwa wadau mbalimbali.
Makabidhiano ya michango hiyo yamefanyika leo (Ijumaa, Oktoba 14, 2016) kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.
Akiwashukuru wadau hao Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.
“Nawashukuru kwa kuamua kutumia siku ya leo ya kukumbuku ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere kuwachangia wenzetu waliopatwa na maafa,” amesema.
Waziri Mkuu amesema michango hiyo ni muhimu na inaonyesha mshikamano wa dhati uliopo baina ya Watanzania.

MAKAMU WA RAIS AHANI MSIBA WA MASABURI LEO

October 14, 2016

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapa pole ndugu marehemu Dk. Didas Masaburi mapema leo Chanika,jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole Bw. Deogras Didas Masaburi (Ojambi) ambaye ni mtoto wa  Marehemu Dk. Didas Masaburi na Diwani wa  kata ya Chanika,jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Profesa Philemon Sarungi mara baada ya kukutana kwenye msiba wa Marehemu Dk. Didas Masaburi mapema leo Chanika,jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole na kumfariji Bi.Janeth Masaburi ambaye ni mke wa  Marehemu Dk. Didas Masaburi na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea,jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi wakimpa pole na kumfariji Bi.Janeth Masaburi ambaye ni mke wa  Marehemu Dk. Didas Masaburi na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea,jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini kwenye kitabu cha maombelezo cha marehemu Dk. Didas Masaburi  nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea,jijini Dar es salaam.  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.

BENKI YA POSTA TANZANIA (TPB) YAMALIZA TATIZO LA UHABA WA VYOO KWA WALIMU WA SHULE YA MSINGI IPINDA KYELA

October 14, 2016
Meneja Mahusiano kwa Umma benki ya Posta Tanzania (TPB) Noves Moses akizungumza katika hafla ya Makabidhiano ya mradi wa vyoo vya walimu vyenye matundu matano katika shule ya Msingi Ipinda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya ambavyo ujenzi wake umeghalimu kiasi cha shilingi milioni 8kwa msaada wa benki hiyo ya Posta Tanzania.

Baadhi ya wananchi,walimu na wazazi pamoja na wanafunzi shule ya Msingi Ipinda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya vyoo vya walimu vilivyo jengwa kwa msaada wa benki ya Posta Tanzania TPB.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ipinda Wilayani kyela Mkoani Mbeya wakitoa burudani katika hafla ya makabidhiano ya vyoo vya walimu vyenye matundu matano ambavyo vimejengwa kwa msaada wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa thamani ya shilingi milioni 8.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ipinda Subira Gwakabale akishukuru kwa kupatiwa msaada na benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa kujengewa vyoo vya walimu vyenye matundu 5 kwa thamani ya shilingi milioni 8 ,ambapo pia katika katika shukrani zake ameelezea changamoto mbalimbali walizonazo ikiwa ni pamoja na Idadi kubwa ya wananfunzi kuliko vyumba vya madarasa walivyo navyo ambapo kwa sasa  wana jumla ya wanafunzi 948 huku vyumba vya vya madarasa vikiwa 8 tu hali ambayo inawawia vigumu katika utoaji wa huduma kwa wanafunzi hao.

BONANZA LA MWALIMU NYERERE ARUSHA LAFANA

October 14, 2016

Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akizungumza kwenye Bonanza la Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jiji Arusha,kushoto ni Afisa Michezo wa Jiji,Benson Maneno na kulia ni Katibu Tawala wa wilaya(DAS)David Mwakiposa.

Katibu Tawala wilaya ya Arusha,David Mwakiposa akizungumza kwenye Bonanza la Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jiji Arusha,katikati ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akifatilia kwa makini na kushoto ni Afisa Michezo wa Jiji,Benson Maneno .

Katibu Tawala wilaya ya Arusha,David Mwakiposa akiangalia michoro yenye sura ya hayati Mwalimu Nyerere ilichorwa na vijana wazalendo  kwenye Bonanza la Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jiji Arusha.

Watoto wakichuana kukimbia mbio za mita 50 kwenye Bonanza hilo.


Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro(wa pili kushoto)akiwa na Mwenyekiti wa mchezo wa Karate mkoa wa Arusha,Richard Kitoro pamoja Sensei Dad na Sensei David wakifatilia michezo iliyokua ikiendelea.

Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Edmund Rice akionyesha umahiri wake kwenye mchezo wa Karate 

Kikundi cha Karate kikonyesha mbinu za mchezo huo

Kikundi cha Karate kikonyesha mbinu za mchezo huo kwenye Bonanza la Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jiji Arusha

Burudani nayo ilikua sehemu ya kunogesha Nyerere Day
LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA OKTOBA 15 N 16

LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA OKTOBA 15 N 16

October 14, 2016
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Oktoba 15, 2016 kwa michezo mitatu ambako Simba inayoongoza katika msimamo wa kuwania taji hilo katika timu 16 itaikaribisha Kagera Sugar ya Kagera kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Na.73, mwamuzi atakuwa Hussein Athuman kutoka mkoani Katavi ambako pembeni atasaidiwa na Joseph Bulali wa Tanga na Silvester Mwanga wa mkoani Kilimanjaro wakati Soud Lila wa Dar es Salaam atakuwa mwamuzi wa akiba huku Kamishna wa mchezo akiwa Pius Mashera wa Dodoma.

Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya JKT Ruvu na Mwadui ya Shinyanga. Ni mchezo Na. 74 utakaofayika Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani ambako utachezeshwa na Mwanamama mwamzi mwenye beji la FIFA, Mwanahamisi Matiku wa Dar es Salaam, akisaidiwa na Shafii Mohamed pia wa Dar es Salaam na Gesper Ketto wa Arusha.
Mwamuzi wa akiba atakuwa Abdallah Rashid wa Pwani wakati Kamishna wa mchezo huo atakuwa Charles Mchau wa Kilimanjaro.
Pia Stand United ya Shinyanya itaikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa CCM Kambarage katika mchezo Na. 75 ambao utachezeshwa na Eric Onoka wa Arusha akisaidiwa na Agnes Pantaleo pia wa Arusha na Omary Juma wa Dodoma wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Joseph Pombe wa Shinyanga. Kamishna wa mchezo atakuwa Hamisi Kitila wa Singida.
 RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA BIASHARA WA JAMHURI YA WATU WA CHINA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA BIASHARA WA JAMHURI YA WATU WA CHINA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

October 14, 2016
b1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming  aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
b2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini  Dkt. Lu youqing  Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming .
b3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya EXIM ya China Sun Ping ambaye aliambatana na Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming, pamoja na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu youqing.
b4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming watatu kutoka kulia  aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo. Wengine katika picha ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango wakwanza (kushoto) Makamu wa Rais wa Benki ya EXIM ya China Sun Ping wapili kutoka (kushoto) Balozi wa China hapa nchini Dkt. Dkt. Lu youqing watatu kutoka (kushoto),Pamoja na  Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage wapili kutoka kulia.
b5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
b6 b7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi wa China hapa nchini  Dkt. Lu youqing mara baada ya kumaliza mazungumzo ya pamoja na ujumbe wa Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa Jamhuri ya China uliofika Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Dk.Kigwangalla na Mwigulu Nchemba waombewa dua na Sheikh Mkuu wa jumuiya ya Bohora Duniani

October 14, 2016

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla jioni hii ya leo Oktoba 13.2016 amekaribishwa na dhehebu la Bohora na kuombewa dua maalum na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin katika msikiti wa dhehebu hilo Upanga Jijini Dar es Salaam.

Mbali na kutoa dua kwa Dk. Kigwangalla, Sheikh Dkt. Syedna ameahidi kuleta wawekezaji wa Kibohora kutoka sehemu mbalimbali Duniani kwa ajili ya kuwekeza kwenye ujenzi wa Mahospitali ikiwemo Hospitali za Rufaa za kisasa pamoja na Viwanda vya Dawa hali ambayo itapunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kufuata matibabu.

Pia viwanda vya dawa vitashusha gharama za dawa nchini na kupunguza ucheleweshaji unaosababishwa na kuagiza dawa nje ya nchi.

Aidha, katika tukio hilo, usiku huu, Dk.Kigwangalla ameweza kushuhudia ndoa za Vijana zaidi ya 50 zikifungishwa na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna.

Mbali na Dk.Kigwangalla kuombewa dua maalum na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna, Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba aliungana katika kuombewa na Shehe huyo.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin (kulia) wakati wa kuombewa dua maalum usiku huu.
Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin (kulia) akimuombea Dua maalum Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto aliyefumba macho)
Dua zikiendelea
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akibusu mkono wa Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin isharara ya kupokea dua katika tukio hilo
Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin akimuaga Dk.Kigwangalla baada ya dua

Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba akiombewa dua katika tukio hilo.
Watu kutoka Mataifa mbalimbali Duania ikiwemo jamii ya Bohora ambao pia wapo hapa nchini nao wamepata bahati ya kuombewa dua maalum na Shehe huyo Mkuu