MABALOZI WAIPONGEZA TAASISI YA JKCI KWA KUFANYA UPASUAJI WA MOYO

October 22, 2015

Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi amezungumza na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini kuhusu shughuli za upasuaji wa moyo zinazofanywa na taasisi hiyo. Profesa Janabi amezungunza na mabalozi hao katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
 Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku (kushoto) na Balozi wa Rwanda hapa nchini, Eugene Kayihura (kulia) wanamsikiliza Profesa Mohamed Janabi wakati akieleza mambo ambayo watu wanapaswa kuzingatia ili kuepuka shinikizo la damu kwenye mkutano uliofanyika Hoteli leo Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Judith Kangoma (kulia) na mwenzake wa Malawi, Hawa Ndilowe wakimsikiliza Profesa Mohamed Janabi leo.
Picha zote kwa Hisani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
 MABALOZI wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania wameipongeza Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa kuanzisha huduma ya upasuaji wa moyo.

Mabalozi hao wamefurahishwa na huduma hiyo na kueleza kwamba watawashauri raia wao kwenda kupatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo.

Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Balozi Edzai Chimonyo amesema kwamba wamefurahishwa na juhudi za taasisi hiyo na kwamba wanapenda kujua jinsi ya kuzuia matatizo ya moyo.

“Napenda kujua ni vipi mtu anaweza kuzuia matatizo ya moyo,” amesema Balozi Chimonyo.
Naye Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku amesema kwamba ataitumia taasisi hiyo kupima afya yake na kwamba endapo atatozwa fedha kwa ajili kupatiwa matibabu yupo tayari kutoa ili kusaidia wagonjwa wa kawaida wanaopatiwa matibabu hapo.

Akizungumza na mabalozi hao, Kaimu Mkuu wa taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi amesema ili watu wasipate shinikizo la damu wanapaswa kufanya mazoezi, kupima afya mara kwa mara na kuchunguza endapo familia ina tatizo la shinikizo la damu.

Profesa Janabi amesema kwamba endamba mabalozi hao watazingatia hayo wataepuka kupata shinikizo la damu.

Awali Profesa Janabi amewaeleza mabalozi hao huduma zinazotolewa na taasisi hiyo ikiwamo kufanya upasuaji kwa watoto 37 hivi karibuni wakimo watoto wawili kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC).

Profesa Janabi amesema upasuaji wa moyo unaofanywa na hospitali hiyo unasaidia kupunguza gharama za matibabu endapo wangekwenda kutibiwa India.
Amesema gharama za mgonjwa kufanyiwa upasuaji wa moyo India ni kuanzia Dola 10,000 hadi 12,000 wakiwamo ndugu wanaomsindikiza mgonjwa nchini humo.

TAARIFA YA CCM JUU YA KUFUNGA KAMPENI ZAKE KATIKA MIKOA MBALI MBALI

October 22, 2015
CCM inapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wake na kwa umma wa Watanzania.
Kufunga Kampeni
CCM itafunga kampeni zake kwa utaratibu mpya na kwa kishindo. Kampeni za CCM zitafungwa Kitaifa kwa mikutano mikubwa ya kampeni katika mikoa mitano. Mikutano hiyo itaongozwa na viongozi wa CCM Kitaifa waliopo madarakani na wastaafu. Mikoa hiyo na viongozi watakaoongoza mikutano hiyo ni kama ifuatavyo:
1. Mwanza – Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, Mgombea Urais, na Ndugu Samia Hassan Suluhu, Mgombea Makamu wa Rais
2. Tanga – Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM
3. Mbeya – Ndugu Benjamin William Mkapa, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
4. Mtwara – Ndugu Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
5. Kigoma – Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM
6. Kilimanjaro – Ndugu Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu
7. Mara – Ndugu Joseph Warioba, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu
Kati ya leo na kesho, maeneo mengine yanaweza kuongezeka. Mikutano hii itaanza saa sita mchana na itarushwa, yote kwa pamoja, kwa matangazo ya moja kwa moja ya vituo vya televisheni vitano na vituo vya redio 67. Vilevile, watakaohudhuria katika mikutano hii wataunganishwa moja kwa moja na mkutano wa Mwanza, alipo Mwenyekiti, Mgombea na Mgombea Mwenza, na wataweza kusikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli moja kwa moja kupitia screens zitakazokuwa katika viwanja vyote hivi saba.
Namna hii ya ufungaji wa kampeni itakuwa ni ya kihistoria, na inadhihirisha nguvu ya CCM inayoiwezesha kufanya mikutano mikubwa ya kampeni kwa siku moja katika maeneo mbalimbali nchini. Lakini pia tutaweka historia katika tasnia ya utangazaji wa televisheni hapa nchini kwa kutangaza na kuunganisha kwa pamoja matukio saba kwa wakati mmoja.
Kwa upande wa Dar es Salaam, tutafanya mkutano mkubwa wa ufungaji wa kampeni za Mkoa wa Dar es Salaam, katika Uwanja wa Jangwani, kesho, Ijumaa, tarehe 23 Oktoba 2015. Siku ya Jumamosi, tarehe 24 Oktoba 2015, Wagombea Ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao kwa namna mahsusi.
Tathmini ya Kampeni
Kama Chama, tumeridhika na ubora na ukubwa wa kampeni tulizofanya licha ya changamoto za hapa na pale. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wamefanya kazi kubwa, na kwa bidii kubwa, na maarifa makubwa. Wamekuwa barabarani kwa siku 57 wakifanya mikutano kati ya 8 hadi 12 kwa siku. Imani yetu ya ushindi inatokana na kazi kubwa waliyofanya. Pia, CCM inawashukuru viongozi, wapenzi wa washabiki wake – wa makundi mbalimbali ya kijamii - kote nchini kwa kazi kubwa ya kampeni waliyoifanya.
Kutokana na kazi kubwa na nzuri iliyofanyika, na kutokana na mwenendo wa tafiti huru na tafiti zetu za ndani, CCM inategemea ushindi wa asilimia zisizopungua 69.
Uchaguzi wa Amani
CCM haitachoka kuendelea kusisitiza uchaguzi wa amani na utulivu. Sisi kama chama kikubwa cha siasa nchini, chenye wafuasi wengi zaidi, na chenye dhamana ya uongozi wa dola, tutatimiza wajibu wetu wa kuhimiza utulivu kwa wapenzi, washabiki na wanachama wetu. Tunawataka na wenzetu wafanye hivyo.
Kauli za wenzetu kwamba kura zitaibiwa ni kauli za kutojiamini na kujiandaa kufanya vurugu. Kauli za kwamba washabiki wa UKAWA wakishapiga kura wabaki vituoni kulinda kura si kauli za wanaotaka uchaguzi wa amani.
Kwa utaratibu wetu wa uchaguzi, utaratibu wa pekee kwa Chama kulinda kura zake ni kwa kupitia wakala wa vyama waliopo kwenye kila kituo cha kupiga kura na wenye nguvu na mamlaka ya kisheria ya kushuhudia zoezi zima, kuanzia kupiga kura, kuhesabu kura hadi kutangaza matokeo. Kura zinapigwa na kuhesabiwa vituoni mbele ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Mawakala wa vyama na Waangalizi wa Uchaguzi wa ndani na nje ya nchi. Mawakala wa vyama na Wasimamizi wa Uchaguzi wanaweka sahihi kwenye fomu za matokeo, na matokeo hayo yanatangazwa na kubandikwa kwenye kituo. Kwenye kituo kikuu cha Tume cha kujumlisha matokeo, mawakala wa vyama pia huwepo na Tume hujumlisha matokeo kutoka kwenye fomu za matokeo za vituo vya nchi nzima zilizosainiwa na mawakala wa vyama kwenye kila kituo. Kwa viongozi wa UKAWA kuwaambia watu waingie barabarani au kuvizunguka vituo vya kupigia kura eti ili kulinda kura hakuna maana yoyote zaidi ya kutafuta namna ya kuhalalisha fujo, vurugu na uporaji na kuwazuia watu wengine, hasa wanawake, kupiga kura. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vizuie hili jambo kwa sababu halina nia njema.
Mkakati wa UKAWA ni kufanya vurugu baada ya kushindwa na kutengeneza mazingira ya mgogoro wa kisiasa ili Jumuiya ya Kimataifa iingilie kati na kupendekeza kugawana madaraka. Mkakati huo hautafanikiwa. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vihakikishe ulinzi na usalama wa watu wote na mali zao siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.
CCM haitakubali hata kidogo ushindi wake kuhojiwa au kutiliwa shaka kwa sababu tu ya vurugu zilizoanzishwa na watu wengine.
Siku ya Jumamosi, CCM itatangaza namba maalum za simu kwa Watanzania wote ili siku kabla ya Uchaguzi, siku ya Uchaguzi na mara baada ya uchaguzi, waweze kupiga simu au kutuma ujumbe pale watakapokuwa wanabaini au kushuhudia vitendo vya kuvuruga amani na kuvuruga utaratibu mzima wa Uchaguzi.
Kupokea Matokeo
CCM imeweka utaratibu wa kupokea matokeo kwa kutumia Mawakala wake moja kwa moja vituoni na kupitia mtandao wa Chama. CCM inategemea kuwa na matokeo ya Uchaguzi nchi nzima ifikapo saa nne usiku, siku ya Uchaguzi, tarehe 25 Oktoba 2015.
Imetolewa na:
January Makamba
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
MJUMBE WA KAMATI YA KAMPENI
22 OKTOBA 2015.
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

DK. JOHN MAGUFULI AOMBA KURA KUPITIA SIMU

October 22, 2015
CHAMA cha Mapinduzi CCM kimezidi kujitengenezea mazingira mazuri ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka unaotarajiwa kufanyika Jumapili, Oktoba 25 baada ya kubuni mkakati mpya
wa ushindi ambapo mgombea wa nafasi ya urais Dk. John Magufuli kuwapigia simu wananchi akiomba wampigie kura. Ujumbe huo unaokwenda kwa watumiaji wa simu za mitandao mbalimbali humfikia mmiliki wa simu kupitia namba +255622333333 na mara baada ya simu hiyo kupokelewa husikika sauti ya Dk. Magufuli akiwaomba watanzania kumpigia kura ili aweze kushinda na hatimaye aweze kuwa rais. Hatua hiyo ni moja ya njia muhimu za kuwafikia watanzania wote bila kujali itikadi zao na zaidi wale baadhi ya wananchi waliokosa fursa ya kusikia mambo yapi yatafanywa na mgombea huyo endapo kama atafanikiwa kuwa rais. Ukiacha utaratibu wa kampeni za moja kwa moja majukwaani, mabango, mahojiano katika televisheni, hatua ya Chama cha Mapinduzi kubuni njia ya kutuma ujumbe huo kwa wananchi utawasaidia kujiongezea kura katika uchaguzi huo unaonekana kuwa na ushindani mkubwa. Pengine hili ndio bao la mkono lililowahi kusemwa kipindi cha nyuma na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Nape Nnauye kutokana na hatua hiyo kuwa muhimu hususani wakati huu ambao watanzania wengi wanamiliki simu za mkononi. Kutokana na hatua hiyo ina maana kuwa watanzania wengi wataweza kumsikia mgombea huyo akiwaomba kura mbali na maeneo mengine waliyozoea kusikia sauti yake ikiomba kumchagua katika uchaguzi huo unalenga kumpata rais wa awamu ya tano wa taifa hili. Chama cha Mapinduzi CCM kimemsimamisha Waziri huyo wa Ujenzi kushika kijiti kinachotarajiwa kuachwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete siku chache zijazo.

JOYCE MSIRU ,MKURUGENZI MTENDAJI MPYA WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI.MUWSA.

October 22, 2015
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji sa na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWASA,Sharry Raymond akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo wakati wa utamburisho wa Mkurugenzi mpya wa MUWSA.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA.
Mwenyekiti wa Bodi ya MUWSA,akizungumza.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA,Sharry Raymond akimtamburisha Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo,Joyce Msiru mbele ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,Joyce Msiru akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo mara baada ya kutamburishwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Mamlaka hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA wakiwa katika kikao hicho.
Aliyekuwa kaimu mkurugenzi wa Mamlaka hiyo,Mhandisi Patrick Kibasa akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa MUWSA,Mhandisi Alfred Shayo akizungumza katika kikao hicho.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa MUWSA kutoka wizarani,Abdalah Mkufunzi akizungumza katika kikao hicho.  
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya MUWSA,Hajira Mmambe akizungumza katika kikao hicho.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya MUWSA,Boniface Mariki akizungumza katika kikao hicho.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa MUWSA,Elizabeth Minde akizungumza katika kikao hicho.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakzi,TUICO tawi la MUWSA,Masudi Barie akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wakati wa kikao cha utamburisho wa mkurugenzi mpya.
Afisa habari wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA,Florah Nguma akisema neno la mwisho mara baada ya utamburisho wa mkurugenzi mpya wa Mamlaka hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

October 22, 2015

CCM inapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wake na kwa umma wa Watanzania.

Kufunga Kampeni
CCM itafunga kampeni zake kwa utaratibu mpya na kwa kishindo.  Kampeni za CCM zitafungwa Kitaifa kwa mikutano mikubwa ya kampeni katika mikoa mitano. Mikutano hiyo itaongozwa na viongozi wa CCM Kitaifa waliopo madarakani na wastaafu. Mikoa hiyo na viongozi watakaoongoza mikutano hiyo ni kama ifuatavyo:
 1.    Mwanza – Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, Mgombea Urais, na Ndugu Samia Hassan Suluhu, Mgombea Makamu wa Rais
 2.    Tanga – Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM
 3.    Mbeya – Ndugu Benjamin William Mkapa, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
 4.    Mtwara – Ndugu Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
5.    Kigoma – Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM
6.    Kilimanjaro – Ndugu Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu
7.    Mara – Ndugu Joseph Warioba, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu  Mstaafu
Kati ya leo na kesho, maeneo mengine yanaweza kuongezeka. Mikutano hii itaanza saa sita mchana na itarushwa, yote kwa pamoja, kwa matangazo ya moja kwa moja ya vituo vya televisheni vitano na vituo vya redio 67. Vilevile, watakaohudhuria katika mikutano hii wataunganishwa moja kwa moja na mkutano wa Mwanza, alipo Mwenyekiti, Mgombea na Mgombea Mwenza, na wataweza kusikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli moja kwa moja kupitia screens zitakazokuwa katika viwanja vyote hivi saba.
Namna hii ya ufungaji wa kampeni itakuwa ni ya kihistoria, na inadhihirisha nguvu ya CCM inayoiwezesha kufanya mikutano mikubwa ya kampeni kwa siku moja katika maeneo mbalimbali nchini.  Lakini pia tutaweka historia katika tasnia ya utangazaji wa televisheni hapa nchini kwa kutangaza na kuunganisha kwa pamoja matukio saba kwa wakati mmoja.
Kwa upande wa Dar es Salaam, tutafanya mkutano mkubwa wa ufungaji wa kampeni za Mkoa wa Dar es Salaam, katika Uwanja wa Jangwani, kesho, Ijumaa, tarehe 23 Oktoba 2015. Siku ya Jumamosi, tarehe 24 Oktoba 2015, Wagombea Ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao kwa namna mahsusi.

Tathmini ya Kampeni
Kama Chama, tumeridhika na ubora na ukubwa wa kampeni tulizofanya licha ya changamoto za hapa na pale. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wamefanya kazi kubwa, na kwa bidii kubwa, na maarifa makubwa. Wamekuwa barabarani kwa siku 57 wakifanya mikutano kati ya 8 hadi 12 kwa siku.  Imani yetu ya ushindi inatokana na kazi kubwa waliyofanya. Pia, CCM inawashukuru viongozi, wapenzi wa washabiki wake – wa makundi mbalimbali ya kijamii - kote nchini kwa kazi kubwa ya kampeni waliyoifanya.
Kutokana na kazi kubwa na nzuri iliyofanyika, na kutokana na mwenendo wa tafiti huru na tafiti zetu za ndani, CCM inategemea ushindi wa asilimia zisizopungua 69.

Uchaguzi wa Amani
CCM haitachoka kuendelea kusisitiza uchaguzi wa amani na utulivu. Sisi kama chama kikubwa cha siasa nchini, chenye wafuasi wengi zaidi, na chenye dhamana ya uongozi wa dola, tutatimiza wajibu wetu wa kuhimiza utulivu kwa wapenzi, washabiki na wanachama wetu. Tunawataka na wenzetu wafanye hivyo.
Kauli za wenzetu kwamba kura zitaibiwa ni kauli za kutojiamini na kujiandaa kufanya vurugu. Kauli za kwamba washabiki wa UKAWA wakishapiga kura wabaki vituoni kulinda kura si kauli za wanaotaka uchaguzi wa amani.
Kwa utaratibu wetu wa uchaguzi, utaratibu wa pekee kwa Chama kulinda kura zake ni kwa kupitia wakala wa vyama waliopo kwenye kila kituo cha kupiga kura na wenye nguvu na mamlaka ya kisheria ya kushuhudia zoezi zima, kuanzia kupiga kura, kuhesabu kura hadi kutangaza matokeo. Kura zinapigwa na kuhesabiwa vituoni mbele ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Mawakala wa vyama na Waangalizi wa Uchaguzi wa ndani na nje ya nchi. Mawakala wa vyama na Wasimamizi wa Uchaguzi wanaweka sahihi kwenye fomu za matokeo, na matokeo hayo yanatangazwa na kubandikwa kwenye kituo. Kwenye kituo kikuu cha Tume cha kujumlisha matokeo, mawakala wa vyama pia huwepo na Tume hujumlisha matokeo kutoka kwenye fomu za matokeo za vituo vya nchi nzima zilizosainiwa na mawakala wa vyama kwenye kila kituo.  Kwa viongozi wa UKAWA kuwaambia watu waingie barabarani au kuvizunguka vituo vya kupigia kura eti ili kulinda kura hakuna maana yoyote zaidi ya kutafuta namna ya kuhalalisha fujo, vurugu na uporaji na kuwazuia watu wengine, hasa wanawake, kupiga kura. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vizuie hili jambo kwa sababu halina nia njema.
Mkakati wa UKAWA ni kufanya vurugu baada ya kushindwa na kutengeneza mazingira ya mgogoro wa kisiasa ili Jumuiya ya Kimataifa iingilie kati na kupendekeza kugawana madaraka. Mkakati huo hautafanikiwa. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vihakikishe ulinzi na usalama wa watu wote na mali zao siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi. 
CCM haitakubali hata kidogo ushindi wake kuhojiwa au kutiliwa shaka kwa sababu tu ya vurugu zilizoanzishwa na watu wengine.
Siku ya Jumamosi, CCM itatangaza namba maalum za simu kwa Watanzania wote ili siku kabla ya Uchaguzi, siku ya Uchaguzi na mara baada ya uchaguzi, waweze kupiga simu au kutuma ujumbe pale watakapokuwa wanabaini au kushuhudia vitendo vya kuvuruga amani na kuvuruga utaratibu mzima wa Uchaguzi.

Kupokea Matokeo
CCM imeweka utaratibu wa kupokea matokeo kwa kutumia Mawakala wake moja kwa moja vituoni na kupitia mtandao wa Chama. CCM inategemea kuwa na matokeo ya Uchaguzi nchi nzima ifikapo saa nne usiku, siku ya Uchaguzi, tarehe 25 Oktoba 2015. 
Imetolewa na:

January Makamba
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
MJUMBE WA KAMATI YA KAMPENI
22 OKTOBA 2015
KAMATI YA STARS YATOA NAMBA ZA UCHANGIAJI

KAMATI YA STARS YATOA NAMBA ZA UCHANGIAJI

October 22, 2015

tedy 
Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda leo amefanya makutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume, ambapo ametumia nafasi hiyo kutangaza namba za simu za uchangiaji kwa Watanzania kwa ajili ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Akiongea na waandishi wa habari, Teddy amesema watanzania wanaweza kuichangia Taifa Stars kiasi chochote cha fedha kuanzia shilingi mia moja (TZS 100) kwenda namba 0654-888868 (Tigo Pesa) na 0789-530668 (Airtel Money) ambazo zitatumika kwa ajili ya motisha kwa wachezaji, uhamasishaji/masoko na maboresho ya kambi za ndani na nje ya nchi.
Aidha Teddy amesema Kamati ya Taifa Stars inaandaa utaratibu kwa ajili ya washabiki watakaotaka kusafiri kuelekea nchini Algeria katika mchezo wa marudiano, waweze kuchangia gharama za usafiri ili waweze kwenda kuipa sapoti Stars katika mchezo wa marudaiano Novemba 17, 2015.
“KamatI inaendelea na mchakato wa kukamilisha suala la kambi ya Taifa Stars, na mpaka sasa tunasubiri majibu kutoka katika vyama vya soka vya vya nchi tunazotaka kuweka kambi ambazo ni Afrika Kusini, Dubai na Oman kabla ya kutangaza rasmi kambi itakapokuwa” Alisema Teddy.
Kamati inawaomba watanzania, wadau, washabiki na wapenzi wa mpira miguu nchini kuichangia timu ya Taifa kupitia namba zilizotolewa na pia kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja wa Taifa siku ya mchezo wa tarehe 14 Novemba, 2015

JESHI LA POLISI KUIMARISHA ULINZI SIKU YA KUPIGA KURA

October 22, 2015

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25.

 Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo Mkuu wa Jeshi hilo IGP Ernest Mangu amesema kuwa ulinzi utaimarishwa maeneo yote kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kuwa taifa linapita salama katika kipindi hiki cha kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo ya uchaguzi.

 Ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kupiga kura siku  hiyo bila wasiwasi wa aina yoyote ili kuweza kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi.
(Picha na Francis Dande)
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 ambapo amewataka watu wote kutii sheria bila shuruti wakati wa uchaguzi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akifafan jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MSAJILI WA MAHAKAMA YA RUFAA NA MSAJILI WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA.

October 22, 2015

 Mhe. John Lugalema  Kahyoza akila kiapo mbele ya Rais Jakaya kikwete baada ya kuteuliwa kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufaa mapema hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam, awali mhe. Kahyoza alikuwaMsajili Mahakama Kuu ya Tanzania.
 MheKatarina Tengia Revocati akila kiapo mbele ya Rais Jakaya kikwete baada ya kuteuliwa kuwa Msajili Mkuu  wa Mahakama  mapema hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam, awali  Mhe. Katarina alikuwa Msajili wa Mahakama ya rufani.
 Waheshimiwa John Lugalema  Kahyoza na Bi. Katarina Tengia Revocati wakisubiri kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete mapema hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Viongozi na Wageni mbalimbali wakisubiri tukio la kuapishwa kwa waheshimiwa John Lugalema Kahyoza na Bi. Katarina Tengia Revocati mapema hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na majaji wanawake waliohudhuria sherehe za kuapishwa wa heshimiwa John Lugalema  Kahyoza na Bi. Katarina Tengia Revocati mapema hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo.

WAZIRI MEMBE AAGANA NA WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE

October 22, 2015

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akifungua hafla ya kumuaga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe iliyoandaliwa na watumishi wa Wizara hiyo na kufanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa waliohudhuria hafla hiyo
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya akitoa muhtsari wa shughuli chache ambazo Waziri Membe alizisimamia kwa umahiri mkubwa katika kipindi chake cha miaka 9 ya Uwazi wa Mambo ya Nje. Waliokaa ni Mhe. Membe na Balozi Mulamula ambao wanasikiliza kwa maikini shughuli zilizotekelezwa na Mhe. Waziri Membe.
Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali, Wakuu wa Idara/Vitengo na watumishi wakisikiliza kwa makini shughuli ambazo Mhe. Waziri Membe amezisimamia ipasavyo ikiwemo suala la maslahi ya watumishi.
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali, Wakuu wa Idara/Vitengo na watumishi wakisikiliza kwa makini shughuli ambazo Mhe. Waziri Membe amezisimamia ipasavyo ikiwemo suala la maslahi ya watumishi
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga akitangaza Tuzo na Zawadi mbalimbali ambazo zitatolewa kwa ajili ya Mhe. Waziri na Naibu Waziri na Wenza wao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (kushoto) akisoma maneno yaliyoandikwa katika Tuzo ya Uongozi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na kukabidhiwa na Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula
Waziri Membe akifurahia zawadi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje.
Waziri Membe akipokea zawadi kwa niaba ya Mama Membe ambaye hakuweza kufika katika hafla hiyo. Bi. Amisa Mwakawago, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu alikabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya Wizara.
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Begum Karim Taj naye akikabidhi zawadi kwa Mhe. Waziri kwa niaba ya Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania
Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahya akipokea zawadi kwa niaba ya Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim ambaye hakuweza kuhudhuria hafla hiyo kutokana na majukumu ya kitaifa.
Balozi Mulamula na Mama Mwakawago wakionesha zawadi ya Mama Mahadhi Juma Maalim.
Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali, Wakuu wa Idara/Vitengo na watumishi wakishuhudia zoezi la utoaji wa zawadi.
Waziri Membe akiongea na watumishi wa Wizara wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Itifaki, Balozi Juma Maharage akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy naye akiongea machache katika hafla hiyo
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Elibariki Maleko akionekana mtu mwenye furaha katika hafla hiyo, baada ya kutangazwa kuwa ameteuliwa kuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uganda. Wengine waliotangazwa kuwa Naibu Mabalozi ni Bi. Rosemary Jairo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora ambaye anakuwa Naibu Balozi nchini Afrika Kusini na Bw. Andy Mwandembwa, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Itifaki ambaye anakuwa Naibu Balozi nchini Sweden.
Wakati wa maakuli. Mhe. Waziri akiwa ameshikilia sahani ya chakula na anyemfuatia ni Katibu Mkuu anayeonekana akichota chakula
Naibu Katibu Mkuu naye anajichotea chakula
Waheshimiwa Mabalozi nao wanajichotea chakula
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Idara/Vitengo
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara/Vitengo.
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Wasaidizi wa Waziri na Naibu Waziri.
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu.
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi Wanawake.