PROFESA MARK MWANDOSYA ATOA YA MOYONI KUHUSU MAREHEMU DR. ABDALLAH OMARI KIGODA

October 14, 2015

Na Profesa Mark Mwandosya
Imenichukua muda wa zaidi ya saa ishirini kuandika machache kuhusu Dr. Abdallah Omari Kigoda, aliyetutoka akiwa Hospitali ya Apollo, New Delhi, India baada ya kuugua kwa muda mfupi.  
Katika kipindi hicho nimekuwa nikitafakari maneno gani yanaweza kumwelezea Dr. Abdallah Omari Kigoda, maneno ambayo yanaweza kumtendea haki, kuonyesha masikitiko yangu na familia yangu, na kutoa pole kwa familia yake, mkewe, watoto na ukoo wote wa Kigoda, wakiwa Handeni na popote pengine.  
Sijaweza kuyapata maneno hayo.
Kwani yangekuwa maneno mengi, na yenye kubeba ujumbe mzito.  Nakiri sina umahiri wa lugha hasa katika kipindi cha majonzi.  Neno kubwa na zito la kiswahili ni POLE kwa wote, labda kuongezea uzito ni kusema POLE SANA.  Pole hizi pia ni kwa wana Handeni aliowatumikia kwa muda mrefu wa maisha ya kazi; Mkoa wa Tanga, na wana Tanga, mliompa heshima ya uongozi wa kisiasa na maendeleo ya jamii; jamii (fraternity) ya uchumi na wachumi; na Watanzania kwa ujumla wetu.

MAMA SALMA KIKWETE KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI LINDI MJINI, NACHINGWEA NA LIWALE

October 14, 2015

  Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,CCM, Mama Salma Kikwete akimnadi mgombea Urais kupitia CCM, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mpilipili huko Lindi Mjini tarehe 12.10.2015.
 Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete mara baada ya kumwombea kura kwa wananchi wa Manispaa ya Lindi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili tarehe 12.10.2015. Aliyesimama kulia ni Mgombea Ubunge katika Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Mama Salma Kikwete akiwa katika kijiji cha Ngunichile kilichoko katika Wilaya ya Nachingwea kwa ajili ya kuwanadi wagombea wa Chama Cha Mapinduzi kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe nchini tarehe 25.10.2015.  Katika mikutano hiyo Mama Salma alimnadi Dkt. John Magufuli kwenye urais na Ndugu Hassan Elias Masala kwenye Ubunge wa Jimbo la Nachingwea na Madiwani wote katika wilaya hiyo tarehe 13.10.2015.

Na Anna Nkinda – Maelezo, Liwale
Wananchi wa mkoa wa Lindi wameaswa kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujiletea mabadiliko ya kweli katika maisha yao kwani kuna baadhi ya watu hawapendi kufanya kazi huku wakisubiri mabadiliko.

Rai hiyo imetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwa nyakati tofauti na wananchi wa  vijiji vya Ngunichile na Mbaya vilivyopo katika majimbo ya Nachingwea na Liwale waliohudhuria mkutano wa kampeni ya kuwanadi wagombea wa nafasi za udiwani, ubunge na urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mama Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini alisema mabadiliko ya kweli hayawezi kupatikana bila ya kufanya kazi kwani kuna baadhi ya watu hasa vijana hawafanyi kazi wakiamka asubuhi kitu wanachokifanya ni kucheza  pool huku wakisubiri mabadiliko.

“Hata katika vitabu vya dini imeandikwa asiyefanya kazi na asile kwani kazi ni msingi wa maendeleo,  hata ukipiga kelele kiasi gani kama hufanyi kazi huwezi kupata mabadiliko katika maisha yako”.

“Ndugu zangu Mwenyezi Mungu ametupa akili ya kutambua mema na mabaya tusikubali kudanganywa, mabadiliko ya siku hizi siyo mazuri yanaleta uvunjifu wa Amani kwani watu wamepandikizwa maneno ya chuki wanafanya vurumai na kuharibu vya kwao, wanawachukia ndugu zao imefikia hatua watu hawazikani, hawasalimiani. Lakini hao aliowapandikiza chuki kwao kuna maendeleo”, alisisitiza.

Mama Kikwete alisema yeye kama MNEC anadhamana  kubwa ya  kuhakikisha anakisemea na kukipigania chama chake na kuwataka wananchi hao kushikamana na kuwa kitu kimoja kwa kufanya hivyo wataitunza Amani ya nchi na kuzidi kudumisha upendo katika jamii yao.

Aidha aliwasihi wananchi hao kutokubali kurubuniwa na kitu chochote bali wazitunze kadi zao za kupigia kura na siku ya uchaguzi ikifika wasipoteze haki yao ya msingi ya kupiga kura wajitokeze kwa wingi na kuwachagua viongozi kutoka CCM ambao watawaletea maendeleo ya kweli.

Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la Nachingwea  Hassan Massala aliahidi kama atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo atasimamia ilani ya uchaguzi ya CCM na kuhakikisha huduma za elimu zinaboreshwa hii ni pamoja na  shule kuwa na  vitabu na walimu wa kutosha na kujenga nyumba za walimu ili watoto wapate elimu bora. Ataboresha  huduma za afya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na Zahanati na dawa zinapatikana kwa wakati.

Massala alisema, “Katika jimbo hili, maeneo ya mjini kuna maji ya kutosha lakini kijiji cha Ngunichile kuna tatizo ingawa vyanzo vya maji vipo. Nitahakikisha maji yanapatikana. Kuhusu umeme  Serikali inampango wa kusambaza katika vijiji vyote,  nguzo zimeanza kusambazwa kinachohitajika ni kusimamia ili zoezi hili liende haraka”.

Mgombea huyo wa nafasi ya Ubunge alimuomba Mama Kikwete awasaidie ili mnara wa mawasiliano ya simu uweze kujengwa  katika kata ya  Ngunichile kwani eneo hilo linashida ya mawasiliano.

“Ukiwa katika kijiji hiki  huwezi kuwasiliana na mtu yeyote kwa njia ya simu kwa kuwa hakuna mnara wa mawasiliano.  Hivi sasa simu ni pesa na simu ni Benki tunaomba Mama yetu utusaidie ili mnara wa mawasiliano ujengwe katika kijiji hiki”, Massala aliomba.

Kuhusu ombi la kujengewa mnara wa mawasiliano ya simu katika kijiji hicho ambacho ni kata ya Ngunichile Mama Kikwete aliahidi kulifanyia kazi na kulifikisha kunakohusika.

Naye mgombea ubunge wa jimbo la Liwale Faith Mitambo aliwaomba wananchi wamchague ili aendelee kuwatumikia kwa kipindi kingine cha miaka mitano na kuhakikisha maendeleo yanazidi kupatikana katika jimbo hilo.

Mitambo alisema, “Ilani ya uchaguzi ya CCM inasema itaendelea kuboresha huduma ya afya na ndani ya mwaka mmoja baada ya uchaguzi Zahanati ya kijiji cha Mbaya itakuwa kituo cha Afya. Aidha Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni  tatu kwa ajili ya kuhakikisha umeme unapatikana vijijini kati ya vijiji hivyo kimojawapo ni kijiji hiki.

“Nawaomba kura zenu ili mtuchague viongozi kutoka CCM ambao ni madiwani, mbunge na rais ili tuweze kusimamia na kutekeleza kwa vitendo na kuhakikisha yale yote yaliyoandikwa katika ilani ya uchaguzi yanatekelezwa”,.
DUNIA YAHIMIZWA KUWAJIBIKA KWA AJILI YA AMANI

DUNIA YAHIMIZWA KUWAJIBIKA KWA AJILI YA AMANI

October 14, 2015
IMG_5771
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kushiriki katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. ( Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
JUMUIYA ya Kimataifa imetakiwa kuwajibika kuhakikisha kwamba wanaweza kuwepo na amani na usalama kwa kuwa hilo ndilo tatizo kubwa duniani.
Hayo alisema Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard membe katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Hafla hiyo imefanyika viwanja vya Mnazi Mmoja mapema zaidi kuliko tarehe iliyopaswa ya Oktoba 24 kutokana na Tanzania kuwa katika mchakato wa uchaguzi.
Waziri Membe alisema kwamba dunia kwa sasa ipo katika changamoto kubwa ya usalama kutokana na mizozo inayoendelea katika nchi kadhaa duniani.
Alisema kumekuwepo na wimbi kubwa la mapigano ndani ya nchi mbalimbali katika nchi mashariki ya kati, Ulaya na hata Afrika, kukua kwa ugaidi na siasa za kibaguzi.
“ Sote tunafahamu shida iliyopo katika nchi kama Syria, Iraq, Somalia, Libya, Afghanistan, Yemen na jamhuri ya Afrika Kati” alisema waziri Membe na kuongeza kuwa matukio ya vita ya mara kwa mara, misimamo mikali na ugaidi vimekuwa vikisababisha vifo vingi na mateso kwa jamii.
Kutokana na hali ilivyo kwa sasa dunia haiko katika hali ya amani na hivyo juhudi zaidi zinatakiwa kufanyika ili kurejesha amani ambayo ni kiungo muhimu katika maendeleo.
Pamoja na kuzungumzia haja ya amani kutokana na dunia sasa hivi kufikia kiwango cha juu cha wakimbizi ndani na nje ya nchi zao, Waziri Membe alihimiza mabadiliko katika uendeshaji wa Umoja huo ili kuleta uwiano wa uwajibikaji kimataifa.
IMG_5783
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akisalimiana na baadhi ya wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini huku akiwa ameambatana na pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Liberata Mulamula (kushoto).
Mwaka 2005 idadi ya wakimbizi duniani ilikuwa milioni 38 lakini miaka kumi baadae takwimu zinaonesha kwamba kuna wakimbizi milioni 60 ikimaananisha kwamba katika kila watu 122 duniani, mmoja ni mkimbizi.Tanzania ina wakimbizi 169, 874.
Aidha alisema kwamba bara la Afrika linastahili kuwa na kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama ili maamuzi kuhusu Afrika yawe na mamlaka ya Afrika yenyewe.
Katika hotuba yake pia alizungumzia mafanikio ya Umoja wa Mataifa ikiwamo utengenezaji wa malengo mapya 17 ya maendeleo endelevu na pia ufanisi katika utekelezaji wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yakifanyakazi kama kitu kimoja.
Alisifu mafanikio makubwa yaliyotokana na uongozi wa Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez tangu alipofika nchini miezi 13 iliyopita.
Alisema utendaji wake unaozingatia ngazi za chini hadi juu na vijijini hadi mjini umeleta mafanikio makubwa kutokana na kuwa sehemu kamili ya utekelezaji wa mambo mbalimbali ya maendeleo na kupiga vita umaskini.
Pia alishukuru mchango wa Umoja wa Mataifa katika kufanikisha elimu ya uchaguzi hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi ambao utafanyika siku 12 zijazo.
Umoja wa Mataifa na wadau wake wametoa jumla ya dola za Marekani milioni 22.5 kwa ajili ya shughuli za uchaguzi mkuu nchini na kuimarisha demokrasia na utawala bora.
Naye Rais mstaafu Benjamin Mkapa akizungumza katika hafla hiyo alitaka dunia kutambua kwamba madhumuni ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa bado yapo palepale na kutaka nchi wanachama kutoa michango yao kuendelea kupambana na changamoto mpya za dunia katika masuala anuia ikiwamo vita, umaskini, chakula na mabadiliko ya tabia nchini.
IMG_5777
Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akisalimiana na Waziri Membe mara tu baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
Mataifa 51 yalikutana mjini San Francisco, Marekani baada ya vita kuu ya pili ya dunia na kuanzisha Umoja wa Mataifa. Wakati wa uanzishaji wa Umoja huo mataifa manne tu ya Afrika yalikuwepo nayo ni Liberia, Ethiopia, Misri na Afrika Kusini.
Hata hivyo rais huyo mstaafu alisema ili Umoja wa Mataifa ufanikiwe ipo haja ya kubadili mifumo yake ili iweze kuwajibika kikamilifu kwa dunia na wala si kwa matakwa ya waasisi na matajiri.
Pamoja na mabadiliko hayo nchi nyingi zinazoendelea zinataka kuwa na haki ya upigaji kura katika vyombo kadha vya Umoja wa Mataifa ikiwamo shirika la Fedha na Benki ya Dunia.
Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika hafla hiyo katika viwanja vya Mnazi Mmoja alisema kwamba Umoja huo utaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuwezesha amani na maendeleo.
Pamoja na kushukuru kwa wananchi wa Tanzania kuwa pamoja na Umoja wa Mataifa katika sherehe hizo muhimu sana Dunia nzima, alisisitiza, ushirikiano kuendelea kuwapo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wadau wa maendeleo, na mashirika ya Umoja wa Mataifa.
“Kwa kuadhimisha siku hii ya Umoja wa Mataifa kwa pamoja, tunaimarisha ushirikiano wetu, katika masuala ya msingi, ambayo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, wamekubaliana nayo. “ alisema.
Aidha alizungumzia mapatano ya mashirika ya Umoja wa Mataifa na Tanzania na utekelezaji wa mipango ya maendeleo inayoichangiwa na UN nchini Tanzania chini ya UNDAP na kusema imeleta mafanikio makubwa.
Katika wiki ya Umoja wa Mataifa, wafanyakazi na viongozi wa serikali, wadau wa maendeleo na wananchi waliwafanya shughuli mbalimbali zikiwamo za upandaji miti, usafi na miradi ya nishati mbadala.
IMG_5788
Gwaride maalum katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa likitoa heshima kwa mgeni rasmi Waziri Membe (hayupo pichani).
IMG_5795
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
IMG_5805
Waziri Membe akitoa heshima kwa bendera ya Umoja wa Mataifa ikipandishwa kama ishara ya kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_5821
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum akisoma dua kubariki sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_5826
Kiongozi wa madhehebu ya Kikristo akiongoza sala katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_5842
Meza kuu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa pamoja na mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe wakishiriki sala maalum ya kuombea amani ya nchi na Umoja wa Mataifa.
IMG_7499
Baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakitoa heshima kwa wimbo wa taifa.
IMG_6282
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akitoa hotuba katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_6487
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_6501
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe (kulia) akimpongeza Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa kwa hotuba nzuri aliyoitoa.
IMG_6518
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akizungumza machache kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa kabla ya kumkabidhi tuzo maalum Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe (wa pili kushoto) iliyoshuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Liberata Mulamula na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto).
IMG_7769
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe tuzo ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa kwa kuzingatia mchango wake katika Maendeleo ya Milenia (MDGs) na Maendeleo Endelevu (SDGs) katika maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja huo jana katika viwanja vya Mnazi mmoja.
IMG_7774
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (katikati) akimpongeza Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe mara ya kukabidhiwa na Umoja wa Mataifa kwa kutambua mchango wake katika Maendeleo ya Milenia (MDGs) na Maendeleo Endelevu (SDGs) katika maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja huo jana katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar.
IMG_6303
Mshehereshaji katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ambaye pia Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Mindi Kasiga akifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
IMG_7565
Meza kuu.
IMG_7573
Mabalozi, Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Wadau wa Maendeleo pamoja Viongozi wa Serikali wakiwa jukwaa kuu.
IMG_6385
Wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mmoja wa viongozi wa madhehebu ya dini wakifuatilia jambo kwa umakini katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_6334
Pichani juu na chini ni sehemu ya wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja Mataifa walioshiriki katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_5876
IMG_6351
IMG_6341
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulida Hassan na Eliet Magogo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
IMG_7610
IMG_5907
IMG_7624
IMG_6264
IMG_6331
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakibadilishana mawazo wakati wa sherehe hizo.
IMG_7557
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali nao walishiriki.
IMG_7529
Maafisa wa jeshi nao walishiriki.
IMG_7810
Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini.
IMG_7865
Meza kuu katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini pamoja na wadau wa maendeleo.
IMG_7821
Meza kuu katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali walioshiriki kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_7855
Meza kuu katika picha ya pamoja na wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
IMG_7884
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.
IMG_7906
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
IMG_8011
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wanafunzi walioshika mabango ya malengo endelevu.
IMG_7918
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa wakiondoka kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
IMG_7947
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akiteta jambo na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum wakati akiondoka kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.
KAWAIDA -- Zainul A. Mzige, Operation Manager, MO BLOG, www.modewjiblog.com +255714940992.