HIS HIGHNESS THE AGA KHAN MEETS WITH TANZANIA VICE PRESIDENT AT STATE HOUSE
The two leaders in a briefly close discussions before their meeting at State House in Dar es Salaam, Monday August 4, 2014 |
Your welcome sir: His Highness the Aga Khan, (L), is being welcomed by his host, The Vice President, Dr. Bilal |
His Highness The Aga Khan, and his host, Vice President, Dr. Mohammed Gharib Bila, leave the State House after their meeting |
Welcome to the State House |
SITTA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI, BUNGE LA KATIBA KUANZA JUMANNE
RAGE APATA AJALI AKIWA NJIANI KUELEKEA DODOMA
Mbunge wa Sikonge mkoani Tabora kupitia CCM, ambaye pia ni Mujumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Said Nkumba, akimjulia hali Rage, hospitalini mjini Dodoma, Jumatatu Agosti 4, 2014 |
RAIS KIKWETE ALIPOKUTANA NA WANAJUMUIYA YA WATANZANIA WA DMV KATIKA MKUTANO WA DIASPORA JIJINI WASHINGTON
Viongozi
wa Jumuiya ya Watanzania DMV wakati wakimsubiri Rais Jakaya Mrisho
Kikwete Jumapili Julai 3, 2014 katika hoteli ya Marriot jijini
Washington DC
Viongozi
wa Jumuiya ya Watanzania DMV wakati wakimsubiri Rais Jakaya Mrisho
Kikwete Jumapili Julai 3, 2014 katika hoteli ya Marriot jijini
Washington DC
Viongozi
na wanachama wa Jumuiya ya Watanzania DMV wakati wakimsubiri Rais
Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili Julai 3, 2014 katika hoteli ya Marriot
jijini Washington DC
Wajumbe wa Bodi ya Jumuiya ya Watanzania DMV
Rais Kikwete akimsalimia mmoja wa watoto waliokuwepo kumlaki
Miss Tanzania 2012, JAT kusomesha albino 50
Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred
akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa kutoa elimu kwa wajasiliamali kwa
albino 50, kushoto ni Kaimu katibu Mkuu wa Jumuiya wa watu wenye ulemavu wa
ngozi (albino), Mohamed Chanzi.
Kaimu katibu Mkuu wa Jumuiya wa watu wenye
ulemavu wa ngozi (albino), Mohamed Chanzi (Kushoto) akisisitiza jambo katika
uzinduzi wa mpango huo. Wengine katika picha ni Brigitte Alfred (katikati) na
Maria Ngowi ambaye ni mkurugenzi wa JAT
Viongozi wa Taasisi ya Brigitte Alfred
Foundation, TAS na JAT katika picha ya pamoja mara baada ya kuzinduzi mpango wa
kusomesha albino 50 masomo ya Ujasiriamali.
***********
Na Mwandishi wetu
Taasisi ya ya Miss Tanzania 2012, Brigitte
Alfred ijulikanayo kwa jina na Brigitte Alfred Foundation (BAF) ikishirikiana
na taasisi ya Junior Achievement Tanzania (JAT) inazindua rasmi mafunzo ya
ujasiriamali kwa jamii ya Albino.
Akizungumza katika uzinduzi huo jana,
Brigitte alisema kuwa taasisi yake kwa kushirikiana na JAT itaanza na mafunzo
kwa albino 50.
Brigitte alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga
sehemu kuu mbalimbali ambazo ni kujitambua (Life skills), kutathmini aina
mbalimbali za biashara (Business Analysis), namna ya kutunza pesa ( How to
save), kuandika mchanganuo wa biashara (Business Plan), kutembelea sehemu
mbalimbali zinazoendana na biashara atakayoifanya na jinsi ya kuanza biashara.
Alisema kuwa BAF ikishirikiana na wadau
mbalimbali na pia itagharimia gharama za mafunzo na mahitaji mbalimbali ya
kuboresha hali yao.
“Mafunzo haya yatachukua muda wa mwaka mmoja
yaani watashiriki na yataanza rasmi Agosti 18, kila mshiriki wa mafunzo haya
atapatiwa kitabu chenye masomo yote ili aweze kuendelea kujisomea,” alisema
Brigitte.
Mkurugenzi wa JAT, Maria Ngowi alisema kuwa
wamejipanga kufanikisha mpango huo na wanaamini albino watakaopata mafunzo hayo
watafanikiwa katika maisha yao ya kila siku.
Ngowi alisema kuwa JAT imejikita katika
Nyanja tatu ambazo ni ujasiria mali, elimu ya kuzalisha, kuiwekeza na kutunza
fedha na elimu ya kazi.
Alisema kuwa taasisi yao ni sehemu ya taasisi
kubwa ulimwenguni inayoitwa Junior Achievement International ambayo iko katika
nchi 120 duniani huku afrika ikiwa katika nchi 17.
Kaimu Katibu Mkuu wa Tanzania Albino Society
(TAS), Mohamed Chanzi alimshukuru Brigitte na JAT kwa kuwajali na kuomba wadau
mbali mbali kuwaunga mkono.
“Wamelenga kutusaidia kimaisha, kwani msaada
wa elimu ni mkubwa kulinganisha misaada mingine, naomba wadau wawaunge mkono,”
alisema Chanzi.
MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA WANAWAKE WATANZANIA WAJASIRIAMALI WA DMV JIJINI WASHINGTON
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea shada la maua kutoka kwa Ndugu
Juster Mutakyawa mara baada ya kuwasili kwenye ofisi ya ubalozi wa
Tanzania nchini Marekani iliyoko Washington tarehe 3.8.2014.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama
Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake
wajasiriamali cha Watanzania wanaoishi Washington kiitwacho TANO Ladies
Ndugu Asha Hariz wakati alipotembelea ofisi ya ubalozi wa Tanzania
nchini Marekani tarehe 3.8.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kipeperushi kutoka kwa Rais na
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Help for Underserved Communities (HUC) ya
nchini Marekani Ndugu Zawadi Sakapalla baada ya kupata taarifa ya huduma
mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo. Kampuni hiyo husaidia familia
maskini kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwa kuwachimbia
visima pamoja na kutoa vifaa vya elimu kwa wanafunzi.
Baada
ya kutembelea maonesho ya wanawake wajasiriamali Mama Salma Kikwete
akifuatana na Afisa Tawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama
Lily Munanka kwenda kuweka saini kwenye kitabu cha wageni.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kwenye kitabu cha wageni.
Aliyesimama kushoto ni Bibi Lily Munanka, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania
nchini Marekani.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitambulishwa kwa wana kikundi wa TANO
Ladies. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti Asha Hariz, akifuatiwa na Asha
Nyang’anyi, Isca Kauga, Juster Mutakyawa na Tumaini Kaisi aliyeshika
kipaza sauti.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kikundi cha TANO
Ladies cha nchini Marekani. Anayekabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya
wanakikundi wenzake Ndugu Juster Mutakyawa.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akina mama wa kitanzania
wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani kwenye ukumbi wa ofisi ya
ubalozi wetu mjini Washington tarehe 3.8.2014.
Baadhi
ya wanawake wajasiriamali na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akina mama wa kitanzania wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na baadhi ya wanawake mwishoni mwa
mazungumzo yake na wanawake hao yaliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya
ubalozi wa Tanzania nchini Marekani huko Washington tarehe 3.8.2014.
Mke wa Rais akipiga picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula.
Balozi
wa Tanzania nchni Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula akimuaga Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kutembelea ofisi za ubalozi huo
na kuongea na wanawake wa Tanzania wanaoishi nchini Marekani. PICHA NA
JOHN LUKUWI.
OMARI NUNDU,AMINA MWIDAU WAHUDHURIA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA KUJADILI MASUALA YA MAENDELEO LEO
MEYA WA JIJI LA TANGA,OMARI GULEDI KUSHOTO NA KULIA NI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA JULIANA MALANGE |
MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA TANGA,OMARI GULEDI AKIPITIA MAKBRASHA MBALIMBALI. |
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA,JULIANA MALANGE. |
MBUNGE WA JIMBO LA TANGA OMARI GULEDI AKIPITIA MAKABRASHA ,MBALIMBALI YA VIKAO |
WAJUMBE WAKIFUATILIA MIJADALA MBALIMBALI LEO |
DIWANI WA KATA YA MSAMBWENI KUPITIA CUF ABDURHAMANI AKITOA HOJA YAKE LEO |
Subscribe to:
Posts (Atom)