TUKISHIRIKIANA TUTAOKOA MAISHA YA AKINA MAMA WENGI NA WATOTO

March 10, 2015

Balozi Tuvako Manongi Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa akizungumza wakati wa uzinduzi wa onyesho la picha lililoandaliwa kwa ubia baina ya Wakilishi za Kudumu za Italia na Tanzania. Onyesho hilo linahusu huduma za afya ya mama na mtoto zinazotolewa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Doctors with Africa CUAMM katika hospitali ya Tosamaganga, Mkoani Iringa. Kushoto kwa Balozi Manongi ni Balozi wa Italia katika Umoja wa Mataifa, Bw. Sebastioano Cardi na kulina ni mmoja wa Wabunge kutoka Italia anayehudhuria mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu Hadhi ya Wanawake.
Balozi Manongi akiteta jambo na Dkt. Andrea Atzori ambaye katika maelezo yake amesema taasisi hiyo ya Doctors with Africa CUAMM inampango wa kupanua huduma zake katika maeneo mengine ya pembezoni mwa Tanzania, mbali ya Tosamaganga na Mikumi.
Dkt. Andrea Atzori akiwa na Bi. Tully Mwaipopo, Afisa wa Uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa mara baada ya uzinduzi wa onyesho hilo. 
baadhi ya picha zinazoonesha huduma ya utoaji wa afya ya mama na mtoto katika Hospitali ya Tosamaganga , huduma hiyo ainayoendana manafumzo kwa wataalamu wa afya imeweza kuokoa maisha ya wanawake wajawazito pamoja na watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya muda.

Na  Mwandishi Maalum, New York

Tanzania  imeelezea kuridhishwa kwake na ushirikiano  uliopo baina ya  Serikali na  Taasisi Binafsi   katika  uboreshaji na utoaji wa huduma  za afya  zikiwamo zinazomlenga mama na mtoto. Na hivyo kuchangia katika upiguzaji wa vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga.

Kauli hiyo imetolewa  siku ya  jumatatu na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako  Manongi, wakati wa   uzinduzi wa onyesho  kwa njia ya picha kuhusu huduma  za afya zinazotolewa na   Taasisi isiyo ya kiserikali  ya  Doctors with Africa CUAMM inayofanya shughuli za   utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto katika Hospitali  ya Tosamaganga,  Mkoani  Iringa.

Picha hizo zinaonyeshwa katika  corridor za  Umoja wa Mataifa, sambamba na  mkutano wa 59 wa Kamisheni ya Hadhi ya Wanawake ( CSW) unaofanyika hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa,  mkutano unaojadili masuala mbalimbali yanayomhusu mwanamke na mtoto wa kike, kuanzia elimu, fursa na haki sawa,  huduma bora za afya,  uwezeshwaji , haki za mwanamke na mtoto wa kike pamoja na changamoto zinazo wakabili.

Balozi Manongi amesema  ni kwa kushirikiana ndipo  nchi kama  Tanzania  inaweza  kuongeza kasi ya kuwafikishia huduma za afya wananchi wengi, na kuwa  uwepo wa Taasisi kama  ya  Doctors with Africa CUAMM na  mchango wake katika utoaji wa huduma za afya huko  Tosamaganga na maeneo mengine ni kielelezo  sahihi cha ushirikiano anaouzungumzia.

Akasema    mchango wa  Taasisi hiyo ni mfano wa kuigwa na  ndiyo maana Tanzania katika   maandalizi ya  malengo mapya  ya  maendeleo baada ya 2015 moja ya maeneo inayoyapigia chapuo ni pamoja na hilo la afya ya mama na mtoto pamoja na ushirikiano  miongoni mwa wadau mbalimbali.

“ Nyinyi ni kielelezo sahihi cha ubia na ushirikiano  tunaouhimiza. Asanteni sana kwa mchango wenu na asanteni  kwa kudhirisha kwamba inawezekana kufanya kazi kwa ushirikiano”. akasema Balozi.

Kwa upande wake  Mwakilishi wa Taasisi hiyo,  Bw. Andrea Atzori,  amesema Taasisi yake  ambayo  imekuwa nchini Tanzania  tangu mwaka 1968 imejielekeza   Zaidi katika utoaji wa huduma za afya katika maeneo ya  vijijini  hususani kwa akina  mama wajawazito na watoto  wachanga wakiwamo wanaozaliwa kabla ya muda.

 Huduma nyingine   zinatolewa na taasisi hiyo  ni pamoja na mafunzo kwa wataalamu wa afya,  huduma za uzazi salama kupitia mpango wao wa miaka mitano   walioupa  jina la “mama na mtoto kwanza”.

Aidha kwa mujibu wa Dkt. Andrea Atzori,  Taasisi hiyo inatarajiwa kupanua huduma zake katika maeneo mengine Zaidi  ya pembezoni kwa lengo la kuhakikisha kwamba wananchi wengi wanapata huduma ya afya pale walipo.

Pamoja na  Tanzania,   Doctors with Africa CUAMM  iliyoanzishwa mwaka 1950 na makao yake yakiwa nchini Italia,pia inaendesha shughuli zake katika nchi za  Angola,  Ethiopia, Msumbiji,  Sudani ya Kusini, Uganda na  Sierra leone.

MWANAFUNZI WA SEKONDARI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMNYAMG'ANYA SILAHA ASKARI JIJINI TANGA.

March 10, 2015


























https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVavAFXbwLnq1mVv4PwoCfR2pPJHbLsIYWOoycBcTSgzAq0qop8Nzj4JewyqogxZrTihhc6TrizXblQGnwNbj6CYJ4pWicGaV23jnxbZ9pTARHVKCFdIhkdOPcsHMTKVy0VWr2cdf8Xdk/s1600/Tanga,_Tanzania,_town_centre-1.JPGSehemu ya mji wa Tanga.

WAKAZI 10 wa jijini hapa, akiwemo mwanafunzi wa sekondari wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wakikabiliwa na makosa matano tofauti kuhusu tukio la kuwanyang’anya polisi silaha pamoja na kumuua askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Sajenti Mohamed Rashid Kajembe.
Mwanafunzi aliyefikishwa mahakamani ni Rajab Bakari (19) wa shule ya sekondari na mkazi wa Makorora jijini hapa. 

Watuhumiwa tisa wameelezwa kuwa ni wafanyabiashara, nao ni Mbega Seif (25) maarufu ‘Abuu Rajab’ mkazi wa Kiomoni, Amboni, Ayubu Ramadhani (27) maarufu ‘Chiti’ ambaye ni fundi umeme na mkazi wa Kona Z Kiomoni, Hassani Mbogo (20) maarufu ‘Mpalestina’ mkazi wa Makorora, Mohamed Ramadhani (19) mfanyabiashara na mkazi wa Makorora, Sadiki Mdoe (25) maarufu ‘Kizota au Kisaka’ mkazi Magaoni.

Washtakiwa wengine ni Saidi Omari (26) mkazi wa Magaoni Tairi Tatu, Nurdin Mbogo (27) Makorora, Ramadhan Mohamed (18) mkazi wa Donge pamoja na Omari Harubu Abdala (55) maarufu ‘Ami’ mkazi wa Dunia Hoteli Makorora.

Wakisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Aziza Rutala, Wakili wa Serikali, George Barasa akisaidiana na MariaClara Mtengule, walidai kuwa kosa la kwanza hadi la tatu linawahusisha washitakiwa namba moja mpaka nane (1 -8) ambao wanatuhumiwa kushiriki kula njama ya kutenda kosa kinyume cha sheria.

Barasa alidai kuwa katika maeneo tofauti ya jijini Tanga kati ya Septemba mosi 2014 hadi Januari 26 mwaka huu, washitakiwa wote wanane kwa pamoja walitenda kosa la kula njama na kufanya kosa la unyang’anyi wa silaha.

Katika kosa la pili, Barasa alidai mahakamani hapo kwamba mnamo Januari 26 mwaka huu, katika mgahawa wa Jamali ulipo kati ya barabara ya Nne na ya Tano jijini Tanga, washitakiwa wote wanane waliiba silaha moja aina ya SMG namba za usajili 14303545 mali ya Polisi na muda mfupi kabla ya kutenda kosa hilo walitumia visu kumchoma askari H 501 Mwalimu ili kupata silaha hiyo.

Kosa la tatu la washitakiwa hao ni unyang’anyi wa kutumia silaha, na washitakiwa wote wanane wanadaiwa kuwa katika mgahawa wa Jamali uliopo kati ya barabara ya nne na ya tano waliiba silaha nyingine yenye namba za usajili 14301230 SMG mali ya polisi na kwamba muda mfupi kabla ya kutenda kosa hilo walimtishia kwa kutumia nguvu kumnyang’anya silaha PC H Mansoor kinyume na sheria.

Hata hivyo, katika kosa la nne ambalo limemhusisha mshitakiwa namba tisa Nurdin Mbogo wakili huyo wa Serikali, alidai kuwa Februari 6 mwaka huu, katika sehemu isiyofahamika jijini Tanga, mshtakiwa huyo akijua kuwa Hassan Mbogo (Mshitakiwa Na. 4) alitenda kosa Septemba mosi 2014 na Januari 26 mwaka huu alimsaidia kumwezesha kukwepa kushtakiwa na kuadhibiwa kinyume na sheria.

Katika hatua nyingine, Wakili wa Serikali Mtengule alisoma shitaka jingine jipya ambalo liliwahusisha watuhumiwa watatu akiwemo namba 1 na 2 (Mbega Rajabu na Rajabu Bakari) pamoja na mshtakiwa mwingine Omari Harub Abdallah ‘Ami’ wakidaiwa kwa pamoja kuhusika kumuua askari wa JWTZ, Sajenti Mohamed Rashid Kajembe mnamo Februari 13 mwaka huu katika Mapango ya Amboni Jijini Tanga kinyume cha sheria namba 196 na 197 ya makosa ya adhabu ya mwaka 2002 .

Washtakiwa hao watatu hawakutakiwa kujibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo ya mauaji.

Hata hivyo, washitakiwa wote 10 kwa pamoja wamekana makosa yao, na mahakama imewanyima dhamana washitakiwa tisa kutokana na makosa waliyotenda kutokuwa na dhamana.

Mshitakiwa namba tisa Nurdin Mbogo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana baada ya kutakiwa kutoa Sh milioni moja na mdhamini mmoja mwenye mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh milioni moja.

Washitakiwa wote wamerudishwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Machi 23 mwaka huu kwa kuwa upelelezi wake haujakamilika.

Mnamo Februari 13 mwaka huu katika eneo la Amboni Jijini Tanga palizuka mapigano baina ya askari polisi wakishirikiana na JWTZ dhidi ya watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi, waliokuwa wamejificha kwenye mapango ya Majimoto.

Katika tafrani hiyo, kulisababish kifo cha askari wa JWTZ na majeruhi watano wakiwemo wanajeshi wawili na Polisi watatu, hali iliyozua hamaki kwa wakazi wa jijini hapa.

Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake mwezi uliopita alielezea matukio hayo kuwa ni ya ujambazi, lakini pia yana mwelekeo wa ugaidi na akalitaka jeshi la polisi kuwasaka watuhumiwa wote na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Chanzo:Habari Leo.

LINNAH SANGA, MASOGANGE NA RAFIKA YAKO WAONYESHA UZURI WAO WAKIWA WAMEJIACHIA SWIMMNIG POOL

March 10, 2015
Rais Dk.Ali Mohamed Shein akabidhi Vihori

Rais Dk.Ali Mohamed Shein akabidhi Vihori

March 10, 2015

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mwakilishi wa VSO Tanzania Jean Van Wetter wakati alipowasili katika viwanja  vya Ukimbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo katika hafla ya sherehe ya kukabidhi Vihori kwa wakulima wa Mwani,[Picha na Ikulu.] dr2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto Bi Zainab  Omar Mohamed  (wa pili kushoto) na Katibu wa Wizara hiyo Bi Asha Ali Abdalla (kulia)wakati alipowasili katika viwanja  vya Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo katika hafla ya sherehe ya kukabidhi Vihori kwa wakulima wa Mwani,[Picha na Ikulu.] dr3 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia bidhaa mbali mbali zilizotengenezwa kwa kutumia zao la mwani na kikundi cha Ulezi ni Kazi cha shehia ya Fujoni Jimbo la Kitope) wakati wa sherehe za kukabidhi Vihori kwa wakulima wa mwani hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.] dr4 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Kihori Bw.Kombo Salim Hamadi mkulima wa mwani wa Tumbe Magharibi Kaskazini Pemba wakati wa sherehe za kukabidhi vihori kwa wakulima wa mwani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] dr5 
Baadhi ya Viongozi,Wananchi na wakulima wa mwani wakiwa katika sherehe za kukabidhi vihori kwa wakulima wa mwani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ,[Picha na Ikulu.] dr6 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa wananchi wakati sherehe za kukabidhi Vihori kwa wakulima wa mwani katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]
dr7 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Kihori Bi.Zainab Daudi Haji mkulima wa mwani wa Uroa Wilya ya Kati Mkoa wa Kusini  wakati wa sherehe za kukabidhi vihori kwa wakulima wa mwani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AFANYA ZIARA MTERA KWA LUSINDE A.K.A (MTALIMBO)

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AFANYA ZIARA MTERA KWA LUSINDE A.K.A (MTALIMBO)

March 10, 2015

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Manzase kata ya Fufu  jimbo la Mtera wilayani Chamwino, Katika mkutano huo Kinana amewaahidi wananchi hao kushughulikia matatizo ya maji, Umeme , Huduma za Afya na Mawasiliano kwa kushirikiana na Mbunge wa jimbo hilo Mh. Livingstone Lusinde na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Chiku Galawa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Manzase na kuwaambia CCM Ipo Imara inajenga nchi na kuwataadharisha vijana wasikimbilie vyama visivyo na sera za maendeleo. 3 
Mbunge wa Jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde akihutubia wakazi wa Manzase ambapo aliwaambia kuwa watendaji wa Serikali wajitahidi kufuata maagizo na maelekezo ya Mheshimiwa Rais Kikwete kwa wakati. 4 
Mkuu wa wilaya ya Chamwino Bi. Farida Mgomi akiwasalimia wananchi. 7 
Umati wa wananchi wakisubiri mkutano huo kuanza  8 
Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde akizungumza, huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza wakati alipotembelea  Kijiji cha Suli, kata ya Mvumi Makulu ambapo alijionea ujenzi wa shule ya Msingi Suli unavyoendelea ikiwa ni msaada wa Shirika la Maendelea la Korea (KOICA) wanaofurahia hotuba ya mbunge huyo kutoka kulia ni Mh. Chiku Galawa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM. 10 
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano huo wa ndani ambao umefanyika eneo la shule ya sekondari ya Mvumi Mission. 13 
Mbunge wa Jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde akihutubia wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Mtera. 14 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi kabla ya kuzindua kisima cha maji ambapo aliwaambia wananchi hao watunze  sana miundo mbinu ya maji ili iendelee kudumu na kuwasaidia. 18 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama huku Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde akishiriki  kupampu maji ya kisima cha mkono kilichopo katika shule ya msingi Mvumi Mission mara baada ya kukagua na kuuzindua mradi huo wa maji. 20 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde wakifurahia jambo mara baada ya kuvishwa Migorole kama heshima ya wazee wa kijiji cha Manzase kwa kutambua mchango wao kwa taifa na kijiji hicho kwa ujumla.
19

Tatizo la mgawo wa umeme Arusha kumalizika Juni

March 10, 2015

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Jimbo la Singida, Martha Mlata (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Dkt. Miganda Manyahi (kulia), jijini Arusha kabla ya kuanza kwa ziara kwenye miradi ya umeme. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini inafanya ziara katika miradi ya umeme iliyopo katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ili kujionea hatua ya utekelezwaji wake pamoja na kuzungumza na watendaji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Richard Ndassa (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Felix Ntibenda (kulia) mara baada ya Kamati hiyo kuwasili ofisini kwake kwa ajili ya kupokea taarifa ya mkoa kabla ya kuanza kwa ziara kwenye miradi ya umeme.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Felix Ntibenda ( wa nne kutoka kushoto waliosimama mbele), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Richard Ndassa ( wa tano kutoka kushoto waliosimama mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini mara baada ya kumalizika kwa kikao.
Meneja Mradi wa Kusambaza Umeme unaojulikana kwa jina la Electricity V unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mhandisi Florence Gwang’ombe (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Richard Ndassa (kulia) mara baada ya kamati hiyo kuwasili kwenye eneo la mradi huo ili kujionea maendeleo ya utekelezwaji wake.
Mtaalam kutoka Kampuni ya Sweco International AB, Pal Aberg (kushoto) akiielezea Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Njiro kilichopo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikiendelea na ziara katika eneo la kituo cha kupooza na kusambaza umeme kilichopo Njiro nje kidogo ya jiji la Arusha.
Mtaalam kutoka Kampuni ya Sweco International AB, Pal Aberg (kulia) akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwenye eneo la kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Njiro kilichopo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Wataalam kutoka kampuni ya Sweco International AB, wakiendelea na ujenzi katika kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Njiro kilichopo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Mtaalam kutoka Kampuni ya Sweco International AB, Pal Aberg (kushoto) akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwenye chumba cha kuendesha mitambo ya umeme ( control room) ndani ya kituo cha kupooza na kusambaza umeme kilichopo Njiro nje kidogo ya jiji la Arusha.
Meneja Mradi katika Kituo cha Kupooza na Kusambaza Umeme cha KIA Mhandisi Emmanuel Manirabona (kulia) akiielezea Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo hicho kilichopo mkoani Kilimanjaro
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Richard Ndassa (wa kumi na moja kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Felchesmi Mramba (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini mara baada ya kukamilisha ziara yake katika kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha KIA kilichopo mkoani Kilimanjaro.
PINDA ATEMBELEA SOKO LA MIEMBENI DODOMA

PINDA ATEMBELEA SOKO LA MIEMBENI DODOMA

March 10, 2015

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua bei ya mahindi katika soko  la Miembeni mjini Dodoma Machi 8, 2015. Alipita sokoni hapo kukagua upatikanaji wa vyakula. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
pi2 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa maelezo kuhusu kilimo cha zabibu Walimu wa Shule za Kata ya Zuzu, Dodoma waliokwenda shambani kwake Machi 8, 2015 kwa ziara ya kujifunza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Rais Kikwete afungua Mkutano Mkuu wa Wahasibu Wakuu nchi za Mashariki na Kusini Mwa Afrika

Rais Kikwete afungua Mkutano Mkuu wa Wahasibu Wakuu nchi za Mashariki na Kusini Mwa Afrika

March 10, 2015

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Wahasibu Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika(ESSAG) uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Conference Centre JNICC jijini Dar es Salaam leo. Walioketi meza kuu kutoka kulia ni Waziri wa Fedha Mh.Saada Mkuya, Katibu Mkuu wizara ya Fedha Servacius Likwelile, manaibu katibu wakuu hazina Dkt.Hamisi Mwinyimvua na Bi.Dorothy Mwanyika. JK2 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Mwaka wa Wahasibu Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika(ESSAG) uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Conference Centre JNICC jijini Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro).,