Mkoa Wa Tanga Kuwa Mwenyeji Wa Maadhimisho Ya Siku Ya Utepe Mweupe Kitaifa Machi 15

March 02, 2015

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Magalula S. Magalula akizungumza  na Waandishi wa Habari  Leo Ofisini kwake 
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Ramadhani Kaswa  (Kushoto ) na baadhi ya Waandishi wakati wa mkutano
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakati wa mkutano

Taarifa zaidi

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga kwa niaba ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama Tanzania inapenda kuwatangazia Wananchi  kuwa Mkoa wa Tanga unatarajia kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya Siku ya Utepe Mweupe Kitaifa itakayofanyika Machi 15, Mwaka huu.

Siku ya Utepe Mweupe ni mwendelezo wa juhudi za Serikali katika kupunguza  na kutokomeza kabisa vifo vya akina mama na watoto wachanga.Maadhimisho haya ambayo hufanyika  Machi 15 kila mwaka yana lengo la kuwakumbuka na kuwaenzi wanawake waliopoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi.

Siku hii pia hutumika kujadili mikakati ya kuzuia vifo vingine visitokee. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “WAJIBIKA MAMA NA MTOTO MCHANGA AISHI”.  Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha uwajibikaji wa kila mmoja wetu kuanzia mama mjamzito nwenyewe na familia yake,  jamii na uongozi katika kuhakikisha kuwa hakuna mama wala mtoto mchanga anayepoteza maisha kutokana na sababau ambazo zingeweza kuzuilika.

Aidha, kutakuwepo na shughuli mbalimbali ambazo zitaambatana na maadhimisho haya katika wiki ya kuelekea siku yenyewe ambazo ni pamoja na uchangiaji damu salama, kushiriki katika zoezi la sauti ya jamii,kushiriki katika matembezi ya mshikamano na mkutano siku ya kilele.

 Asilimia 75 ya vifo vingi nchini vinatokana na kutoka damu kwa wingi, maambukizi, shinikizo la damu na utoaji mimba. Wanawake 24 wanafariki kila siku na wengine hupata ulemavu wa kudumu.

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kuweka mikakati madhubuti ili kupunguza vifo vya mama na mtoto. Kwanza imeelekeza nguvu zake katika kutoa elimu ya uzazi salama na pia imeelekeza Halmashauri zote Mkoani kuwa na kipengele mahususi cha bajeti kinacholenga kuhakikisha kuwa huduma za dharura za uzazi zinapatikana karibu na akina mama na watoto.

Kutokana na juhudi za serikali na wadau mbalimbali, matunda yameshaanza kuonekana miongoni mwetu. Kwa mfano katika Mkoa wa Tanga vifo vya mama na mtoto vimepungua kutoka idadi ya akina mama 101 kati ya wakina mama 45,256 waliojifungua kwa mwaka 2013 hadi kufikia idadi ya akinamama 69 kati ya wakina mama 47,692 waliojifungua kwa mwaka 2014 na idadi ya watoto 429 kati ya watoto 44,852 waliozaliwa  kwa mwaka 2013.   Serikali inaendelea na mapambano kuhakikisha afya ya mama na mtoto iko salama.

Kupunguza vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na matatizo wakati wa kujifungua ni  moja ya malengo 8 ya Milenia. Hili ni lengo namba tano ambalo linalenga kupunguza vifo vya akina mama vinavyoyokana na matatizo wakati wa kujifungua kwa asilimia sabini na tano (75%) ifikapo mwaka 2015.

Nawashukuru na kuwapongeza wenzetu wa Utepe Mweupe na wadau wengine kwa kujikita katika kampeni ya uhamasishaji ili kupunguza na kutokomeza vifo vya mama na mtoto.

Napenda kutoa wito kwa wananchi kuhakikisha kuwa kila mmoja anatekeleza wajibu wake ili kuokoa maisha ya mama na mtoto. Pia naviomba vyombo vya habari kuungana na makundi mengine katika jamii kuwa sauti ya akina mama ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Kwa pamoja tunaweza kuzuia vifo vya mama na watoto wachanga

“Wajibika Mama na Mtoto Mchanga Waishi”

Msanii Maarufu Rwanda Kiziti Mihigo Afungwa Miaka 10 Jela kwa Kupanga Njama njama za kupindua serikali na kuua viongozi wake

March 02, 2015

Muimbaji maarufu wa Rwanda Kizito Mihigo amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kushtakiwa kwa njama za kutaka kupindua serikali na kuua viongozi wake na kuonyesha chuki dhidi ya serikali.

Kizito Mihigo awali alisema alikuwa na makosa na kuomba msamaha, akimaanisha hukumu yake ipunguzwe.

Kizito Mihigo amekuhumiwa jela miaka 10 kwa njama za kutaka kupindua serikali na kua viongozi wake.

Mshtakiwa mwenzake, Cassien Ntamuhanga kiongozi wa kituo cha redio ya Kikristo, alifungwa miaka 25 kwa ugaidi na matusi. Ameendelea kukataa mashtaka yote. 

Mihigo alikubali kutumiana ujumbe na kundi la upinzani lenye maskani Afrika Kusini, Rwanda National Congress (RNC). Alifutiwa mashtaka ya ugaidi huku Ntamuhanga alifutiwa kosa la kupanga kumuua Rais Kagame.
chanzo: http://www.newtimes.co.rw
HOTUBA YA MWISHO WA MWEZI FEBRUARI, 2015, YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ILIYOTOLEWA TAREHE 1 MACHI, 2015

HOTUBA YA MWISHO WA MWEZI FEBRUARI, 2015, YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ILIYOTOLEWA TAREHE 1 MACHI, 2015

March 02, 2015
17
Utangulizi
Ndugu Wananchi;
Kama ilivyo ada tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuzungumza kupitia utaratibu wetu huu mzuri wa hotuba za kila mwisho wa mwezi. Kwa mwisho wa mwezi wa Februari nina mambo matano ninayopenda kuyazungumzia.
Zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura
Ndugu Wananchi;
Jambo la kwanza ni uandikishaji wa Wapiga Kura. Tarehe 24 Februari, 2015 Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda alizindua rasmi uandikishaji wa wapiga kura ikiwa ni sehemu ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura nchini. Zoezi hili lilizinduliwa Makambako, Mkoani Njombe na litaendelea nchini kote mpaka litakapokamilika kwa mujibu wa ratiba itakayopangwa na Tume ya Uchaguzi. Uandikishaji unatumia teknolojia ya kisasa ya utambuzi wa alama za vidole (BVR) na macho ya mtu anayeandikishwa. Teknolojia hii itatusaidia kuondoa kutoaminiana, manung’uniko na madai kuhusu udanganyifu katika chaguzi zetu kwamba wamepiga kura wasiostahili. Kuanza kutumika kwa teknolojia hii ni kielelezo cha utashi wa Serikali kuwa nchi yetu iwe na chaguzi zilizo huru, wazi na haki.
Ndugu Wananchi;
Mtakumbuka kuwa, kabla ya uzinduzi wa zoezi hili, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilifanya zoezi la majaribio ya uandikishaji wa wapiga kura kwa kutumia mashine za teknolojia hii mpya katika kata 10 katika Halmashauri za Kinondoni, Kilombero na Mlele kati ya tarehe 15 hadi 23 Desemba, 2014.
Habari njema ni kuwa, kwa kutumia mashine za BVR, idadi ya waliojiandikisha ilivuka lengo la uandikishaji kwa kipindi kilichopangwa katika Kata hizo. Katika Halmashauri ya Kilombero walioandikishwa walifikia asilimia 110.9 ya lengo, katika Halmashauri ya Mlele uandikishaji ulifikia asilimia 101 ya lengo na katika Jimbo la Kawe, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni walioandikishwa walikuwa asilimia 105.67 ya lengo. Mafanikio haya ni ya kutia moyo pamoja na changamoto za kiufundi zilizojitokeza na zile zinazotokana na upya wa mfumo wenyewe kwa watumiaji. Changamoto hizo zimefanyiwa kazi na watengenezaji wa vifaa vinavyotumika katika awamu hii ya uandikishaji wa wapiga kura nchi nzima.
Ndugu Wananchi;
Nimefarijika na taarifa kuwa zoezi la uboreshaji wa Daftari na uandikishaji wa wapiga kura limeanza vizuri Makambako. Wananchi wamejitokeza kwa wingi kuliko ilivyotarajiwa. Kati ya tarehe 23 hadi 25 Februari, 2015 kwa mfano, Tume ilitegemea kuandikisha wapiga kura 9,541 lakini kutokana na mwamko wa wananchi kuwa mkubwa wameweza kuandikisha wapiga kura 13,042. Kila kituo kilikuwa kinaandikisha kati ya wapiga kura 80 na 150 kwa siku. Lengo la Tume ni kuandikisha wapiga kura 32,000 katika Halmashauri ya Makambako ambako kwa siku wanatarajia kuandikisha watu 4,320. Naambiwa kuwa hesabu za juzi na jana wameandikisha hadi wapiga kura 6,000 kwa siku. Kwa kasi hii na kama mambo yatakwenda kama inavyotarajiwa, lengo hilo litafikiwa na hata kuvukwa.
Ndugu Wananchi;
Hatuna budi kutoa pongeza kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa hatua hii ya kutia moyo tuliyofikia katika mchakato huu. Inaondoa hofu iliyoanza kuingia miongoni mwa baadhi ya watu kuwa huenda zoezi hili lisingefanikiwa. Tunachokitaka kwa Tume ni kuona zoezi hili linaendelea na kukamilika kama ilivyopangwa. Napenda kurudia ahadi niliyokwishaitoa kwa Tume kwamba Serikali itafanya kila linalowezekana kuiwezesha kirasilimali ili iweze kutimiza jukumu lake hilo. Nimekwishawakumbusha Hazina kuhusu umuhimu wa zoezi hili kufanikiwa kama ilivyopangwa. Hivyo basi, nimewataka wahakikishe kutoa kipaumbele cha kwanza katika mgao wa fedha. Kama haifanyiki nawaomba Tume waniambie mimi mwenyewe.
Wito wangu kwenu, wananchi wenzangu, ni kujitokeza bila ya kukosa kwenda kujiandikisha kwa mujibu wa ratiba ya uandikishaji katika maeneo yenu kama itakavyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Msifanye ajizi maana hakutakuwepo na fursa nyingine ya kujiandikisha kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu baada ya fursa hii kupita.
Ndugu Wananchi;
Kama ilivyoelezwa na Tume na mimi kusisitiza mara kadhaa kuwa watakaojiandikisha wakati huu ndio watakaopiga kura ya maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa na ndio watakaopiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu. Vitambulisho vya zamani vya mpiga kura havitatumika, hivyo watu wote ambao ni Watanzania na wana umri wa miaka 18 au zaidi lazima wajitokeze kuandikishwa upya. Watu pekee ambao hawatapaswa kujiandikisha tena ni wale tu walioandikishwa katika zoezi la majaribio lililofanyika katika zile kata 10 za Halmashauri za Kinondoni, Ifakara na Mlele mwezi Desemba, 2014. Vitambulisho walivyopata ndivyo vyenyewe.

Ndugu Wananchi; Napenda kutumia nafasi hii pia kuwaomba viongozi wa vyama vya siasa, Serikali, dini na asasi za kiraia kuungana na Serikali na Tume ya Uchaguzi katika kuwakumbusha na kuwahamasisha wananchi wakajiandikishe. Naomba tusiwachanganye wananchi kwa kutoa taarifa zisizokuwa za kweli na kuwafanya wakaacha kujiandikisha. Sisi katika Serikali tunafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa kila atakayejitokeza kujiandikisha anaandikishwa. Aidha, tutahakikisha kuwa kila panapojitokeza changamoto zinatafutiwa ufumbuzi kwa wakati mwafaka. Tunatambua kuwa mfumo huu ni mpya hivyo panaweza kujitokeza changamoto zinazosababishwa na upya wake. Nawaomba wahusika kuendelea kuwaelimisha watendaji wanaohusika ili wapate uzoefu unaostahili. Aidha, nawasihi wananchi kuwa wavumilivu na waelewa pale ambapo wakati mwingine watalazimika kukaa kwenye mistari kwa muda mrefu kusubiri kujiandikisha, au wakalazimika kuja siku ya pili. Ndugu Wananchi; Kupiga kura kuamua kuhusu Katiba Inayopendekezwa au kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani ni haki na wajibu wa kila raia. Lakini, kuipata haki hiyo na kuweza kutimiza wajibu huo kunategemea kuwa na kitambulisho cha mpiga kura. Bila ya hivyo haiwezekani. Haya shime jitokezeni, mjiandikishe, ili muweze kuitumia haki yenu na kutimiza wajibu wenu wa kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa na kuchagua viongozi mnaowaona wanafaa kuongoza nchi yetu, jimbo lako na kata yako. Kura ya Maoni Ndugu Wananchi; Jambo la pili ninalotaka kulizungumzia ni kuhusu Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa. Kama mjuavyo, baada ya Bunge Maalumu la Katiba kutunga Katiba Inayopendekezwa na Rais kuchapisha Katiba hiyo katika Gazeti la Serikali na kutangaza siku ya kupiga kura ya maoni, kinachoendelea sasa ni matayarisho ya kufanyika kwa kura hiyo. Yapo majukumu ya Serikali, yapo majukumu ya Tume ya Uchaguzi, na yapo majukumu ya Serikali na Tume kwa pamoja. Utekelezaji umeishaanza na unaendelea. Miongoni mwa mambo yanayotakiwa kufanyika ni uandikishaji wa wapiga kura ambao umekwishaanza na unaendelea. Ipo pia kazi ya kuchapisha na kusambaza Katiba Inayopendekezwa ili wananchi waweze kuisoma na kuielewa kabla ya kupiga kura ya maoni. Tayari Katiba Inayopendekezwa imetangazwa katika tovuti za Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo na katika tovuti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Pia imechapichwa magazetini. Hadi tarehe 27 Februari, 2015 vitabu 1,558,805 vilikuwa vimechapishwa na nakala 1,341,300 kusambazwa. Nakala 1,141,300 zimesambazwa kwenye mikoa 25 ya Tanzania Bara na nakala 200,000 zimegawiwa kwa Zanzibar. Kwa upande wa Tanzania Bara kila Kata imepewa vitabu 300. Kwa vile Kata zina wastani wa vijiji vitano (5) hii ina maana kwamba kila kijiji kimepata vitabu 60 kwa kila kijiji ambayo si haba. Ndugu Wananchi; Tume ya Uchaguzi itatoa maelekezo kuhusu utaratibu wa kutoa elimu kwa umma. Nimeambiwa tayari asasi za kiraia 420 kwa upande wa Bara na 75 kwa upande wa Zanzibar zimejiandikisha kwa ajili ya zoezi hilo. Halikadhalika, Tume itatoa maelekezo husika kuhusu kampeni ya Kura ya Maoni wakati ukiwadia. Naomba watu wawe na subira na kuzingatia masharti ya Sheria ya Kura ya Maoni na Kanuni zake. Tukifanya hivyo, zoezi hili muhimu na la kihistoria litatekelezwa kwa usalama na utulivu. Watu watafanya uamuzi kwa uhuru, uelewa, amani na usalama. Hali ya Usalama Nchini Ndugu wananchi; Jambo la tatu ninalotaka kulizungumzia ni hali ya usalama nchini. Kwa jumla hali ya usalama ni nzuri, hata hivyo kuna matukio ya kiusalama ambayo ningependa kuyazungumzia. La kwanza ni mashambulizi yenye sifa za ujambazi na mwelekeo wa kigaidi. Na, la pili ni la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi. Katika kipindi cha miezi 12 hivi kumekuwa na matukio ya watu kuvamia vituo vya Polisi, wengine wanachoma moto au wengine wanapora silaha. Pia kumekuwepo na matukio ya kuwashambulia Polisi walioko kwenye doria na wengine kuporwa silaha. Vituo vya Polisi vilivyovamiwa na silaha kuporwa ni vya Newala Mkoani Mtwara silaha tatu ziliporwa, Ikwiriri katika Wilaya ya Rufiji silaha saba, Kimanzichana, Wilaya ya Mkuranga silaha tano, mbili za polisi na tatu za raia waliokwenda kuzihifadhi pale, na Ushirombo Wilaya ya Bukombe silaha 18. Pugu Machinjioni na Tanga, askari waliokuwa katika shughuli za ulinzi na doria walishambuliwa na kuporwa silaha tatu. Kule Songea kulikuwepo na matukio mawili ya Polisi kushambuliwa lakini silaha hazikuporwa. Bahati mbaya, vijana wetu saba wa Jeshi la Polisi walipoteza maisha katika matukio hayo. Newala alikufa Polisi mmoja, Kimanzichana mmoja, Ikwiriri wawili, na Ushirombo watatu. Wapo Polisi kadhaa waliopata majeraha ya namna mbalimbali katika mashambulizi haya. Ndugu Wananchi; Silaha zote 18 zilizoporwa Ushirombo zimepatikana na watu 10 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo wamekamatwa. Katika tukio la Tanga silaha moja kati ya mbili zilizoporwa imepatikana. Watuhumiwa saba wametiwa mbaroni, wanne kati yao ni wale waliokuwa wamejifisha katika mapango ya Kiomoni katika Kitongoji cha Karasha-mikocheni, kilichoko kijiji cha Mzizima wilayani Tanga. Tayari watu wanne wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la Ikwiriri wamekamatwa. Polisi wanaendelea na upelelezi kuwapata watu wengine na kuzipata silaha saba zilizoporwa kituoni hapo. Kwa tukio la Newala silaha zote tatu zimepatikana pamoja na bastola moja ya mtuhumiwa aliyehusikaa na watu wawili wametiwa nguvuni. Hali kadhalika, upelelezi unaendelea wa kuzipata silaha zilizoporwa ambazo hazijapatikana mpaka sasa: yaani Kimanzichana moja, Pugu Machinjioni moja na Tanga iliyosalia moja.

UMOJA WA WATU WA MWANGA WAFANYA MKUTANO MKUU NA KUFANA TANGA

March 02, 2015
JAMII imetakiwa kuwa na mshikamano katika kujiletea maendeleo  na kuacha mifarakano isiyo na tija jambo ambalo linaweza kurejesha nyuma nguvu kazi katika kujileta kipato

Akizungumza katika mkutano mkuu wa mwaka, Umoja wa Wanamwanga (Uwamwa) waishio Tanga jana,  mgeni rasmi katika mkutano huo, Simba Msuya, alisema vikundi vya umoja ni jambo muhimu na lenye kuleta maendeleo.

Alisema umoja ndani ya taasisi na jamii za watu ziko na msaada mkubwa katika kuharakisha maendeleo yakiwemo ya elimu na vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

“Fursa ya kuwa mgeni rasmi katika mkutano huu wa mwaka wa umoja wa wanamwanga ni jambo la kufurahisha na kuweza kutoa neno ambalo linaweza kuwa msaada kwa wengine” alisema Msuya na kuongeza

“Mimi niwaombeni katika umoja wenu huu pia iwe msaada kule mutokako kwa kusaidia shughuli za maendeleo kama upungufu wa vyumba vya madarasa na madawati” alisema

Alisema imekuwa ada kwa baadhi ya watu wanaounda umoja  kuacha kuchangia huduma za maendeleo katika maeneo yao na hivyo kusema kuwa huko hakutoweza kuleta maana ya umoja wao.

Akizungumza katika mkutano huo, Makamo Mwenyekiti wa Umoja huo, Yahya Mruma, alisema wanachama wake wamekuwa wakishiriki katika kazi za maendeleo zikiwemo za ujenzi wa maabara.

Alisema wamekuwa wakishiriki kikamilifu ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali na nguvu za wananchi katika ujenzi wa taifa na kuhakikisha malengo ya Serikali yanatimia.

“Mbali na kazi za umoja wetu lakini pia tumekuwa tukishiriki katika kazi za maendeleo kama ujenzi wa maabara kwa baadhi ya shule hapa Tanga na kule Mwanga” alisema Mruma

Amevitaka vikundi vyengine vinavyounda umoja kutumia fursa wanazozipata kusaidia jamii na kushiriki katika kazi mbalimbali za maendeleo ili kurahisisha huduma maeneo yao.


 Mlezi wa Umoja wa Wanamwanga (Uwamwa) waishio Tanga, akizungumza katika mkutano mkuu wa umoja huo uliofanyika ukumbi wa Tanga hoteli jana.
 Mwanachama wa umoja wa Wanamwanga (Uwamwa) waisho Tanga , Geofrey Msuya, akitoa ushauri wa jambo katika mkutano mkuu wa mwaka wa umoja huo uliofanyika jana Tanga.


HALIMA MDEE KUWAONGOZA WANAWAKE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

March 02, 2015

MWENYEKITI wa Taifa  baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , Halima Mdee, anatarajiwa kuwaongoza wanawake siku ya wanawake Duniani mjini hapa pamoja na kuzindua matawi  mapya ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari , Mwenyekiti  wa Bawacha Wilaya ya Tanga, Gress Joseph, alisema siku hiyo pamoja na mambo mengine Mdee atazindua matawi na kutoa kadi kwa wanachama wapya.

Alisema siku hiyo Chadema itaitumia kwa  kuwaelimisha wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za kuongoza  na kuacha woga na kuwa mstari wa mbele  kuweza kutetea maslahi yao.

Alisema kuna baadhi ya wanawake wako na uwezo wa kuongoza lakini bado hawajawa na utayari wa kufanya hivyo jambo ambalo limechangia kwa kiwango kikubwa wanawake kuwa nyuma katika sekta mbalimbali za maendeleo.

“Siku ya wanawake Duniani Tanga itazidi kunogeshwa na wabunge wengi wanawake akiwemo Halima Mdee----atatoa misaada katika vituo vya watoto wanaoishi mazingira hatarishi” alisema na kuongeza

“Haitoshi pia atazindua  matawi mapya ya Chadema na kutoa kadi kwa wanachama wapya katika mkutano wa hadhara ambao utafanyika kata ya Nguvumali” alisema Gress

Alisema kwa sasa taratibu zote zikiwemo za  kibali cha mkutano zimeshafanyika na hivyo kuwataka wakazi wa jiji la Tanga kukiunga mkono chama hicho ili kuweza kushika nafasi za kuongoza katika uchaguzi wa Wabunge na Urais.

Kwa upande wake, Katibu wa Bawacha Wilaya, Amina Mahmood, aliwataka vijana kujiunga na chama hicho kwani ndicho ambacho kitaweza kuwakomboa katika  dimbwi la umasikini uliowajaa.

Alisema hali ya maisha ya  Mtanzania imekuwa ngumu huku Serikali ikiwabana katika nyanja mbalimbali za kujikwamua kiuchumi na hivyo kuwataka kukiunga mkono ili kukiweka kando chama kilicho madarakani..

Alisema utitiri wa kodi zimekuwa kikwazo cha maendeleo na kusema kuwa hakuna chama chochote ambacho kitaweza kuzikomesha zaidi ya Chadema kwani kiko na dhamira ya kweli ya kumkomboa Mtanzania.

“Chadema kila siku kimekuwa kikipiga kelele za kuwaelisha wananchi kukiunga mkono  kwani ndicho  kinachoweza  kuwapunguzia mzigo wa kodi na makali ya maisha” alisema Amina

Alisema mwaka huu Chadema imedhamiria kuchukua viti vya Udiwani na Ubunge jimbo la Tanga kwa kufanya mikutano ya uhamasishaji mjini na vijijini ikiwemo kufungua matawi na kuunda timu moja ya ushindi.

MHE. JANET MBENE AKAMILISHA ZIARA YAKE UINGEREZA KWA KUKUTANISHWA NA WAFANYABIASHARA WA KITANZANIA JIJINI LONDON

March 02, 2015

 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Tanzania, Mheshimiwa Janeth Mbene(kulia), akiongea na Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza katika masuala ya Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania, Lord Clive Hollick, walipokutana kuzungumzia masuala ya Biashara ya kati ya nchi mbili ya Tanzania na Uingereza na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Uingereza kusaidia wawekezaji wa Kiingereza kuwekeza Tanzania.
 Mheshimiwa Janeth Mbene, akiongeza na Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Kiingereza alipokutana nao kwa mwaliko wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa East African Association. Mheshimiwa Naibu Waziri alikutana na Wafanyabiashara hao kwa lengo la kuwashawishi kuja kuwekeza nchini Tanzania
 Mheshimiwa Waziri Janeth Mbene(kulia), alipokutana na Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza na Chama cha Wafanyabiashara na Wawekezaji wa nchini Uingereza (UKTI) (kati mwa picha), kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania nchini Uingereza, Bwana Yusuf Kashangwa.
 Wawakilishi wa Jumuiya za Wafanyabiashara na Wanachama wa chama cha Wafanyabiashara wa Tanzania nchini Uingereza (Tanzania Business Group) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda, Mheshimiwa Janeth Mbene, alipokutana na kuzungumza nao siku ya Ijumaa tarehe 28 Februari 2015, mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, London. Mheshimiwa Waziri alikutana nao kuzungumzia hali ya Siasa na Uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla. Mheshimiwa Waziri aliwakumbusha Wafanyabiashara hao kutumia fursa zilizopo na kuwekeza nyumbani Tanzania, kwa lengo la kuongeza ajira na kuinua uchumi wa nchi.
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mheshimiwa Peter Kallaghe, akiongea machache kumkaribisha Mheshimiwa Naibu Waziri Janeth Mbene, kwenye Ofisi za Ubalozi huo zilizopo London. Naibu Waziri Mbene ameondoka usiku wa jumapili tarehe 1 kurejea Tanzania, alikuwa nchini Uingereza kwa ziara ya kikazi na kutembelea Vituo vya Kibiashara vya Tanzania na Dubai.
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Janeth Mbene, akiwa pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Saccoma, Mhe. Waziri alipokutana Viongozi wa Jumuiya hiyo ya Saccoma kuangalia jinsi gani inaweza kushirikiana na Tanzania kuwawezesha Wafanyabiashara wa Tanzania kuleta bidhaa zao nchini Uingereza kama ilivyo kwa Wafanyabiashara wa nchi nyingine za Afrika, ambazo bidhaa zao zimejaa nchini Uingereza tofauti na bidhaa za Tanzania ambazo hazipo. Pichani(kulia) Mheshimiwa Waziri Janeth Mbene, Mama Perez Ochieng (Saccoma - CEO), Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London, Bwana Yusuf Kashangwa, Mwakilishi wa Saccoma na Dada Magdalena Hall, msaidizi wa Waziri.
 Mheshimiwa Waziri Janeth Mbene(nne kushoto), Naibu Balozi wa Tanzania, Bwana Msafiri Marwa (tano kushoto),wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Ubalozi, alipokutana nao kwa mazungumzo mafupi kwenye ofisi za Ubalozi, London.

 Mheshimiwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene akiwa kwenye Ofisi za Kituo cha Biashara cha Tanzania, London. Pichani kulia ni Bwana Yusuf Kashangwa, Mkurugenzi wa Kituo na Dada Magdalena Hall msaidizi wa Waziri.
 Waziri Janeth Mbene (pili kulia), alipokutana kuzungumza na Wafanyabiashara wa Tanzania waishio nchini Uingereza na baadhi ya Wawakilishi wa Jumuiya za Watanzania. Pichani (kushoto), Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe, Bwana Msafiri Marwa (pili kushoto) na Bwana Khaki, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kitanzania waishio nchini Uingereza.
Naibu Waziri wa Viwanda, Mhe. Janeth Mbene akiongea na Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza Tanzania, alipokutana nao katika Mkutano ambao uliandaliwa na Chama cha Biashara na Wawekezaji wa Afrika kijulikanacho kama Business Council for Africa (BCA). Picha zote na Ally Rashid Dilunga
 NYALANDU AWAAGA WAFANYABIASHARA WANAOENDA KUSHIRIKI MAONYESHO YA ITB, BERLIN UJERUMANI

NYALANDU AWAAGA WAFANYABIASHARA WANAOENDA KUSHIRIKI MAONYESHO YA ITB, BERLIN UJERUMANI

March 02, 2015
Waziri wa Utalii na Maliasili Razalo Nyarandu akitoa nasaha za kuwaaga wafanyabiashara wa Tanzaia wanaoenda Berlin Ujerumani 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akitoa nasaha za kuwaaga wafanyabiashara wa Tanzania wanaoenda Berlin, Ujerumani kushiriki maonyesho makubwa Duniani ya biashara maarufu kama ITB kuanzia Machi 4-8 mwaka huu.(Picha zote na modewjiblog)
Na Andrew Chale wa modewji blog
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu amewataka wafanyabiashara wa Tanzania wanaoenda kushiriki maonyesho makubwa Duniani ya biashara maarufu kama ITB, mjini Berlin, Ujerumani Machi 4 hadi 8, mwaka huu, kubeba uzalendo na kuitangaza Tanzania hususani vivutio vya Utalii na utajiri wa maliasili ili kuvutia wawekezaji.
Nyalandu aliyasema hayo usiku wa Februari 27, wakati wa halfa fupi ya kuwaaga wafanyabiashara hao ambapo alisema kuwa, kwenda kwao huko kushiriki maonyesho hayo makubwa kabisa duniani, ni fursa kama Tanzania kupata kujitangaza zaidi na kuvutia wawekezaji.
DSC_0151 
Deputy Head of Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.
“Leo hii tunawaaga hapa. Nyie ndio Tanzania hivyo mnapokuwa huko mjue mmebeba watanzania wengine zaidi ya Milioni 40. Ni wakati wa kuvitangaza vivutio na uzuri wa Tanzania na ilikuongeza soko letu la Utalii na uwekezaji” alieleza Nyalandu.
Pia aliongeza kuwa, Wizara yake ya Utalii itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha Taifa la Tanzania linafikia malengo yake yaliyokusudiwa ikiwemo kujitangaza ndani na nje ikiwemo kuendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na Uharamia dhidi ya meno ya Tembo, wanyama na nyara za serikali kiwemo pembe za ndovu.
Maofisa wa T.T.B, Devota Mdachi (kushoto) akiwa na Dorothy Masawe (Kulia) wa wizara ya Utalii, wakifuatilia jambo kwa makini wakati wa halfa hiyo 
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi (kushoto) akiwa na Dorothy Masawe (Kulia) kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wakifuatilia jambo kwa makini wakati wa halfa hiyo.
DSC_0131 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akibdilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa.
DSC_0202 
Deputy Head of Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels (kulia), Afisa wa Ubalozi wa Ujerumani kitengo cha habari, John Meirikion (kushoto) wakiteta jambo na mmoja wa wageni waalikwa.
CEO wa DHL ukanda wa  Eastern Africa, Pramod Bagalwadi akisalimiana na Waziri wa Utalii, Razalo Nyalandu 
CEO wa DHL ukanda wa Eastern Africa, Pramod Bagalwadi, akisalimiana na Waziri Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu kwenye hafla hiyo.
DSC_0103 
Baadhi ya wageni waalikwa ambao ni wafanyabiashara katika sekta utalii wakibadilishana mawazo kwenye hafla hiyo.
DSC_0237
DSC_0231 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu katika picha ya pamoja na Afisa wa Ubalozi wa Ujerumani kitengo cha habari, John Meirikion wakati wa hafla hiyo.
DSC_0222Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu katika picha ya pamoja na wafanyabiashara akiwemo Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Bw. Florenso Kirambata ( wa pili kushoto).
DSC_0101Mkurugenzi wa Biashara wa Flight Link, Bw. Ibrahim Bukenya akiwa na Deputy Head of Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels wakati wa hafla hiyo.
DSC_0145 
Wadau wakifurahi jambo.
WAGANGA WA TIBA ASILI ZANZIBAR WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA MADAKTARI WA WIZARA YA AFYA

WAGANGA WA TIBA ASILI ZANZIBAR WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA MADAKTARI WA WIZARA YA AFYA

March 02, 2015

Mkuu wa kliniki ya Kisukari Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt. Faiza Kassim (aliesimama) akizungumza na Waganga wa tiba asili na tiba mbadala kuhusu mashirikiano ya utibabu wa magonjwa ya kisukari na presha.Ili kuepuka mgonjwa mmja kutumia dawa za Hospitali na zile zinazotolewa na waganga hao.  wa3 
Mmoja wa Waganga wa Tiba asili Bi. Zahra Hassan Ali akichangia katika semina hiyo iliyofanyika ukumbi wa Wizara ya Afya mnazi mmoja Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

NHIF YAZINDUA HUDUMA ZA MATIBABU ZINAZOTOLEWA BURE NA MADAKTARI BINGWA-TABORA

March 02, 2015

Mkuu wa mkoa wa Tabora akihutubia wakati wa Uzinduzi wa huduma ya Madaktari bingwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete,huduma ambayo inaratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF ikiwa ni hatua ya kuwahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko huo.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa  Bima ya Afya NHIF Bw.Charles Kajege akitoa maelezo kuhusu kuanzishwa kwa huduma hiyo ya Madaktari bingwa katika mikoa mbalimbali nchini ambayo imelenga kusaidia kutoa huduma za matibabu kwa watanzania kulingana na mahitaji ya maeneo husika. 
Mkuu wa mkoa wa Tabora  Bw.Ludovick Mwananzila akikabidhi msaada wa shuka kwa Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete Dr.Gunini Kamba,katikati ni Katibu tawala mkoa wa Tabora Bi.Kudra Mwinyimvua.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini NHIF Bw.Charles Kajege akikabidhi msaada wa vifaa tiba vitakavyosaidia zoezi la utoaji wa huduma za matibabu zitakazotolewa na madaktari bingwa kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Moi jijini Dar-es-Salaam.
Madaktari bingwa ambao watatoa huduma za matibabu bure kwa wananchi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete kwa muda wa siku saba.
Baadhi ya wananchi wakipanga hospitali ya rufaa Kitete wakisubiri kuonana na madaktari bingwa kwa ajili ya kupatiwa uchunguzi na matibabu.
Mganga mkuu wa mkoa wa Tabora Dr.Gunini Kamba akijaribu kuteta na viongozi wa ngazi ya juu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambapo katikati ni Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa NHIF Bw.Charles Kajege,na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini Bw.Athuman Rehan.

AZAM FC YAMFUKUZA KAZI OMOG, MSAIDIZI WAKE, TIMU APEWA MGANDA

March 02, 2015


Azam FC imetangaza kumfukuza kazi Kocha Joseph Omog raia wa Cameroon.

Pamoja na Omog, Msaidizi wake, Ibrahim Shikanda ametimuliwa na mikoba amepewa George Best Nsimbe raia wa Uganda ambaye ni msaidizi wake namba moja.
ALIVYOKARIBISHWA NA UONGOZI WA AZAM FC, MWENYEKITI WA AZAM FC, SAID AKIMKARIBISHA.


Best ambaye ameanza kazi Azam FC msimu uliopita, sasa ndiye ataongoza jahazi.

Ingawa uongozi wa Azam FC haujaanika kila kitu, lakini inaonekana Omog anaondoka baada ya Azam FC kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa mabao jumla ya mabao 3-2.

Azam FC ilianza kwa kushinda 2-0 jijini Dar lakini ikakubali kipigo cha mabao 3-0 jijini Kharthoum.

Omog ndiye aliyeipa Azam FC ubingwa wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara na ushindi wake wa kwanza katika Ligi ya Mabingwa Afrika .

RAIS KIKWETE AONGOZA MAELFU YA WAOMBOLEZAJI KATIKA SHUGHULI YA KUAGA MWILI WA KAPTENI JOHN KOMBA,KAJIMJEE JIJINI DAR LEO

March 02, 2015

Jeneza lenye mwili wa aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM,Marehemu Kapteni John Komba likiwa kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam,wakati wa shughuli ya kuaga.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kapteni Komba anatarajiwa kuzikwa kijijini Kwake Litui wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.
 Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal na wake zake Mama Asha na Mama Zakhia wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassa Mwinyi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiifariji familia ya marehemu.
 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania,Luteni Kanali Samuel Ndomba akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. Jenista Mhagama akitoa heshima za mwisho akifuatana na Naibu IGP,Abdulrahman Kaniki.
 Kingunge Ngombale–Mwiru akitoa heshima za mwisho.
Kamanda Kova.
Baadhi wa Waheshimiwa Wabunge wakiifariji familia ya Marehemu.
Mhe. Ole Sendeka akibubujikwa na machozi kuondokewa na Mbunge mwenzake.
Familia ya Marehemu.
Watoto wa Marehemu Kapteni John Komba wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu baba yao.
Mjane wa Marehemu,Kapteni John Komba,Mama Salome Komba akiaga mwili wa mumewe
Khadija Kopa.
Umati wa viongozi mbali mbali pamoja na wananchi wakiwa kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. Jenista Mhagama akitoa salamu za Serikali wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii,Mh. Saidi Mtanda akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Kamati yake.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Mh. Joshua Nassari.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akitoa salamu za Chama.
Mh. Muhongo akitoka kuaga mwili wa Kapteni Komba.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akisungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana.kushoto ni Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda.
Mama Regina Lowassa akizungumza jambo na Mama Sophia Kawawa.
Mh. Mkapa akizungumza jambo na Mh. Anne Makinda.




Mjane wa Marehemu.