WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI SWALA YA IDD EL FITRI KATIKA MSIKITI WA RIADHA MJINI MOSHI

June 26, 2017
Waziri Mkuu wa Tanzania,Kassim Majaliwa akiwasili katika msikiti wa Riadha mjini Moshi kwa ajili ya Swala ya Eid el Fitri iliyofanyika kitaifa mjini Moshi.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa katika Msikiti wa Riadha mjini Moshi.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa aikishiriki Swala ya Idd el Fitri iliyofanyika kitaifa katika msikiti wa Riadha mjini Moshi.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakishitiki Swala Idd.
Swala ya Idd ikifanyika katika msikiti wa Riadha mjini Moshi.
Waziri Mkuu wa Tanzania,Kassim Majaliwa,akiwa na Sheakh Mkuu wa Tanzania ,Mufti Abubakary Zubery ,Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu ,Said Mwema.
Mshindi wa kuhifadhi Quran tukufu ,Ibrahim Mitigo akionesha namna ambavyo alivyohifadhi Quran wakati wa Swala ya Idd el Fitry iliyofanyika katika msikiti wa Riadha mjini Moshi.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakishiriki Swala ya Idd mjini Moshi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ,akizungumza wakati wa Swala ya Idd el Fitry iliyofanyika kitaifa katika Msikiti wa Riadha mjini Moshi.
Mufti wa Tanzania na Sheakh Mkuu,Abubakary Bin Zubery akitoa nasaha zake wakati wa Swala ya Idd iliyofanyika kitaifa mjini Moshi.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakishiriki katika Swala ya Idd El Fitry iliyofanyika mskiti wa Riadha mjini Moshi

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

WAISLAMU WATAKIWA KUENDELEZA UCHA MUNGU

June 26, 2017
Na Swahilivilla Washington Waislamu wametakiwa kuendeleza Ucha Mungu na mema waliyokuwa wakiyafanya katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Sheikh Yussuf Mecca, kutoka Columbus, Ohio
Wito huo ulitolewa jana na Sheikh Yussuf Mecca alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Iddi zilizoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu wa Tanzania wa Jiji la Washington na Vitongoji vyake ijulikanayo kwa jina la TAMCO.
"Kwa vile mwezi wa Ramadhani umekwisha isiwe yale yote mazuri tuliyokuwa tunayafanya ikawa ndiyo basi, na tusubiri Ramadhani nyengine" alisema Sheikh Yussuf.
Aliendelea kusisitiza umuhimu wa kujitahidi kumcha Mungu wakati wowote na kujitahidi katika kutenda mambo mema na ibada ili kujiandaa na safari ya Akhera ambayo inanaweza kumfikia mtu wakati wowote.
" Hakuna hata mmoja ambaye anajua ni siku gani atafumba jicho na atakufa", alisisitiza Mgeni huyo rasmi kwenye shere hizo, huku akitilia nguvu hoja yake kwa Aya ya Qur'an isemayo: "كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ" (Kila nafsi itaonja mauti/kifo), akigogoteza kuwa hakuna mtu yoyote anayejua atakufa lini au mahali gani.
Aliongeza kusema kuwa kurejea kwenye maasi baada ya juhudi kubwa za ucha Mungu na ibada katika mwezi wa Ramdhani ni sawa na kuiharibu kazi ya kiufundi liyofumwa kwa juhudi na ustadi mkubwa.
Mwenyekiti wa TAMCO Bwana Ali Muhammed
Sherehe za Iddi za Waislamu wa Tanzania katika Mji huo Mkuu wa Marekani, ni utamaduni ulioanza tangu mwaka 1998, ambapo Waislamu waliona haja ya kuwa na mjumuiko wa pamoja katika Siku Kuu, ikizingitwa kuwa Marekani si nchi ya Kiislamu na kwa hivyo hakuna sherehe rasmi za Iddi, kama alivyoelezea Mwenyekiti wa TAMCO Bwana Ali Muhammed:
"Wazee na vijana waliokuwepo hapa katika miaka hiyo waliona kuna haja ya kuanzisha Umoja ambao utawasaidia katika mambo yao ya Kidini, siyo tu kwenye sherehe za Iddi, bali pia katika maswala mengine ya sherehe na misiba. Na baada ya chombo hicho kuanzishwa ndipo ukaanza utaratibu wa kuandaa sherhe kama hizi za Iddi".

WAZIRI MAKAMBA AWATAKA WAISLAMU KUENDELEZA MSHIKAMANO.

June 26, 2017
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba akizungumza wakati wa baraza la Eid lililofanyika kwenye shule ya Sekondari Jumuiya mjini Tanga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto ni Shehe wa mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza katika baraza hilo kushoto ni  Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.
Shehe wa mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu akizungumza katika baraza hilo ambapo aliwataka waislamu kuendelea kutenda mambo mema kulia ni Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba na mkuu wa mkoa wa Tanga,Martine Shigella
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akilakiwa na waumini wa dini ya kiislamu wakati akipokwenda kwenye baraza la Eid ambalo lilifanyika katika shule ya Sekondari Jumuiya
 Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba akilakiwa na waumini wa dini hiyo wakati alipokwenda kwenye Baraza la Iddi ambalo lilifanyika katika shule ya sekondari Jumuiya

 Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali katika Baraza hilo
 Sehemu ya waumini wakimsikiliza Waziri Makamba kwenye Baraza hilo leo
  Sehemu ya waumini wakimsikiliza Waziri Makamba kwenye Baraza hilo leo
  Sehemu ya waumini wakimsikiliza Waziri Makamba kwenye Baraza hilo leo



 Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba kulia akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella
WAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI WA CHAKULA NJE YA NCHI

WAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI WA CHAKULA NJE YA NCHI

June 26, 2017
KIL1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa nasaha kwa waumini (hawapo pichani) waliohudhuria Swala ya Eid el Fitr na Baraza la Eid Kitaifa kwenye msikiti wa Masjid Riadha mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KIL2
Waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria Swala ya Eid el Fitr na Baraza la Eid Kitaifa kwenye msikiti wa Masjid Riadha mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akitoa nasaha za Eid, tarehe 26 Juni, 2017. (
KIL3 KIL5 KIL6
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally wakati wa stafutahi kwenye Ikulu ndogo ya Moshi, mara baada ya Swala ya Eid el Fitr na Baraza la Eid Kitaifa mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017.
KIL7
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally mara baada ya stafutahi kwenye Ikulu ndogo ya Moshi, mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KIL8
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo, nyumbani kwa marehemu Dk. Philemon Ndesamburo, eneo la Kiboriloni, Moshi, mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KIL9
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa pole na neno la faraja kwa wanafamilia, nyumbani kwa marehemu Dk. Philemon Ndesamburo, eneo la Kiboriloni, Moshi, mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KIL10
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa pole mjane wa marehemu, mama Ndehorio P. Ndesamburo alipofika nyumbani kwao eneo la Kiboriloni, Moshi, mkoani Kilimanjaro kuwafariji kutokana na msiba wa Dk. Philemon Ndesamburo, leo tarehe 26 Juni, 2017. 
KIL11
Kaka wa marerehemu Dk. Philemon Ndesamburo, Bw. Zablon Sindato Kihwelu akimshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyefika nyumbani kwao eneo la Kiboriloni, Moshi, mkoani Kilimanjaro kuwafariji kutokana na msiba wa Dk. Philemon Ndesamburo, leo tarehe 26 Juni, 2017.
KIL12
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bibi Anna Mgwira (wa tatu kushoto), mjane wa marehemu na Kaka wa marehemu wakiomba dua na wanafamilia kwenye kaburi la Dk. Philemon Ndesamburo, aliyezikwa nyumbani kwake eneo la Kiboriloni, Moshi, mkoani Kilimanjaro. Wa kwanza kulia ni mtoto wa marehemu.
DK SHEIN ATOA MKONO WA EID EL FITRI IKULU

DK SHEIN ATOA MKONO WA EID EL FITRI IKULU

June 26, 2017
baw1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Dini na Mashekhe wa Dini ya Kiislamu waliofika  Ikulu Mjini Unguja   leo kumtakia  Rais Sikukuu njema baada ya kumalizika kwa  Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
baw2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) pampja na Viongozi mbali mbali wa Dini na Mashekhe wa Dini ya Kiislamu waliofika  Ikulu Mjini Unguja   leo kumtakia  Rais Sikukuu njema baada ya kumalizika kwa  Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wakiitikia Dua Iliyoombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibae Sheikh Saleh Omar Kabi,(wa pili kushoto),[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
baw3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pampja na Makamu wa Pili wa Rais  Balozi Seif Ali Iddi wakiaagana na Viongozi mbali mbali wa Dini na Mashekhe wa Dini ya Kiislamu waliofika  Ikulu Mjini Unguja   leo baada ya  kutakiana Kheri katika Sikukuu ya Eid El Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
baw4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akisalimiana na Mjukuu wake Ali Abdalla Mitawi katika Kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
baw5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akifanya mahojiano na Watoto Nabil Mohamed Said na Ahmed Mohamed Said  (kushoto) waliofika Ikulu Mjini Unguja kutoka Shirika la Utangazaji ZBC kwa ajili ya kutayarisha Kipindi cha Watoto sambamba na Sikukuu ya  Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
baw6
Baadhi ya Akinamama na Watoto waliofika katika viwaja vya Ikulu Mjini Unguja kwa ajili ya kusalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) na Kupokea Mkono wa Eid katika kusherehekea Sikukuu ya  Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
baw7
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akitoa Sikukuu kwa Mzee Juma Kesi (kulia) alipojumuika na Wazee mbali mbali waliofika katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja  kupokea mkono Eid el Fitri katika kusherehekea Sikukuu ya  Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.  
baw8
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akitoa Sikukuu kwa Mzee Salum  Othman Haji (kulia) alipojumuika na Wazee mbali mbali waliofika katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja  kupokea mkono Eid el Fitri katika kusherehekea Sikukuu ya  Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.  
baw9
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akitoa Sikukuu kwa Mtoto Othman Khamis (mwenye ulemavu) alipojumuika na Wazee mbali mbali na Wananchi waliofika katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja  kupokea mkono Eid el Fitri katika kusherehekea Sikukuu ya  Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.