Kampuni 3 Kuuza Tanzanite katika Mnada Wa Mirerani

December 20, 2017
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila( katikati) akielezwa jambo na Vikosi vya ulinzi na usalama, katika eneo linalotumika kufanyia mnada wa Madini ya Tanzanite katika eneo la Naisinyai lililoko kwenye mji mdogo wa Mirerani.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila( katikati) akiangalia mapambo na vitu mbalimbali vinavyotengezwa na Kituo cha Uongezaji thamani Madini ya vito na Miamba( TGC),kilichopo mkoani Arusha, wakati Mnada wa Madini ya Tanzanite unaofanyika katika Mji mdogo wa Mirerani mkoani Manyara.
Wanunuzi kutoka mataifa mbalimbali wakifanya uthamini wa Madini ya Tanzanite kabla ya mnada kufanyika katika eneo la Naisinyai lililoko kwenye mji mdogo wa Mirerani.
Vifaa maalum( drum) vilivyohifadhia madini ya Tanzanite.
Madini ya Tanzanite yakipimwa kabla ya kuanza kufanyiwa mnada.
Mjiolojia Ester Njiwa wa Kituo cha Jemolojia Tanzania( TGC)akionenya vitu Mbalimbali vinavyotengenezwa na kituo hicho, wakati mnada wa Madini ya Tanzanite utakaofanyika katika mji mdogo wa Mirerani.
Usajili wa washiriki wa Mnada wa Madini ya Tanzanite ukiendelea katika mji mdogo wa Mirerani mkoani Manyara.
Ukaguzi ukiendelea kwa wanunuzi wanaofika katika eneo linalofanyika mnada wa Madini ya Tanzanite katika Mji mdogo wa Mirerani.




Na Zuena Msuya, Manyara.

Kampuni tatu za uchimbaji madini ya Tanzanite zimejitokeza kuuza madini hayo katika mnada wa tatu wa madini ya Tanzanite unaofanyika katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Mshindi wa mnada huo atatangazwa Desemba 21 katika eneo la Naisinyai lililoko kwenye mji mdogo wa Mirerani.

Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka amezitaja kampuni hizo kuwa ni Tanzaniteone yenye ubia na Shirika la Madini Tanzania( STAMICO), Tanzanite Afrika na Classic Gems.

Akizungumzia mnada huo, Kamishna Mchwampaka alisema kuwa utaratibu wa kufanya Mnada wa Tanzanite ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje nchi na pia kuwasaidia wachimbaji na wafanyabiashara wazalendo kuuza madini yao kwa bei ya ushindani inayoendana na soko la dunia.

Mchwampaka alifafanua kuwa, mnunuzi atakayefanikiwa kununua madini katika mnada huo ni yule tu atakayetoa bei ya juu ambayo imefikia au kuvuka bei inayotokana na Wathamini wa Serikali (Reserve Price).

Aliweka wazi kuwa zoezi hilo linafanyika kwa njia ya uwazi ambapo wanunuzi wa ndani na nje wanapata fursa ya kutazama madini na hatimaye kupata nafasi ya kutayarisha bei zao kwa siri ambazo zitatumbukizwa kwenye sanduku la Zabuni. Aidha, viongozi wa Wizara ya Madini, Wizara ya Fedha, Viongozi wa Mkoa wa Manyara, TRA na Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya mkoa wa Manyara wanashirikiana kwa pamoja kuhakikisha kuwa mnada huo unafanyika kwa ufanisi.

Aidha, mnada huo utaiwezesha Serikali kupata mrabaha stahiki na kodi nyingine ikiwa ni pamoja na tozo ya Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro.

Hadi kufikia Desemba, 19,2017, zaidi ya wanunuzi 55 tayari wamejaza fomu za kuwawezesha kushindana kwenye zabuni za kununua madini hayo,wakiwepo watanzania 39 na wanunuzi 16 kutoka nje ya Tanzania

Kamishna Mchwampaka alisema kuwa minada kama hiyo pia hufanyika kwa nchi za Afrika zenye madini ya Vito kama vile Zambia( emerald), Zimbabwe ( Almasi) pamoja na Afrika kusini ( Almasi).

SHUWASA,POLISI WATEKETEZA VIFAA VINAVYOTUMIKA KUHARIBU VYANZO VYA MAJI BWAWA LA NING'WA SHINYANGA

December 20, 2017
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA) kwa kushirikiana na jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga wameendesha zoezi la kuteketeza vifaa vinavyotumika kuharibu vyanzo vya maji katika bwawa la Ning’wa.

Miongoni mwa vifaa vilivyoteketezwa kwa moto ni nyavu za kuvulia samaki,mitumbwi na vibanda vinavyotumiwa na wavuvi kujihifadhi karibu na bwawa hilo.Zoezi hilo limefanyika leo Jumanne Desemba 19,2017 katika bwawa hilo lenye mita za ujazo milioni 10.9 linalopatikana katika kata za Old Shinyanga,Chibe na Pandagichiza zilizopo katika wilaya ya Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa zoezi hilo,Mkurugenzi wa SHUWASA,Injinia Sylivester Mahole alisema lengo la oparesheni hiyo aliyodai ni endelevu, ni kuhifadhi vyanzo vya maji kwani bwawa hilo ni moja vya vyanzo muhimu vya maji vya mamlaka hiyo ukiachilia mbali Ziwa Victoria. 

“Tumeteketeza kwa moto vifaa vilivyokuwa vinatumika kwa shughuli za uvuvi katika bwawa hili ikiwemo mitumbwi,nyavu na vibanda vilivyokuwa vinatumiwa na wavuvi,tunataka waache mara moja kufanya uvuvi hapa kwani wanaharibu vyanzo vya maji”,alieleza Injinia Mahole. 

Aidha alisema shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo,uvuvi na ufugaji zinaharibu vyanzo vya maji katika bwawa hilo ambapo kina chake kimekuwa kikipungua mara kwa mara. 

“Umeibuka utamaduni wa wananchi kulima bustani pembezoni mwa bwawa kisha kuweka pampu majini wakati huo watumia dawa za mazao ambazo siyo nzuri kwa afya ya binadamu,wananywesha mifugo hapa na kuvua samaki kwa kutumia nyavu na vyandarua”,alifafanua Injinia Mahole. 

Alisema pamoja na kuendelea kufanya vikao na mikutano na wananchi kuwapa elimu ya hifadhi ya vyanzo vya maji bado wananchi wamekuwa wakifanya shughuli za kibinadamu katika bwawa hilo hivyo wataendelea oparesheni ya kuharibu vifaa na kukamata watu wote wanaokiuka sheria na kanuni za utunzaji mazingira na vyanzo vya maji. "Tulifanya vikao na mikutano na viongozi pamoja na wananchi wao ndiyo wakatoa azimio la kuondoa watu wote wanaofanya shughuli za kibinadamu katika bwawa hili huku wakiipa SHUWASA jukumu la kusimamia zoezi zima,na sisi tangu mwezi Septemba mwaka huu tumekuwa tukiendesha oparesheni ya kuondoa watu wanaoharibu vyanzo vya maji",aliongeza. 

Aidha aliwataka wananchi kuzingatia kanuni na sheria za hifadhi ya vyanzo vya maji na kwamba hawatasita kuwachukulia hatua wale watakaobainika kuendelea kuharibu vyanzo vya maji katika bwawa hilo. Vyanzo vikuu vya maji vya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA) ni Ziwa Victoria na bwawa la Ning’wa. 

Mpaka mwezi Novemba 2017 idadi ya maunganisho ya maji yaliyofanywa na SHUWASA mjini Shinyanga ni 18,900 ambapo zaidi ya watu 200,000 wanapata huduma ya maji kutoka SHUWASA. 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA),Injinia Sylivester Mahole akielezea lengo la kuendesha oparesheni ya kuteketeza kwa moto vifaa vinavyotumiwa na wananchi kuharibu vyanzo vya maji katika bwawa la Ning'wa.Kulia ni mwandishi wa habari wa Radio Faraja na DW,Veronica Natalis - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA),Injinia Sylivester Mahole akionesha mifugo katika bwawa la Ning'wa 
Kushoto ni ng'ombe wakiingia katika bwawa la Ning'wa, katikati ni askari polisi akitoa maelekezo kwa wananchi waliokutwa katika bwawa hilo na kuambiwa waondoe mitego ya samaki iliyowekwa katika bwawa hilo. 
Askari polisi akishirikiana na mwananchi kuondoa mtego wa samaki katika bwawa la Ning'wa 
Zoezi la kuondoa mtego wa samaki likiendelea 
Askari polisi aliyevaa kiraia akiondoa nyavu ya chandarua katika bwawa la Ning'wa 
Zoezi la kubomoa mtumbwi likiendelea
Askari polisi wakiendelea kubomoa mtumbwi kwa kutumia nyundo 
Askari polisi akimwaga mafuta kwa ajili ya kuchoma moto nyavu zinazotumika kuvua samaki katika bwawa la Ning'wa 
Moto ukiteketeza nyavu 
Nyavu zikiteketea kwa moto 
Zoezi la kuchoma moto nyavu likiendelea 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA),Injinia Sylivester Mahole akizungumza na mmoja wa wananchi aliyekutwa akifanya shughuli za kibinadamu katika bwawa hilo Jackson Kabanda 
Askari polisi wakiangalia vibanda vinavyotumiwa na wavuvi kujihifadhi karibu na bwawa la Ning'wa. 
Vibanda vinavyotumiwa na wavuvi katika bwawa la Ning'wa vikiteketezwa kwa moto 
Moto ukiteketeza vibanda vya wavuvi katika bwawa la Ning'wa. 

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

WAHAMIAJI HARAMU 55 WAMAKATWA WILAYANI MKINGA

December 20, 2017
ZAIDI ya wahamiaji 50 raia kutoka nchini Ethiopia wameka matwa eneo la Duga wilayani Mkinga mkoani Tanga kwa kosa la kiungia nchini kinyume cha sheria.
Wahamiaji hao wamekamatwa ndani ya kipindi cha mwezi Desemba mwaka huu kutokana na operesheni ambazo zimekuwa zikiendeshwa na Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ya kuhakikisha wanazibiti wimbi la uingiaji huo.
Hayo yalisemwa jana na Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Tanga DCI Crispian Ngonyani wakati akizungumza na gazeti hili ofisi kwake ambapo alisema wahamiaji hao hivi sasa wanaendelea na kesi zao zinazowakabili kutokana na kuingia nchini kinyume na utaratibu uliopo.
Alisema hatua ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao inatokana na kuwepo kwa misako ya kushtukiza katika maeneo mbalimbali hasa ya mipakani mkoani hapa ambapo wahamiaji hao wamekuwa wakitumia kama njia ya kuingilia.
“Sisi kama Uhamiaji mkoani Tanga tumejipanga vizuri kuhakikisha wimbi la wahamiaji haramu hawaingii kutokana na doria ambazo tumekuwa tukizifanya mara kwa mara lakini kubwa zaidi ni kuwepo kwa vituo eneo la mipakani hususani Horohoro “Alisema.
Aidha alisema pia ili kuhakikisha suala hilo linazibitiwa kwa vitendo tayari wamekwisha kuweka kituo eneo la Vijinga wilayani Mkinga kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wanakagua magari ambayo yamekuwa yakitokea nchini Jirani ya Kenya  ili kuweza kubaini iwapo wahamiaji haramu wamebebwa.
Hata hivyo alisema kuelekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya wamejiandaa vizuri kuweza kukabiliana na wimbi la wahamiaji haramu wanaoweza kuingia mkoani hapa kwa kuendelea operesheni kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo nyumba za kulala wageni na kwenye hoteli.
“Licha ya kuendelea na operesheni hizo lakini nisema idadi ya wahamiaji haramu wanaoingia mkoani Tanga kwa sasa imepungua kwa sababu wakiwakamata wanawapeleka mahakamani pamoja na mawakala wao"Alisem
Afisa Uhamiaji huyo alisema lakini bado tunaendelea kuhakikisha ina koma kabisa kwa kuwachukulia hatua kali na watanzania ambao watabainika wanashirikiana nao kuwaingia mkoani hapa.

Ziara ya Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Mkoa wa Kusini Pemba

December 20, 2017
 Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Hassan A. Ramadhan (kulia) akifafanua jambo kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kulia) kuhusu mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inavyosaidia kurahisisha mawasiliano na utendajikazi katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba.  Kamishna Sururu akiendelea na ziara ya kikazi, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 – 19 Disemba, 2017.

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Juma A. Khamis (aliesimama) akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (hayupo pichani) na Watumishi wa Idara ya Uhamiaji walioko Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 19 Disemba, 2017. Alisema “Ongezeko la Bandari Bubu ndani ya Wilaya ya Mkoani ni changamoto kubwa katika utekelezaji wa majukumu yetu. Tunazo takriban Bandari bubu 103, tunaomba Idara itupatie gari la kufanyia doria katika maeneo hayo”. Kwa upande wake Kamishna Sururu katika ziara yake hiyo ya kikazi Mkoani humo, aliahidi kulifanyia kazi ombi mapema iwezekanavyo.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (kushoto) akikagua baadhi ya magari chakavu yaliyopo katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, yanayosubiri kupigwa mnada baada ya kukamilika kwa taratibu za uuzaji wa Mali za Serikali. Wakati wa ziara ya kikazi Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 – 19 Disemba, 2017. Pamoja na kutembelea maeneo mbali mbali ya utendaji kazi Mkoani humo ikiwemo Bandari ya Mkoani, Bandari ya Wesha iliyopo Chake Chake na Bandari bubu kadhaa. Kulia kwake ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdi Bulushi. 

 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akikagua kitabu cha utoaji wa Hati za Dharura za Kusafiria “ETD” katika Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Mkoani, zinazotolewa kwa Watanzania wanaohitaji kusafiri nje ya Nchi. Huku akiwasisitiza Maofisa Uhamiaji katika utoaji wa Hati hizo wazingatie vyema Sheria na Taratibu zilizopo ili kuepusha matumizi yasiyo sahihi. Aliyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 – 19 Disemba, 2017. Hati za Kusafiria za Dharura ni miongoni mwa Hati mbali mbali za Kusafiria zinazotelewa na Idara ya Uhamiaji Nchini
 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini Magharibi mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii, ambazo hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka visiwani humo kinyume na taratibu za Uhamiaji. Wakati alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali mbali ndani ya Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 Disemba, 2017. 
 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akitoa nasaha zake kwa Maafisa, Askari na watumishi Raia wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, wakati akihitimisha ziara ya kikazi Mkoani humo Leo tarehe 19 Disemba, 2017. Aidha, Kamishna Sururu aliwataka watumishi wote kuzingatia maadili ya kazi, pamoja na kutilia mkazo matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii. “Naelewa tupo kwenye utandawazi, lakini narudia kuwasihi matumizi ya Mitandao ya kijamii itumike kwa kuzingatia Kanuni na Miongozo ya Serikali, pia mjiepushe na utoaji wa Siri na Taarifa za serikali, ni mwiko kutoa taarifa yoyote. fuateni Sheria na Taratibu tulizowekewa”. 
 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini Magharibi mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii, ambazo hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka visiwani humo kinyume na taratibu za Uhamiaji. Wakati alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali mbali ndani ya Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 Disemba, 2017. 
 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini Magharibi mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii, ambazo hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka visiwani humo kinyume na taratibu za Uhamiaji. Wakati alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali mbali ndani ya Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 Disemba, 2017. 

 Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdi Bulushi akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kulia) na Maafisa Uhamiaji aliombatana nao, matunzo na usafi wa mazingira katika nyumba za Makaazi ya Askari wa Uhamiaji, zilizoko eneo la Ndugukitu, Wilaya ya Chake chake, Mkoa wa Kusini Pemba. Kamishna Sururu yupo Mkoa wa Kusini Pemba kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 18 – 19 Disemba, 2018. Aidha, Nyumba hizo zilifunguliwa rasmi na Mhe. Makamo wa Pili wa Rais, Balozi Seif Iddi mapema mwezi Januari, 2017.

Mojawapo ya nyumba za Makaazi ya Askari wa Uhamiaji, zilizoko eneo la Ndugukitu, Wilaya ya Chake chake, Mkoa wa Kusini Pemba. Kamishna Sururu yupo Mkoa wa Kusini Pemba kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 18 – 19 Disemba, 2018. Aidha, Nyumba hizo zilifunguliwa rasmi na Mhe. Makamo wa Pili wa Rais, Balozi Seif Iddi mapema mwezi Januari, 2017.

KONGAMANO LA UTALII NA WANAHABARI NA WADAU WA UTALII KUFANYIKA JANUARI 19, ARUSHA

December 20, 2017
ANDREA NGOBOLE


Katibu mtendaji wa vyama vya waongoza watalii nchini (TTGA) Emmanuel Mollel akizungumza katika kongamano la utalii na kuiomba serikali kuondoa kero zao ikiwepo malipo duni na kutokuwepo kwa mtaala wa kitaifa wa waongoza utalii, kongamano hilo lilifanyika Arusha Palace Hotel.

Mratibu wa mradi wa jumuiko la maliasili Tanzania (TNRF) Jumapili Chenga akitoa mada katika kongamano la utalii kuhusiana na umuhimu wa hifadhi za jamii (WMA) katika uhifadhi nchini katika ukumbi wa Arusha Palace Hotel, kongamano hilo liliandaliwa na taasisi ya Arusha Media.

Afisa utalii katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha Flora Basir, akizungumza katika kongamano la utalii mkoani Arusha na kueleza jinsi serikali mkoani Arusha ilivyojipanga kuhakikisha mkoa wa Arusha inakuwa kitovu kikuu cha utalii barani Afrika, kwa kuondoa kero katika sekta ya utalii, kongamano hilo lilifanyika Palace Hotel kwa kuwashirikisha wanahabri na wadau wa utalii
Mratibu wa Tamasha hilo, Andrea Ngobole   katikati akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari awapo pichani
 NA: MWANDISHI WETU ARUSHA

Kongamano la pili la  utalii na amani ambalo hushirikisha wanahabari, wanafunzi  na wadau wa utalii nchini, linatarajiwa kufanyika  mkoani Arusha, Januari 19,2018.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mratibu wa kongamano hilo la pili kufanyika mkoani hapa, Andrea Ngobole alisema, kongamano  hilo, limeandaliwa na taasisi ya Arusha Media kwa kushirikiana na Shahanga sports promotion.

Ngobole alisema, lengo la kongamano hilo ni kuhamasisha utalii wa ndani na kupinga vita ujangili na kuhamasisha uhifadhi endelevu ambao utashirikisha jamii.
Alisema katika kongamano hilo,wanahabari watajadili mchango wa vyombo vya habari katika kukuza  utalii na  vita dhidi ya ujangili  pia umuhimu wa jamii kushiriki katika uhifadhi endelevu kwa maslahi ya taifa.

“kama ilivyokawaida mada mbali mbali zitatolewa na wahifadhi, watafiti katika masuala ya uhifadhi na utalii na pia waandishi wa habari waliobobea katika masuala ya uhifadhi  ”alisema.

Alisema kongamano hilo pia litaambatana na mashindano ya riadha ya Tourism Marathon ambayo pia yatafanyika Arusha kuhamasha utalii.
Mkurugenzi wa taasisi ya Alfredo  Shahanga promotion, Alfredo Shahanga  alisema wanariadha zaidi ya 200 wanatarajiwa kushiriki.
"kwa ujumla kongamano la mashindano hayo ni sehemu ya tamasha la Arusha tourism Festival  ambalo linatarajiwa kuwakutanisha wanahabari, wadau wa utalii na wanariadha "alisema
Wanahabari ambao watashiriki kongamano hilo ni kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini, Dar es Salaam, Mara na maeneo mengine yenye vivutio vya utalii.

Na haya ni baadhi ya matukio yaliyotokea katika kongamano la mwaka jana hapa mkoani Arusha

Mwenyekiti wa kamati ya amani mkoa wa Arusha(APET) Petro Ahham akimkabidhi kikombe cha ushindi  wa bonanza la amani na utalii mkoa wa Arusha,nahodha wa timu ya Kitambi Noma, James Lugangira lililofanyika vuwanja vya general tyre jijini arusha
Wanamichezo wa kitambinoma wakiwa wanashabikia ushindi mara baada ya kukabidhiwa kombe katika kiwanja cha General Tyre jijini Arusha

Katibu wa Kamati ya Olympic Taifa.Filbert Bayi akimkabidhi zawadi mwanariadha Fabian Joseph kwa kushika nafasi ya pili michuano ya Arusha tourism Marathon.zawadi ya 250,000

 
Washindi wa mashindano ya riadha ya utalii mita 5000,kuanzia kulia mshindi wa kwanza, Emmanuel GIriki, akifatiwa na Gabriel Geay na mshindi wa tatu Ismail Juma mara baada ya kumaliza mbio hizo katika uwanja wa sheikh Amri Abeid.
Washindi riadha mita 3000 la mashindano ya Utalii, wa kwanza kuanzia kulia, Angelina Tsere, wa pili Jackline Sakito na wa tatu Cesilia Gonoka jana baada ya kumaliza mbio hizo katika uwanja wa sheikh Amri Abeid.
Washiriki wa mashindano ya Utalii ya riadha yaliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mwezi January mwaka huu



Afisa Michezo Mkoa wa Arusha.Mwanmvita Okeng'o akimkabidhi zawadi ya kwanza Angelina Tsere baada ya kushinda Arusha tourism Marathon alizawadiwa sh 500,000.

TUME YA ARDHI KUANZISHA KANZIDATA YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI

December 20, 2017

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) ipo mbioni kuanzisha Kanzidata (Database) ya mipango ya matumizi ya ardhi iliyofanyika nchini na wadau mbalimbali wa sekta ya ardhi.

Kwa kushirikiana na wadau wa upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi wa taasisi za serikali pamoja na asasi za kiraia, Kanzidata hiyo itabeba taarifa zitakazoonyesha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali kama vile kilimo, malisho, huduma za jamiii, n.k itarahisisha utendaji kazi kwa Tume, mamlaka zingine za upangaji, wadau pamoja na wananchi kwa ujumla ambao watatumia teknolojia kujua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali nchi nzima
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya mipango ya matumizi ya Ardhi(NLUPC) Dkt. Stephen Nindi akifungua mkutano wa kikosi kazi kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzidata ya mipango ya matumizi ya ardhi,Mjini Morogoro
Mwenyekiti wa Kikao Bw. Jamboi Baramayegu kutoka ujamaa Community akielezea utaratibu wa namna kazi itakavyofanyika
Afisa Tehama kutoka wakala wa Serikali Mtandao Bw. Thomas Malinga akitoa maelezo ya malengo ya wao kushiriki katika mchakato wa uanzishwaji wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango na matumizi ya ardhi.
Afisa Mipango wa Tume ya Taifa ya mipango ya matumizi ya Ardhi Bw. Gelard Mwakipesile, akielezea kwa kina kwa wajumbe wa mkutano kuhusu mipango ya matumizi ya ardhi,mchakato ulipo anzia hadi kuanza kwa  mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi
 Bw. Paulo Tarimo kutoka Wizara ya Kilimo akichangia jambo wakati wa kikao cha mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi.
 Baadhi ya wanakikosi kazi kutoka sekta mbalimbali wakiendelea na majadiliano ya kutoa maoni yao juu ya kuandaa mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi.
 Katibu Mkuu wa Chama cha wafugaji Tanzania Bw. Magembe Makoye akiwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la wafugaji
 Bw. Godfrey Massay Meneja utetezi kutoka LANDESA  akiwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Kilimo
 Afisa Sheria kutoka NLUPC Bi. Devotha Selukele akichangia jambo wakati makundi mbalimbali wakiwasilisha maoni yao juu ya kanzi data
 Afisa programu kutoka Haki Ardhi Bw. Joseph Kiombola   akiwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Asasi za Kiraia.
 Afisa wanyama pori (TAWA) Bw. Herman Nyanda   akiwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Maliasili
 Afisa Mpelembaji kutoka TNRF Bw. Wilbard   akiwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Utafiti
 Wadau wakiendelea na mkutano huo.
Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa Tanzania