*PROF. MBARAWA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA TEHAMA

April 24, 2014


Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau wa Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia John Mngondo (kulia) akiwa miongoni mwa washiriki wa mkutano wa siku mbili 
wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la Ufa leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Digital Network Oy nchini Finland, Cipa Ojala akisisitiza umuhimu wa mkutano wa wadau wa TEHAMA katika nchi za Bonde la Ufa na msatakabali wa vyombo vya habari ikiwemo televisheni kuhama kutoka analogia kwenda dijiti.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa TEHAMA kutoka nchi za Bonde la Ufa wakimsikiliza Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa TEHAMA kutoka nchi za Bonde la Ufa wakimsikiliza Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (katikati) akisalimiana na baadhi ya washiriki mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam. Picha zote na Eleuteri Mangi MAELEZO

*KUTOKA BUNGE MAALUM LA KATIBA MMOJA AANGUKA KWA PRESHA MJENGONI DODOMA

April 24, 2014

 Wauguzi na Waganga wa Zahanati ya Bunge mjini Dodoma wakitoa msaada wa huduma ya kwanza na kufanya maandalizi ya kumpeleka Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ziana Mohamed Haji katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma leo baada ya kupata matatizo ya  mshutuko.
 Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambapo pia ni Ndugu na Jamaa wa Mjumbe wa Bunge hilo Ziana Mohamed Haji wakijadiliana na watendaji wa Bunge hilo jinsi ya kumsaidia baada ya kupata matatizo ya mshutuko leo mjini Dodoma.
 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambapo pia ni Ndugu na Jamaa wa Mjumbe wa Bunge hilo Ziana Mohamed Haji wakijadiliana na watendaji wa Bunge hilo jinsi ya kumsaidia baada ya kupata matatizo ya mshutuko leo mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiwasili katika Ukumbi wa Mikutano kwa ajili ya kuendelea kujadili Sura ya Kwanza na Sita ya rasimu ya Katiba Mpya leo mjini Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiwasili katika Ukumbi wa Mikutano kwa ajili ya kuendelea kujadili Sura ya Kwanza na Sita ya rasimu ya Katiba Mpya leo mjini Dodoma.
 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Esther Juma (kushoto) na Catherine Saruni (kulia) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma mara baada ya mapumziko ya kujadili Sura ya Kwanza na Sita ya rasimu ya Katiba Mpya.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Saada Mkuya Salum akichangia maoni yake leo mjini Dodoma kuhusu Sura ya Kwanza na Sita ya rasimu ya Katiba mpya.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mizengo Pinda (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na Watendaji wa Bunge na Wajumbe wenzake Nassoro Salim (kulia),Haji Omar Heri(wa tatu kulia), Mohamed Aboud Mohamed(wa pili kushoto) , Dkt. Tereza Huvisa(kushoto) na Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Yahaya Hamis Hamad(wa tatu kushoto) leo mjini Dodoma wakati wa mapumziko mafupi ya kujadili Sura ya Kwanza na Sita ya rasimu ya Katiba mpya. Picha na Ofisi ya Bunge Maalum la Katiba

MKENYA OGWAYO KUCHEZESHA STARS, BURUNDI

April 24, 2014
NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
 Mwamuzi Anthony Ogwayo mwenye beji ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kutoka Kenya ndiye atakayechezesha mechi kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Burundi (Intamba Mu Rugamba) itakayochezwa keshokutwa (Aprili 26 mwaka huu)  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ogwayo katika mechi hiyo ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, atasaidiwa na Gilbert Cheruiyot na Oliver Odhiambo wote pia kutoka Kenya. Mwamuzi wa mezani atakuwa Israel Mujuni wa Tanzania.


Burundi inatarajia kuwasili nchini leo (Aprili 24 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya Kenya Airways na itafanya mazoezi kesho (Aprili 25 mwaka huu) saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa.

Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi hiyo ambayo itakuwa ya kwanza tangu kuanza kwa mpango wa maboresho wa timu hiyo.

Makocha wa timu zote mbili pamoja na manahodha wao kesho (Aprili 25 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia mechi hiyo
.

Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh. 10,000.

ZASWA FC YAWACHAPA MAVETERAN WA MJI WA CHAKE CHAKE MABAO 3-1.

April 24, 2014
Na Masanja Mabula –Pemba .24/04/2014.
 
Timu ya Wandishi wa Habari za Michezo  Zanzibar (ZASWA SC)  imekamilisha ziara yake Kisiwani Pemba kwa kuwafundisha soka Mavetarani   wa Mji wa Chake Chake kwa kuwafunga mabao 3-1, katika mchezo uliopigwa ndani ya dimba la Gombani .
 
Ushindi huo wa tatu kwa timu ya ZASWA SC ni  salamu kwa timu ambazo zitakutana na kikosi hicho cha wanahabari  kwenye michuano ya Kipwita CUP  ambapo ZASWA imepangwa kundi moja na  timu ya Miembeni FC.
 
 Katika mchezo huo  maveterani ndiyo walikuwa wa kwanza kuliona lango la ZASWA Mapema dakika ya 20 kwa bao safi lililofungwa na mchezaji Ali Kibenzi aliyeunganisha vyema krosi iliyotoka winga wa kulia.
 
Hata hivyo furaha ya maveterani ilizimwa mnamo dakika ya 35 baada ya mchezaji Abdul watif kuuwahi mpira uliotemwa na mlinda mlango wa Maveterani hao kufuatia shuti kali la umbali wa mita 28 lililopigwa na kiungo wa ZASWA Kombo Ali Kombo .
 
Kuingia kwa bao hilo kulizidisha ari kwa wachezaji wa ZASWA ambao walionekana kuutawala mchezo hali iliyosababisha  washambuliaji wa ZASWA kuweka kambi ya muda langoni kwa Maveterani hao  .
 
Wakicheza kandanda safi ZASWA waliongeza bao la pili katika 42 ambao liliwekwa ndani ya kamba na Kiungo Hilali   Banka baada ya kuichambua ngome ya maveterani na kisha kuukwamisha mpira ndani ya nyavu .
 
 Wakati akijiandaa kumpisha kiungo Khamis Dadi kuchukua nafasi yake  Kocha Mchezaji wa ZASWA SC Ali Bakar Cheupe aliiandikia timu yake bao la tatu kunako dakika ya 76 , akimalizia pasi ya Hilali Banka aliyekuwa nyota wa mchezo huo .
 
Kikosi hicho cha Wandishi wa Habari za Michezo Zanzibar kimekamilisha ziara yake  Kisiwani  Pemba ambapo kimeshinda michezo mitatu kwa kuzifunga timu za Wilaya ya Wete , Mkoani n Chake Chake huku kukipoteza mchezo katika Wilaya ya Micheweni .