WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APOKEA MSAADA WA SH. MIL. 121.679

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APOKEA MSAADA WA SH. MIL. 121.679

September 16, 2016
m1
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akipokea kiasi cha Shilingi Milioni 1.6 kutoka kwa Mratibu Taifa wa Mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi Bi. Mariam Kilembe wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, kwa ajili ya Kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, leo Bungeni Mjini Dodoma.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa sh. milioni 121.679 ili kusaidia wananchi waliothirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, Jumamosi, Septemba 10, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17.
Msaada huo umetolewa leo (Ijumaa, Septemba 16, 2016) na wadau mbalimbali wakiwemo Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Caspian, Bw. Omid Karambech aliyetoa sh. milioni 100.
Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bordar Limited, Bw. Wu Yahui aliyetoa sh. milioni 20 pamoja na Bi. Mariam Kitembe aliyetoa sh. milioni 1.679 kwa niaba ya Wauguzi walioshiriki mafunzo ya Utafiti wa viashiria na matokeo ya ukimwi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Akipokea msaada huo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Waziri Mkuu amewashukuru kwa michango yao ya fedha na kuwaomba wananchi wengine wajitokeze kwa wingi ili kuwasaidia watu walioathirika na tetemeko hilo ambalo ni kubwa na halijawahi kutokea nchini.
Jumapili, Septemba 11, mwaka huu, Waziri Mkuu alifanya ziara mkoani Kagera ili kuwapa pole waathirika wa tetemeko hilo pamoja na kujionea madhara yaliyojitokeza.
Pia aliongoza maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba kuaga miili ya watu 16 waliofariki kutokana na tetemeko hilo. Aliwaomba wananchi wawe watulivu na kuwaahidi kuwa Serikali itakuwa pamoja nao.
Jumanne, Septemba 13 mwaka huu Waziri Mkuu aliongoza hharambee ya kuchangia waathirika wa teteme hilo na kupokea zaidi ya sh. bilioni 1.4 kutoka kwa mabalozi wa nchi za nje nchini Tanzania na Jumuia ya Wafanyabiashara wa Kitanzania.
Mbali na kusababisha vifo, watu wengine 253 walijeruhiwa na maelfu ya wananchi walikosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1,264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
  1. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, SEPTEMBA 16, 2016

MATUKIO YA BUNGENI MJINI DODOMA LEO.

September 16, 2016
 Spika wa Bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiingia katika ukumbi wa Bunge kuongoza kikao cha saba cha bunge la kumi na moja leo mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha saba cha bunge la kumi na moja ambapo pia alisema kiasi cha shilingi milioni themanini na tano na laki tano zimechangwa kutokana na makato ya posho ya siku moja yawabunge kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
 Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (MB) picha juu ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki wakati wa kikao cha saba cha bunge la kumi na moja leo mjini Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo (MB) akijibu swali bungeni ambapo alisema kuwa serikali itaendelea kupeleka fedha katika serikali za mitaa kwa kuzingatia hali ya makusanyo ya kila mwezi.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akijibu swali bungeni ambapo alitoa wito kwa wabunge kuisaidia kutoa elimu kwa wananchi waliovamia maeneo ya jeshi kuondoka ili kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi baina ya jeshi na wananchi, wakati wa kikao cha saba cha bunge la kumi na moja leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akijibu swali bungeni ambapo alisisitiza kuwa Serikali inatekeleza program ya maendeleo ya Sekta ya maji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, wakati wa kikao cha saba cha Bunge la kumi na moja leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Jumanne Maghembe (MB) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula (MB), wakati wa kikao cha saba cha Bunge la kumi na moja leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mhe. Joseph Haule akiuliza swali bungeni kutaka kujua mikakati ya serikali katika kutatua migogoro baina ya wakulima na wafugaji inayopelekea mauaji ya raia ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi alisema Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaohusika na mauaji ya raia nchini hasa ikiwemo wanaohusika kwenye migogoro hii.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.

Kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini watatu na dereva teksi mmoja: Christopher Bageni ahukumiwa kunyongwa hadi kufa, zombe na wenzie wawili waachiwa huru

September 16, 2016

Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Ilala Christopher Bageni amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya Mahakama ya Rufani Tanzania kutengua hukumu iliyomwachia huru na kumtia hatiani kwa kosa la mauaji ya wafanyabiashara wa madini watatu na dereva teksi mmoja.
Kadhalika mahakama hiyo imewaachia huru  Mkuu wa Upelelezi wa zamani (wakati huo Mkoa wa Dar es Salaam) (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi  mstaafu Abdallah Zombe na wenzake wawili baada ya ushahidi wa rufaa hiyo kushindwa kuwatia hatiani.

Mara baada ya hukumu kusomwa, ghafla Bageni aliduwaa wakati wenzake wakimkumbatia huku  wakibubujikwa na machozi wakiwa kizimbani. 
Wanaodaiwa kuwa wanafamilia wa washtakiwa hao waliangua vilio huku washtakiwa wenzake walisikika wakieleza masikitiko yao. Wengine walisikika wakisema angejua asingekuja mahakamani kusikiliza hukumu hiyo.
“Namshukuru Mungu...Lakini nasikitika kwa Bageni kukutwa na hatia sina raha kabisa....” alisema ASP Makele wakati akitoka katika ukumbi namba moja wa mahakama hiyo. 
Akizungumza baada ya hukumu hiyo,  ACP mstaafu Zombe alisema anamshukuru Mungu na kuhusu Bageni alisema hana cha kuzungumzia.
Hukumu hiyo imesomwa leo na Msajili wa mahakama hiyo Mhe. John Kahyoza baada ya rufani iliyokatwa na upande wa Jamhuri  kusikilizwa na jopo  la majaji watatu likiongozwa na Mwenyekiti, Jaji Bernard Luanda, Jaji Sauda Mjasiri na Jaji Semistocles Kaijage.
Msajili alisema awali Mahakama Kuu iliyoketi chini ya Jaji Salum Massati (wakati huo kabla ya kupanda kuwa jaji wa rufani), ilimuona Zombe na wenzake hawana hatia na kwamba haiwezi kuwahukumu kwa kosa la kusaidia kufanyika mauaji hayo.
Alisema Mahakama ya Rufani inakubaliana na Jaji Massati  kwamba mtuhumiwa hawezi kutiwa hatiani bila kuthibitisha mtu aliyetenda kosa hajashtakiwa na kutiwa hatiani.
“Jopo la majaji wa mahakama hii limeona ushahidi ulioeleza kwamba Bageni alikuwa eneo la tukio na kwamba alikuwa na mamlaka ya kuzuia mauaji yasitokee pamoja na kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba aliona mauaji hayo yaliyofanywa na PC Saadi ambaye hajawahi kushtakiwa na siyo miongoni mwa washtakiwa waliotuhumiwa na mashtaka hayo.” Alisema wakati akichambua hukumu ya rufani hiyo.
Akifafanua zaidi hukumu hiyo alihoji, hakuna ubishi kwamba wafanyabiashara hao wakati wa uhai wao walipelekwa katika msitu wa Pande mahali ambako hakuna makazi ya watu wala nyumba kwa nini?  
“Katika ushahidi inasemekana kwamba Bageni kwa wadhifa aliokuwa nao, aliamrisha askari wa chini yake na gari kuelekea msitu wa Pande… Amri hiyo aliitoa kuelekeza gari hizo mahali ambako hakuna nyumba za kuishi bila sababu za msingi ili tukio ovu liweze kufanyika kwa kibali chake kama mkuu wa upelelezi” alisema msajili.
LIGI KUU YA VODACOM MECHI SITA KESHO

LIGI KUU YA VODACOM MECHI SITA KESHO

September 16, 2016
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2016/2017 inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Septemba 17, 2016 kwa michezo sita ambayo itazikutanisha timu pinzani 12 katika viwanja sita tofauti.

Michezo ya kesho ni Mwadui FC itakayoikaribisha Young Africans kwenye Uwanja wa CCM Kambarage. Mwadui ambayo inaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Stand United wakati Young Africans ina makali ya kuilaza Majimaji ya Songea mabao 3-0.
Mechi nyingine yenye mvuto ni kati ya Tanzania Prisons kuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wakati Azam ambayo inaongoza ligi sawa Simba kwa kuwa zina pointi sawa, zitakutana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Timu za Simba na Azam zina pointi 10 kila moja baada ya kucheza mechi nne ambako kila moja imeshinda mechi tatu na kutoka sare mmoja.
Mtibwa Sugar na Kagera Sugar zinatarajiwa kukutana kwenye Uwanja wa Manungu kwenye mchezo mwingine wa Ligi Kuu. Mtibwa ambayo imetoka kulazwa na Simba Jumapili iliyopita, Kagera inakwenda ugenini Morogoro ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare tasa na Ndanda ambayo pia kesho itakuwa ugenini kucheza na Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji.
Katika mchezo mwingine wa kesho, Ruvu Shgooting itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Keshokutwa Stand United ya Shinyanga itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa CCM Kambarage.
Mzunguko wa tano wa ligi hiyo utafungwa kwa mchezo kati ya African Lyon ya Dar es Salaam dhidi ya Toto African ya Mwanza kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam Jumanne Septemba 20, 2016. African Lyon inaingian uwanjani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuilaza Mbao FC mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

WAREMBO 16 KUWANIA TAJI LA MISS TEMEKE 2016

September 16, 2016

Washiriki wa Miss Temeke 2016 wakifanya mazoezi ya kujiandaa na shindano lao jijini Dar es Salaam. Shindano hilo, litakalofanyika Viwanja vya Sigara TCC Chang'ombe Septemba 24 mwaka huu.

Na Dotto Mwaibale

WAREMBO 16 wanatarajia kupanda jukwaani katika shindano la kumpata Miss Temeke 2016 litakalofanyika Septemba 24 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam  katika mazoezi yao, Mwalimu wa warembo hao Neema Honest alisema warembo wote wapo fiti na wanaendelea vizuri na mazoezi Chang'ombe Sigara TCC.

"Washiriki wote wapo katika hali nzuri na sasa wanaendelea na mazoezi tayari kwa shindano hilo litakalofanyika Chang'ombe Sigara TCC" alisema Honest.

Aliwataja warembo kuwa ni Jesca  Nassary, Diana Nyaki, Juliet Pallangyo, Irene Tomitho, Macrina Kudema, Anitha Mugisha, Khadija Masoud na Sia Kiweru.

Aliwataja wengine kuwa ni Sara Bigambo, Nancy Mushi, Mwantum, Esther Mnaki, Anitha Kisimba na Clara Premsinga.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

MALINZI AMPONGEZA RAIS MPYA UEFA

MALINZI AMPONGEZA RAIS MPYA UEFA

September 16, 2016
Rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Alexander Ceferin kuchaguliwa kuwa Rais Mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Ulaya (UEFA) katika uchaguzi mkuu uliofanyika jijini Athens nchini Ugiriki Jumatano Septemba 14, 2014.

Katika salamu zake, Rais Malinzi ameelezea kuwa kuchaguliwa kwa Ceferin  ambaye ni Rais wa Chama cha Soka Slovakia ni kilelelezo cha familia ya mpira wa miguu ya Ulaya kuona umuhimu wake katika kutumikia shirikishi hilo sambamba na kuwa kiongozi wa FA ya Slovekia.
Rais Malinzi amesema ana imani na Ceferin kuwa ataweza kutumikia vema nafasi zote. Malinzi ana imani Caferin ataunganisha nguvu kwa maendeleo ya soka kwa kushirikiana na Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou.
Ceferin amechaguliwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Michel Platini ambaye alifungiwa na FIFA kwa miaka minane Baada ya kukutwa na kosa la kupokea rushwa ya Pauni 1.3mil.
Rais huyu mpya alimshinda Michael Van Praag Rais wa chama cha mpira cha Uholanzi katika kura zilizopigwa huko Athens. Ceferin atashika kiti hicho cha uraisi mpaka mwaka 2019.

TPSF. Pietro Fiorentini enter partneship to organize private sector workshop on Uganda-Tanzania Crude Oil Pipeline Project

September 16, 2016
The Deputy Director of The Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) (left), Mr Louis P. Accaro speaks to the media on the partnership between TPSF and Pietro Fiorentini to organize private sector workshop on Uganda-Tanzania Crude Oil Pipeline Project on 16th September 2016. The workshop will be held at the Dar es Salaam Serena Hotel on Tuesday, 27th September 2016. At the center is the Director of Pietro Fiorentini (TZ), Mr. Abdulsamad Abdulrahim flanked by the Sales Area Manager, Pietro Fiorentini (Italy), Mr. Davide Moiraghi.

The Director of Pietro Fiorentini (TZ), Mr. Abdulsamad Abdulrahim (Centre) speaks to the media on the partnership between Pietro Fiorentini and Pietro Fiorentini to organize private sector workshop on Uganda-Tanzania Crude Oil Pipeline Project on 16th September 2016. The workshop will be held at the Dar es Salaam Serena Hotel on Tuesday, 27th September 2016. On his right and left are the Deputy Director of TPSF, Mr. Louis Accaro and The Area Sales Manager, Pietro Fiorentini (Italy), Mr. Davide Moiraghi respectively.



·         Workshop to unveil business opportunities available before, during and after pipeline construction, role of value chain and local content

Dar es Salaam, September 16th 2016: The Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) has partnered with Pietro Fiorentini to organize a big workshop private sector workshop in which the technical pipeline team, along with the Senior Management of TOTAL will make a detailed presentation of the Uganda-Tanzania Crude Oil Pipeline Project, that will include the introduction of the project and the potential opportunities that are likely to be tapped by local and international companies. The Technical and Senior Management team will explain how the local workforce will be engaged, what the expected procurement packages entail and the extent to which procurement will be local. Technical and commercial experts who will oversee the entire value chain during this workshop will accompany the TOTAL Senior Management.


The Government of the Republic of Uganda has decided to export its crude oil through a pipeline to be constructed from HoimaDistrict in the South Western Uganda to the port of Tanga in the North Eastern Tanzania.

The crude oil pipeline which will be constructed by Total E&P (French multinational integrated oil and Gas Company and one of the seven "Super Major" oil companies in the world) will cross the Tanzania-Uganda border through several regions of Tanzania from Kagera region down to the Port of Tanga.

Speaking during a press conference held at TPSF offices in Dar es Salaam, TPSF Executive Director, Godfrey Simbeye who was represented by the Deputy CEO OF TPSF, Lois P. Accaro explained that the crude oil pipeline project will provide enormousnumber of business opportunities to various companies, enterprises and individuals in addition to providing employment to many Tanzaniansas well as foreign experts before, during and after the construction.

“The main focus of this workshop is to brief Tanzanians who are interested in participating in the value chains and also to give suppliers the channels, tools and means to harness and cater for this project”, said Simbeye.

Top on the list of priorities for the workshop, explained Simbeye, will be to hearplans on how to preparelocal workforce and engagement of local enterprises to maximize the national economic benefit from this project, a part from the introduction to the project and added that it  will  also address skills shortages in the country, both in technical and professional areas, significant investment required to provide relevant skills tolocal staff and build the capacity of the local supply chain to international standards and project timelines.

The workshop, whose main agenda is to determine opportunities for the successful localization and preparation of value chain for the pipeline project,will be held on Tuesday,27thSeptember 2016 from 0830-1430hrs at the Dar es Salaam Serena Hotel.

According to the CEO,the workshop will also offer an unrivalled opportunity to establish and formalize relationship with key decision makers in other sectors, set out localization plans, and collaboratively formulate a strategy for supply chain development to meet local content goals.

Companies from the following sectors are highly recommended to participate in this workshop:Transport & Logistics (Goods and People), Cement Manufacturing, Bulk Construction Materials, Reinforcement Steel Manufacturing, Light Iron/Steel Products (structural and flat steel), Civil Construction Services, Mechanical Construction Services, Road Construction, Generic Waste Management, Hazardous Waste Management, General Maintenance Services, Production Operations Services, Security Services, Domestic Airline Services, Fuel Wholesale, Manpower Agencies, Catering, Facility Management Services, Food Supply, Work Safety Products, Light Equipment Manufacturing, Technical Consulting Services, Vendors, Furniture Manufacturing, Oil and Gas, Agriculture, Shipping, Land Surveyors and Valuers, Legal Practitioners, Freight Forwarders, Insurers, Fire Fighters, Bankers

In addition to the above sectors any businesses not mentioned above are welcome to attend the workshop.


Registration

Participants will be required to register with Tanzania Private Sector Foundation by filling the available online registration forms. Alternatively, participants can register by email and phone contact as follows: - Ms. Rehema Mtingwa through email address:rehema@tpsftz.org or mobile number +255 784 605 479 and Mr. Onesmo Ngelleshi through email address:oagustine@tpsftz.org or mobile number +255 784 151 434. Deadline for registration is on Monday 26thSeptember, 2016 at 1630hrs. A token registration fee will be charged to share the costs for this workshop.



The token registration fee of TZS 50,000/= only will be for TPSF members and TZS 75,000/= only for non TPSF members. Payment of registration fee should be made through the following Bank Account: Account Name-Tanzania Private Sector Foundation (TPSF); CRDB Bank Account Number 01J 102 704 3900. Also can be made by cash during the event at hotel or at before the event at TPSF Offices.
………………………………………………………………………………….
For Further information, please contact:

Godfrey Simbeye
Executive Director
Tanzania Private Sector Foundation (TPSF)


SENSEI MTSHALI (7TH DAN) ATUA KATIKA SEMINA YA KARATE, MITIHANI KUFANYIKA KESHO JUMAMOSI

September 16, 2016
Sensei Mtshali akirekebisha mkanda wa Sensei Florence Kieti kutoka Mombasa, Kenya.

Sensei Mtshali (kulia) akitoa maelekezo.

Wakati semina ya kimataifa ya Shotokan Karate imeingia katika siku ya tano leo hii hapa kwenye ukumbi wa Don Bosco, Upanga jijini Dar es Salaam, tunashuhudia ujio wa mwalimu mkongwe kabisa wa mchezo huo barani Afrika, Edward Mtshali Sensei (7th Dan) kutoka nchini Afrika Kusini.

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA OZONI DUNIANI

September 16, 2016
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA MAKAMU WA RAIS TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI  ILIYOTOLEWA NA JANUARY Y. MAKAMBA (MB.), WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA
 KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA HIFADHI YA TABAKA LA OZONI
16 SEPTEMBA, 2016



 Ndugu Wananchi,
  1. Tarehe 16 Septemba mwaka huu tutaungana na Jumuiya ya Kimataifa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni kama ilivyoagizwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Azimio lake nambari 49/114 la tarehe 19 Desemba 1998 kama kumbukumbu ya tarehe ya kutiwa saini Mkataba wa Montreal (Montreal Protocol - 1987) kuhusu kemikali zinazomongonyoa Tabaka la Hewa ya Ozoni angani.

Ozoni ni hewa iliyoko kwenye angahewa ya juu, takribani kilometa 10 hadi 50 juu ya ardhi. Kazi yake kubwa ni kuchuja sehemu kubwa ya mnururisho wa mionzi kama “Ultraviolet B” isifike kwenye uso wa dunia. Ujumbe wa mwaka huu ni “Kuhuisha Tabaka la Ozoni na Tabia-Nchi kwa pamoja Duniani”. Ujumbe huu umeambatana na Kauli mbiu isemayo “Kukabiliana na ongezeko la gesi  Joto  Duniani  HFCs chini ya  Itifaki ya Montreal”.

  1. Tabaka la Ozoni linapoharibiwa huchangia kuruhusu mionzi zaidi ya Ultraviolet B kufika kwenye uso wa dunia na hivyo kusababisha kuongezeka kwa magonjwa kama vile saratani ya ngozi, uharibifu wa macho yaani "mtoto wa jicho" unaosababisha upofu, upungufu wa kinga dhidi ya maradhi na kujikunja kwa ngozi. Aidha, madhara mengine ni kuharibika kwa mimea hasa mazao ya kilimo kutokana na kuathirika kwa maumbile na mifumo ya ukuaji. Vile vile, baadhi ya kemikali hizi husababisha kuongezeka kwa joto duniani na hivyo kuchangia katika mabadiliko ya tabianchi.