HATIMAYE FILAMU YA KUSISIMUA YA MBINGU YA WAKOSEFU YAINGIA MTAANI PATA NAKALA YAKO KWA TSH 5,000 TU

September 18, 2016
 Hii ndio Filamu yenyewe ya Mbingu ya Wakosefu  
Ili kupata nakala yako tafadhali wasiliana nasi kwa kutumia namba 0713455232
 Mkurugenzi Mkuu wa Mwamba's Film Casting  Stephen Mapunda akiwa na CD za Mbingu ya Wakosefu
 Msimamizi Mkuu wa Blogs za Mikoa Tanzania Fredy Anthony Njeje  akiwa na DVD zake za Mbingu ya Wakosefu
 Mmoja wa vijana wa Mwamba's Film Casting Montana akiwa tayari kuelekea kusambaza DVD hii sehemu mbalimbali
 Faith anakwambia "Bado haujachelewa kupata nakala yako ya Mbingu ya Wakosefu ambayo ambapo utajifunza mengi"
 Kijana Juma ambaye yupo Mwamba's Firm Casting  akiwa na DVD ya Mbingu ya Wakosefu 
Mwanadada Lilian Michael anasema "Filamu hii ya Mbingu ya wakosefu inamafunzo tosha sana kwa watu wa rika zote hivyo si ya kuikosa"
 Kijana Samson Tarimo nae anasema kwamba "Kijana na watu wa zima kwa kuangalia Filamu hii utapata chakula cha Ubongo na kujifunza mengi"
 Filamu hii kwa hakika sio ya kuikosa kabisa , na utafikishiwa pale ulipo
 Mmoja wa wateja Atrey (Kusoto) akipata DVD yake ya Mbingu ya Wakosefu
 Bi dada nae akipata Filamu yake ya Mbinu ya Wakosefu kutoka wa Faith
Waaaah.....
Watembelee hapa http://mwambasfilmcasting.blogspot.com  kuona Shughuli zao za mazozi
Picha zote na Fredy Njeje


“ZAIDI YA WATOTO 4000 WENYE VICHWA VIKUBWA NA MGONGO WAZI HUZALIWA KILA MWAKA NCHINI LAKINI WANAORIPITIWA HOSPITALINI SI ZAIDI YA 500”

September 18, 2016

ZAIDI ya Watoto 4000 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi huzaliwa kila mwaka nchini na wanaoripotiwa hospitalini si zaidi ya 500 hatua ambayo imechangia kwa asilimia kubwa ongezeko la watoto wenye mtindio wa ubongo huku baadhi yao wakipoteza maisha kwa sababu ya kukosa Tiba.
 
Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakazi wa zoezi la Upasuaji wa watoto hao lilipokuwa likiendeshwa na madaktari Bingwa, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji ya (MOI)iliyopo Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili,Dkt Othman Kiloloma alisema ongezeko la watoto hao linatokana na ukosefu wa lishe yenye virutubisho vijulikanavyo kwa jina la “Folic Acid”
Alisema kukosekana kwa lishe hiyo kumesababisha tatizo hilo kwa watoto ambalo lisipopatiwa ufumbuzi wa kina linaweza kupelekea athari kubwa kwao ikiwemo vifo hali inayoweza kupunguza jamii ambayo ingeweza kuchangia ukuaji wa uchumi katika shughuli za uzalishaji.
  “Ukiangalia kwa hivi sasa zaidi ya watoto wapato 4000 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi huzaliwa kila mwaka nchini na wanaoripotiwa hospitalini si zaidi ya 500 hatua ambayo imechangia kwa asilimia kubwa ongezeko la watoto wenye mtindio wa ubongo huku baadhi yao wakipoteza maisha kwa sababu ya kukosa hivyo jamii inapaswa inapaswa kuwapeleka katika Hospitali ili kuweza kuchangia ukuaji wao na maendeleo “Alisema
Akizungumzia kuhusu changamoto zinazosababisha watoto hao kukosa huduma za upasuaji, Afisa Habari wa Taasisi ya Afya inayojihusisha na Upasuaji wa watoto hao, Khalfani Kiwamba alisema kuwa upungufu wa madaktari wenye taaluma ya upasuaji wa waathirika hao ni mkubwa kwa sababu nchini wapo saba ambapo sita wapo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na mmoja yupo hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Bugando
Kufuatia hatua hito, Viongozi wa Taasisi za dini nchini zimeshauriwa kuwahamasisha waumini wao wenye watoto wa aina hiyo kuwafikisha katika Hospitali kubwa za Rufaa ili waweze kushauriwa badala ya kuwaficha watoto hao majumbani ambapo wanapofikisha miaka kumi na kuendelea uwezekano wa kupoteza maisha ni mkubwa sana.
 “Kwani hatua hiyo imechangia kwa asilimia kubwa ongezeko la watoto wenye mtindio wa ubongo huku baadhi yao wakipoteza maisha kwa sababu ya kukosa tiba “Alisema
Awali akizungumza katika zoezi hilo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Godwin Gondwe aliipongeza taasisi inayojihusisha kusaidia sekta ya Afya na Elimu hapa nchini (GSM) kwa kutoa matibabu ya upasuaji huo kwa watoto hali ambayo itawasaidia kuweza kurejea kwenye hali zao za kawaida.
Alisema katika suala kama hilo jamii haina budi kuacha kuwaficha watoto wenye matatizo hayo badala yake waona namna ya kuwasiliana na viongozi wao ngazi za chini kuwaepusha na vifo ambavyo vinaweza kuwakumba kutokana na hali walizonazo.

  “Lakini pia lazima jamii ibadilike kuona umuhimu wa kuacha kuwaficha watoto wenye matatizo hayo badala yake wawapeleke kwenye hospitali zilizopo karibu nao kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambayo yatawasaidia kupona “Alisema.

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam,Dkt Othumani Kiloloma kulia akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Godwin Gondwe  kushoto ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni alipotembelea Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kunapofanyika zoezi la upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi lililofanywa na Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI)

 Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma kulia akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Godwin Gondwe  kushoto ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni alipotembelea Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kunapofanyika zoezi la upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi lililofanywa na Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga,Dkt Karia

 Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(RAS) Zena Saidi akisisitiza jambo wakati Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Godwin Gondwe kushoto mwenye shuti nyeusi alipotembelea kuona zoezi la upasuaji upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi lililofanywa na Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) chini ya Ufadhili wa Taasisi ya GSM wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe akitoa nauli kwa mmoja kati ya wakazi wa wilaya ya Handeni ambaye alikwenda kupata matibabu ya mtoto wake mwenye kichwa kikubwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kwa ajili ya matibabu yanayotolewa na  Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI)chini ya Ushirikiana wa Taasisi ya GMS kulia kwake ni  Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma

  Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma akimjulia hali mmoja kati ya watoto wenye matatizo ya migongo wazi wakati wa zoezi la
upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi lililofanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kwa ajili ya matibabu yanayotolewa na  Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI)

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(Ras) Mhandisi Zena Saidi akitoa zawadi kwa mama wa mtoto Salehe Abdallah ambaye amelazwa kwenye wodi ya wakina mama na watoto kwenye hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya upasuaji wa mgongo wazi na vichwa vikubwa unaofanywa na Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) ya Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili chini ya Ufadhili wa GSM.
 Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(Ras)Mhandisi Zena Saidi na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Godwin Gondwe
 Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma akiwaonyesha Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Godwin Gondwe kulia na Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi namna mtoto aliyekuwa na kichwa kikubwa alivyofanyiwa upasuaji

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(Ras) Mhandisi Zena Saidi akitoa zawadi kwa mama wa mtotoambaye alifanyiwa upasuaji wa kichwa
 Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma akisisitiza jambo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi

 Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma akimuangalia mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma kushoto akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Godwin Gondwe na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi mara baada ya kufanyika zoezi la upasuaji wa kwa watoto wenye mgongwa wazi na vichwa vikubwa

 Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma aksisitiza jambo kwa viongozi hao kuhusiana na huduma hizo
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma akizungumza na waandishi wa habari
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Taasisi ya  GSM mara baada ya kufanyika zoezi la upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi lililofanywa na Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar Es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni akitazama jambo mara baada ya kumalizika zoezi la upasuaji huo