SERIKALI YATOA BARAKA SHINDANO LA MISS TANZANIA,SASA RASMI KUBEBA SURA YA NCHI

March 31, 2018


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea mpango mkakati wa Mashindano ya urembo nchini (Miss Tanzania) kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi ambaye sasa ndiye muendeshaji wa Mashindano hayo. Serikali imetoa baraka zake kwa uongozi wa The Look Company Limited kwa nia yake ya kurudisha heshima, hadhi na mvuto wa tasnia ya urembo hapa nchini kupitia Mashindano hayo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) na Naibu wake, Juliana Shonza (kushoto) wakifurahi jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi baada ya mazungumzo yao, jana katika ofisi za Ukombozi wa bara la Afrika, zilizopo Garden avenue, Jijini Dar es salaam.

MAASKOFU,WACHUNGUJI KANDA YA ZIWA WABARIKI TAMASHA LA PASAKA 2018,WAMPONGEZA MSAMA PROMOTIONS.

March 31, 2018


Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo mbele ya Maaskofu na Wachungaji wa mkoa wa jiji la Mwanza mapema leo jijini humo kuhusu upokeo na maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika hapo kesho Aprili Mosi,ndani ya uwanja wa CCM Kirumba mkoani humo.
MKurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na Maaskofu na Wachungaji wa mkoa wa jiji la Mwanza mapema leo kwenye moja ya hoteli jijini humo,akieleza kukamilika rasmi kwa maandalizi ya tamasha la pasaka,linalotarajiwa kufanyika hapo kesho Aprili Mosi katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani humo.

Msama amewashukuru Maaskofu hao na Wachungaji kwa kujitoa na kuunga mkono Tamasha la Pasaka 2018,ambalo kwa mara ya kwanza linaanzia kufanyika jijini Mwanza na baadae kuhamia mkoa wa Simiyu ndani ya mji wa Bariadi April 2 ndani ya uwanja wa Halmashauri,aidha tamasha hilo litakuwa na waimbaji lukuki ambao tayari wameishatangazwa kushiriki,kuhakikisha tamasha hilo linafana.

Kwa upande wa Maaskofu wameipongeza Kampuni ya Msama Promotions,chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama kwa kuupa mkoa wa Mwanza kipaumbele kwa kuleta tamasha hilo mkoani humo,Wameongeza kuwa tamasha hilo litawavuta waumini wengi na wapenzi wa muziki wa injili na kuwaleta pamoja ili kupata neno la mungu na uponyaji kwa njia ya uinjilisti wa nyimbo za injili .





katika picha kutoka kushoto ni Askofu Charles Sekelwa Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Mwanza na Askofu Zenobius Isaya kutoka kanisa la Philadephia Gospel Asembly na mlezi wa Msama Promotion Kanda ya Ziwa.


Askofu Zenobius Isaya kutoka kanisa la Philadephia Gospel Asembly na mlezi wa kampuni ya Msama Promotion Kanda ya Ziwa,akitoa ufafanuzi wa namna tamasha hilo la Pasaka 2018 lilipofikia na maandalizi yake kwa ujumla,mbele ya kikao cha Maaskofu na Wachungaji kilichofanyika mapema leo jijini humo,kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama na kushoto ni Askofu Charles Sekelwa Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Mwanza.



Mmoja wa maaskofu akitoa mchango wake katika kikao hicho kilichofanyika jijini Mwanza leo.
Askofu Joyce Mangu wa kanisa la Calvary Assemblies Of God Mjini Kati jijini Mwanza akizungumza wakati akitoa mchango wake katika kuboresha tamasha hilo siku za usoni na kwamba amefurahishwa sana na ujio wa tamasha hilo kwa jiji la Mwanza.




Baadhi ya maaskofu na wachungaji wakifuatilia kikao hicho.
-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.