TEHAMA YAKUZA UFANISI MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA (TPA)

June 09, 2017

Serikali Mtandao inarahisisha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma. Usikose kuangalia kipindi hiki cha Seikali Mtandao katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) uone jinsi wanavyotumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika kazi zao za kila siku.

SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) IMETOA GAWIWO LA SHILINGI BILIONI 1.7 KWA SERIKALI

June 09, 2017
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Sam Kamanga, akizungumza jambo wakati wa tukio la Shirika hilo kukabidhi gawiwo kwa Serikali, kiasi cha Sh. Bil. 1.7, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha, mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (MB) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Sam Kamanga, katika hafla ya makabidhiano ya gawiwo la Sh. Bil.1.7 liyofanyika mjini Dodoma.
Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakishiriki tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuikabidhi Serikali gawiwo la Sh. Bil. 1.7 baada ya Shirika hilo kufanya vizuri kibiashara katika Mwaka wa Fedha 2016/2017, tukio lililofanyika makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, mjini Dodom
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika, akifurahia jambo wakati wa tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuikabidhi Serikali gawiwo la Sh. Bil. 1.7 baada ya Shirika hilo kupata faida katika mwaka wa fedha 2016/2017
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akisisitiza jambo wakati wa tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kukabidhi Serikalini gawiwo la Sh. bil. 1.7, baada ya Shirika hilo kupata faida kibiashara katika mwaka wa Fedha 2016/2017, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma

ORIFLAME YASHEREHEKEA MIAKA 50 YA UTOAJI HUDUMA NA UUZAJI BIDHAA ZAKE ZA VIPODOZI DUNIAN

June 09, 2017
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kusheherekea miaka 50 ya kampuni hiyo katika utoaji huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani. Wapili kushoto ni Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Katarina Rangnitt, Mtaalamu wa masuala ya siasa na biashara kutoka ubalozini, Ludvig Bontell na Meneja Masoko wa Oriflame Afrika Mashariki, Mary Riungu.
 Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Katarina Rangnitt (wapili kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kutimiza miaka 50 ya kampuni hiyo katika utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra,Mtaalamu wa masuala ya siasa na biashara kutoka ubalozini, Ludvig Bontell na Meneja Masoko wa Oriflame Afrika Mashariki, Mary Riungu. 
 Meneja Masoko wa Oriflame Afrika Mashariki, Mary Riungu jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kutimiza miaka 50 ya kampuni hiyo katika utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani. Wapili Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Katarina. 
 Balozi wa bidhaa za Oriflame Tanzania, Missie Popular akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kutambulishwa na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo katika nchi za Afrika Mashariki, Mary Riungu wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani.

Baadhi ya wadau waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 50 ya utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za Oriflame, wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na viongozi wakuu wa Kampuni hiyo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA VENANCE NESTORY)

WANACHUO 592 KUTOKA CHUO CHA MIPANGO NA ST. JOHN DODOMA,WAPEWA ELIMU KUHUSU PSPF NA KUJIUNGA NA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI (PSS)

June 09, 2017

Afisa Matekelezo kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Albert Feruzi akitoa elimu kuhusu Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa wanafunzi wa Chuo cha St. John Dodoma hivi karibuni.

SHIRIKA LA BRAC LAKABIDHI VIFAA VYA MILIONI 153 KWA WASICHANA WAJASIRIAMALI 700 TANGA.

June 09, 2017
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa halfa ya shirika la BRAC kuwakabidhi vifaa vyenye thamani ya milioni 153 wasichana wajasiriamali kutoka Mkoani Tanga kulia ni Meneja Mipango wa Elimu kutoka BRAC Tanzania Amina Shabani kushoto ni Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee
Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee akizungumza katika Halfa hiyo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi

Meneja Mipango wa Elimu kutoka BRAC Tanzania Amina Shabani akizungumza katika halfa hiyo

Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali katika halfa hiyo
 Mmoja kati ya wasichana wanaoishi kwenye mazingira magumu ambao wamejengewa uwezo na kupata fursa ya kujiendelea kukuza na kujiendeleza kiuchumi Aisha Mohamed akiishuru Brac kwa kuwawezesha ili waweze kukabiliana na maisha bnaada ya kupatiwa mafunzo
 Baadhi ya wananchi na wazazi wa wasichana wakifuatilia matukio mbalimbali ya makabidhiano vifaa vyenye thamani ya sh.,milioni 153 wasichana wajasiriamali 700 kutoka mkoani Tanga ili waweze kujikwamua kiuchumi
 Baadhi ya wananchi na wazazi wa wasichana wakifuatilia matukio mbalimbali ya makabidhiano vifaa vyenye thamani ya sh.,milioni 153 wasichana wajasiriamali 700 kutoka mkoani Tanga ili waweze kujikwamua kiuchumi
Walimu ambao walikuwa wakiwafundisha wasichana hao masuala mbalimbali ya ujasiriamali wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa halfa hiyo

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wasichana wajasiriamali 700 mkoani hapa ambao walikabidhiwa vifaa vyenye thamani ya milioni 153 ambavyo ni vyerahani 90,mashine za kukaushia nywele 90,vifaa vya ufugaji wa kuku,vifaa vya kilimo,vifaa vya upishi,vifaa vya kwa ajili ya utengenezaji wa batiki na mabegi ya kike
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wasichana wajasiriamali 700 mkoani hapa ambao walikabidhiwa vifaa vyenye thamani ya milioni 153 ambavyo ni vyerahani 90,mashine za kukaushia nywele 90,vifaa vya ufugaji wa kuku,vifaa vya kilimo,vifaa vya upishi,vifaa vya kwa ajili ya utengenezaji wa batiki na mabegi ya kike
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wasichana wajasiriamali 700 mkoani hapa ambao walikabidhiwa vifaa vyenye thamani ya milioni 153 ambavyo ni vyerahani 90,mashine za kukaushia nywele 90,vifaa vya ufugaji wa kuku,vifaa vya kilimo,vifaa vya upishi,vifaa vya kwa ajili ya utengenezaji wa batiki na mabegi ya kike
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kushoto akimkabidhi cherehani cha kusonea nguo Aisha Mohamed wakati alipokwenda kuwakabidhi vifaa vyenye thamani ya sh.milioni 153 wasichana wajasiriamali 700 vilivyotolewa na Shirika la BRAC kwa wasichana waliopata mafunzo ya ujasiriamali na shirika hilo
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kushoto akimkabidhi mashine ya kukaushia nywele mwanafunzi Thabituwa Shabani wakati wa halfa hiyo kulia ni Meneja Mipango wa Elimu kutoka BRAC Tanzania Amina Shaban
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi katikati akikabidhi mabegi ya kike kwa wasichana 700 wa mkoa wa Tanga kushoto ni Meneja Mipango wa Elimu kutoka BRAC Tanzania Amina Shabani

MPINA ATOKEA TAARIFA YA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

June 09, 2017
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina katikati, akiongea wakati wa kupokea taarifa ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais kutoka kwa mwakilishi wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Injinia Mtapuli Juma (hayupo katika Picha) katika Ofisi hiyo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam Leo, kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Muungano wa Ofisi Hiyo Bw. Baraka Baraka.
Kulia Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na kushoto ni mkurugenzi wa Idara ya Muungano wa Ofisi hiyo wakifuatilia Taarifa ya ujenzi wa jengo ikitolewa na Injinia Mtapuli Juma hayupo katika picha kutoka wakala wa majengo nchini (TBA)
Injinia Mtapuli Juma kutoka wakala wa majengo nchini (TBA) akiwasilisha taarifa ya jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais leo katika ofisi hiyo jijini Dar es Salaam

 Kushoto Mkurugenzi wa Manunuzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Monica Kasuma akiongea jambo katika kikao cha kupokea Taarifa ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi hiyo Jijini Dar es Salaam Leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Ofisi hiyo Bi Mary Fidelis ( Picha na Evelyn Mkokoi w Ofisi ya Makamu wa Rais.)
 Sehemu ya Washiki katika Picha wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais katika kikao kilichofanyika Ofisini hapo jijini Dar es Salaam leo.

WAAMUZI WA DJIBOUTI KUCHEZESHA TAIFA STARS v LESOTHO

June 09, 2017
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limetangaza wamuzi wa mchezo kati ya Tanzania na Lesotho unaotarajiwa kufanyika Jumamosi Juni 10, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa CAF, waamuzi hao ni Abdillah Mahamoud - atakayekuwa mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Gamaladen Abdi na Farhan Bogoreth wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Twagirumukiza Abdoulkarim kutoka Rwanda huku Kamishna akiwa ni Amir Hassan wa Somalia

Waamuzi hao pamoja na kamishna wanatarajiwa kufika Dar es Salaam, Tanzania kesho Ijumaa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) wakati wapinzani wa Taifa Stars wanaingia jioni ya saa 11.55 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini. Timu hiyo itafikia Hoteli ya Southern Sun, Dar es Salaam.

Mchezo kati ya Taifa Stars na Lesotho, utafanyika kuanzia saa 2.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam uliko Chamazi, Dar es Salaam na ili kuwapa fursa Watanzania wengi kushuhudia mchezo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeondoka kiingilio cha Sh 15,000.

Hivyo sasa Viingilio katika mchezo huo vitakuwa ni Sh 10,000 kwa Jukwaa Kuu wakati mzunguko itakuwa ni Sh 5,000.

Kujiandaa na Mchezo huo Taifa Stars ilipiga kambi hapa nchini kuanzia Mei 23, mwaka huu kabla ya kwenda Alexandria, Kaskazini kabisa mwa nchi ya Misri ambako ilipiga kambi ya wiki. Kambi hiyo ilifurahiwa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga.

Mchezo huo dhidi ya Lesotho utakuwa ni wa kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi ‘L’ kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.

Mbali ya Lesotho na Tanzania, mataifa mengine katika Kundi ‘L’ ni Uganda na Cape Verde ambao pia wikiendi ya Juni 9, 10 na 11, mwaka huu watakuwa katika mchezo wa kwanza pia kuwania nafasi hiyo.

MSANII IRENE VEDA AULA UBALOZI WA UTALII KUPITIA BODI YA TAIFA YA UTALII TANZANIA (TTB)

June 09, 2017
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) Bi. Devotha Mdachi(kulia) Akimkabidhi mkataba Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda mara baada ya kusaini.
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) Bi. Devotha Mdachi(kulia) akimwelekeza Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda sehemu za kusaini mkataba wake wa miaka miwili.
Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda(kushoto) akiendelea kusaini mkataba wake .
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) Bi. Devotha Mdachi(kulia) akimalizia kumwelezea Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda sehemu za mwisho za kusaini katika Mkataba huo.
Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda akimalizia kusaini Mkataba wake ili kuanza rasmi kazi za kupeperusha Bendera ya kutangaza Utalii nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) Bi. Devotha Mdachi(kulia) pamoja na Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda wakionesha Mikataba yao baada ya kumaliza kusaini.
Kuona kazi ambazo ameanza kuzifanya bofya

Instagram: www.instagram.com/twendetukataliitz

 Twitter: www.twitter.com/TukataliiTz 

Facebook: www.facebook.com/TwendeTukataliiTz



DC MUHEZA AFUTURISHA WAKAZI WA WILAYA HIYO.

June 09, 2017
 Wageni wilayani Muheza Mkoani Tanga wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi,Hajat Mwanasha Tumbo 
  Wageni wilayani Muheza Mkoani Tanga wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi,Hajat Mwanasha Tumbo 
  Wageni wilayani Muheza Mkoani Tanga wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi,Hajat Mwanasha Tumbo 
 MKUU wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi katikati anayefuatia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza (DAS) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Luiza Mlelwa wakipata futari iliyoandaliwa na mkuu huyo wa wilaya nyumbani kwake.
 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu huyo wa wilaya.
 Baadhi ya waalikwa wakipata futari hiyo
 Baadhi ya wageni waalikwa wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo
 Wageni waalikwa wakipata futari nyumbani kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza.

 Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Muheza,Makame Seif katikati akiwahudumia wageni waalikuwa kwenye futari hiyo anayepokea chai ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew Mganga
 Waalikwa wakipata futari hiyo wa pili kutoka kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,MathewMganga
Wageni waalikuwa kwenye futari hiyo katikati ni Amina Omari Mwandishi wa gazeti la Mtanzania Mkoa wa Tanga na kulia ni Mariam Shedafa kutoka Azam TV Tanga
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa katikati akiwa na wageni wengine wakishiriki kwenye futari hiyo ambayo iliandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo 
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na waandishi wa habari ambapo alitoa shukrani kwa kuitikia mwitikio wa futari hiyo
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akiagana na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika futari hiyo.