March 12, 2014

Tanzania Kuwa na Ubalozi wa Tanzania Nchini Korea

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda akimweleza Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon, Mipango mbalimbali inayofanywa na Tanzania kuimarisha uhusiano na Korea Ikiwamo ufunguaji wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Korea, wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon akimweleza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda mpango wa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala yatakayochangia maendeleo kwa nchi na wananchi husika.
March 12, 2014

Megawati 150 kuongezeka katika Gridi ya Taifa

1 (3)Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Uwekezaji Mhandisi Decklan  Mhaiki (katikati) akimweleza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo  (kushoto) pamoja na Waandishi wa habari moja ya mashine za kufua Umeme zitakazofungwa katika  eneo la Kinyerezi I jijini, Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Mradi wa ujenzi huo, Bw. Shaun Moore.
2 (1)Mmoja wa mitambo ya kufua umeme ambao utafungwa katika eneo la Kinyerezi I mara baada ya ujenzi kukamilika. Mitambo hiyo, inatarajiwa kuzalisha kiasi cha megawati za umeme 150 ambazo zitaunganishwa katika gridi ya Taifa.
March 12, 2014

MHE. PINDA AKUTANA NA WAZIRI WA UCHUKUZI WA BURUNDI NA MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE YA BUNGE LA JAMHURI YA KOREA

PG4A1670 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na   Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya  Mambo ya Nje na Muungano wa Jamhuri ya Korea, Ahn Hong Joon (kulia kwake) na msafara wake baada ya mazungumzo, kwenye makazi ya Waziri Mkuumjini Dodoma Machi 12, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
March 12, 2014

MWENYEKITI TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI AELEZEA MAANDALIZI YA MWISHO UCHAGUZI KALENGA

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji  Mstaafu Damian Lubuva akifafanua jambo kwa msisitizo kuhusia na maandalizi ya mwisho ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, unaotarajiwa kufanyika Machi 16, mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya Siasa,vyombo vya usalama na wadau wengine
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji  Mstaafu Damian Lubuva akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo,kuhusu uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga katika kikao cha pamoja na vyama vilivyosimamisha wagombea kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo ulioko Halmashauri ya wilaya ya Iringa Vijijini.Uchaguzi wa Jimbo hilo unatarajiwa kufanyika Machi 16.Ambapo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ameeleza kuwa idadi ya wapiga kura jumla yao ni 71,765.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji  Mstaafu Damian Lubuva akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid kwenye mkutano uliohusu kupeana taarifa ya maandalizi ya mwisho ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga,unaotarajiwa kufanyika Machi 16,mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya Siasa,vyombo vya usalama na wadau wengine,mkutano huo umefanyika leo asubuhi kwenye ukumbi wa Siasa ni Kilimo zilizomo ndani ya Ofisi za Halmashauri Wilaya ya Iringa.
March 12, 2014
Stori: Makongoro Oging’ na Harun Sanchawa
MAJONZI, huzuni na masikitiko vimeikumba familia ya Lwena kufuatia mtoto wao mpendwa Dorryce Lwena (27) kufariki dunia kwa kupigwa risasi mkono wa kushoto na ubavu wa kushoto na watu wasiojulikana, Uwazi lilifuatilia.


Jeneza lenye mwili wa Dorryce Lwena.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea mwanzoni mwa mwezi huu, saa tatu usiku, Uwanja wa Edosi, Kitunda, Ilala hatua chache kutoka nyumbani kwa marehemu huyo.