NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI,DK.MEDARD KALEMANI AZINDUA MRADI WA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI MKOA WA SHINYANGA AWAMU YA TATU

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI,DK.MEDARD KALEMANI AZINDUA MRADI WA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI MKOA WA SHINYANGA AWAMU YA TATU

April 02, 2017

A 1
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani akizungumza na wananchi kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu jana wakati wa uzinduzi wa mradi wa kusambaza umeme vijiji katika mkoa wa Shinyanga awamu ya tatu.
A 2
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani akibonyeza kitufe kuwasha kifaa maalumu cha Umeme Tayari (UMETA) kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu jana wakati wa uzinduzi wa mradi wa kusambaza umeme vijiji katika mkoa wa Shinyanga awamu ya tatu jana.
A 3
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani (katikati) akikata utepe jana kuashiria uzinduzi wa mradi wa kusambaza umeme vijiji katika mkoa wa Shinyanga awamu ya tatu jana kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu.
A 4
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack katika uzinduzi wa mradi wa kusambaza umeme vijijini.
A 6
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga akizungumza.
A 5
Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi akizungumza na wananchi baada ya kutambulishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (pembeni yake).
A 7
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani akifurahia ngoma na kikundi cha utamaduni wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
A 8
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani akimzawadia kifaa maalumu cha Umeme Tayari (UMETA) ambacho kinatumika bila utandazaji nyaya (wiring) katika nyumba, mkazi wa kijiji cha Negezi wakati wa uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini.

FNB KUTOZA GHARAMA MOJA KWA MIAMALA YA KIBENK

April 02, 2017
 Mkuu wa Huduma za Rejareja wa First National Bank, Bw. Francois Botha (Kushoto) na Mkuu wa Matawi na za Huduma za kibenki, Bw. Kitumari Massawe (Kulia) wakishilia Bango wakati wa mkutano na waandishi wa habari kama ishara ya kuanzisha huduma ya kutoza gharama moja kwa miamala ya kibenki kwa wateja wake ambao wana akaunti ya Gold ya Hundi. (Picha: Mpiga Picha Wetu)
Mkuu wa Matawi na Huduma za Kibenki, Bw. Kitumari Massawe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya faida ya akaunti ya Gold ya Hundi ambapo wateja watalipa shillingi elfu kumi na sita kwa mwezi ambayo ni gharama moja na kuondoa adha na utaratibu wa kulipa huduma kwa muamala mmoja mmoja.( Kushoto) ni Mkuu wa Huduma za Rejareja wa Benki hiyo, Bw. Francois Botha na Meneja Masoko wa First National Bank, Bi. Blandina Mwachang’a (Kulia).
Mkuu wa Huduma za Rejareja wa First National Bank, Bw. Francois Botha ( Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, na kutangaza benki hiyo kuanza kutoza gharama moja kwa miamala mbalimbali kwa wateja wake ambao wanatumia akaunti ya Gold ya Hundi. ( Kushoto ) ni Mkuu wa Matawi na Huduma za kibenki wa First National Bank, Kitumari Massawe. --- First National Bank Tanzania imetangaza kuanza kutoza gharama moja kwa miamala mbalimbali kwa wateja wake ambao wana akaunti ya Gold ya hundi ikiwa ni mojawapo ya jitihada za benki hiyo kuwapa unafuu watumiaji wa huduma za kibenki. Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha amesema jijini Dar es salaam leo kwamba benki hiyo itawapatia wateja wake fursa ya kufanya miamala mbalimbali ya huduma za kibenki mara nyingi wawezavyo kwa gharama moja iliojumuishwa na bila kulipa gharama za ziada. “Wateja watalipa shilingi elfu kumi na sita tu kwa mwezi ambayo ni gharama moja, hii itaondoa adha na utaratibu wa kulipia huduma kwa muamala mmoja mmoja. Mpango huu unatarajiwa kuwanufaisha wateja wetu kwa kuwapunguzia gharama za miamala huku wakitumia fedha hizo kujiongezea akiba zaidi kwenye akaunti zao. Hatua hii ni ya faida kubwa kwa wateja wetu wa akaunti ya Gold ya hundi na wateja wengine kwa ujumla”. Mpango wa gharama moja kwa miamala utajumuisha utoaji wa fedha kwenye ATM yoyote, miamala ya TigoPesa, malipo ya bidhaa kama DSTV, LUKU na muda wa maongezi, kuweka maelezo ya kuhamisha fedha toka kwenye akaunti, kufanya manunuzi ya bidhaa kwa kutumia kadi katika vituo vya mauzo popote duniani, pamoja na kuweka fedha taslimu na hundi kwenye akaunti ikiwemo kwenye mpango huu. -- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

MKUTANO NA WANAHABARI KUHUSU SHINDANO LA HOJA JUU YA SIFA ZA RAIS BORA WA NCHI KAMA TANZANIA

April 02, 2017
 
TAREHE 1 APRILI, 2017 WASHINGTON
Ndugu Wanahabari na Watanzania wenzangu;
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa fursa hii. Pia niwashukuru ninyi nyote mlioweza kufika hapa. Vilevile nawashukuru wote walioanza kuunga mkono harakati hizi na hatimae tumeweza kufikia hatua hii ya kuwepo kwa mkutano huu muhimu sana katika mstakabali wa taifa letu.
Ndugu Wanahabari na Watanzania wenzangu;
Tumekutana hapa kwa nia ya kukumbushana sisi kwa sisi, wapi hapajakaa sawa na ni vipi tutaweza kurekebisha kwa haraka, ili taifa letu liwe katika hali ya kuridhisha na kuheshimika.
Katika kutimiza nia hii ya kukumbushana, imeonekana ni muhimu tutumie njia ya kuweka Shindano la Hoja juu ya “jambo mtambuka” ambalo likisimamiwa na kuenziwa inavyostahili, tutaweza kuondokana na hali ya sintofahamu inayolikumba taifa letu sasa. Shindano hili litajenga hoja juu ya Sifa za Rais Bora wa Nchi kama Tanzania.
Shindano hili ni mwendelezo wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa ambayo ilizinduliwa tarehe 14 Januari 2017 na kilele chake ni tarehe 10 Disemba, 2017. Taarifa zaidi ya Kampeni hii inapatikana: www.maadilkitaifa.blogspot.com

CHADEMA YAPATA PIGO MUHEZA,MWENYEKITI WA WILAYA YA MUHEZA AJIUNGA NA CCM

April 02, 2017
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Muheza, Rwebangira Mathias Karuwasha akizungumza na waandishi wa habari mapema leo kutangaza azma ya kuondoka Chadema na kuhamia CCM 

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani Tanga kimepata pigo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Muheza, Rwebangira Mathias Karuwasha kuamua kutangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) leo kutokana na chama hicho kupoteza dira na mwelekeo.

Lakini kubwa zaidi inatokana na mambo yanayofanywa na chama hicho kwa kuiondoa uhalisi wa chama hicho ambayo wananchi walikuwa wanaitegemea kuwa chama cha kuwa mshindani na CCM ili kuleta mabadiliko.

Hatua ya mwenyekiti huyo kutangaza kujiuzulu inakuja siku chache baada ya maamuzi wa mkutano mkuu wa viongozi wa chama kanda ya kaskazini mjini Tanga uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kuridhia kuvunja uongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya ya mkoa wa Tanga.

Akitangaza uamuzi huo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa BMK uliopo Sahare Jijini Tanga,Rwebangira Karuwasha alisema hayo ndio mambo makubwa yaliyopelekea kuamua kukaa pembeni na kujiunga na CCM ambako anaona kuna sera makini zinazotekelezeka .

Alisema kutokana na matukio mbalimbali anayoyafanya Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe sitegemei kuendelea kubaki kwenye chama hiki cha watumwa  na watwana hivyo nimeamua kujiunga na CCM kwani ndio chama kinachoweza kutekeleza sera makini na zenye mafanikio.

“Kwa mfumo wa uongozi unaongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe haukubaliki na hakuweza kuvumilia.... sitegemei kuendele kuwepo kwenye chama hicho kilichokuwa cha watwana na watumwa hivyo nimeridhia kujiunga na CCM “Alisema.

“Kuanzia leo mimi sio mwanachama wa Chadema  na nitajiungha na CCM ya sasa chini ya Rais Dokta John  Magufuli sababu Chadema wameacha sera na makini kwa ajili ya kuwapa maendeleo wananchi.

Alisema pia sababu nyengine ni kutokana na utendaji wa Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambao umekuwa mstari wa mbelea kujali wanyonge na kusaidia harakati za kimaendeleo hapa nchini.

Aidha alisema wameshindwa kuelewa kuwa Mwenyekiti Mbowe alipangua gia angani kumuondoa dkta Slaa wakati alipokuwa kwenye chama hicho jambo ambalo ni hatari kwa ukuaji wa chama hicho.

RAIS MAGUFULI ZITUPIE MACHO BANDARI BUBU

April 02, 2017
SERA ya RAIS Dkt John Magufuli ya Serikali ya Viwanda ni nzuri kwani ina lengo kubwa la kuhakikisha inarudisha Tanzania ya Viwanda ili kufungua fursa na kimaendeleo na kukuza uchumi.
 
Jitihada hizo zimeanza kuzaa matunda kwenye maeneo mbalimbali kutokana na kuanzishwa viwanda ambazo leo hii vimekuwa na faida kubwa kwa watanzania kwa kupata ajira ambazo zimewasaidia kukabiliana na ugumu wa maisha.

Lakini pia kusaidia wakulima ambao wamekuwa wakizalisha mazao
mbalimbali yatokanayo na matunda kupata soko la uhakika kutokana nauwepo wa viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali zinazotokana nauzalishaji wao.

Licha ya kuwepo kwa jitihada hizo za Serikali ya Viwanda lakini bila kuangaliwa kwa umakini maeneo ya usafirishwaji ikiwemo Bandari Bubu ambazo zimekuwa ni sehemu kubwa ya kuingiza na kusafirisha bidhaa mbalimbali bila kulipa kodi jambo ambalo linachangia kurudisha nyuma fursa ya kimaendeleo na kukuza uchumi wa nchi ikiwemo kupotea kwa mapato.
 
Hali hii imekuwa ikijitokeza kwenye mikoa mbalimbali ambayo
imezungukwa na ukanda wa bahari ya hindi na hata wakati mwengine maziwa kitendo ambacho kinachangia kukwamisha juhudi za serikali kukusanya ushuru ambao unaweza kuwasaidia harakati za kiuchumi.

Licha ya maeneo hayo kutumika na wafanyabiashara kwa kukwepa kulipa ushuru lakini hali hiyo pia inasababusha shehena ambazo zilikuwa zikipita kwenye Bandari mbalimbali kupungua kitendo ambacho ni hatari kwa ufanisi wao.
 
Kwa mkoa wa Tanga zipo Bandari Bubu zipatazo 45 ambazo zimekuwa zikifanya shughuli zao nyakati mbalimbali licha ya kufanya hivyo ni kinyume cha utaratibu uliowekwa na hivyo kuisababishia mamlaka husika kukosa mapato.
 
Bandari Bubu ambazo zimekuwa zikitumika kwa wingi kuingiza mizigo na bidhaa mbalimbali kwa njia za magendo zipo ambazo zimekuwa zikifanya kazi hizo ni Kigombe iliyopo wilayani Muheza,Kipumbwi iliyopo wilayani Pangani,Jasini wilayani Mkinga na Sahare iliyopo wilaya ya Tanga.

Kama utakuwa na kumbukumbu nzuri Badari Bubu ya Sahare ni miongoni mwa eneo ambalo mwanzoni mwa mwaka huu kulitokea kazia ya Jahazi kuzama likiwa na bidhaa zilizodaiwa kuingizwa kimagendo mkoani hapa .
 
Jahazi hilo lilizama baada ya kupigwa na dhoruba kubwa ya mawimbi na hivyo kupoteza mwelekeo na kuzama licha ya kwamba nahodha wao kuwataka wenyewe mizigo kuipunguza.
 
Uwepo wa Bandari hizo kumechangia kwa asilimia kubwa upungufu wa shehena inayosafirishwa kupitia Bandari ya Tanga pamoja hali iliyosababisha kupungua uwezo wao kukusanya mapato .
Jambo hilo linapaswa kuangalia kwa umakini na mamlaka husika ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama ili kuweza kudhibiti hali hiyo kabla haijaleta athari kubwa kwa ukuaji na ustawi wa Bandari
Kwani jambo hilo limekuwa changamoto kubwa sana kwao kuweza kufikia malengo yao ambayo ni kuongeza wigo mpana wa ukusanyaji wa mapato ambayo yanaweza kusaidia kukuza kipato chao na Taifa kwa ujumla.

“Kama ni kikwazo kwa Bandari ya Tanga hili nalo lipo hivyo ni wajibu wa mamlaka husika kuakikisha wanalivalia njuga jambo hilo kwa mapana kusudi changamotohiyo iweza kuondoka”
 
Kwani ni dhahiri kubwa iwapo shehena inayosafirishwa kwa njia zisizo rasmi inasababisha kupotea kwa mapato ambayo yangeweza kuongeza kasi na ufanisi wa Bandari ya Tanga kutokana na kukusanya mapato.
 
“Kwa kweli uwepo wa Bandari zisizo rasmi hii umekuwa changamoto kubwa sana na imechangia hata upungufu wa shehena inayosafirishwa kupitia Bandarini na kama usipozibitiwa hali inaweza kuwa mbaya”
Katika jambo hilo lazima kuwepo kwa juhudi za makusudi kwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kuangalia namna ya kuzifuatilia kwa karibu uondoaji wa Bandari Bubu ambazo zimekuwa kikwazo cha maendeleo.

Lakini pia watu wanaotumia Bandari hizo kuachana na shughuli
hizo kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria za hapa nchini na kuwepo kwa adhabu kali kwa watakaobainika kujihusisha na suala hilo ili kuweza kulitokomeza la sivyo tutaendelea kuongeza kila siku bila majibu
 
Nimalizie kwa kumuomba Rais Magufuli atupie macho na uwepo wa Bandari hizo kwani nazo zimekuwa kikwazo kikubwa kwa mamlaka za Bandari maeneo mengine kupungua kwa shehena za mizigo jambo linaathiri ukuaji na ustawi wake

RC PWANI AAGIZWA APIGE KAMBI MIONO BAGAMOYO

April 02, 2017

*Waziri Mkuu amtaka amalize migogoro ya wakulima, wafugaji

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Eng. Evarist Ndikilo apige kambi katika kata ya Miono wilayani Bagamoyo na kuwasaka wafugaji wanaopiga wakulima.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wakazi wa kata hiyo ambao walisimamisha msafara wake wakati akienda kukagua miundombinu ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyoko wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

Akitoa kero za eneo hilo, Diwani wa Kata ya Miono, Bw. Juma Mpwimbwi alisema kata hiyo inakabiliwa na tatizo la wakulima kupigwa na wafugaji na wakipelekwa kituo cha polisi hawachukuliwi hatua yoyote.

“Wafugaji wanatupiga lakini wenzetu hawachukuliwi hatua na hata ukienda kushtaki polisi, hawakai kwa sababu wanadai wao wana fedha,” alisema diwani huyo.

Pia alisema mbali ya kero sugu ya maji, waliahidiwa barabara ya lami tangu miaka saba iliyopita lakini hadi sasa hawana hata kipande kidogo tu cha barabara hiyo.

Naye Bw. Shabani Mkwimbi ambaye alipewa nafasi ya kuzungumza kwa niaba ya wananchi wenzake, alisema kata hiyo ina kituo cha polisi na mahakama lakini utendaji kazi wa viongozi waliopo hapo unatia shaka.

“Waziri Mkuu tunataka ukimaliza kuongea na sisi, uondoke na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Miono, Bw. Maro na msaidizi wake Bw. Rashidi pamoja na Hakimu wa hapa, kwa sababu hawa watu habari yao ni nyingine. Mkulima akienda polisi au mahakamani hashindi kesi hata siku moja, lakini mfugaji akienda anashinda,” alisema huku akishangiliwa.

“Hawa watu wanadai wana hela na wanafanya chochote wanachotaka, na ndiyo maana hawalali polisi hata kama wameua mtu,” aliongeza.

Akijibu kero zao, Waziri Mkuu aliwahakikshia wakazi hao kwamba Serikali iliyopo madarakani ni yao na hakuna hata mtu mmoja ambaye yuko juu ya sheria.

Alisema suala la polisi wa kituo cha Miono litashughulikiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ambaye alikuwepo katika msafara wake. “Tena Mkuu wa Mkoa yuko hapa na yeye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huu, atasimamia hilo.”

Akifafanua kuhusu suala la wafugaji kuwapiga wakulima, Waziri Mkuu alisema msimamo wa Serikali ni kuwaona wakulima wanafanya kazi zao kwa uhuru na wafugaji nao wanafanya kazi zao kwa uhuru. “Hakuna mfugaji anayeruhusiwa kupeleka ng’ombe wake kwenye mashamba yenye chakula. Hili haliruhusiwa hata kidogo,” alisisitiza.

“Mkuu wa Mkoa hili ni agizo. Njoo upige kambi hapa na watu wako, na usake  wahusika hadi wabainike. Ni lazima tuwajue ni akina nani wamehusika na hili,” alisema.

Aliwataka maafisa mifugo wa mkoa huo waende kwa wafugaji na kutambua mifugo waliyonayo na kama kuna maeneo wahakikishe wanapatiwa maeneo rasmi ili waweze kupatiwa matibabu kwa ajili ya mifugo yao.

Aliwataka wafugaji wanaokata mabomba ya maji ya mradi wa maji wa Chalinze (CHALIWASA) ili kupata maji ya kunywesha mifugo yao, waache tabia hiyo mara moja na akaonya kuwa watakaokamatwa, wachukuliwe hatua za kisheria mara moja. Katika ziara hiyo fupi, Waziri Mkuu alikuwa amefuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa pwani, Eng. Evarist Ndikilo, viongozi wa wilaya ya Bagamoyo na Mbunge wa jimbo hilo, Ridhiwani Kikwete.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa (pichani kulia) akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Eng. Evarist Ndikilo alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.

Vijana wametakiwa kutumia sekta isiyo rasmi kujiajiri kwa maendeleo ya Taifa

April 02, 2017

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akifungua kongamano la Vijana kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
JENI2
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga akizungumza na Vijana (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kongamano la Vijana kuelelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
JENI3
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico akizungumza na Vijana na watendaji wa Mkoa wa Katavi (hawapo katika picha) juu ya matumizi ya Tovuti ya Mkoa kabla ya kuzindua Tovuti hiyo leo Mkoani Katavi.
JENI4
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Tovuti ya Mkoa wakati wa kongamano la Vijana kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
JENI5
Baadhi ya Vijana wa Mkoa wa Katavi wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikitolewa wakati wa kongamano la vijana kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM


Na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi

Vijana Mkoani Katavi wametakiwa kujitambua, kuchukua fursa na kuchangia maendeleo ya mkoa na taifa kwa kutumia malighafi zinazopatikana mkoani humo kuwekeza na kuacha kusubiria wawekezaji kutoka mikoa mingine ama nchi za nje kufaidika na malighafi za mkoa huo.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama alipokua akifungua kongamano la Vijana kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi na kuwataka vijana hao kuacha uvivu kwani maendeleo huletwa na jitihada za mtu binafsi.

Mhe. Jenista amesema kuwa vijana wanaweza wakajiwekeza katika sekta isiyo rasmi kwani sekta hiyo huajiri asilimia kubwa na kuwagusa vijana wengi katika kutengeneza ajira na kuwafanya vijana wasiwe tegemezi ndani ya jamii.

“Vijana wa Mkoa wa katavi mnayo kila sababu kujitafiti na kujua ni namna gani mtatumia sekta isiyo rasmi kutengeneza ajira ambazo zitawasaidia kuonyesha mchango wenu wa asilimia 55 kama vijana katika nchi ya tanzania ukaweza kutumika   kuleta maendeleo ya Mkoa na taifa kwani mnaweza, sababu mnayo, nguvu mnayo na uwezo mnao” amesema Mhe. Jenista

Kwa upande wake Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico amewataka vijana wa Mkoa wa Katavi kutumia Tovuti ya Mkoa iliyozinduliwa wakati wa kongamano hilo kupata taarifa kwa wakati ili waweze kuendana na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga amesema kuwa Tovuti ya Mkoa yenye kikoa/domeini ya www.katavi.go.tz itakua na taarifa za uhakika na za wakati hivyo kuwawezesha wananchi wa Mkoa wa Katavi wakiwemo vijana kujua taarifa za maendeleo za mkoa pamoja na masuala mengine muhimu kama vile kuelimisha vijana masuala muhimu ya kilimo bora, ujenzi wa viwanda vidogo na vikubwa, afya ya jamii, taaluma za kibenki na ujuzi wa aina mbalimbali za kiteknolojia utakaowawezesha vijana kujaribu.