FIFA KUONGEZA FEDHA ZA MAENDELEO NA KUJIENDESHA KWA SHIRIKISHO

FIFA KUONGEZA FEDHA ZA MAENDELEO NA KUJIENDESHA KWA SHIRIKISHO

February 24, 2018

PIX 1
Waziri Wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu mambo mbalimbali serikali iliyozungumza na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani Gianni Infantino na Rais wa CAF Ahmad Ahamad alipokuwa nchini kwa ajili ya mkutano wao leo jijini Dar es Salaam.
PIX 2
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu hali ya kifedha kwa shirikisho hilo na matarajio baada ya FIFA kuwapa maelekezo ya kufuatilia fedha ambazo hawakuingiziwa kutokana na matatizo ya viongozi waliyopita leo jijini Dar es Salaam.
……………….
Na Anitha Jonas –WHUSM
Dar es Salaam.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuendeleza viwanja tisa nchini kufuatia kuongezeka kwa dau la pesa za Maendeleo na Kujiendesha zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA kuanzia mwaka 2019 .
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mambo mbalimbali serikali iliyojadili na Rais wa FIFA Gianni Infantino alipokuwa nchini kwa mkutano wake hivi karibuni.
‘’Rais wa FIFA alieleza kuongeza mara nne ya kiwango cha pesa za maendeleo na kujiendesha walizokuwa wanatoa kwa mashirikisho kama TFF mpaka kufikia Dola Milioni Moja na Laki Mbili na Nusu kwa mwaka na kusema pesa hizo ndiyo zitumike kuendeleza viwanja vya michezo kwani uwepo wa viwanja ndio unaosaidia kukuza vipaji vya soka,’’alisema Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari Waziri Mwakyembe alisisitiza kuwa Rais huyo wa FIFA ametoa msisitizo wa kutokuwa na huruma kwa kiongozi yoyote wa shirikisho atakayekuwa na matumizi mabaya ya pesa pamoja na kufanya udanganyifu kwani yeye yuko mstari wa mbele kupinga ufisadi katika sekta ya maendeleo ya Soka duniani.
Pamoja na hayo nae Rais wa TFF  Bw. Wallace Karia alitoa ufafanuzi wa hali ya kifedha kwa shirikisho na kueleza kufuatia kuwepo na matatizo katika shirikisho hilo FIFA ilikuwa imesitisha kuwapatia fedha hizo za maendeleo na kujiendesha tangu mwaka 2015 lakini baada ya kuingia uongozi mpya ambao FIFA wameridhika nao na wameshaupa utaratibu wa kufuatilia fedha hizo.
‘’Rais wa FIFA alitueleza kuwa fedha hizo ziko salama nchini Zurich ni kwamba tu hazikuwa zimeruhusiwa kuingia nchini na kwa sasa tumeshaanza mchakato wa kufuatilia fedha hizo kwa kuzingatia maelekezo ya FIFA hivyo basi tutakapo pata fedha hizo Shirikisho  litaendeleza baadhi ya miradi ambayo tumekwisha iandaa,’’alisema Bw. Karia.
Pamoja na hayo rais huyo alitoa wito wa wakazi wa jiji la Tanga waliyovamia eneo linalotarajia kujengwa Technical Center  ya mchezo wa soka basi waondoke mara moja kabla hawajachukuliwa hatua.(Chanzo Fullshangweblog)

WAZIRI KIGWANGALLA ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA ARUSHA, ATUMA SALAMU KWA MUWEKEZAJI ANAECHOCHEA MGOGORO KATIKA HIFADHI HIYO

February 24, 2018

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na viongozi wa TANAPA alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ausha jana na kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa lengo la kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua mazingira ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha alipotembelea hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa lengo la kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. Katikati ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA, Martin Loibooki na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Steria Ndaga (kulia). 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia moja ya eneo lenye mgogoro ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha alipotembelea hifadhi hiyo jana na kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. Katikati ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA, Martin Loibooki na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Steria Ndaga (kulia). 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA, Martin Loibooki  alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha jana na kukagua shughuli mbalimbali  za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. Kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Steria Ndaga.
Picha ya pamoja Waziri Kigwangalla na baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA.
Waziri wa Malisili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA, Martin Loibooki kuhusu Kreta ya Hifadhi ya Ziwa Manyara muda mfupi kabla ya kuhitimisha ziara yake katika hifadhi hiyo jana jioni. (Picha na Hamza Temba-WMU)

OSHA YASISITIZA KADA YA USALAMA KAZINI KUTAMBULIKA RASMI

February 24, 2018
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) unakusudia kuishawishi serikali na waajiri katika sekta binafsi hapa nchini kuitambua kada ya Usalama na Afya mahali pa kazi na kuiweka katika mfumo rasmi wa ajira.
RAIS MHE.DKT.MAGUFULI AREJEA NCHINI KATIKA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA AKITOKEA NCHINI UGANDA ALIPOHUDHURIA MKUTANO WA 19 WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

RAIS MHE.DKT.MAGUFULI AREJEA NCHINI KATIKA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA AKITOKEA NCHINI UGANDA ALIPOHUDHURIA MKUTANO WA 19 WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

February 24, 2018


2
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa MKoa wa Mwanza  John Mongella mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea Nchini Uganda alipohudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
3
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) MKoa wa Mwanza ndugu Anthony Dialo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea Nchini Uganda alipohudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
4
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ndugu  Kheri Jamesn mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea Nchini Uganda alipohudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
5
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea Nchini Uganda alipohudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
6 7
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akitazama ngoma  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea Nchini Uganda alipohudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
9 10
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi  wa uwanja wa ndege wa MKoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea Nchini Uganda alipohudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
11
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi,nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula,Mkuu wa MKoa wa Mwanza John Mongella na wacheza ngoma waliofika kumlaki uwanjani hapo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea Nchini Uganda alipohudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
PICHA NA IKULU.
RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI ULIOMALIZIKA LEO JIJINI KAMPALA NCHINI UGANDA

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI ULIOMALIZIKA LEO JIJINI KAMPALA NCHINI UGANDA

February 24, 2018
1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Rais wa Uganda Yoweri Museveni pamoja na viongozi wengine wa Jumuiya hiyo katika siku ya mwisho ya Kikao chao kilichofanyika Kampala nchini Uganda.
2
3
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anatoka katika ukumbi wa mkutano pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kumalizika kwa vikao vya Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC vilivyofanyika Kampala nchini Uganda.
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir pamoja na viongozi wengine wa Jumuiya hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa EAC katika siku ya mwisho jijini Kampala nchini Uganda. PICHA NA IKULU

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AONDOKA UGANDA MARA BAADA YA KUHUDHURIA VIKAO VYA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC)

February 24, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika uwanja wa ndege wa Entebe mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ambao ulimalizika hapo jana jijini Kampala nchini Uganda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Kijeshi kutoka Uganda kabla ya kurejea nchini. PICHA NA IKULU

MADINI YOTE NCHINI NI SHARTI YA WANUFAISHE WATANZANIA

February 24, 2018
Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Mhandisi Joseph Mwakabage Meneja Mradi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe (Aliyenyoosha mkono) akimuonyeshaNaibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko mitambo ya uchimbaji madini  alipotembelea mgodi huo uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua eneo la uchimbaji madini ya makaa ya mawe alipotembelea mgodi wa Edenville Tanzania Ltd uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.
Mhandisi Joseph Mwakabage Meneja Mradi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe (Kulia) akimueleza Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko juu ya uchimbaji wa makaa ya mawe alipotembelea mgodi huo uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.

Na Mathias Canal, Rukwa

Serikali imesema kuwa sheria mpya ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 inaelekeza wazi kuwa Madini yote nchini ni Mali ya watanzania hivyo wanapaswa kutambua umuhimu wa rasilimali.

Wawekezaji na wachimbaji wote wa madini nchini wanapaswa kutambua kuwa wanalo jukumu muhimu la kurejesha kwa jamii asilimia chache ya kile wanachozalisha kwa kuunga mkono juhudi za serikali Back to the Community) katika kuboresha miundombinu, sekta ya elimu, afya N.K

Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko amesisitiza hayo Leo 23 Februari 2018 wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe Mkoani Rukwa Magharibi mwa Tanzania.

Mradi huo unaosimamiwa na kampuni ya Edenville Tanzania Ltd kwa ubia na kampuni ya Edenville Energy of Uk na Upendo Group (Kampuni ya kizawa) ilianza shughuli za majaribio ya uchimbaji na uoshaji mwezi wa kumi mwaka Jana 2017 na mkaa wa kwanza kuuzwa kwa majaribio ni mwezi Novemba mwaka 2017.

"Nataka niwajulishe tu watanzania wenzangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli aliniteua kusimamia Wizara ya Madini nikimsaidia Waziri wetu Mhe Anjelina Kairuki ili kuboresha sekta hii ya Madini hatimaye kuwanufaisha watanzania kuliko ilivyokuwa awali ambapo Madini yalikuwa yanachimbwa nchini lakini faida inaenda nchi zingine" Alisema Mhe Biteko na Kuongeza kuwa

Wawekezaji hao wanapaswa kutoa ajira zisizo za utaalamu kwa wananchi wanaozunguka migodi yao sambamba na watanzania wote huku akiwaagiza kuwaajiri wataalamu wa Madini wa ndani ya nchi kwa kazi ambazo wanaweza kuzifanya sio kuajiri wageni.

Aidha, aliwasisitiza wananchi hao pindi wanapopata ajira zao katika migodi mbalimbali wanapaswa kuwa waaminifu ili kuwavutia wawekezaji hao jambo litakalopelekea wawekezaji kuwa na imani na watanzania na hatimaye kuongeza chachu ya ajira nyingi zaidi.

Sambamba na hayo amekemea baadhi ya wafanyakazi katika migodi mbalimbali ambao wameaminiwa na kupatiwa ajira lakini wanageuza muda wa kazi kuwa muda wa starehe kwa kunywa pombe na utoro kazini.

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Rukwa kutembelea na kukagua uchimbaji wa Madini.

RC TELACK AHAMASISHA WANANCHI KUTOA TAARIFA SAHIHI UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI

February 24, 2018

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack amewataka wananchi mkoani Shinyanga kutoa taarifa sahihi kwa watafiti wanaofanya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi mkoani humo.

MPINA APIGA FAINI SHILINGI BILIONI 19 MELI 19 ZILIZOTOROKA BILA KUKAGULIWA

February 24, 2018
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga  Joelson Mpina (mwenye koti jekundu)akimsikiliza Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya  Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed ofisini kwake leo  wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Kisiwa Unguja. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlakaya Kusimamia  Uvuvi wa Bahari Kuu(DSFA),Hosea Gonza Mbilinyi. (Picha na John Mapepele)
 Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed(mwenye suti nyeupe) kushoto kwake ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga  Joelson Mpina (mwenye koti jekundu) na kulia kwake ni Katibu Mkuu Uvuvi Tanzania Bara Dkt. Yohana Budeba wakiwa katika picha ya pamoja  na Wakurugenzi na Watendaji wa Sekta ya Uvuvi mara baada ya Waziri Mpina na Watendaji wake kuwasili leo Unguja kwa ziara ya kikazi. (Picha na John Mapepele)
 Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Kusimamia  Uvuvi wa Bahari Kuu(DSFA) wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga  Joelson Mpina  (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika leo katika ofisi ya Mamlaka hiyo Fumba katika kisiwa cha Unguja leo. (Picha na John Mapepele)
Kiongozi wa Kampuni ya  Linghang kutoka china inayoshughulika  na uendelezaji wa Utalii wa Zanzibar nchini china  Tom Zhang (katikati) akiwa na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed(mwenye suti nyeupe) kushoto kwake ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga  Joelson Mpina (mwenye koti jekundu) wakiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya Waziri Mpina na Watendaji wake kuwasili leo Unguja kwa ziara ya kikazi. (Picha na John Mapepele)

 Na John Mapepele
Serikali imezipiga faini ya bilioni kumi na tisa  meli 19 ikiwa ni shilingi bilioni moja kwa kila meli na kuamuliwa kulipa faini hiyo ndani ya wiki mbili kwa kukiuka kanuni ya 10 ikisomeka pamoja na kanuni ya 68 ya kanuni za uvuvi wa Bahari Kuu za mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kutoripoti katika bandari Dar es Salaam, Zanzibar, Mtwara ama Tanga kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kutoka katika bahari kuu ya Tanzania.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, katika Ofisi za Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari  Kuu zilizopo Fumba kisiwani Unguja, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina  amesema pamoja na meli hizo kuamriwa kulipa faini ya Shillingi Billioni moja (Tshs. 1,000,000,000) kila moja zinatakiwa kurejea katika bandari za Tanzania kwa ajili ya ukaguzi kwa kuwa leseni zao bado hazijaisha muda wake hadi sasa ili kubaini thamani halisi ya kiasi cha fedha zitakazotozwa kwa ajili ya samaki waliovuliwa bila kukusudia(Bycatch).
Aidha Mpina amesema meli hizi zimetakiwa kuilipa Tanzania kiwango cha pesa kwa mujibu wa soko la kimataifa kutokana na kuondoka na Bycatch waliyoripoti kuwa wanayo kabla ya kutoroka.
Waziri Mpina amemuagiza Katibu Mkuu Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba  kuiamru Mamlaka ya uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) iwaandikie notisi wahusika wa meli hizi kuwajulisha kuhusiana na maamuzi haya pia kuwajulisha Kamisheni ya Jodari kwenye Bahari ya Hindi, (IOTC) kuhusiana na hatua zilizochukuliwa na Tanzania dhidi ya meli hizo ili isaidie kuwabaini na kuwachukulia sheria kwa mujibu wa Sheria husika.
Aidha imeamriwa kwamba Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu pia iandae barua/ andiko kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili aweze kuiandikia Barua Wizara ya Mambo ya Nje kwa lengo la kuwasiliana na Flag States (Mataifa ambayo meli hizi zimesajiliwa) ili kuwajulisha makosa yaliyotendwa na meli husika pamoja na hatua ambazo Tanzania imechukua. Amesema meli zote zilizotoroka zimesajiliwa nchini China.
Wakati huo huo Waziri Mpina amesema meli ya Tai Hong 1 imekiuka Kifungu cha 18 cha Sheria ya uvuvi wa Bahari kuu No. 1 ya Mwaka 1998 na marekebisho yake ya mwaka 2007 pamoja na Kanuni ya 66 ya kanuni za uvuvi wa Bahari kuu za Mwaka 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kukutwa na mapezi ya papa yasiyoendana na miili iliyokutwa kwenye meli hiyo baada ya kukaguliwa katika bandari ya Dar es Salaam mnamo tarehe 25/01/2018-27/01/2018. 
Pia meli hii imebainika kukiuka kanuni ya 10 ikisomeka pamoja na kanuni ya 68 ya kanuni za uvuvi wa Bahari Kuu za mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kuhaulisha mabaharia kutoka kwenye meli nyingine ambao idadi yao ilikuwa mabaharia 10.
Aidha meli hii pamoja na kukutwa na makosa hayo iliondoka nchini bila kufuata taratibu zinazotakiwa kwa mujibu wa vifungu tajwa hapo juu.
Kutokana na makosa hayo imeamriwa na Mamlaka ya Bahari kuu (DEEP SEA FISHING AUTHORITY) kulipa jumla ya faini ya Shillingi Billion moja (Tshs. 1,000,000,000) ambapo Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu itawasilisha notisi ya adhabu hii kwa wahusika wa Meli hii ya TAI HONG 1.
Mbali na Tai Hong 1 Mpina amezitaja Meli hizo zilizopigwa faini ya Bilioni moja kila moja kuwa ni pamoja na TAI HONG NO2 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/453, TAI HONG 8 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/454, ,TAI XIANG 2 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/455, TAI XIANG 5 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/456, TAI XIANG 1 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/457, TAI XIANG 8 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/458 na TAI XIANG 9 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/459.

Meli nyingine ni TAI XIANG 10 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/460, TAI XIANG 7 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/461, TAI XIANG 6 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/462, TAI HONG 6 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/463,  TAI HONG 7 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/464, XIN SHIJI 81 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/466, XIN SHIJI 82 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/467, XIN SHIJI 83 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/468, XIN SHIJI 86 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/470, XIN SHIJI 72 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/471, XIN SHIJI 76 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/472 na JIN SHENG 1 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/473.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba amewataka wawekezaji kwenye  bahari ya Tanzania kuwa waaminifu na kuzingatia masharti na taratibu za kisheria  ili nchi na wawekezaji waweze kunufaika.
“Taratibu zipo wazi ni muhimu  kuzinangatia sheria  namna nyingine tutaendelea kusimamia sheria za nchi yetu kwa faida ya sasa na vizazi vya baadaye” Alisisitiza Dkt. Budeba
Amesema  hatua iliyochukuliwa na Serikali  ya kuzipiga faini meli hizo ni somo kwa meli nyingine na kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa yoyote atakayebainika kutenda  makosa  ya uvuvi haramu katika bahari na maziwani.
Aidha amesema Serikali ipo tayari kufanya biashara  na mtu yoyote ambaye atazingatia masharti ya nchi, na kwamba taifa linajipanga ili kuwa na makampuni yake ya TAFICO na ZAFICO yatakayoshuhulika na uvuvi ili kunufaika na raslimali za uvuvi kama ambavyo inafanyika katika nchi mbalimbali duniani.
Amesema hatua hiyo itasaidia kukuza ajira kwa wananchi, uchumi wan chi na kuanzisha viwanda vya kuchakata samaki na mazao yake.
Aliwashukuru  wadau wote wanaoshiriki kwenye mapambano ya uvuvi ambapo kipekee alilishukuru shirika lisilo la kiselikali la Sea worrior kwa kutoa mchango mkubwa kwenye operesheni Jodari ambayo imefanywa  na wadau mbalimbali nchini.