DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOITEKA MWANZA KWENYE FIESTA; NI SHIDAAAAH!

August 10, 2014

ona

Gala ilianza kunguruma Jana kwenye viwanja vya CCM Kirumba ambapo mkali wa Bongofleva,Diamond Platnumz alifanya vitu vyake . Hizo ni baadhi ya picha za hiyo show Jana.
Dkt. Bilal afungua kongamano la Kimataifa la Sayansi kwa nchi za Afrika na Kusini mwa jangwa la Sahara, Jijini Arusha

Dkt. Bilal afungua kongamano la Kimataifa la Sayansi kwa nchi za Afrika na Kusini mwa jangwa la Sahara, Jijini Arusha

August 10, 2014

1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa  Chuo cha Nelson Mandela cha jijini Arusha wakati alipowasili kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. (Picha na OMR).
Kongamano hilo la siku tatu limefanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) Jijini Arusha  Agosti 5, 2014, na kushirikisha mabingwa mbalimbali wa tafiti ndani ya Afrika na nchi za ukanda wa Jangwa la Sahara.
Kongamano hilo ambalo limedhaminiwa na Shirika la misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) linalenga kukuza tafiti za kisayansi na kutanua maendeleo ya tafiti hizo ili yasaidie wananchi wa nchi za ukanda huu hasa vijana ambao wanaelezwa kuwa na idadi kubwa kulinganisha na wazee na akina mama.
Katika Hotuba ya mgeni rasmi Makamu wa rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alisema kuwa, dhana ya umuhimu katika uwekezaji na utanuaji wa sayansi katika Afrika, inahitaji kutazama kundi la vijana na kulihamasisha kushiriki katika masomo ya sayansi ili kuharakisha maendeleo kwa Bara la Afrika.
2
Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha Nelson Mandela, Bernard Mussa, aliyetafiti kuhusu kuongeza joto katika Majiko kwa kutumia mwanga wa jua, wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara.
3
Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa mradi wa Masai Stove’s & Solar, Kisioki Moitiko aliyetafiti kuhusu mzunguko wau meme wa Jua kutumika katika nyumba za kabila la kimasai (Maboma) wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara.
4
Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Hassna Founoune, kutoka Taasisi ya Tafiti ya Kilimo ya Senegal, wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara.
5.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo katika Screen na Makamu Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela, Prof. Bulton Mwamila, wakati wakiangalia mjadala uliokuwa ukiendelea kupitia ‘Video Conference’ kati ya Marekani na Tanzania, kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara.
6
7
Makamu wa Rais Dkt. Bilal katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo, baada ya ufunguzi.

WAZIRI WA HABARI NA VIONGOZI WA WIZARA NA TAASISI ZIARANI NCHINI CHINA

August 10, 2014
Waziri wa Habari,  Vijana,  Utamaduni na Michezo Dkt.  Fenela Mukangala yuko nchini China katika ziara ya kuangalia maendeleo ya Sekta ya Utangazaji na kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Utangazaji kati ya Tanzania na China.

Katika ziara hiyo ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Sihaba Nkinga,  Mkurugenzi Mkuu wa TBC Bw. Clement Mshana na Mkurugenzi wa Utangazaji TCRA Bwana Habbi Gunze. 

ujumbe wa Waziri ukitembelea sehemu mbalimbali zikiwemo studio na vivutio mbalimbali vya Utangazaji katika kituo cha Tv cha Jimbo la Sichuan nchini China.

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YASHIRIKI KIKAMILIFU MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE KITAIFA MKOANI LINDI

August 10, 2014
Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwa katika banda lao wakati wa Maonesho ya Wakulima Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
  Watoto waliotembelea Banda lka WQizara ya Viwanda na Biashara.
Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwa katika banda lao wakati wa Maonesho ya Wakulima Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Mmshiriki akionesha bidhaa za Ngozi ndani ya mabanda ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
Naibu Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia akizungumza na Waandishi wa habari.
Naibu Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia akiwa anatembelea mabanda ya maonesho.


Naibu Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia akipiga picha ya pamojanaViongozi mbalimbali waserikali katika maonyesho ya Nanenane 2014, Lindi.

Naibu Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia akipokea zawadi baada ya kutembelea mabanda.
Naibu Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia akiwa anatembelea mabanda ya wadau.