Bayport Financial Services yazindua tovuti ya mikopo ya haraka

March 09, 2015
Msimamizi wa michezo ya kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Milao kulia akipata maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya mtandao (Online) wa Bayport Financial Services, Zainabu Kalufya, katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao kwa www.kopabayport.co.tz, uzinduzi uliofanyika leo Makao Makuu ya Bayport, jijini Dar es Salaam. Picha kwa Hisani ya Bayport.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI yaKifedhaya Bayport Financial Services, yenye Makao Makuu yake jijini Dar es Salaam, Tanzania, imezindua tovuti yake ya www.kopabayport.co.tz, itakayowezesha wateja wake kupata mikopo ya haraka na kwa njia rahisi.

Kwa kupitia tovuti hiyo, watu mbalimbali wanaweza kupata huduma za Bayport, sanjari na kupata mkopo ndani ya saa 24 baada ya kuidhinishwa, huku akijibiwa ombi lake la mkopo, ndani ya masaa mawili tangu alipojisajiri kwa mara ya kwanza.

Akizungumzia huduma hiyo mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam leo mchana, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba huduma hiyo sasa itawawezesha wateja wao kukopa mahala popote atakapokuwa, tofauti na awali.

Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services kitengo cha Huduma kwa Wateja, wakiwajibika wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao onlinewww.kopabayport.co.tz, jijini Dar es Salaam leo.

Alisema kuwa lengo la uanzisha kwa tovuti hiyo ya www.kopabayport.co.tz ni kutokana na kuweka sera ya mikakati ya kuwapatia huduma hiyo watu wengi iliwaweze kukopa na kujikwamua kiuchumi, ikiwa ni maalum kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa na Bayport.

“Bayport sasa imezidi kupiga hatua, kwa sababu mteja wetu hata kama akiwa nyumbani kwake, kwa kupitia huduma yetu hii anaweza kujisajiri na kukopeshwa anachokihitaji kutoka kwetu bila kupata usumbufu wa aina yoyote.

“Hayani mambo mazuri na naamini ni wakati wa wateja wetu na Watanzania wote kuendelea kuchangamkia huduma zetu za mikopo, ukizingatia ni Bayport pekee inayoweza kukupatia mkopo wa Chagua chochote Bayport italipia, Bima ya Elimu ya Uwapendao, mikopo ya fedha na mingineyo muhimu,” alisema Cheyo.

Naye Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Mrisho Millao, alisema utaratibu wa kukopa kwa njia ya Internet kutoka Bayport ni mzuri na utarahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa wateja wao na Watanzania kwa ujumla.

“Nimeangalia ni mfumo mzuri na rahisi kwa mteja wa Bayport kupata mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao huku ukiwa katika lugha mbili za Kiswahili na Kingereza,” alisema Millao.

Kwa mujibu wa Cheyo, hiyo ni njia rahisi na ya haraka mno inayomuwezesha kumpatia mkopo mteja wao, bila kusumbuka kwenda kwenye tawi kuanza taratibu za kujiunganisha kwenye huduma za mikopo ya taasisi yao.

Ili mtu aweze kuingia kwenye huduma hiyo, atalazimika kutumia simu yake ya mkononi yenye uwezo wa internet bila kusahau kompyuta, ikiwa hatua rahisi za kumpatia mkopo huo mteja, huku Cheyo akitumia muda huo kuwataka wateja wao na Watanzania kuiunga mkono Bayport ili kujikwamua kiuchumi kutokana na huduma zao za mikopo isiyokuwa na dhamana wala amana.

KAMPENI YA MWANAMKE NA UCHUMI YAZINDULIWA MKOA WA PWANI

March 09, 2015

Mkurugenzi wa Kampuni ya Angels Moment, Naima Malima akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya Mwanamke na Uchumi uliofanyika Mkuranga mkoani Pwani. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,  Abdallah Kihato na Mkurugenzi wa Mwang'amba Communication, James Mwang'amba. (Picha na John Dande)
Mkuu wa  Wilaya ya Mkuranga,  Abdallah Kihato akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya Mwanamke na Uchumi lililofanyika Mkuranga mkoani Pwani.
 Mkurugenzi wa Mwang'amba Communication, James Mwang'amba akitoa mada kwa wanawake wajasiriamali.
Mada zikitolewa.
Wanawake wajasiriamali wakiwa katika kampeni ya mwanamke na uchumi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Angels Moment, Naima Malima (kulia) akipeana mkono na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Abdallah Kihato.
Mkuu wa  Wilaya ya Mkuranga,  Abdallah Kihato(wa tatu kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Angels Moment, Naima Malima. 

Na Mwandishi Wetu


MKURUGENZI  kuu wa Angels Moment, Naima Malima, amesema utafiti mbalimbali umethibitisha kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanawake wa Bara la Afrika katika masuala ya fedha na fursa zinazowazunguuka ni ukosefu wa elimu.
Kauli hiyo aliitoa juzi wakati ufunguzi wa Kampeni ya Mwanamke na Uchumi iliyofanyika wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Kampeni hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Abdallah Kihato, Madiwani na maofisa maendeleo ya jamii, wawakilishi wa taasisi mbalimbali.
Naima, alisema hali hiyo ya ukosefu wa elimu ya kutosha imekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya wanawake wa Tanzania  na Bara la Afrika katika mapambano dhidi ya umasikini uliokithiri mwa jamii hizo.
“Hali hii inaamanisha kuwa, mwanamke akipatiwa elimu ya msingi ya biashara, ataweza kuwa na uwezo mkubwa wa kutumia fursa nyingi zinazomzunguuka katika kubadili hali zao kiuchumi na kujisogezea maendeleo,”alisema Naima.
Alisema kampeni hiyo inatoa elimu ya msingi katika maeneo makuu ya kama vile ujasiriamali na fursa zilizopo na usimamizi binafsi wa fedha na uwekaji akiba.
“Tunaweza kuchukulia mfano wa mikopo ya bidhaa za akinamama kama vile mikoba, viatu na vipodozi,”aliasema. 
Naima, alisema AMCL kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto waliandaa kampeni hiyo kwa jina la Mwanamke na Uchumi ikiwa na lengo la kuwawezesha wanawake katika kujijengea uwezo na ujuzi wa kusimamia masuala ya fedha zao.
“Kaulimbiu ya Kampeni yetu ni Ukimuelimisha Mwanamke Umeelimisha Jamii Nzima,”alisema Naima.
Kampeni hiyo ilizinduliwa na Waziriri wa Maendeleo ya Jamii, Sofia Simba, Oktoba  mwaka 2014 mkoani Dodoma.

HIVI NDIVYO BAWACHA TANGA WALIVYOSHEHEREKEA SIKUKUU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUWAFARIJI WATOTO YATIMA JIJINI TANGA.

March 09, 2015

Katibu wa Baraza laWanawake Chadema mkoa wa
Tanga(Bawacha)Recho Sadick akizungumza na watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Casafamilia Losseta kilichopo Kata ya Central eneo la Raskazone jijini Tanga ikiwa ni siku ya wanawake duniani


Katibu wa Baraza laWanawake Chadema mkoa wa
Tanga(Bawacha)Recho Sadick  akizungumza na mtoto anaolelewa kwenye kituo cha Casafamilia Losseta kilichopo Kata ya Central eneo la Raskazone jijini Tanga ikiwa ni siku ya wanawake duniani

Katibu wa Baraza laWanawake Chadema mkoa wa
Tanga(Bawacha)Recho Sadick akiimba wimbo na watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Casafamilia Losseta kilichopo Kata ya Central eneo la Raskazone jijini Tanga ikiwa ni siku ya wanawake duniani

Katibu wa Baraza laWanawake Chadema mkoa wa
Tanga(Bawacha)Recho Sadick wa kwanza kushoto aliyevalia shati la kaki akiimba wimbo na watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Casafamilia Losseta kilichopo Kata ya Central eneo la Raskazone jijini Tanga ikiwa ni siku ya wanawake duniani



Katibu wa Baraza laWanawake Chadema mkoa wa
Tanga(Bawacha)Recho Sadick wa kwanza kulia aliyevalia shati la kaki akiwa amesmhika mmmoja kati ya watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Casafamilia Losseta kilichopo Kata ya Central eneo la Raskazone jijini Tanga ikiwa ni siku ya wanawake duniani





  KATIBU wa Baraza la Wanawake Chadema
Mkoa wa Tanga (Bawacha), Recho Sadick kushoto akimkabidhi zawadimbalimbali mlezi wa kituo cha kulea watoto cha Casa Familia Lossetakilichopo Kata ya Central eneo la Raskazone jijini Tanga ikiwa ni sikuya wanawake dunia jana


TANZANIA YAONGOZA AFRIKA MASHARIKI KATIKA USHIRIKI WA MAONESHO YA ITB 2015.

TANZANIA YAONGOZA AFRIKA MASHARIKI KATIKA USHIRIKI WA MAONESHO YA ITB 2015.

March 09, 2015

T10 
Waziri wa Maliasilina Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akihojiwa na mtangazaji Amina Abubakary wa radio sauti ya Ujerumani katika Banda la Tanzania.
TE1 
Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania Bw. Geofrey Tengeneza (kushoto) akizungumza na mmoja wa washiriki wa maonesho kutoka Tanzania Bw. Joackim Minde ili kupata maoni yake kuhusu maonesho hayo.
TE2 
Washiriki wa Tanzania katika maonesho ya ITB wakiwa kazini katika mazungumzo ya biashara na kuitangaza Tanzania.
………………………………………………………………………..
Na: Geofrey Tengeneza – Berlin
Tanzania ndio nchi iliyoongoza katika nchi za Afrka Mashariki kwa idadi kubwa ya makampuni binafsi, taasisi za umma na waonyeshaji walioshiriki katika maonesho ya ITB Berlin mwaka huu. Aidha banda la Tanzania limekuwa likiongoza katika nchi za Afrika Mashariki kwa kutembelewa na idadi kubwa watu na wafanyabiashara wa utalii kutoka nchi mbali mbali katika maonesho ya mwaka huu.

Akizungumza na Sauti ya Ujerumani katika banda la Tanzania katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya utalii jijini Berlin Ujerumani amesema idadi kubwa ya washiriki wa maonesho haya kutoka Tanzania unapolinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki, ni jambo linalotia moyo na linaloashiria kuendelea kukua kwa sekta ya utalii Tanzania.

Idadi ya taasisi na makampuni yanayoshiriki maonesho haya kutoka Tanzania chini ya uratibu wa Bodi ya Utalii Tanzania –TTB mwaka huu ni sitini (60) wakati makampuni mengine kadhaa yanashiriki yakiwa na mabanda yao binafsi. Baadhi ya makampuni hayo ni pamoja Leopard tours, Safari rangers, Tanganyika Wildness Camps, Kanzan wildlife safaris, na Moivaro Lodges & tented camps. AIdha makapuni mengine 17 kutoka Zanibar yanashiriki chini ya uratibu wa Jumuia ya makampuni ya usafirishaji watalii Zanzibar (ZATO).

Akizungumzia kuhusu Umoja wa forodha wa jumuia ya Afrika Mashariki Waziri Nyalandu amesema umoja huo ni muhimu sana katika kuimarisha jumuia ya Afrika Mashariki. “ Tunafurahi kuona kuwa umoja wa forodha unafanikiwa japokuwa wengi walidhani tusingefanikiwa, kwa kweli umoja huu ni muhimu sana kwa mustakabali wa jumuia yetu’ alisema.

Katika hatua nyingine washiriki wengi walioshiriki maonesho ya ITB kutoka Tanzania wameelezea kufurahishwa kwao na mafanikio waliyoyapata katika kutengeneza mahusiano ya kibiashara na wafanyabiashara wenzao katika sekta ya utalii na hoteli kutoka mataifa mengine “ Nilikuwa na mikutano mingi mizuri sana na wafanya biashara wa mataifa mengine, nashukuru nimefanya biahara” anasema Niccy Kiefer mfanyabiashara wa hoteli kutoka Zanzibar.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya usafirishaji watalii ya Laitolya tours & Safaris ya jijini Arusha Bw. Joackim Minde yeye alisema mwaka huu hali ya biashara katika maonesho haya haikuwa nzuri. Ametaja baadhi ya sababu zilizochangia hali hii kuwa ni pamoja na taarifa za ugonjwa wa Ebola katika nchi za magharibi mwa Afrika, na Tanzania kuwa eneo ghali sana la kiutalii ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Maonesho haya ya Kimataifa ya Utalii ya ITB ambayo ni makubwa kuliko yote duniani na yaliyohudhuriwa na nchi 190 ikiwemo Tanzania yanafikia kilele chake leo tarehe 8 Machi 2015.
MAMA SALMA KIKWETE MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOANI DAR

MAMA SALMA KIKWETE MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOANI DAR

March 09, 2015

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Raymond Mushi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Dar esb Salaam terehe 8.3.2015. RAY3 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipunga mkono ikiwa ni ishara ya kuyapokea  maandamano ya akina mama wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani tarehe 8.3.2015. RAY4 Wafanyakazi akina mama kutoka Jeshi la Polisi wakipita mbele ya Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete wakifuatiwa na Jeshi la zimamoto. RAY5Wafanyakazi akina mama kutoka Jeshi la Polisi wakipita mbele ya Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete wakifuatiwa na Jeshi la zimamoto. RAY7 RAY10 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na mamia ya akina mama kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Dar es Salaam tarehe 8.3.2015. RAY13 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi iliyotolewa na akina mama kutoka moja ya wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwee akitembelea mabanda ya maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wanawake katika Mkoa wa Dra es Salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani tarehe 8.3.2015. RAY16 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitazama vijarida mbalimbali vinavyotolewa na wanawake katika mkoa wa Dar es Salaam kuhusiana na nmasuala ya tafiti mbalimbali.
PICHA NA JOHN  LUKUWI.
RAIS DR. SHEIN AFUNGUA WA HOTELI YA PARK HYATT ZANZIBAR

RAIS DR. SHEIN AFUNGUA WA HOTELI YA PARK HYATT ZANZIBAR

March 09, 2015


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar (kulia) Kaimu Waziri wa Fedha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini (katikati) Mmiliki wa Hoteli hiyo Sheikh Ali Sayeed  Albawardy [Picha na Ikulu.] sh2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar (kulia) Kaimu Waziri wa Fedha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini (kushoto) Mmiliki wa Hoteli hiyo Sheikh Ali Sayeed  Albawardy [Picha na Ikulu.] sh3Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifuatana na Sheikh Ali Sayeed  Albawardy mmiliki wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar alipotembelea sehemu mbali mbali za Hoteli hiyo iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar baada ya kuifungua rasmi leo, [Picha na Ikulu.] sh4 
Wasoma utenzi Amina Mohamed na Khadija Ridhiwani (kulia) walipokuwa wakitoa burudani hiyo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi mbali mbali wakati wa sherehe za Ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo mtaa wa Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo ,[Picha na Ikulu.]
sh5 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini akiwa Kaimu waziri wa Fedha alipokuwa akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar kwa wananchi pamoja na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein azungumze na Wananachi baada ya kuifungua Hoteli hiyo iliyopo mtaa wa Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo ,[Picha na Ikulu.] sh6 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akitoa hutuba yake wakati alipokuwa akizungumza na wananchi na Viongozi mbali mbali na wawekezaji walioalikwa katika ufunguzi wa  Hotel ya Park Hyatt Zanzibar yenye hadhi ya juu  katika mtaa wa Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo ,[Picha na Ikulu.] sh7 
Baadhi ya waalikwa mbali mbali wakiwemo wawekezaji na wafanyabiashara wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akizungumza na wananchi na Viongozi mbali mbali na wawekezaji walioalikwa katika ufunguzi wa  Hotel ya Park Hyatt Zanzibar yenye hadhi ya juu  katika mtaa wa Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo ,[Picha na Ikulu.] sh8 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akiaaga na Sheikh Ali Sayeed  Albawardy baada ya kumalizika kwa sherehe za ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar (katikati) Meneja Mkuu wa Hoteli hiyo Bi Mercela Heeendoerfer,[Picha na Ikulu.]

VETA YAKUTANA NA WADAU WA VIWANDA VYA UMEME NA MAGARI KUJADILI KUHUSU MRADI WA MAFUNZO YANAYOTOLEWA NA VETA KWA KUSHIRIKIANA NA VIWANDA

March 09, 2015

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) imekutana na wadau wa viwanda vya umeme na magari jijini Dar es Salaam kujadili utekelezaji wa mradi wa mafunzo yanayotolewa na VETA kwa kushirikiana na viwanda ujulikanao kama Dual Apprenticeship Training Project.

Mradi huo uliopo kwenye majaribio tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011 kwa ushirikiano kati ya Hamburg Chamber of Skills Craft ya Ujerumani na VETA,unalenga kuandaa idadi kubwa ya mafundi stadi wenye ujuzi zaidi kwa vitendo kwa kuwa sehemu kubwa ya mafunzo hayo inafanyika viwandani.

Akifungua rasmi warsha hiyo mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi-VETA Leah Lukindo alisema kwamba ni muhimu kwa vyuo vya ufundi stadi kutoa stadi zinazohitajika na viwanda kwa kuwa viwanda vinategemea nguvu kazi hiyo ili kufanikisha malengo yake.

Alisema kukosekana kwa ushirikiano kati ya vyuo vya ufundi stadi na viwanda kunasababisha malalamiko mara kwa mara kutoka viwandani ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi nchini.

Alisisitiza kuwa mfumo wa Dual Apprenticeship Training unamwezesha kijana kupata ujuzi wa fani husika wakati anafanya kazi kwenye kiwanda hivyo kumuwezesha kwa kiasi kikubwa kujifunza zaidi kwa vitendo na kuendana na mahitaji ya soko la ajira pmaoja na kupata uzoefu na uelewa wa mazingira halisi ya kufanyia kazi.

Aliwataka wenye viwanda kuonyesha ushirikiano kwa kujiunga na mradi huu ambao una faida kubwa kwao kwani unawasaidia kupata mfanyakazi mwenye ujuzi unaotakiwa pamoja na uzoefu wa kazi kwa kuwa muda mmwingi wa masomo anakuwa kwenye kiwanda husika.
Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi-VETA Leah Lukindo akizungumza wakati akifungua rasmi warsha hiyo katika ukumbi wa hoteli ya Giraffe-Dar es Salaam.
Washiriki wa warsha hiyo ambao ni wadau wa viwanda vya umeme na magari wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.
Mratibu wa mradi huo Francis Komba akisisitiza jambo kwa washiriki wakati akiwasilisha mada inayohusu wajibu wa wadau wa viwanda katika utekelezaji wa mradi.
Meneja mradi Martin Mac Mahon akiwasilisha mada juu ya utekelezaji wa mradi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011 na mikakati iliyopo kuhakikisha mradi huo unafikia malengo waliyojiwekea.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizotolewa kuhusu mradi.
Mshauri wa mradi Ahmed Athuman (kulia) akijadili jambo juu ya mradi na Mkuu wa chuo cha VETA-Dar es Salaam Samuel Ng`andu wakati wa mapumziko.
Washiriki wa warsha wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi-VETA Leah Lukindo.