UN YATAKA VYOMBO VYA HABARI KUKAZANIA UWAJIBIKAJI

April 29, 2018


Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile akifungua kikao kati ya Jukwaa hilo na Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu akisoma hotuba kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.

Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika linaloshughulikia Watoto la Umoja wa Mataifa, Usia Nkhoma-Ledama akizungumzia uhusiano na ushirikiano kati ya TEF na mashirika ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.


Washiriki wa kikao cha Jukwaa la Wahariri (TEF) wakifuatilia kwa umakini mada ya Malengo ya Dunia na ushirikiano wa kuwezesha malengo hayo kutekelezeka wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.

Allan Lawa wa Mwananchi Communications akizungumzia ushirikiano kati ya TEF na UN wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.

Mwenyekiti wa zamani wa Jukwaa la Wahariri (TEF) ambaye pia ni mmoja wa waanzilishi wa TEF, Theophil Makunga akitoa maoni yake kuhusu namna ambavyo Umoja wa Mataifa na TEF wanavyoweza kushirikiana wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.

Zourha Malisa wa Mwananchi Communications akielezea umuhimu wa ushirikiano wa UN na Jukwaa la Wahariri kuhusisha pia Vyombo vya Mitandaoni na Bloggers wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.

Katibu wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Neville Meena akielezea kwa undani namna ambavyo mafunzo yaliyo katika mkataba wao na UN yatakavyoendeshwa wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.

Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu akisaini kanuni za ushirikiano kati ya TEF na UN kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.

Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu na Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile wakibadilishana nakala za ushirikiano kati ya TEF na UN wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.


Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Umoja wa Mataifa (UN) umetaka Vyombo vya Habari nchini kuweka mkazo katika kuandika na kutangaza masuala ya maendeleo na ya kiutu, hasa yale yanayoweza kujenga uelewa zaidi na kuchochea vitendo na uwajibikaji kwa manufaa ya Watanzania walio wengi.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez, katika mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofanyika mwishoni mwa juma mjini Morogoro.

Katika hotuba yake hiyo iliyosomwa na Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Hoyce Temu alisema, kwa kuwa Vyombo vya habari ndiyo kiunganishi kikuu kati ya watu, serikali na mashirika ya kimataifa hivyo ni wajibu wao kuandika habari zinazochochea maendeleo.

Aidha alisema kwa namna ya pekee, angependa kusisitiza umuhimu wa kuandika habari za hatua zinazopigwa katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano na vilevile MKUZA II na III.

“Haya ni maeneo muhimu kwa sababu aina ya mabadiliko tunayotaka kuyaona nchini Tanzania katika miaka michache ijayo yatawezekana tu ikiwa mipango hii mitatu itatekelezwa kwa ufanisi na kikamilifu kwa kuzingatia muda uliopangwa. Ni wajibu wenu, kama waandishi wa habari wanaojua kazi yao kushiriki kikamilifu katika wajibu huu wa kusimamia na kutolea taarifa masuala haya ili kuimarisha uwajibikaji” alisema Rodriguez.

Aidha alisema kwa kuwa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania unatekeleza mpango wa UNDAP II, ambao ni mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo unaolenga kuainisha vema programu ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Timu ya UN ya Nchi, ambao hatimaye utaimarisha fursa za maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa, vyombo vya habari vitaweza kusaidia kuhakikisha kwamba hakuna yeyote anayeachwa nyuma.

Serikali ya Tanzania na Timu ya Nchi ya UN zinashirikiana Dira ya Taifa na SDGs kwa kushughulikia maeneo matano ya kimaudhui ambayo ni Utawala wa Kidemokrasi, Haki za Binadamu & Usawa wa Jinsia—kuleta taasisi zenye uwazi na zenye kuwajibika na kuleta usawa wa jinsia.

Maeneo mengine ya kimaudhui ni Uwezo wa kujinusuru kwa kuimarisha usimamizi wa mazingira, upatikanaji wa nishati na kusaidia usimamizi wa wakimbizi na wahamiaji na kujenga taifa lenye ustawi kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya, maji safi, usafi wa mazingira; kuimarisha lishe kwa wanawake na watoto wa chini ya umri wa miaka mitano.

Aidha maeneo mengine ni Ukuaji jumuishi ambao unasaidia, kupunguza umaskini na kuongeza fursa za kuongeza ajira, upatikanaji wa elimu ya msingi na usalama wa kijamii hasa kwa makundi ya maskini/wanyonge na mwisho ni kuwezesha mawasiliano, Huduma za Uwandani, Utetezi na Ushirika

Wakati huo huo UN na TEF wametiliana saini mkataba utakaowezesha kujenga uwezo kwa waandishi wa habari kufuatilia utekelezaji wa malengo ya Dunia yalihuishwa katika Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano na Mkuza III.

Mpango huo ambao umo ndani ya UNDAP ll unashirikisha maarifa, uvumbuzi mpya, utetezi na kutomwacha yeyote nyuma na kuunga mkono sera mpya ambazo zitasaidia utekelezwaji wa Malengo ya Dunia.

“Tuna matumaini makubwa na ushirikiano huu na TEF ili kuhakikisha mpango wetu kama unavyoelewa katika Kanuni za Ushirikiano ambao tumetia saini leo unatekelezwa kikamilifu na kuleta matokeo yanayotakiwa.” Alisema Zaman.


Ushirikiano kati ya TEF na UN kwa sasa una miaka mitano.
Usalama Mahala pa Kazi, TANESCO yaibuka Kidedea yakabidhiwa Ngao, IRINGA

Usalama Mahala pa Kazi, TANESCO yaibuka Kidedea yakabidhiwa Ngao, IRINGA

April 29, 2018
Shirika la Umeme TANESCO, limeibuka Kidedea Kwa Kupata Ushindi Kwenye Shindano la Usalama Mahali pa Kazi lililoendeshwa na Taasisi ya OSHA katika Viwanja vya Kichangani Manispaa ya IRINGA.

TANESCO imepata Ushindi huo Kupitia Sekta ya Huduma, ambapo imekabidhiwa Ngao na Cheti ikiwa ni Heshima ya Kutambuliwa Kama Taasisi ambayo imefanya Vizuri Kwa Kuzingatia Usalama Mahala pa Kazi.

Baada ya Shirika hilo la Umeme Kutangazwa Mshindi na Kukabidhiwa Ngao, Afisa Afya na Usalama Makao makuu NELSON MNYANYI amesema Elimu ya Afya na Usalama imekuwa Kichocheo Kikubwa katika Kupunguza Ajali kwa Wafanyakazi wa TANESCO pamoja na Wananchi kwa Ujumla.

Kwa Upande wake Afisa Afya na Usalama FRED KAYEGA akielezea Ushindi huo amesema licha ya Kupokelewa kwa Faraja, ni Motisha kwa TANESCO kuendelea Kufanya Vizuri zaidi Kwenye Sekta ya huduma Kwa Kuzingatia Usalama Mahala pa Kazi.

Katika Banda la TANESCO elimu mbalimbali kuhusu Afya na Usalama na Elimu Kuhusu Matumizi Bora na Sahihi ya Umeme iliweza Kutolewa kwenye Viwanja vya Kichangani Manispaa ya Iringa.

Waziri wa Viwanda, Biashara ya Uwekezaji CHARLES MWIJAGE akiangalia Baada la TANESCO mara Baada ya Kulitembelea Katika Viwanja vya Kichangani Manispaa ya Iringa, ambapo Shirika hilo limeibuka Mshindi Kwenye Sekta ya Huduma Kupitia Mashindano ya Usalama Mahala pa Kazi yaliyoendeshwa na Taasisi ya OSHA.
Maaofisa wa Shirika la Umeme TANESCO, Kutoka Kushoto Sylvester Matiki ( Afisa Masoko ), Nelson Mnyanyi ( Afisa Usalama ), Fred Kayenga ( Afisa Muandamizi Usalama na Afya Mahali pa kazi ) pamoja na Hassan Athumani (Mwenyekiti wa majadiliano TUICO TANESCO) wakifurahia Ushindi wa Ngao na Cheti Baada ya Kukabidhiwa Kama Washindi Kwenye Sekta ya Huduma Kupitia Mashindano yaliyoendeshwa na Taasisi ya OSHA katika Viwanja vya Kichangani Manispaa ya Iringa.



Wananchi Mbalimbali Katika Manispaa ya Iringa Waliofika Katika Banda la TANESCO katika Viwanja vya Kichangani Wakipewa Elimu Kuhusu Afya na Usalama pamoja na Matumizi Bora na Sahihi ya Umeme.
Afisa wa TANESCO, Kitengo cha Huduma kwa Wateja ENIDY ELSON akitoa Elimu ya matumizi Bora ya Umeme kwa Wanafunzi na Wananchi Waliofika Kwenye Banda la Shirika hilo Wakati wa Shindao la Usalama Mahala pa Kazi lilioendeshwa na Taasisi ya OSHA katika Viwanja vya Kichangani Manispaa ya Iringa.

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI(WCF) UMEKUWA MSHINDI WA PILI KATIKA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI

April 29, 2018
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba (kulia), akipokea tunzo na cheti kutoka kwa Bw. Eric Shitindi katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu baada ya MFuko kushinda nafasi ya pili katika masuala ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani tarehe 28 Aprili katika Uwanja wa Kichangani Iringa.


                          NA MWANDISHI WETU, IRINGA

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeibuka mshindi wa pili katika masuala ya usalama na afya mahala pa kazi katika maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi nchini ambayo huadhimishwa duniani kote tarehe 28 Aprili kila mwaka.

Maadhimisho haya huratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) nchini na kwa mwaka huu yamefanyika Mkoani Iringa yakitanguliwa na maonyesho kutoka kwa wadau kuanzia tarehe 26 Aprili na kufikia kileleni leo tarehe 29.

Mgeni Rasmi katika kilele cha Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu ameipongeza WCF kwa ushindi walioupata na kuwasihi kuendelea kutoa elimu kwa wadau wake.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF Masha Mshomba, amefafanua kuwa moja ya malengo ya uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni kukuza na kuendeleza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo mahala pa kazi.

Mshomba ametoa ufafanuzi huo leo katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa baada ya kupokea tuzo na cheti cha Mshindi wa pili katika masuala ya afya ya usalama mahala pa kazi.

Aidha, akikabidhi tunzo hiyo kwa niaba ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi ameupongeza Mfuko kwa kuendelea kufanya kazi vizuri katika nyanja tofauti tofauti pamoja na kwamba hauna miaka mingi sana toka uanzishwe. “Tunajivunia sana kuona ya kwamba Mfuko umeweza kulipa fidia stahiki kwa wakati, kitu ambacho kilikuwa changamoto hapo awali” Aidha, pongezi zangu ziwafikie kwa kuanzisha mifumo inayoboresha huduma kwa waajili na waajiliwa wote ikiwemo mifumo ya ki- electroniki inayowazezesha waajili kujisajili, kulipia michango na kufuatilia michango yao.

Mfuko umehitimisha maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi katika Mkoa wa Iringa na unajiandaaa na semina ya wadau itakayofanyika tarehe 30 Aprili na hatimaye kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Tarehe 01 May 2018.

Katikati Bw. Eric Shitindi Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko baada ya kupokea tunzo na cheti katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi katika Uwanja wa Kichangani Iringa. (Akishikilia kombe pamoja na Bw. Shitindi ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba

Bw. Ibrahim Mussa Afisa Madai Mwandamizi – WCF akimhudumia mteja aliyetembelea banda ya WCF katika maonyesho yaliyofanyika katika viwanja vya Kichangani Iringa.
 Bw. Masha Mshomba akionyesha tuzo na cheti ambavyo Mfuko umetunukiwa.
  Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Uendeshaji Bw. Anselim Peter wakiwa ameshika tuzo hiyo huku, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia) na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Bi. Amina Likungwala, wakionyesha vyeti vya ushindi wa pili na cha ushiriki.
Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (katikati), akiwa ameshika tuzo hiyo huku, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia) na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Bi. Amina Likungwala, wakionyesha vyeti vya ushindi wa pili na cha ushiriki.







Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Bw. Fulgence Sebera, akizungumza

WANAWAKE 35,763 WAFANYIWA UCHUNGUZI WA AWALI WA SARATANI LA MLANGO WA KIZAZI MIKOA SITA INAYOFADHILIWA NA SHIRIKA LA AGPAHI

April 29, 2018

Mratibu wa Shirika la AGPAHI Mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon wakati akielezea kuhusu utekelezaji wa shughuli za kinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Tanga katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi na uchunguzi wa saratani kwa wakinamama.

Mratibu wa Shirika la AGPAHI Mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon akiteta jambo na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji mara baada ya kuelezea utekelezaji wa shughuli za kinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Tanga katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi na uchunguzi wa saratani kwa wakinamama kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Mratibu wa Shirika la AGPAHI Mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon katika mwenye miwani akifuatilia kwa umakini matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo
Mratibu wa Shirika la AGPAHI Mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon kulia akiteta jambo na Dkt Hamisi mara baada ya kumalizika uzinduzi huo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya uzinduzi huo wa tatu kutoka kushoto nyuma mwenye miwani ni Mratibu wa Shirika la AGPAHI Mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon

WANAWAKE 35,763 wamefanyiwa uchunguzi wa awali wa saratani ya mlango wa kizazi kwenye mikoa sita nchini inayofadhiliwa na shirika la AGPAHI  kwa njia ya Visual Inspection with Acetic (VIA) kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari mwaka 2017 hadi Machi mwaka 2018.

Hayo yalibainishwa  na Mratibu wa Shirika la AGPAHI Mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon wakati akielezea kuhusu utekelezaji wa shughuli za kinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Tanga katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi na uchunguzi wa saratani kwa wakinamama ambapo mikoa hiyo sita ni mkoa wa Tanga,Mwanza ,.Mara,Geita ,Shinyanga na Simiyu.
Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwenye kituo cha Afya Ngamini Jijini Tanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa na wilaya ambapo alisema kati yao wanawake 16561 sawa na asilimia 46.5 wanaishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi

Alisema kati ya wote waliofanyiwa uchunguzi kwa njia ya VIA,2154 sawa na asilimia 6 walikutwa na dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi huku 150 sawa na asilimia 0.4 walikutwa na eneo kubwa kwenye mlango wa kizazi lenye dalili za kansa hiyo .

Aidha alisema pia wengine 534 ambao ni sawa na asilimia 1.4 walishukiwa kuwa na kansa hiyo ambapo huduma za matibabu na rufaa zilitolewa kwa watu hao kwa kuzingatia mwongozo husika.

Alieleza kuwa mojawapo ya kazi ambazo shirika la Agpahi limefanikisha kwa kushirikiana na mkoa, halmashauri katika kufikia ufanisi wa huduma za kinga ya saratani ya mlango wa kizazi kwa kutoa vifaa tiba kwenye halmashauri zote zenye vituo 54 vinavyotoa huduma hizo.

Mratibu huyo alisema kwa mkoa wa Tanga katika halmashauri ya Jiji mwezi Aprili shirika hilo limetoa vifaa tiba vyenye thamani ya fedha za kitanzania milioni 50,934,200.00 ambapo baadhi hya vifaa hivyo ni pamoja na Autoclave Steam Sterilizer,Metal Punch Biopsy Machine,Medical Trolley,Kidney Dishes na Privacy Screen.

Alisema pia shirika hilo limeendelea kuwajengea uwezo watumishi wanaotoa huduma za afya kupitia ufadhili mafunzo (Training na Mentorship) ambapo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 wamewapatia mafunzo watumishi 90.

Mwisho.