WAKUU WA IDARA WA BOMBO HOSPITALI WAKABIDHIWA LAPTOP.

February 05, 2024



Na Mwandishi Wetu, Tanga

UONGOZI wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo katika kuboresha huduma leo umekabidhi vitendea kazi Kompyuta Mpakato (Laptop) kwa Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali kwa ajili ya kuwarahisishia utendaji kazi wao wa kila siku.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo ambapo Matron wa Hospitali hiyo Beatrice Rimoy ambapo aliwakabidhi wakuu wa vitengo mbalimbali vitendea kazi hivyo huko akiwataka kuhakikisha wanavitumia kwenye matumizi yaliyokusudiwa na sio vyenginevyo.

“Leo tunapokea laptop tunakwenda kuzitumia kwenye kazi na sio za kwenda nazo nyumbani kwani zinapaswa kutumika kwenye matumizi yaliyokusudiwa ya kiofisi na sio vyenginevyo Alisema Matron

Alisema hatua ya uongozi wa Hospitali hiyo kukabidhi vifaa hivyo kutokana na kwamba hivi sasa vitu vingi vinaendelea kufanyika kwa kuondoka kwenda kwenye mfumo wa makaratasi na kwenda kwenye mfumo wa mtandao.

“Nitoe wito kwamba mhakikishe mnazitunza lakini kubwa kuhakikisha zinatumika kwenye matumizi yaliyokusudiwa ya Kiserikali na sio vyenginevyo ikiwemo yale ya binafasi”Alisema Matron huyo.

Naye kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Tehama katika Hospitali hiyo William Masika aliwataka kuhakikisha wanatumia kompyuta hizo mpakato kwa ajili ya kuongeza ufanisi na tija katika kuhakikisha taarifa mbalimbali zinajazwa kwa ushahihi.



KATAMBI: KIWANGO CHA PENSHENI YA KILA MWEZI KWA WASTAAFU KIMEBORESHWA

KATAMBI: KIWANGO CHA PENSHENI YA KILA MWEZI KWA WASTAAFU KIMEBORESHWA

February 05, 2024

 




NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi, akijibu swali la Mbunge wa Segerea (CCM), Mhe.Bonnah Kamoli leo Februari 5,2024 bungeni jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, DODOMA

NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi amesema katika kanuni mpya ya mafao iliyoanza kutumika Julai mosi 2022, serikali iliboresha kiwango cha mafao ya pensheni ya kila mwezi kwa wastaafu kutoka asilimia 50 hadi 67.

Mhe.Katambi ameyasema hayo Februari 5, 2024 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Segerea (CCM), Mhe.Bonnah Kamoli ambaye amehoji lini kanuni mpya za malipo ya pensheni kwa wastaafu ya kila mwezi ya kutoka asilimia 50 hadi 67 itaanza kutumika.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Katambi amesema kupitia gazeti la serikali namba 357 la Mei 20, 2022 ilitangaza kanuni hiyo iliboresha kiwango cha mafao ya pensheni ya kila mwezi kwa wastaafu.

Amesema kanuni hizo ziliandaliwa kwa kushirikisha wadau wote (Serikali, Wafanyakazi na Waajiri) kwa lengo la kufanya maboresho ya pensheni ili kuwianisha mafao ya wanachama na kuifanya mifuko kuwa endelevu.

UTAFITI: MABAKI YA MKONGE HUZALISHA PROTINI, MBOLEA

February 05, 2024

 Imezoeleka mkonge baada ya kuchakatwa na kupatikana singa (sisal fibre) mabaki yake (sisal waste) hutupwa kama uchafu kwa kuwa hayana matumizi mengine.


Hatua hiyo ni tofauti kwa Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD), katika Chuo Kikuu cha Afrika cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia (NM-AIST) kilichopo mkoani Arusha, Aziza Konyo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), amefanya utafiti na kuzalisha nzi chuma (black soldier flies) na mbolea kwa kuongeza thamani kwa kutumia mabaki hayo ya mkonge.

Akizungumza baada ya kikao cha uwasilishaji wa ugunduzi wa utafiti huo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona amesema utafiti huo ambao umesajiliwa kwa hati miliki pia umebaini licha ya kuzalisha nzi chumaa hao ambao hutumika kama protini kwenye chakula cha mifugo lakini pia mabaki ya chakula wanachokula nzi chuma hao ni mbolea nzuri inayotumika katika mazao mbalimbali.

“Bodi imepokea wasilisho la utafiti huo na imefurahi kuona kwamba zao la mkonge linazidi kupata thamani kwa sababu tumezoea baada ya kupatikana singa basi kinachobaki chote ni uchafu kinatupwa.

“TSB ina mahusiano ya muda mrefu na Chuo cha Nelson Mandela katika kufanya tafiti mbalimbali kuhusu uongezaji thamani wa zao la mkonge. Kwa hiyo Aziza chini profesa wake Anthony Mshandete na Revocatus Machunda amefanya utafiti wa kuzalisha nzi chuma (black soldier flies) kutokana na mabaki ya mkonge (sisal waste) ambayo hutumika kama protini kwenye chakula cha mifugo jamii ya ndege wanyama na binadamu,” amesema Kambona.

Utafiti huu ni wa pili kufanyika na chuo hicho ambapo utafiti wa kwanza unatekelezwa na chuo hicho kwa ushirikiano na Serikali ya Denmark kupitia Shirika lake la Maendeleo (Danida), ambapo umejikita katika maeneo matatu ambayo ni uzalishaji gesi asilia, ujenzi na kile kitakachozalishwa kutokana na gesi asilia.

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Carbonovia ya nchini  Uingereza, inayohusika masuala ya biashara ya hewa ukaa (carbondioxide) Dk. Mike Mason akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona jijini Tanga alipotembelea ofisi za bodi hiyo kwa ajili ya mazungumzo ya kufanya utafiti wa kuzalisha protini kutokana na mabaki ya mkonge, wengine ni watumishi wa TSB na Chuo Kikuu cha Afrika cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia (NM-AIST).

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Bw. Saddy Kambona akipokea nzi chuma (black soldier flies) na mbolea kutoka kwa Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD), katika Chuo Kikuu cha Afrika cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia (NM-AIST), kilichopo mkoani Arusha, Bi. Aziza Konyo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) aliyefanya utafiti huo kwa kuongeza thamani kwa kutumia mabaki ya Mkonge (sisal waste).

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Carbonovia ya nchini  Uingereza, inayohusika masuala ya biashara ya hewa ukaa (carbondioxide) Dk. Mike Mason akimwonyesha protini iliyozalishwa na mabaki ya mkonge (sisal waste) Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona jijini Tanga alipotembelea ofisi za bodi hiyo kwa ajili ya mazungumzo ya kufanya utafiti wa kuzalisha protini hiyo ambayo ni gharama nafuu zaidi, wengine ni watumishi wa TSB na Chuo Kikuu cha Afrika cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia (NM-AIST).





ST MARY'S YAZAWADIA WALIOPATA DIVISION ONE

February 05, 2024

 


Mwenyekiti wa Bodi ya shule za St Marys Dallas Mhoja akimpa cheti na zawadi ya fedha taslim mwalimu wa shule ya sekondari St Mary’s Mbezi Beach, Angel Focus, baada ya shule hiyo kufanya vizuri kwenye mkitihani ya kidato cha nne kufanikiwa kutoa wanafunzi wengi wa daraja la kwanza na daraja la pili. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa bodi, John Kibona.
 Mwenyekiti wa Bodi ya shule za St Marys Dallas Mhoja akimpa cheti na zawadi ya fedha taslim Makamu mkuu wa shule ya St Mary’s Mbezi Beach, Rajab Balele kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya shule za St Marys Dallas Mhoja akimpa cheti na zawadi ya fedha taslim Mkuu wa taaluma wa St Mary’s Mbezi Beach High School, Shadrack Mgaya baada ya shule hiyo kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne mwaka huu.
Picha ya pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri


Na Mwandishi Wetu
WANAFUNZI waliomaliza kidato cha nne kwenye shule ya sekondari St Mary’ s Mbezi Beach na kufaulu kwa daraja la kwanza wamepewa zawadi mbalimbali kama motisha kwa wanafunzi wengine kuendelea kufanya vizuri kitaaluma.


Hafla ya kuwapongeza wanafunzi hao ilifanyika jana kwenye maeneo ya shule hiyo, Mbezi Beach na kuhudhuriwa na wazazi na wanafunzi waliomaliza kidato cha nne.


Zawadi walizopewa wanafunzi hao ni pamoja na fedha taslim, nguo za michezo pamoja na vitabu mbalimbali vya kitaaluma.


Akizungumza kwenye hafla hiyo, Makamu Mkuu wa shule hiyo, Rajab Balele, alisema mwaka 2020 walimu waliahidi kuleta mageuzi makubwa na walipambana usiku na mchana na kufanikiwa kupata matokeo mazuri.


Alisema wanafunzi 106 wa shule hiyo walihitimu kidato cha nne mwaka jana na miongoni mwao, wanafunzi 29 walipata daraja la kwanza, daraja la II wanafunzi 35 wanafunzi 13 daraja la tatu na kwamba hakuna aliyepata sifuri.




“Walimu kwa kushirikiana na wanafunzi wamefanyakazi kubwa sana usiku na mchana kuwa wabunifu kufundisha mpaka wanafunzi wengi kufaulu kwa alama za juu,” alisema na kuongeza


“Nilipopata matokeo yetu ya kidato cha nne kwa kweli nilichanganyikiwa kwasababu sikuwa natarajia kwamba tutafaulisha kwa kiwango kikubwa namna hii, tulilahidi kufanya vizuri lakini matokeo yamekuwa mazuri sana kuliko nilivyotarajia,” alisema


Balele aliwataka wanafunzi hao wasibweteke na badala yake waendelee kufanya vizuri kwenye elimu ya kidato cha tano na sita ili kupata alama zitakazowawezesha kujiunga na vyuo vikuu bila vikwazo.


“Kuna wakati shule ilikuwa hadi daraja 0 wanafikia wanafunzi 62 lakini kwa sasa hakuna division 0, na daraja la kwanza wameongezeka huu ndo mwaka tumefanikiwa kupata divisheni one nyingi kuliko mwaka wowote,” alisema na kuongeza


“Kuna kufaulu na kufaulu sana, kwa hiyo ukiangalia matokeo yetu ya mwaka huu darala la kwanza za kiwango cha juu tumezipata nyingi na huo ndio utakuwa mwendo wetu tutahakikisha hakuna daraka 0 miaka yote na daraja la kwanza zitaendelea kuongezeka,” alisema


Mkuu wa Taaluma wa shule hiyo, Shadrack Mgaya, alisema wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali ya kitaaluma.


Alisema mafanikio ya wanafunzi yanategemea pembe tatu ambazo ni mwalimu, mwanafunzi na mzazi ambapo kila mmoja anapotimiza wajibu wake matokeo yanakuwa mazuri kama ambayo shule hiyo imepata kwa kidato cha nne.