ZIARA ya Rais wa Zanzibar DK.SHEIN- Nchini Ujerumani ATEMBELEA HOSPITALI WURZBURG

ZIARA ya Rais wa Zanzibar DK.SHEIN- Nchini Ujerumani ATEMBELEA HOSPITALI WURZBURG

June 07, 2015

???????????????????????????????????? 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) na ujumbe wake wakipewa maelezo na Mkuu wa Idara ya maradhi ya Tropic Prof.Dr.med,August Stich wakati  alipotembelea katika Chuo cha Afya  cha Wurzburg Nchini Ujerumani katika ziara ya kikazi .
[Picha zote na Ramadhan Othman,]
???????????????????????????????????? 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiuliza swali wakati alipotembelea katika Chuo cha Afya  cha Wurzburg Nchini Ujerumani ambacho hutoa matibabu na kufanya tafiti mbali zinazohusu maradhi ya Binadamu baada ya kupata maelezo kwa Mkuu wa Idara ya maradhi ya Tropic Prof.Dr.med,August Stich wakati alipoelezea  mambo mbali mbali (kulia) Balozi Philip Marmon na (kushoto)Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,
???????????????????????????????????? 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya maradhi ya Tropic Prof.Dr.med,August Stich wakati alipotembelea katika Chuo cha Afya kinachotoa huduma ya matibabu  kujishuhulisha na tafiti mbali mbali za maradhi ya Binadamu akikwa katika ziara ya kikazi katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani Chuo hicho  kimetoa mchango mkubwa katika kupambana na maradhi ya Ebola yaliyotokea katika Nchi za Magharibi.
????????????????????????????????????Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiwa na ujumbe wake wakipewa maelezo na Mkuu wa Idara ya maradhi ya Tropic Prof.Dr.med,August Stich wakati walipokuwa wakiwaangalia madaktari waliovalia vazi rasmi la kujikinga na maradhi ya Ebola  wakati alipotembelea katika Chuo cha Afya  cha Wurzburg Nchini Ujerumani
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya maradhi ya Tropic Prof.Dr.med,August Stich wakati alipotembelea katika Chuo cha Afya kinachotoa huduma ya matibabu  kujishuhulisha na tafiti mbali mbali za maradhi ya Binadamu akikwa katika ziara ya kikazi katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani Chuo hicho  kimetoa mchango mkubwa katika kupambana na maradhi ya Ebola yaliyotokea katika Nchi za Magharibi.
????????????????????????????????????
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (kushoto) akiwa katika chakula maalum kwa ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati ujumbe huo ukiwa katika ziara ya kikazi katika Mji wa Wurzburg uliposhiriki katikaTamasha la Maonesho ya Muziki na Utamaduni liliofanyika na kujumuisha Wasanii na Wanamuziki mbali mbali Afrika na Nchi nyengine Duniani ikiwemo Zanzibar,
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi wengine akiwepo mwenyeji wake Mstahiki Meya wa Mji wa Wurzburg  Mhe,Christian Schuehadt (kulia) katika chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa heshma yake akiwa katika ziara ya kikazi katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani alipohudhuria katika Tamasha la 27 la Muziki na Utamaduni lililoshirikisha Wasanii mbali mbali na Wanamuziki wakiwemo wa Nchi za Afrika na Duniani kwa ujumla,
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee (kulia) na Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa na Uchumi Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa (kushoto) na Msaidizi Naibu Mstahiki Meya wa Mji wa Wurzburg Dr.Adolf Bauer wakati wa chakula maalum cha jioni kilichoandaliwa kwa Ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ziara ya kikazi  nchini Ujerumani katika Mji wa Wurzburg alipohudhuria katika Tamasha la 27 la Muziki.

MH. LOWASSA ATUA ZANZIBAR KUSAKA WADHAMINI

June 07, 2015

Waziri Mkuu wa zamaninaMbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowasa, (kulia), akipokewa na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mjini Unguja, Borafia Silima Juma, wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mkoa wa Mjini, Unguja Jumamosi usiku, Juni 6, 2015. Mh.  Lowassa, yuko Zanzibar kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015. (Picha na K-VIS MEDIA)
Mh. Lowassa, akifurahia jambo na Mzee Borafia, mara baada ya kuwasili kisiwani Zanzinzibar, akitokea Mwanza
Wazirti Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mjini, kisiwani Unguja, Zanzibar, Borafia Silima Juma, (kulia), na aliyekuwa Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba, Simai Mohammed Jumamosi usiku Juni 6, 2015 mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar. Mh.  Lowassa, yuko Zanzibar kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015

Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, (kushoto), akiwasalimia wakereketwa wa CCM, waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, Jumamosi usiku Juni 6, 2015. Mh.  Lowassa, yuko Zanzibar kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015

Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, (kushoto), akiwasalimia vijana wa Kimasai, waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, Jumamosi usiku Juni 6, 2015. Mh.  Lowassa, yuko Zanzibar kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, (aliyevaa suti), akiondoka uwanja wa ndege wa Kitaifa wa Zanzibar, muda mfupi baada ya kuwasili huku akipokewa na wakereketwa wa CCM, waliofika kumlaki Jumamosi usiku Juni 6, 2015. 2015. Mh.  Lowassa, yuko Zanzibar kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015
Mh. Lowassa, akiongozana na Mbunge wa Kigoma Mjini, Mh. Peter Serukamba, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar Jumamosi Juini 6, 2015.

NAIBU WAZIRI WA MAILIASILI NA UTALII AFUNGUA MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII YA KILIFAIR 2015

June 07, 2015


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mohamed Mgimwa akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Moshi Club kwa ajili ya kufungua rasmi maonesho ya kimatifa ya Kitalii yajulikanayo kama KiliFair 2015.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii,Mohamed Mgimwa akisalimiana na Naibu waziri wa Habari Utamaduni,Utalii na Michezo wa Zanzabar Bi Hindi Khamis walipokutana katika maonesho hayo.
Mgeni rasmi katika maonesho hayo,Naibu waziri wa utalii,Mohamed Mgimwa akiwa katika picha ya pamoja na iongozi wengine akiwemo kaimu mkuu wamkoa wa Kilimanjaro,Dkt Charles Mlingwa,katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Seveline Kahitwa,Mhifadhi mkuu KINAPA,Erastus Rufunguro.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii,Mohamed Mgimwa akiwa ameambata na naibu waziri wa habari,utamaduni ,utalii na Michezo Zanzibar,Bi Hindi Khamis alipokuwa akitembelea banda la maoensho ya utalii la Zanzibar.
Naibu Waziri ,Mgimwa akizungumza na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya utalii ya Zara tour 
Naibu Waziri ,Mgimwa akinywa kahawa alipotembelea banda la kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines.
Waoneshaji wengine walibuni mbinu zaidi wakiwatumia wafugaji jamii ya maasai katika maonesho hayo.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro KINAPA,Erastus Rufunguro akiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Asante Tour ,Cuthbert pamoja na mkurugenzi wa Kilifair ,Tom.
Naibu waziri Mgimwa akizungumza na Cuthbert.
Naibu Waziri wa maliasili na utalii akisalimiana na Meneja Biashara wa kampuni ya Kibo Palace ,Charity Githinji ,wakati Naibu waziri alipotembelea banda hilo.
Baadhiya wafanyakazi wa kampuni ya Kibo Palace wakiwa katika banda lao la maonesho 
Naibu waziri wa utalii Zanzibar Bi Hindi akipokea zawadi toka Kibo Palace.
Manaibu waziri wa utalii,Tanzania bara na Zanzibar,Mgimwa na Bi Hindi wakiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa Kilifair Dominic Shoo na Tom.
Mkurugenzi wa kampuni ya Kilifair ambao ndio waandaji wamaonesho hayo ,Dominic Shoo akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo .
Naibu waziri wa habari,utamaduni,utalii na Michezo Zanzibar ,Bi Hindi Khamis akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo.
Baadhi ya wageni waliofika kwa ajili ya maonesho hayo.
Naibu Waziri ,Mgimwa akitoa hotuba yake ya ufunguziwa maonesho ya kimataifa ya utalii ya Kilifair 2015 yanayofanyika katika viwanja vya Moshi Club.
Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja.
Naibu waziri Mgimwa akiteta jambo nammoja wa wakurugenzi wa kampunu ya Kilifair Dominic Shoo.
Kikundi cha burudani toka nchini Kenya kikitoa burudani katika maonesho hayo.
Baadhi ya mabanda yaliyopo ndani ya viwanja vya Moshi Club yakionesha bidhaa na huduma zitolewazo na kampuni mbalimbali za utalii.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.