BREAKINGI NEWSSS WATU ZAIDI YA KUMI WAFARIKI KATIKA AJALI MBALIZI MBEYA

August 29, 2014




AFRICAN SPORTS WAANZA VEMA MAANDALIZI YA LIGI DARAJA LA KWANZA.

August 29, 2014
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
TIMU YA African Sports “Wanakimanumanu “jana ilianza vema maandalizi ya kuelekea michuano ya Ligi daraja la kwanza baada ya kuibamiza timu ya Maafande wa Jeshi la Magereza mkoani hapa Small Prison mabao 2-0.

Mchezo huo wa kirafiki ulichezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani na kushuhudiwa na mashabiki mbalimbali wa soka mkoani hapa.

African Sports iliyopanda daraja msimu huu na kufanikiwa kucheza ligi daraja la kwanza ikwisha kucheza michezo mbalimbali ya majaribio ili kuweza kukipa makali kikosi hicho ambacho kitashiriki ligi hiyo kwa mara ya kwanza tokea iliposhuka daraja miaka.

Katika mchezo huo bao la kwanza la African Sports lilifungwa dakika ya 42 kupitia Mohamed Farid ambaye aliweza kutumia uzembe wa mabeki wa wapinzani wao kupachika wavuini bao hilo kabla ya timu hizo haijakwenda mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo timu zote ziliingia uwanjani zikiwa na nguvu mpya baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wao.

Wakionekana kujipanga kwwenye mchezo huo, African Sports waliweza kuongeza wimbi la mashambulizi langoni mwa timu pinzani hali iliyopelekea kuongeza bao la pili ambalo lilifuingwa na Evalisti Joseph ambaye alimaliza kazi nzuri iliyofanywa na Mohamed Farid.

Akizungumza baada ya kumalizika mchezo huo,Ofisa Habari wa timu ya African Sports ,Saidi Karsandas alisema kuwa mipango ya timu hiyo ni kucheza mechi nyingi za majaribio ili kuweza kukiweka kikosi hicho imara kwa ajili ya michuano ya ligi daraja la kwanza.

MWAMBOA WAPANGA KUTOA ELIMU YA UFUNDI SEREMALA KWA VIJANA .

August 29, 2014
KUSHOTO NI RAIS JAKAYA KIKWETE AKISALIMIA NA MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO MKOANI TANGA,ALHAJ MAJID MWANGA WAKATI ALIPOFANYA ZIARA WILAYANI HUMO.
NA MWANDISHI WETU,LUSHOTO.
KIKUNDI cha Ufugaji wa Nyuki na Hifadhi ya Mazingira cha Mwamboa kilichopo Kata ya Mwangoi wilayani Lushoto mkoani Tanga kimepanga kutoa mafunzo kwa vijana wa kike na wa kiume kwenye fani za ufundi seremala kwa ajili ya kutengeneza mizinga ya kisasa,uchakataji wa asali na Nta ifikapo Juni 2015.

Wakiwa na madhumuni ya kutoa ajira kwa vijana wasiopungua 20 lengo
  likiwa kuwakomboa na limbi la umaskini pamoja na kuwaepusha kukaa vijiweni ambapo hutumia muda mwingi kufanya vitendo viovu kwenye jamii zao ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya.

Hayo yalielezwa na Ofisa Ugani wa Kata hiyo, Julius Mshauri wakati
  akizungumza na blog hii ambapo alisema kuwa licha ya hivyo wamepanga kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kutoka kilo 1,000 iliyopo sasa hadi kufikia 2,500 ifikapo Juni 2015.

Mashauri alisema kuwa katika kuhakikisha jambo hilo linapata mafanikio
  tayari wamekwisha kustawisha miche ya miti ya aina tofauti tofauti ipatayo 15,000 na kuiuza kwa wananchi kulingana na mahitaji yao ikiwemo kuigawa kwa wanavikundi kwa lengo la kuhifadhi mazingira wakati msimu wa mvua unapoanza mwaka huu.

Akizungumzia chimbuko la kikundi hicho alisema kuwa ni mradi wa

utafiti wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo kupitia program yao
ijulikanavyo ASARECA(Associationfor Strehgttening Agricultural
Research in Eastern and Central Africa).

Alisema kuwa ndani ya program hiyo kikundi hicho kimeweza kushiriki
  kwenye mafunzo ya aina mbalimbali hasa ya ufugaji bora wa nyuki na utafutaji wa masoko kwa kushiriki kwenye maenyesho hususani ya kibiashara ya kimataifa na pia yale ya nanenane.

Ofisa ugani huyo alisema kikundi hicho kilipata ufadhili kutoka

serikali ya Poland kwa kupitia shirika la Poland East Africa Economic Foundation ambapo waliweza kufanya nao kazi kwa kipidi cha mwaka mmoja.

Hata hivyo alisema kuwa ndani ya kipindi hicho walifanya mambo

mbalimbali ikiwemo ujenzi wa kituo cha kikundi hicho ambapo ujenzi huo uligharimu kiasi cha sh.milioni 45 zilitumika mbali na nguvu za wananchi zilizotumika kwa wanakikundi zilikuwa ni tsh milioni 9.

WEMA SEPETU ANENA HAYA BAADA YA DIAMOND PLATINUMZ KUTANGAZA NDOA

August 29, 2014

BINTI APOTEZA MAISHA ZIKIWA ZIMEBAKI SIKU CHACHE AFUNGE NDOA

August 29, 2014

 Binti ambaye hakuweza kufahamika jina lake kwa haraka (pichani chini), ambaye alikuwa afunge ndoa na mchumba wake hivi karibuni,  amepata ajali na kufariki dunia akiwa na 'mchepuko'.
Aidha imeelezwa kuwa wakati mchumba wake akiwa katika harakati za kukamilisha mipango ya ndoa akapata taarifa kuwa mchumba wake huyo amefariki kwa ajali ambapo hakuweza kuamini hadi alipoonyeshwa picha za ajali hiyo.
Imeelezwa kuwa marehemu alimuaga mchumba wake huyo kuwa anakwenda kulala kwa dada yake na kwenda kinyume na alivyoaga na kukutwa na ajali hiyo iliyompelekea umauti. Katika ajali ya gari hilo lililokuwa na wapenzi wawili wote wamepoteza maisha papo hapo huko mkoani Geita.
marehemu enzi za uhai wake (pichani chini na juu)
Baada ya kupata ajali. Habari na picha kwa hisani ya mdau, Tarime

OKWI AJIFUNGA TENA SIMBA MIAKA MIWILI.

August 29, 2014




STAILI ile ile waliyotumia Yanga SC kumpata mshambuliaji Emmanuel Arnold Okwi ndiyo ambayo klabu yake ya zamani, Simba SC inaitumia kumrejesha kundini Mganda huyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jioni hii mjini Dar es Salaam, Okwi amesema kwamba amesaini Simba SC mkataba huru wa muda, baada ya Yanga SC kumpa barua ya kusitisha mkataba naye jana pamoja na kumshitaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Okwi amesema ameamua kuomba kuichezea Simba SC kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC ili kulinda kipaji chake, kwa kuwa hata FIFA haitaki mchezaji akae bila kucheza.


“Sasa wakati Yanga wanaendelea na kesi yao, mimi ninaomba nichezee Simba SC ili kulinda kipaji changu. Nimewaandikia barua TFF na FIFA pia na nina matumaini usajili wangu utaidhinishwa, kwa sababu mimi si tatizo katika hili,”amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji.
“Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”amesema Poppe.  

Yanga mtanikoma; Okwi akiwa ameshika jezi yake nbamba 25 kwa pamoja na Hans Poppe

Tayari Simba SC imetuma jina la mchezaji huyo katika usajili wake TFF na ataungana na Mganda mwenzake, Joseph Owino, Warundi Pierre Kwizera na Amisi Tambwe na Mkenya, Paul Kiongera katika wachezaji watano wa kigeni. 

“Tumewaandikia barua TFF kuomba kumtumia mchezaji huyu kwa muda wakati kesi yake na Yanga inaendelea, tumeambatanisha na barua yake ambayo yeye anatuomba kucheza kwetu kulinda kipaji chake,”amesema Poppe.

Okwi aliichezea Simba SC tangu mwaka 2009 kabla ya Januari mwaka jana kuuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 Etoile du Sahel ya Tunisia. Etoile haikulipa fedha hizo Simba SC na baadaye ikaingia kwenye mgogoro na Okwi, aliyedai hakulipwa pia mishahara yake kwa miezi mitatu. Okwi akawafungulia Etoile kesi FIFA na akaomba wakati mgogoro wao unaendelea, aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake, ndipo akajiunga na SC Villa ya kwao.

Akiwa SC Villa ndipo aliposaini Yanga SC Desemba mwaka jana na pamoja na mapingamizi yaliyoanzia ndani, na baadaye klabu yake, Etoile- lakini Okwi aliidhinishwa kuichezea timu hiyo ya Jangwani.

Okwi aliichezea Yanga SC mechi 11 na kuifungia mabao matano- lakini kuelekea mechi tano za mwisho za Ligi Kuu msimu uliopita akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo. Okwi alisusa kushinikiza amaliziwe fedha zake za usajili na mgogoro wao umeendelea huku mchezaji huyo akiwa amesusa tangu Machi, miezi minne tu baadaye tangu asajiliwe.

Vikao kadhaa vimekwishafanyika baina ya Okwi na Yanga SC tangu hapo kutafuta suluhu ya suala hilo na kikao cha mwisho leo baina ya mchezo huyo na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji matokeo yake ni nyota huyo kurejea Msimbazi.

Kuhusu deni lao la dola 300,000 kumuuza mchezaji huyo Etoile, Poppe amesema haihusiani kabisa na usajili wake huu wa sasa. “Ile kesi yetu ya madai ya fedha zetu kule FIFA ilikwishamalizika na vielelezo vyote vilipelekwa, bado kutolewa hukumu tu,” amesema